Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 303

10/08/2020

Mwanadamu anashindwa kumpata Mungu sio kwa sababu Mungu ana hisia, au kwa sababu Mungu hataki kupatikana na mwanadamu, bali ni kwa sababu mwanadamu hataki kumpata Mungu, na kwa sababu mwanadamu hana haraka kumtafuta Mungu. Jinsi gani mmoja wa wale ambao kweli wanamtafuta Mungu alaaniwe na Mungu? Ni jinsi gani mwenye akili timamu na dhamiri nzuri anaweza laaniwa na Mungu? Ni vipi yule anayemwabudu kwa kweli na kumhudumia Mungu ataangamizwa na moto wa ghadhabu yake? Ni jinsi gani mwanadamu aliye na furaha ya kumtii Mungu kutupwa nje ya nyumba ya Mungu kwa mateke? Jinsi gani mwanadamu ambaye hawezi kumpenda Mungu vya kutosha aishi katika adhabu ya Mungu? Jinsi gani mwanadamu ambaye ana furaha ya kuacha kila kitu kwa ajili ya Mungu kuachwa bila chochote? Mwanadamu hana nia ya kumfuata Mungu, hana nia ya kutumia mali yake kwa Mungu, hana nia ya kutoa juhudi za milele kwa Mungu, na badala yake anasema kwamba Mungu amepita kiasi, kwamba mengi kuhusu Mungu yanakinzana na dhana za mwanadamu. Na ubinadamu kama huu, hata kama mngekuwa wakarimu katika juhudi zenu bado hamngeweza kupata kibali cha Mungu, bila kutaja kuwa hamumtafuti Mungu. Je, hamjui kwamba ninyi ni bidhaa mbovu za binadamu? Je, hamjui kwamba hakuna ubinadamu ulio mnyenyekevu zaidi kuliko wenu? Je, hamjui “cheo” chenu ni kipi? Wale ambao kweli wanampenda Mungu wanawaita baba wa mbweha, mama wa mbweha, mwanambweha, na mjukuu wa mbweha; nyinyi ni vizazi vya mbweha, watu wa mbweha, na mnapaswa kujua utambulisho wenu na kamwe msiwahi kuusahau. Msidhani kwamba nyinyi ni kiumbe mkubwa zaidi: Nyinyi ni kundi mojawapo la wasio-wanadamu wabaya zaidi miongoni mwa wanadamu. Je, hamjui lolote kuhusu haya? Je, mnajua ni kiasi gani cha hatari Nimechukua ili Nifanye kazi miongoni mwenu? Kama akili yenu haiwezi kurudi kawaida, na dhamiri yenu haiwezi kufanya kazi kwa kawaida, basi kamwe hamtawahi kuwa huru kutokana na jina “mbwa mwitu”, kamwe hamtaitoroka siku ya laana, kamwe hamtaitoroka siku ya adhabu yenu. Mlizaliwa mkiwa duni, kitu kisicho na thamani yoyote. Kwa hivyo nyinyi ni kundi la mbwa mwitu wenye njaa, rundo la uchafu na takataka, na, tofauti na nyinyi, Mimi Sifanyi kazi kwenu ili nipate chochote, lakini kwa sababu ya haja ya kazi. Mkiendelea kuwa waasi kwa njia hii, basi Nitakomesha kazi Yangu, na kamwe sitafanya kazi kwenu tena; badala yake, Nitahamisha Kazi yangu kwa kundi lingine linalonipendeza, na kwa njia hii kuondoka kwenu milele, kwa sababu Mimi sina nia ya kuwaangalia walio katika uadui na Mimi. Hivyo basi, je, mnataka kulingana na Mimi, au katika uadui dhidi Yangu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp