Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Mawazo ya Kidini | Dondoo 299

Mpango wa usimamizi wa Mungu umeenea katika miaka elfu sita na umegawanyika katika enzi tatu kutegemea tofauti katika kazi Yake: Enzi ya kwanza ni Enzi ya Sheria ya Agano la Kale; ya pili ni Enzi ya Neema; na ya tatu ni ile ya siku za mwisho—Enzi ya Ufalme. Katika kila enzi utambulisho tofauti huwasilishwa. Hili linafanywa kwa sababu ya utofauti wa kazi, yaani, mahitaji ya kazi. Hatua ya kwanza ya kazi ilifanyiwa nchini Israeli, na hatua ya pili ya kuhitimisha kazi ya ukombozi ilifanyiwa Uyahudi. Kwa kazi ya ukombozi, Yesu alizaliwa kutokana na utungaji mimba wa Roho Mtakatifu na kama Mwana wa pekee. Haya yote yalitokana na mahitaji ya kazi. Katika siku za mwisho, Mungu anadhamiria kupanua kazi Yake katika watu wa Mataifa, na kuwashinda watu wa huko, ili kwamba jina lake liweze kuwa maarufu miongoni mwao. Anadhamiria kumwongoza mwanadamu katika kuzielewa njia zote za uzima wa mwanadamu, pamoja na ukweli na njia ya uzima. Kazi hii yote inafanywa na Roho mmoja. Ijapokuwa Anaweza kufanya hivyo kutoka mitazamo tofautitofauti, asili na kanuni za kazi zinabaki zile zile. Mara tu ukizifuata kanuni na asili ya kazi Waliyoifanya, basi utagundua kuwa ilikuwa kazi ya Roho mmoja. Hata hivyo, wengine wanaweza kusema; Baba ni Baba; Mwana ni Mwana; Roho Mtakatifu ni Roho Mtakatifu, na mwishowe, Watafanywa kitu kimoja. Je, Utawafanyaje kitu kimoja? Baba na Roho Mtakatifu Wawezaje kufanywa kitu kimoja? Ikiwa Walikuwa wawili kiasili, haijalishi Wamewekwa pamoja kwa namna gani, je, Hawataendelea kuwa sehemu mbili? Unaposema kuwa kuwafanya kuwa kitu kimoja, huko si kuunganisha sehemu mbili kutengeneza kitu kamili? Je, Hawakuwa sehemu mbili kabla ya kufanywa kitu kizima? Kila Roho ana kiini bayana, na Roho wawili Hawawezi kufanywa kitu kimoja. Roho si chombo cha kutengenezwa, si kama chombo chochote katika ulimwengu. Kulingana na mitazamo ya wanadamu, Baba ni Roho mmoja, Mwana ni mwingine, na Roho Mtakatifu tena ni mwingine, halafu Roho Hawa huchanganyika sawa na glasi tatu za maji kuunda kitu kimoja kizima. Je, hizo si sehemu tatu zimefanywa kuwa kitu kimoja? Haya ni maelezo ya kimakosa! Je, huku si kumgawa Mungu? Vipi Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu wafanywe kitu kimoja? Je, Wao si sehemu tatu zenye asili tofauti? Aidha kuna wale wasemao, je, si Mungu alitaja wazi kuwa Yesu ni Mwanawe mpendwa? Maneno “Yesu ni Mwana mpendwa wa Mungu, ambaye anapendezwa Naye” bila shaka yalitamkwa na Mungu Mwenyewe. Huyu alikuwa Mungu akijitolea ushuhuda Mwenyewe, ila kutoka katika mtazamo tofauti, ule wa Roho aliye mbinguni akitolea ushuhuda kupata Mwili Kwake. Yesu ni kupata mwili Kwake, si Mwanake mbinguni. Je, unaelewa? Je, maneno ya Yesu, “Baba Yu ndani Yangu Nami ni ndani Yake,” hayaonyeshi kuwa Wao ni Roho mmoja? Na si kwa sababu ya kupata mwili kulikosababisha kutenganishwa Kwao kati ya mbinguni na duniani? Uhalisi ni kwamba Wao ni kitu kimoja; hata iweje, ni Mungu anajitolea ushuhuda Mwenyewe. Kutokana na kubadilika kwa enzi, mahitaji ya kazi, na hatua mbalimbali za mpango Wake wa usimamizi, vilevile jina wamwitalo wanadamu hubadilika. Alipokuja kufanya hatua ya kwanza ya kazi, Angeweza kuitwa tu Yehova, mchungaji wa Waisraeli. Katika hatua ya pili, Mungu mwenye mwili Angeweza kuitwa tu Bwana, na Kristo. Lakini wakati huo, Roho aliye mbinguni alikariri tu kwamba Alikuwa Mwana mpendwa wa Mungu, bila kutaja kuwa Alikuwa Mwana wa pekee wa Mungu. Hili halikufanyika kabisa. Mungu angewezaje kuwa na Mwana wa pekee? Basi, Mungu asingekuwa mwanadamu? Kwa kuwa Alikuwa Mwili, Aliitwa Mwana mpendwa wa Mungu na kutokana na hili, kukazuka uhusiano wa Baba na Mwana. Ni kwa sababu tu ya utengano kati ya mbingu na dunia. Yesu aliomba kutokana na msimamo wa mwili. Kwa sababu Alikuwa Amepata mwili wa mwanadamu wa kawaida, ni kutokana na msimamo wa mwili ndipo Alisema: umbo Langu la nje ni la kiumbe. Kwa sababu Nilijivisha mwili kuja duniani, sasa Niko mbali, mbali sana na mbinguni. Kwa sababu hii, Angeomba tu kwa Baba kutokana na msimamo wa mwili. Huu ulikuwa wajibu Wake, ambao ni sharti Roho wa Mungu aliyepata mwili anapaswa kupewa. Haiwezekani kusema kwamba Hawezi kuwa Mungu kwa sababu tu Anamwomba Baba kutokana na msimamo wa mwili. Ijapokuwa Anaitwa Mwana mpendwa wa Mungu, Yeye bado ni Mungu Mwenyewe, ni vile tu Yeye ni mwili wa Roho, na kiini chake bado ni Roho. Kama wanavyoona wanadamu, wanashangaa ni kwa nini Anaomba ikiwa yeye ni Mungu Mwenyewe. Hii ni kwa sababu Yeye ni Mungu mwenye mwili, Mungu aishiye mwilini, bali si Roho aliye mbinguni. Kama anavyoona mwanadamu, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu wote ni Mungu. Ni kwamba tu wote watatu wanafanywa kuwa kitu kimoja na kudhaniwa kuwa Mungu wa Kweli, na kwa njia hii, uwezo Wake unakuwa mkuu kupindukia. Kuna wanaosema kuwa ni kwa njia hii tu anakuwa Roho aliyezidishwa mara saba. Mwana alipoomba baada ya kuja Kwake, alimwomba Roho. Kwa hakika, alikuwa Akiomba kutokana na msimamo wa kiumbe. Kwa kuwa mwili si kamili, na Hakuwa mkamilifu na pia Alikuwa na udhaifu mwingi Alipokuja katika mwili. Vivyo hivyo Alisumbuka sana Alipoifanya kazi Yake katika mwili. Hii ndiyo maana Alimwomba Mungu Baba mara tatu kabla ya kusulubiwa Kwake, na hata mara nyingi zaidi kabla ya hapo. Aliomba miongoni mwa wanafunzi Wake; Aliomba peke Yake juu mlimani; Aliomba Akiwa Ameabiri dau la uvuvi; Aliomba Akiwa katika umati; Aliomba akiwa anaumega mkate; na kuomba akiwa Anawabariki wengine. Kwa nini Alifanya hivyo? Ilikuwa ni Roho Aliyemwomba; Alikuwa Akimwomba Roho, Alimwomba Mungu aliye mbinguni; kutokana na msimamo wa mwili. Hivyo basi kutoka katika msimamo wa mwanadamu, Yesu alikuwa Mwana katika hatua ile ya kazi. Katika hatua hii hata hivyo, Haombi. Kwa nini? Hii ni kwa sababu Anachokileta ni kazi ya neno, na hukumu na kuadibu kutumia neno. Hana haja ya maombi kwani huduma Yake ni ya kunena. Hajawekwa msalabani, na hashitakiwi na wanadamu kwa wale walio madarakani. Anafanya tu kazi Yake na yote yanakuwa sawa. Wakati Yesu alipoomba, Alikuwa akimwomba Mungu Baba ili ufalme wa mbinguni ushuke, ili mapenzi ya Baba yatimizwe, na ili kazi ifike. Katika hatua hii, ufalme wa mbinguni umeshuka, basi, Ana haja ya kuendelea kuomba? Kazi Yake ni kuihitimisha enzi, na hakuna tena enzi mpya, basi, kuna haja ya kuombea hatua inayofuata? Ninasikitika hakuna haja!

Kuna ukinzani mwingi katika maelezo ya mwanadamu. Kweli, haya ni mawazo ya mwanadamu; bila uchunguzi zaidi, ambayo nyote mngeamini kuwa yako sahihi. Je, hamjui hii dhana ya Mungu kama Utatu Mtakatifu ni mawazo ya mwanadamu tu? Hakuna ufahamu wa mwanadamu ulio mzima na kamili. Mara zote kuna madoa, na mwanadamu ana mawazo mengi mno; hili linaonyesha kuwa kiumbe hawezi kuieleza kazi ya Mungu. Kuna mengi sana katika akili ya mwanadamu, yote yakitokana na mantiki na tafakari, ambayo hukinzana na ukweli. Je, mantiki yako yaweza kuichangua kazi ya Mungu? Je, waweza kupata utambuzi wa kazi yote ya Yehova? Je, ni wewe mwanadamu uwezaye kuona kila kitu, au ni Mungu Mwenyewe awezaye kuona kutoka milele hadi milele? Je, ni wewe mwanadamu uwezaye kuona tangu milele ya zamani sana hadi milele ijayo, au Mungu ndiye Ana uwezo wa kufanya hivyo? Unasema nini? Unafaa vipi kumweleza Mungu? Maelezo yako yamekitwa katika misingi gani? Wewe ni Mungu? Mbingu na dunia, na vyote vilivyomo viliumbwa na Mungu Mwenyewe. Si wewe ulilifanya hili, basi ni kwa nini unatoa maelezo yasiyo sahihi? Sasa, unaendelea kuamini katika utatu mtakatifu? Hufikirii kuwa huu ni mzigo mkubwa kwa njia hii? Itakuwa bora kwako kuamini katika Mungu mmoja, si watatu. Ni bora zaidi kuwa mwepesi, kwani “mzigo wa Bwana ni mwepesi.”

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp