Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Tabia ya Mungu na Kile Anacho na Alicho | Dondoo 252

21/10/2020

Mungu amekosa usingizi kwa siku nyingi kwa ajili ya kazi ya binadamu. Kutoka vina vya juu hadi vya chini, Amepanda kwenda katika kuzimu ambapo mwanadamu anaishi ili Awe pamoja na mwanadamu, Hajawahi kulalamikia uchakavu walio nao wanadamu, Hajawahi kumlaumu mwanadamu kwa ukaidi wake, lakini Anavumilia mateso makuu kadri Anavyofanya kazi Yake. Inawezekanaje Mungu awe wa kuzimu? Inawezekanaje Aishi maisha yake kuzimu? Lakini kwa ajili ya binadamu wote, ili binadamu wote waweze kupata pumziko mapema zaidi, Amestahimili fedheha na kupitia udhalimu kuja duniani, na kuingia mwenyewe “jahanamu” na “kuzimu,” katika tundu la duma, kumwokoa mwanadamu. Mwanadamu amefuzu vipi kumpinga Mungu? Ana sababu gani tena ya kulalamika kuhusu Mungu? Anawezaje kuwa na ujasiri wa kumwangalia Mungu tena? Mungu wa mbinguni Amekuja katika nchi hii chafu zaidi ya uovu, na Hajawahi kutangaza manung’uniko Yake, au kulalamika kuhusu mwanadamu, lakini badala yake Anakubali kimyakimya maangamizi na ukandamizaji wa mwanadamu. Hajawahi kamwe kuyazuia matakwa ya mwanadamu yasiyokuwa na msingi, Hajawahi kutaka mambo mengi yanayomzidi mwanadamu, na Hajawahi kumwekea mwanadamu matakwa yasiyokuwa na msingi; Anafanya tu kazi zote ambazo mwanadamu anahitajika kufanya bila malalamiko: kufundisha, kutia nuru, kukaripia, usafishaji wa maneno, kukumbusha, kusihi, kufariji, kuhukumu na kufunua. Ni gani kati ya hatua Zake ambazo sio kwa ajili ya maisha ya mwanadamu? Ingawa Ameondoa matarajio na majaliwa ya mwanadamu, ni hatua zipi zilizochukuliwa na Mungu ambazo hazikuwa kwa ajili ya majaliwa ya mwanadamu? Ni ipi kati ya hatua hizo ambayo haijawahi kuwa kwa ajili ya mwanadamu kuendelea kuishi? Ni ipi kati ya hatua hizo haikuwepo kwa ajili ya kumweka mwanadamu huru dhidi ya mateso na minyanyaso ya nguvu za giza ambazo ni nyeusi kama usiku? Ni ipi kati ya hatua hizo si kwa ajili ya mwanadamu? Ni nani awezaye kuuelewa moyo wa Mungu, ambao ni sawa na mama mwenye upendo? Ni nani awezaye kuuelewa moyo wa Mungu wenye shauku? Moyo wa upendo na matarajio ya shauku ya Mungu vimelipwa kwa mioyo ya baridi, na usugu, na macho yanayoonyesha kutojali, kwa makaripio mara kwa mara na matusi ya mwanadamu, kwa maneno yenye kuumiza na dhihaka na udhalilishaji, vimelipwa kwa dhihaka ya mwanadamu, kwa kukanyagwa na kukataliwa kwake, kwa kutokuwa na ufahamu kwake, na kupiga kite, na farakano, na uepukaji, kwa uongo tu, mashambulizi na uchungu. Maneno ya wema ya Mungu yamekutana na nyuso kali na ufidhuli wa maneno makali. Mungu anaweza tu kustahimili, Akiwa Ameinamisha kichwa, Akiwahudumia watu kama ng’ombe aliye radhi. Ni idadi gani ya miezi na jua, ni mara ngapi Amekabiliana na nyota, ni mara ngapi Ameondoka alfajiri na kurudi jioni, na kujipinduapindua na kugaagaa, Akivumilia maumivu makubwa mara elfu moja kuliko maumivu Aliyoyapata Alipokuwa Anaondoka kutoka kwa Baba Yake, Akivumilia mashambulizi na kuvunja kwa mwanadamu, na kumshughulikia na kumpogoa mwanadamu. Unyenyekevu na kufichika kwa Mungu vimelipwa kwa upendeleo wa mwanadamu, kwa mitazamo na vitendo vya mwanadamu visivyokuwa vya haki, na kutojulikana Kwake, ustahimilivu, na uvumilivu vimelipizwa kwa jicho la tamaa la mwanadamu; mwanadamu hujaribu kumkanyaga Mungu hadi afe, bila majuto, na hujaribu kumkanyagia Mungu ardhini. Mtazamo wa mwanadamu katika vile anavyomtendea Mungu ni wa “ujanja adimu,” na Mungu, ambaye Anachokozwa na kutwezwa na mwanadamu, Anakanyagwa na kuwa bapa chini ya miguu ya makumi ya maelfu ya watu wakati mwanadamu mwenyewe anasimama wima, kana kwamba angeweza kuwa mfalme wa kasri, kana kwamba anataka kuchukua mamlaka kamili, kuendesha mahakama akiwa nyuma ya jukwaa, kumfanya Mungu kuwa mwongozaji mwangalifu sana mwenye kufuata kanuni akiwa nyuma ya jukwaa, ambaye haruhusiwi kupigana au kusababisha shida; lazima Mungu ni achukue nafasi ya Mtawala wa Mwisho, ni lazima Awe kibaraka, bila uhuru wote. Matendo ya mwanadamu hayaongeleki, basi ana sifa gani ya kutaka hiki au kile kuhusu Mungu? Ana sifa gani ya kutoa mapendekezo kwa Mungu? Anafaa kwa kiasi gani kumtaka Mungu amhurumie juu ya udhaifu wake? Anafaa kwa kiasi gani kupokea huruma ya Mungu? Anafaa kwa kiasi gani kupokea ukarimu wa Mungu kila mara? Anafaa kwa kiasi gani kupokea msamaha wa Mungu kila mara? Dhamiri yake iko wapi? Aliuvunja moyo wa Mungu muda mrefu uliopita, aliuacha moyo wa Mungu katika vipande kitambo sana. Mungu alikuja miongoni mwa wanadamu Akiwa na nguvu nyingi na mwenye shauku kubwa, Akitegemea kwamba mwanadamu atakuwa mkarimu Kwake, hata kama ni kwa wema kidogo tu. Bado moyo wa Mungu haujafarijiwa na mwanadamu, yote Aliyoyapokea ni mashambulizi na mateso ya kuongezeka haraka; moyo wa mwanadamu ni wenye tamaa sana, tamaa yake ni kubwa sana, hawezi akatosheka, siku zote yeye ni mtundu na jasiri pasi busara, hawezi kamwe kumpatia Mungu uhuru au haki ya kuzungumza, na anamwacha Mungu bila cha kufanya bali kukubali unyanyasaji, na kumruhusu mwanadamu kumtawala anavyotaka.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (9)

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp