Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 337

Nimefanya kazi na kusema kwa njia hii miongoni mwenu, Nimetumia nguvu na juhudi, ila ni wakati upi kamwe mmewahi kusikiliza kile Ninachowaambia wazi wazi? Ni wapi mmeniinamia Mimi, Mwenyezi? Kwa nini mnanitendea namna hii? Kwa nini kila kitu mnachokisema na kufanya huchochea hasira Yangu? Kwa nini, mioyo yenu imeshupaa? Je, Nimewahi kuwapiga kumbo kamwe? Kwa nini hamfanyi kitu chochote kingine ila kunifanya mwenye huzuni na wasiwasi? Mnasubiri siku ya ghadhabu Yangu, Yehova, kuja juu yenu? Je, mnanisubiri Mimi kutuma hasira kwenu iliyochochewa na makosa yenu? Si kila kitu Ninachokifanya ni kwa ajili yenu? Ilhali kila wakati mmenitendea Mimi, Yehova, kwa njia hii: kuiba sadaka Yangu, kuchukua sadaka ya madhabahu Yangu nyumbani kulisha watoto wa mbwa mwitu na vitukuu vyake katika makazi ya mbwa mwitu; watu wanapigana wenyewe kwa wenyewe, wakikabiliana na mtazamo wa hasira kwa panga na mikuki, kurusha maneno ya Mimi, Mwenyezi, kwenye choo kuwa machafu kama kinyesi. Uadilifu wenu uko wapi? Ubinadamu wenu umekuwa unyama! Mioyo yenu kwa muda mrefu imegeuka kuwa jiwe. Je, hamjui kwamba siku Yangu ya ghadhabu itakapofika itakuwa ndio wakati Nitakapokuhukumu mabaya mliyotenda dhidi Yangu leo, Mwenyezi? Je, mnafikiri kwamba kwa kunidanganya Mimi kwa njia hii, kwa kutupa maneno Yangu katika matope na kutoyasikiza—unafikiri kwamba kwa kutenda namna hii nyuma Yangu mnaweza kutoroka macho Yangu ya ghadhabu? Je, hamjui kwamba mlishaonekana na macho Yangu, Mimi Yehova, wakati mliiba sadaka Yangu na kutamani mali Yangu? Je, hamjui kwamba wakati mliiba sadaka Yangu, ilikuwa mbele ya madhabahu ambapo dhabihu hutolewa? Mnawezaje kujiamini wenyewe mlivyo wajanja kutosha kunidanganya Mimi kwa njia hii? Ghadhabu Yangu kali ingewezaje kuondoka kutoka katika dhambi zenu za kuchukiza? Ghadhabu Yangu yenye hasira ingepitaje juu ya matendo yenu maovu? Maovu mnayotenda leo hayawafungulii njia yenu kutokea, bali huhifadhi kuadibu kwa ajili ya kesho yenu; yanachochea kuadibu Kwangu, Mwenyezi, kwenu. Matendo yenu maovu na maneno yenu mabaya yangewezaje kuepuka kuadibu Kwangu? Maombi yenu yangeyafikiaje masikio Yangu? Ningefunguaje njia kwa ajili ya udhalimu wenu? Ningewezaje kuyatupilia mbali matendo yenu maovu ya kunikaidi? Ingewezekanaje Nisizikate ndimi zenu ambazo ni za sumu kama ya nyoka? Hamniombi msaada kwa ajili ya haki yenu, lakini badala yake mnahifadhi ghadhabu Yangu kama matokeo ya udhalimu wenu. Ningewezaje kuwasamehe? Katika macho Yangu, Mwenyezi, maneno na matendo yenu ni machafu. Macho Yangu, Mwenyezi, huona udhalimu wenu kama kuadibu kusikolegea. Kuadibu Kwangu kwa haki na hukumu vingeondokaje kwenu? Kwa sababu mmenitendea hivi, na kunifanya mwenye huzuni na ghadhabu, Ningewaachaje nyinyi muepe kutoka mikono Yangu na muondoke katika siku ambayo Mimi, Yehova, Nawaadibu na kuwalaani wewe? Je, hamjui kwamba maneno yenu yote mabaya na matamko tayari yamefikia masikio Yangu? Je, hamjui kwamba udhalimu wenu tayari umelilaghai vazi Langu takatifu la haki? Je, hamjui kwamba makosa yenu tayari yameichochea hasira Yangu kali? Je, hamjui kwamba kwa muda mrefu mmeniacha Nikitokota, na kwa muda mrefu mmeujaribu uvumilivu Wangu? Je, hamjui kwamba tayari mmeshauharibu mwili Wangu kuwa matambara? Nimevumilia mpaka sasa, kiasi kwamba Natoa hasira Zangu, kutokuwa mvumilivu kwenu tena. Je, hamjui kwamba matendo yenu maovu tayari yamefikia Macho Yangu, na kwamba kilio changu tayari kimefikia masikio ya Baba Yangu? Angewaruhusu vipi mnitendee Mimi jinsi hii? Kuna kazi yoyote Ninayofanya ndani yenu isiyo kwa ajili yenu? Ilhali nani kati yenu amekuwa na upendo zaidi kwa kazi Yangu, Yehova? Ningeweza kutokuwa mwaminifu kwa mapenzi ya Baba Yangu kwa sababu Mimi ni mnyonge, na kwa sababu ya uchungu Nilioupitia? Je, hamwelewi Moyo Wangu? Nasema na ninyi kama Yehova alivyofanya; je, Sijajinyima mengi kwa ajili yenu? Hata ingawa Niko tayari kuvumilia mateso haya yote kwa ajili ya kazi ya Baba Yangu, ni jinsi gani nyinyi mnaweza kuachwa huru kutokana na kuadibu ambako Nawaleteeni kama matokeo ya mateso Yangu? Je, hamjanifurahia kwa wingi sana? Leo, Nimetolewa kwenu na Baba Yangu; hamfahamu kwamba mnafurahia zaidi ya maneno Yangu mengi? Je, hamjui kwamba maisha Yangu yalibadilishwa na maisha yenu na mambo yote mnayofurahia? Je, hamjui kwamba Baba Yangu alitumia maisha Yangu kupigana na Shetani, na kwamba Yeye pia ametoa maisha Yangu kwenu, na kusababisha nyinyi kupokea mara mia zaidi, na kuwaruhusu kuepuka majaribu mengi? Je, hamjui kwamba ni kwa njia ya Kazi Yangu kwamba mmepewa msamaha kutokana na vishawishi vingi, na kuadibu kwingi kukali? Je, hamjui kwamba ni kwa sababu Yangu tu ndio Baba Yangu anawaruhusu kufurahia mpaka sasa? Jinsi gani nyoyo zenu zimebaki ngumu leo, kama kwamba zimekuwa sugu? Maovu mnayoyatenda leo yangeepukaje siku ya ghadhabu itakayofuata kuondoka Kwangu duniani? Ningewezaje kuwaruhusu wale ambao ni wenye mioyo migumu kuepuka hasira ya Yehova?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp