Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Mawazo ya Kidini | Dondoo 293

Kufahamu kazi ya Mungu, athari inayotimizwa kwa mwanadamu, na mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu, hiki ndicho kitu ambacho kila mtu anayemfuata Mungu anapaswa kutimiza. Sasa wanachokosa watu wote ni ufahamu wa kazi ya Mungu. Mwanadamu haelewi wala kufahamu kabisa maana ya vitendo vya Mungu ndani ya mwanadamu, kazi yote ya Mungu, na mapenzi ya Mungu tangu kuumbwa kwa dunia. Huu upungufu hauonekani tu katika ulimwengu mzima wa kidini, lakini zaidi ya hayo kwa waumini wote wa Mungu. Siku itakapofika utakapomtazama Mungu kwa kweli na kutambua hekima ya Mungu; utakapotazama matendo yote ya Mungu na kutambua kile Mungu Alicho na kile Alicho nacho; utakapotazama wingi Wake, hekima, ajabu Yake, na kazi Yake yote kwa mwanadamu, basi hapo ndipo utakuwa umefikia imani ya mafanikio kwa Mungu. Mungu anaposemekana kuwa anajumuisha yote na tele zaidi, ni nini kinachomaanishwa na kujumuisha yote? Na nini kinachomaanishwa na tele? Iwapo huelewi haya, basi huwezi kuchukuliwa kuwa muumini wa Mungu. Mbona Nasema wale walio katika dunia ya kidini hawaamini katika Mungu na ni waovu, walio sawa na ibilisi? Ninaposema ni watenda maovu, ni kwa sababu hawaelewi matakwa ya Mungu, wala kuona hekima Yake. Hakuna wakati ambao Mungu anadhihirisha kazi Yake kwao; ni vipofu, wasioona matendo ya Mungu. Wao ndio walioachwa na Mungu na hawamiliki kabisa utunzaji na ulinzi wa Mungu, sembuse kazi ya Roho Mtakatifu. Wale walio bila kazi ya Mungu ni watenda maovu na humpinga Mungu. Wale Ninaosema wanampinga Mungu ni wale wasiomjua Mungu, wale wanaokiri Mungu na maneno matupu ilhali hawamjui, wale wanaomfuata Mungu lakini hawamtii, na wale wanaofurahia neema ya Mungu lakini hawawezi kumshuhudia. Bila ufahamu wa madhumuni ya kazi ya Mungu na kazi ya Mungu kwa mwanadamu, mwanadamu hawezi kuwa katika ulinganifu na moyo wa Mungu, na hawezi kumshuhudia Mungu. Sababu kwamba mwanadamu humpinga Mungu inatoka, kwa upande mmoja, katika tabia potovu ya mwanadamu, na kwa upande mwingine, kutokana na kutomfahamu Mungu na kutoelewa kanuni za kazi ya Mungu na mapenzi Yake kwa mwanadamu. Vipengele hivi viwili vinaunganishwa katika historia ya upinzani wa mwanadamu kwa Mungu. Wanafunzi katika imani wanampinga Mungu kwa sababu upinzani kama huu uko ndani ya asili yao, ilhali upinzani dhidi ya Mungu wa wale walio na miaka mingi katika imani unatokana na kutomfahamu Mungu, kuongeza kwa tabia yao potovu. Kwa muda kabla ya Mungu kuwa mwili, kipimo cha kama mwanadamu alimpinga Mungu kilikuwa iwapo alihifadhi amri zilizotolewa na Mungu mbinguni. Kwa mfano, katika Enzi ya Sheria, wowote ambao hawakuhifadhi sheria za Yehova walikuwa ndio wale waliompinga Mungu; wowote walioiba sadaka ya Yehova, na wowote waliosimama dhidi ya wale waliofadhiliwa na Yehova walikuwa wale waliompinga Mungu na wale ambao wangepigwa mawe hadi kufa; wowote ambao hawakuheshimu mama na baba zao, na wowote waliompiga ama kumlaani mwingine ni wale ambao hawakufuata sheria. Na wote ambao hawakufuata sheria za Yehova walikuwa wale waliosimama dhidi Yake. Hii haikuwa hivyo tena katika Enzi ya Neema, wakati wale waliosimama dhidi ya Yesu walikuwa wale waliosimama dhidi ya Mungu, na wowote ambao hawakutii maneno yaliyotamka na Yesu ni wale waliosimama dhidi ya Mungu. Katika enzi hii, makusudio ya “upinzani kwa Mungu” yalifafanuliwa zaidi na kuwa halisi. Kwa wakati ambao Mungu bado hakuwa amegeuka mwili, kipimo cha iwapo mwanadamu alimpinga Mungu kilitegemea iwapo mwanadamu alimwabudu na kumheshimu Mungu aliye mbinguni asiyeonekana. Ufafanuzi wa “upinzani kwa Mungu” wakati huo haukuwa halisi, kwani mwanadamu wakati huo hangemwona Mungu wala kujua mfano wa Mungu ama jinsi Alivyofanya kazi na kuongea. Mwanadamu hakuwa na dhana za Mungu na alimwamini Mungu kwa njia isiyo dhahiri, kwani Hakuwa amejitokeza kwa mwanadamu. Kwa hivyo, vile mwanadamu alivyomwamini Mungu katika mawazo yake, Mungu hakumlaumu mwanadamu ama kuulizia mengi kutoka kwa mwanadamu, kwani mwanadamu hangemwona Mungu hata kidogo. Mungu anapopata mwili na kuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu, wote wanamtazama Mungu na kusikia maneno Yake, na wote wanaona vitendo vya Mungu katika mwili. Wakati huo, dhana zote za mwanadamu zinafutwa na kubaki povu tu. Kwa wale wanaomwona Mungu anayejitokeza katika mwili, wote walio na utiifu ndani ya mioyo yao hawalaaniwi, ilhali wanaosimama dhidi Yake kimakusudi watachukuliwa kuwa wapinzani wa Mungu. Wanadamu kama hao ni maadui wa Kristo na ni maadui wanaosimama dhidi ya Mungu kimakusudi. Wale walio na dhana kumhusu Mungu lakini bado wanatii kwa furaha hawatalaaniwa. Mungu anamlaani mwanadamu kulingana na nia yake na vitendo vyake, kamwe sio kwa mawazo na fikira zake. Iwapo mwanadamu angelaaniwa kwa misingi hiyo, basi hakuna mmoja ambaye angeweza kutoroka kutoka katika mikono ya Mungu ya ghadhabu. Wanaosimama makusudi dhidi ya Mungu mwenye mwili wataadhibiwa kwa sababu ya kutotii kwao. Upinzani wao wa makusudi unatokana na dhana zao kumhusu, ambao unasababisha usumbufu wao kwa kazi ya Mungu. Wanadamu kama hao wanapinga na kuiharibu kazi ya Mungu wakijua. Hawana tu dhana za Mungu, lakini wanafanya kile kinachosumbua kazi Yake, na ni kwa sababu hii ndio wanadamu kama hao watahukumiwa. Wale wasioshiriki katika usumbufu wa kazi kimakusudi huwahukumiwa kama wenye dhambi, kwani wanaweza kutii kwa makusudi na kutosababisha vurugu na usumbufu. Wanadamu kama hao hawatahukumiwa. Hata hivyo, wakati wanadamu wamepata uzoefu wa miaka mingi ya kazi ya Mungu, kama bado wanaficha dhana zao za Mungu na kubaki wasioweza kujua kazi ya Mungu mwenye mwili, na licha ya miaka mingi ya uzoefu, wanaendelea kushikilia dhana nyingi za Mungu na hawawezi bado kuja kumjua Mungu, basi hata kama hawasababishi shida yoyote kukiwa na dhana nyingi za Mungu ndani ya mioyo yao, na hata kama dhana kama hizi hazionekani, wanadamu kama hao hawana huduma yoyote kwa kazi ya Mungu. Hawawezi kuhubiri injili wala kumshuhudia Mungu; wanadamu kama hao hawana manufaa na ni wapumbavu. Kwa sababu hawamjui Mungu na hawawezi kuondoa dhana zao za Mungu, wamelaaniwa. Inaweza kusemwa hivi: Ni kawaida kwa wanafunzi wa kidini kuwa na dhana za Mungu ama kutojua chochote kumhusu, lakini sio kawaida kwa wale walioamini kwa miaka mingi na kuwa na uzoefu mwingi wa kazi Yake kushikilia dhana kama hizi, na hata zaidi kwa wanadamu kama hao kutokuwa na ufahamu wa Mungu. Ni kwa sababu ya hali kama hii isiyo ya kawaida ndio wanadamu kama hao wanalaaniwa. Wanadamu wasio wa kawaida kama hao hawana manufaa; ni wale wanaompinga Mungu zaidi na waliofurahia neema ya Mungu bure. Wanadamu wote kama hao wataondolewa mwishoni!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Watu Wote Wasiomjua Mungu Ni Watu Wanaompinga Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp