Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake

(Sehemu ya Nne)

Elewa Mwelekeo wa Mungu na Utupilie Mbali Dhana zote Potovu Kumhusu Mungu

Mungu huyu ambaye kwa sasa mnasadiki, mmewahi kufikiria kuhusu Yeye ni Mungu wa aina gani? Anapomwona mtu mwovu akifanya mambo maovu, je Anayachukia? (Anayachukia.) Anapoona makosa ya mtu asiyejua, mwelekeo Wake ni upi? (Huzuni.) Anapowaona watu wakiiba sadaka Yake, mwelekeo Wake ni upi? (Anawachukia.) Haya yote yako wazi, sivyo? Anapoona mtu akiwa mzembe katika kusadiki kwake Mungu, na mtu huyo akikosa kufuatilia ukweli kwa namna yoyote, mwelekeo wa Mungu ni upi? Bado hamjaelewa jambo hili, sivyo? Uzembe ni mwelekeo ambao si dhambi, na humkosei Mungu. Watu husadiki kwamba haupaswi kuchukuliwa kama kosa. Basi mnafikiria mwelekeo wa Mungu ni nini? (Hayuko radhi kujibu swali hili.) Hayuko radhi kulijibu—mwelekeo huu ni upi? Ni kwamba Mungu huwa anawadharau watu hawa, anawabeza watu hawa! Mungu hushughulikia watu hawa kwa kutowathamini. Mtazamo wake ni kuwaweka pembeni, kutojihusisha na kazi yoyote inayowahusu, ikiwemo kuwapa nuru, mwangaza, kuwarudi au kuwafundisha nidhamu. Mtu wa aina hii kwa kweli si wa thamani kwa kazi ya Mungu. Mwelekeo wa Mungu kwa watu wanaozikera tabia Yake, na kuzikosea amri Zake za kiutawala ni upi? Chuki mno kwa kupindukia! Kwa kweli Mungu hupandwa na hasira kali na watu ambao hawaghairi kuhusu kukera tabia Yake! “Hasira Kali” ni hisia tu, hali ya moyo; haiwezi kuwakilisha mwelekeo kamili. Lakini hisia hii, hali hii ya moyo, itasababisha matokeo kwa mtu huyu: Itamjaza Mungu na chukizo la kupindukia! Ni nini matokeo ya kuchukia huku kwa kupindukia? Ni kwamba Mungu atamweka pembeni mtu huyu, na kutomwitikia kwa sasa. Atasubiri watu hawa waweze kushughulikiwa kwenye kipindi cha adhabu. Hali hii inaashiria nini? Mtu huyu angali anayo matokeo? Mungu hakuwahi kunuia kumpa mtu wa aina hii matokeo! Hivyo basi si jambo la kawaida endapo Mungu kwa sasa hamwitikii mtu wa aina hii? (Ndiyo.) Mtu wa aina hii anafaa kujitayarisha vipi sasa? Wanafaa kujitayarisha kukabiliana na zile athari mbaya zilizosababishwa na tabia zao na maovu waliofanya. Huu ndio mwitikio wa Mungu kwa mtu wa aina hii. Hivyo basi Nasema waziwazi kwa mtu wa aina hii: Usishikilie imani za uwongo tena, na usijihusishe katika kufikiria makuu tena. Mungu hatavumilia watu siku zote bila kikomo; Hatastahimili dhambi zao au kutotii kwao bila kukoma. Baadhi ya watu watasema: “Nimeweza pia kuona watu wachache kama hawa. Wanapoomba wanaguswa hasa na Mungu, na wanalia kwa machungu. Kwa kawaida wao pia wanakuwa na furaha sana; wanaonekana kuwa na uwepo wa Mungu, na mwongozo wa Mungu.” Usiseme huo upuzi! Kulia kwa machungu si lazima iwe kwamba umeguswa na Mungu au unao uwepo wa Mungu, acha hata mwongozo wa Mungu. Kama watu watamghadhabisha Mungu, je, bado Mungu atawaongoza? Nikiongea kwa ujumla, wakati Mungu ameamua kumwondoa mtu, kuwaacha watu hao, tayari mtu huyo hana matokeo. Haijalishi ni vipi wanavyohisi kutosheka kujihusu wao wenyewe wakati wanapoomba, na imani kiwango kipi walichonacho katika Mungu mioyoni mwao; tayari hii si muhimu. Kitu cha muhimu ni kwamba Mungu hahitaji aina hii ya imani kwamba Mungu tayari amemsukumia mbali mtu huyu. Namna ya kuwashughulikia baadaye pia si muhimu. Kilicho muhimu ni kwamba katika muda ule ambao mtu huyu atamghadhabisha Mungu, matokeo yao tayari yameanzishwa. Kama Mungu ameamua kutomwokoa mtu wa aina hii, basi ataachwa na kuadhibiwa. Huu ndio mwelekeo wa Mungu.

Ingawa sehemu ya kiini halisi cha Mungu ni upendo, na Anaitoa rehema yake kwa kila mtu, watu hupuuza na kusahau hoja kwamba kiini Chake halisi ni heshima vilevile. Kwamba Anao upendo haimaanishi kwamba watu wanaweza kumkosea Yeye wapendavyo na kwamba Yeye hana hisia zozote, au majibizo yoyote. Kwamba Anayo rehema haimaanishi kwamba Hana kanuni zozote kuhusiana na namna Anavyoshughulikia watu. Mungu yu hai; kwa kweli Yupo. Yeye si kikaragosi kilichofikiriwa au kitu kingine tu. Kwa sababu Yeye yupo, tunafaa kusikiliza kwa makini sauti ya moyo Wake siku zote, kutilia makini mwelekeo Wake, na kuzielewa hisia Zake. Hatufai kutumia kufikiria kwa watu ili kumfafanua Mungu, na hatufai kulazimisha fikira na matamanio ya watu kwa Mungu, kumfanya Mungu kutumia mtindo na fikira za binadamu katika namna Anavyomshughulikia binadamu. Ukifanya hivyo, basi unamghadhabisha Mungu, unaijaribu hasira ya Mungu, na unapinga heshima ya Mungu! Hivyo basi, baada ya kuelewa ukali na uzito wa suala hili, Ninasihi kila mmoja wenu mlio hapa kuwa makini na wenye busara katika vitendo vyenu. Kuwa makini na wenye busara katika kuongea kwenu. Na kuhusiana na namna mnavyoshughulikia Mungu, mnapokuwa makini zaidi na wenye busara zaidi, ndivyo ilivyo bora zaidi! Wakati huelewi mwelekeo wa Mungu ni nini, usizungumze kwa uzembe, usiwe mzembe katika vitendo vyako, na usipachike majina ovyo ovyo. Na hata zaidi, usikimbilie hitimisho kiholela. Badala yake, unafaa kusubiri na kutafuta; hili pia ndilo dhihirisho la kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kama unaweza kutimiza hoja hii kati ya zote, na kumiliki mwelekeo huu kati ya yote, basi Mungu hatakulaumu wewe kwa upumbavu wako, kutojua kwako, na kutotumia kwako akili. Badala yake, kutokana na hofu yako ya kumkosea Mungu, heshima yako kwa nia za Mungu, na mwelekeo wako wa kuwa radhi kumtii Yeye, Mungu atakukumbuka, atakuongoza na kukuangaza wewe, au kustahimili kutokuwa mkomavu kwako na kutojua kwako. Kinyume chake, endapo mwelekeo wako kwake Yeye utakuwa usioheshimu—kuhukumu Mungu kiholela, kukisia kiholela, na kufafanua maana ya Mungu—Mungu atakupa hukumu, nidhamu, au hata adhabu; au Atakupa taarifa. Pengine kauli hii inahusisha matokeo yako. Hivyo basi, Ningali bado nataka kutilia mkazo jambo hili kwa mara nyingine, na kufahamisha kila mmoja aliye humu ndani kuwa makini na mwenye busara katika kila kitu kinachotoka kwa Mungu. Usiongee kwa uzembe, na usiwe mzembe katika matendo yako. Kabla ya kusema chochote, unafaa kufikiria: Je, kufanya hivi kutamghadhabisha Mungu? Kufanya hivi ni kumcha Mungu? Hata katika masuala mepesi, bado unafaa kujaribu kuelewa hakika maswali haya, yafikirie kwa kweli. Kama unaweza kwa kweli kutenda haya kulingana na kanuni hizi kila pahali, katika mambo yote, na kila wakati, hasa kuhusiana na masuala usiyoyaelewa, basi Mungu siku zote atakuongoza wewe, na siku zote atakupa njia ya kufuata. Bila kujali ni nini ambacho watu wanaonyesha, Mungu anaona yote waziwazi, dhahiri, na Atakupa utathmini sahihi na unaofaa kwa maonyesho haya. Baada ya kupitia jaribio la mwisho, Mungu atachukua tabia yako yote na kuijumlisha ili kuasisi matokeo yako. Matokeo haya yatashawishi kila mmoja bila shaka lolote. Kile ambacho Ningependa kuwaambia ni kwamba kila kitendo chenu, kila hatua yenu, na kila fikira yenu vyote vitaamua majaliwa yenu.

Ni Nani Hupanga Matokeo ya Binadamu

Kunalo jambo jingine muhimu zaidi, na hilo ni mwelekeo wenu kwa Mungu. Mwelekeo huu ni muhimu sana! Huamua kama hatimaye mtatembea kuelekea katika maangamizo, au kwenye hatima nzuri na ya kupendeza ambayo Mungu amewatayarishia. Katika Enzi ya Ufalme, Mungu tayari amefanya kazi kwa zaidi ya miaka 20 na kwenye kipindi cha miaka hii 20 pengine mioyo yenu imekuwa na tashwishi kuhusu utendakazi wenu. Hata hivyo, katika moyo wa Mungu, Ameweka rekodi halisi na ya kweli kwa kila mmoja wenu. Kuanzia wakati ule ambao kila mtu anaanza kumfuata Yeye na kusikiliza mahubiri Yake, kuelewa zaidi na zaidi kuhusu ukweli, hadi pale ambapo wanatekeleza wajibu wao—Mungu anayo rekodi ya kila mojawapo ya maonyesho haya. Wakati mtu anapofanya wajibu wake, wakati anapokabiliwa na kila aina ya hali, kila aina ya majaribio, mwelekeo wa mtu huyo ni upi? Wanatenda kazi vipi? Wanahisi vipi kwa Mungu katika mioyo yao? … Mungu ameweka rekodi ya yote haya, rekodi yote kwa hakika. Pengine kutokana na mtazamo wenu, masuala haya yanakanganya. Hata hivyo, kutoka pale ambapo Mungu yupo, yote yako wazi kabisa, na hakuna hata dalili yoyote ya kutokuwa wazi. Hili ni suala linalohusisha matokeo ya kila mmoja, na majaliwa yao na matarajio yao ya siku za baadaye vilevile. Hata zaidi, hapa ndipo ambapo Mungu anatumia jitihada Zake zote alizomakinikia. Hivyo basi Mungu hathubutu kuipuuza hata kidogo, na hatavumilia kutomakinika kokote. Mungu anarekodi haya yote kuhusu wanadamu, anarekodi mambo kuhusu mkondo mzima wa binadamu anayefuata Mungu, kuanzia mwanzo hadi mwisho. Mwelekeo wako kwa Mungu wakati huu utaamua hatima yako. Je, haya si kweli? Kutoka hapo mpaka sasa, mnasadiki kwamba Mungu ni mwenye haki? Vitendo vya Mungu vinafaa? Bado mnayo picha yoyote ya Mungu vichwani mwenu? (La.) Basi mnasema kwamba matokeo ya binadamu ni kwa ajili ya Mungu kuweza kupanga au kwa ajili ya binadamu mwenyewe kupanga? (Ni kwa Mungu kupanga.) Ni nani basi anayeyapanga? (Mungu.) Hamna hakika, sivyo? Ndugu wa makanisa ya Hong Kong, ongeeni—ni nani anayeyapanga? (Binadamu anayapanga mwenyewe.) Mwanadamu anayapanga? Hivyo basi haimaanishi kwamba haina chochote kuhusu Mungu? Ni nani anayetaka kuongea kutoka kwenye makanisa ya Korea? (Mungu huanzisha matokeo ya binadamu kutokana na hatua na vitendo vyake vyote na kutokana pia na njia wanayotembelea.) Hili ni jibu halisi sana. Kunayo hoja hapa ambayo lazima Niwafahamishe nyinyi: Kwenye mkondo wa kazi ya wokovu wa Mungu, Yeye huweka kiwango kwa binadamu. Kiwango hiki ni kwamba binadamu anaweza kutii neno la Mungu, na kutembea kwa njia ya Mungu. Ndicho kiwango kinachotumika kupima matokeo ya binadamu. Kama utafanya mazoezi kwa mujibu wa kiwango hiki cha Mungu, basi unaweza kupata matokeo mazuri; kama hutafanya hivyo, basi huwezi kupokea matokeo mazuri. Basi ni nani unayesema kwamba anayapanga matokeo haya? Si Mungu pekee anayeyapanga, lakini badala yake Mungu na binadamu pamoja. Hiyo ni sahihi? (Ndiyo.) Kwa nini hivyo? Kwa sababu ni Mungu ambaye anataka kujishughulisha na kujihusisha katika kazi ya wokovu wa wanadamu, na kutayarisha hatima nzuri kwa ajili ya binadamu; binadamu ndiye mlengwa wa kazi ya Mungu, na matokeo haya, hatima hii, ndiyo ambayo Mungu humtayarishia binadamu. Kama kusingekuwa na kilengwa cha kazi Yake, basi Mungu asingehitaji kazi hii; kama Mungu asingefanya kazi hii, basi binadamu asingekuwa na fursa ya wokovu. Binadamu ndiye mlengwa wa wokovu, na ingawa binadamu yumo kwenye upande wa kimya katika mchakato huu, ni mwelekeo wa upande huu ambao unaamua kama Mungu atafanikiwa katika kazi Yake ya kuwaokoa wanadamu au la. Kama si mwongozo ambao Mungu anakupa wewe, basi usingejua kiwango Chake, na usingekuwa na lengo lolote. Kama unacho kiwango hiki, lengo hili, ilhali hushirikiani, hulitilii kwenye matendo, hulipii gharama, basi bado hutapokea matokeo haya. Hii ndiyo maana tunasema kwamba matokeo haya hayawezi kutenganishwa na Mungu, na pia hayawezi kutenganishwa na binadamu. Na sasa unaweza kujua ni nani anayepanga matokeo ya binadamu.

Watu Huishia Kumfafanua Mungu Kutokana na Uzoefu Wao

Wakati wa kuwasilisha mada ya kumjua Mungu, mmegundua kitu? Mmegundua kwamba mwelekeo wa sasa wa Mungu umepitia mabadiliko? Je, mwelekeo wa Mungu kwa wanadamu hauwezi kubadilika? Je, siku zote Mungu atavumilia hivi, huku akimpa upendo Wake wote na rehema kwa binadamu bila kikomo? Suala hili pia linahusu kiini halisi cha Mungu. Hebu turejelee swali la yule mtoto wa kiume mbadhirifu kama aitwavyo kutoka awali. Baada ya swali hili kuulizwa, majibu yenu hayakuwa wazi sana. Kwa maneno mengine, bado hamwelewi vizuri nia za Mungu. Punde tu watu wanapojua kwamba Mungu anawapenda wanadamu, wanamfafanua Mungu kama ishara ya upendo: Haijalishi kile wanachofanya watu, haijalishi namna wanavyotenda mambo, haijalishi vipi wanavyomshughulikia Mungu na haijalishi ni vipi wasivyotii, hakuna chochote kinachojalisha kwa sababu Mungu ni upendo na upendo wa Mungu hauna mipaka na haupimiki. Mungu anao upendo, hivyo basi Anaweza kuvumilia watu; Mungu anao upendo, hivyo basi Anaweza kuwa mwenye rehema kwa watu, mwenye rehema kwa kutokomaa kwao, mwenye rehema kwa kutojua kwao, na mwenye rehema kwa kutotii kwao. Hivi ndivyo ilivyo kwa kweli? Kwa baadhi ya watu, wakati wamepitia subira ya Mungu mara moja, au mara chache, watashughulikia suala hili kama mtaji katika uelewa wao wa Mungu, wakisadiki kwamba Mungu atakuwa mara moja na milele mwenye subira kwao, atakuwa mwenye rehema kwao, na kwenye mkondo wa maisha yao watachukua subira ya Mungu na kuichukulia kama kiwango cha ni vipi ambavyo Mungu anawashughulikia. Kunao pia watu ambao, wakati wamepitia uvumilivu wa Mungu mara moja, daima watamfafanua Mungu kuwa uvumilivu, na uvumilivu huu hauna mipaka, hauna masharti, na hata usio na kanuni zozote. Je, kusadiki huku ni sahihi? Kila wakati mambo kuhusu kiini cha Mungu au tabia ya Mungu yanapozungumziwa, mwaonekana mmekanganywa mno. Kuwaona mkiwa hivi kunanifanya Mimi kukasirika kidogo. Mmeusikia ukweli mwingi kuhusiana na kiini halisi cha Mungu; mmeweza pia kusikiliza mada mengi kuhusiana na tabia ya Mungu. Hata hivyo, katika akili zenu masuala haya, na ukweli wa dhana hizi, ni kumbukumbu tu kutokana na nadharia na maneno yaliyoandikwa. Hakuna kati yenu anaweza kupitia kile ambacho tabia ya Mungu inamaanisha katika maisha yenu halisi, wala hamwezi kuona tu tabia ya Mungu ni nini. Hivyo basi, nyote mmechanganyikiwa katika kusadiki kwenu, nyote mnasadiki bila kujua, hadi kufikia kiwango ambacho mnao mwelekeo usiofaa kwa Mungu, kwamba mnamweka pembeni. Mwelekeo kama huu kwa Mungu unawaongoza wapi? Mnaongozwa katika hali ya kutoa hitimisho siku zote kuhusu Mungu. Punde unapopata maarifa kidogo, unahisi umetosheka kweli, unahisi ni kana kwamba umempokea Mungu kwa uzima Wake wote. Baadaye unahitimisha kwamba hivi ndivyo Mungu Alivyo, na humruhusu kuendelea mbele na shughuli Zake kwa furaha zaidi. Na kila Mungu anapofanya jambo jipya, hukubali kwamba Yeye ni Mungu. Siku moja, wakati Mungu atakaposema: “Simpendi binadamu tena; Sitoi rehema kwa binadamu tena; Sina uvumilivu au subira yoyote kwa binadamu tena; Nimejaa chuki na uhasama kupindukia kwa binadamu,” watu watakinzana na aina hii ya taarifa kutoka kwenye ndani ya mioyo yao. Baadhi yao wataweza hata kusema: “Wewe si Mungu wangu tena; Wewe si Mungu ninayetaka kufuata tena. Kama hivi ndivyo Unavyosema, basi Hujafuzu tena kuwa Mungu wangu, na sitaki kuendelea kukufuata Wewe. Kama Hunipi rehema, hunipi upendo, hunipi uvumilivu, basi nami sitakufuata Wewe tena. Kama Utakuwa mvumilivu tu kwangu bila kikomo, utakuwa mwenye subira kwangu mimi, na kuniruhusu mimi kuona kwamba Wewe ni upendo, kwamba Wewe ni subira, kwamba Wewe ni uvumilivu, hapo tu ndipo nitakapoweza kukufuata Wewe, na hapo tu ndipo nitakapoweza kuwa na ujasiri kukufuata mpaka mwisho. Kwa sababu ninapata subira na rehema Yako, kutotii kwangu na dhambi zangu zinaweza kusamehewa bila kikomo, kuondolewa bila kikomo, na ninaweza kutenda dhambi wakati wowote na mahali popote, kutubu na kusamehewa wakati wowote na mahali popote, na kukughadhabisha wakati wowote na mahali popote. Hufai kuwa na fikira au hitimisho Zako binafsi kuhusiana na mimi.” Ingawa huenda usifikirie kuhusu aina hii ya swali kwa namna ya kibinafsi na ya kufahamu kama hiyo, kila unapomchukulia Mungu kuwa zana ya dhambi zako kusamehewa na kifaa cha kutumika cha kupata hatima nzuri, tayari unamweka kwa njia isiyoeleweka Mungu aliye hai na katika hali ya kukupinga wewe, kuwa adui yako. Hivi ndivyo Ninavyoona. Unaweza kuendelea kusema, “Ninasadiki Mungu”; “Ninafuatilia ukweli”; “Ninataka kubadilisha tabia yangu”; “Ninataka kuwa huru dhidi ya ushawishi wa giza”; “Ninataka kumtosheleza Mungu”; “Nataka kumtii Mungu”; “Ninataka kuwa mwaminifu kwa Mungu, na kufanya wajibu wangu vizuri”; na kadhalika. Hata hivyo; haijalishi ni vipi utakavyosema kinasikika kuwa kizuri, haijalishi ni nadharia kiasi kipi unayojua, haijalishi ni vipi nadharia hiyo inavyovutia, ni vipi nadharia hiyo ilivyo na heshima, hoja ya mambo ni kwamba kunao wengi wenu ambao tayari wamejifunza namna ya kutumia taratibu, falsafa, nadharia mlizojifunza katika kuhitimisha mambo kuhusu Mungu, na kumweka yeye katika upinzani na nyinyi wenyewe kwa njia ambayo ni ya kimaumbile kabisa. Ingawa umejifunza barua na kujifunza falsafa, bado hujaingia kwa hakika katika uhalisia wa ukweli, hivyo basi ni vigumu sana kwako kuwa karibu na Mungu, kumjua Mungu, na kumwelewa Mungu. Hali hii inasikitisha!

Niliiona picha hii kwenye video: Akina dada wachache walikuwa wameshikilia kitabu cha Neno Laonekana katika Mwili, na walikuwa wamekishikilia juu sana. Walikuwa wamekishikilia kitabu hiki kikiwa katikati yao, na juu zaidi kuliko vichwa vyao. Ingawa hii ni picha tu, kile kilichoamshwa ndani Yangu si picha. Badala yake, hiyo picha ilinifanya kufikiria kwamba kile ambacho kila mtu hushikilia juu angani kwenye mioyo yao si neno la Mungu, lakini ni kitabu cha neno la Mungu. Hili ni suala la kusikitisha moyo sana. Njia hii ya kutenda mambo si njia kwa kweli ya kumshikilia Mungu kwa heshima. Ni kwa sababu hammwelewi Mungu kiasi cha kwamba swali wazi, swali dogo sana, linawafanya kuja na mawazo yenu binafsi. Wakati Ninapowauliza maswali, wakati Ninapomakinika na ninyi, mnajibu kwa kubahatisha na kwa kutumia kufikiria kwenu binafsi; baadhi yenu hata huchukua sauti ya shaka na kuuliza tena swali hilo kwangu. Hii inathibitisha hata waziwazi kwangu Mimi kwamba yule Mungu mnayemsadiki si Mungu wa kweli. Baada ya kulisoma neno la Mungu kwa miaka mingi sana, mnalitumia neno la Mungu, kutumia kazi ya Mungu, na falsafa nyingi zaidi katika kuhitimisha mengi kuhusu Mungu kwa mara nyingine. Aidha, hamjawahi kujaribu kumwelewa Mungu; hamjawahi kujaribu kupata kuelewa nia za Mungu; hufanyi jaribio la kuelewa mwelekeo wa Mungu kwa binadamu ni nini; au ni vipi ambavyo Mungu anafikiria, kwa nini Anayo huzuni, kwa nini Anayo ghadhabu, kwa nini Yeye husukumia watu mbali, na maswali mengine kama hayo. Na kwa kuongezea hayo, watu wengi zaidi wanasadiki kwamba Mungu siku zote amekuwa kimya kwa sababu Anaangalia tu vitendo vya wanadamu, kwa sababu Hana mwelekeo wowote kwao, wala Hana fikira zozote Zake binafsi. Kundi jingine linasukumiza mbele zaidi suala hili. Watu hawa wanaamini kwamba Mungu hatamki neno kwa sababu Amekubali, Mungu hatamki neno kwa sababu Anasubiria, Mungu hatamki neno kwa sababu Hana mwelekeo, kwa sababu mwelekeo wa Mungu tayari umefafanuliwa kwa kina ndani ya vitabu, tayari umeelezewa kwa uzima wake kwa wanadamu, na hauhitajiki kurudiwa kwa watu mara kwa mara. Ingawa Mungu yuko kimya, bado Anao mwelekeo, anao mtazamo, na anacho kiwango ambacho Anahitaji kutoka kwa watu. Ingawa watu hawajaribu kumwelewa Yeye, na hawajaribu kumtafuta Yeye, mwelekeo Wake uko wazi sana. Fikiria mtu ambaye aliwahi kumfuata Mungu kwa shauku, lakini wakati fulani akaacha kumfuata Yeye na akaondoka. Mtu huyu akitaka kurudi sasa, jambo la kushangaza ni kwamba, hamjui mtazamo wa Mungu utakuwa upi, na mwelekeo wa Mungu utakuwa upi. Hili si jambo ovyo? Kwa hakika, hili ni suala ambalo kwa kiasi fulani ni la juujuu. Kama kweli mngeelewa moyo wa Mungu, mngejua mwelekeo Wake kwa mtu wa aina hii, na msingelitoa jibu la juujuu. Kwa sababu hamjui, Niruhusu kuwafafanulia pale msipoelewa.

Mwelekeo wa Mungu kwa Wale Wanaotoroka Wakati Kazi Yake Inaendelea

Utampata mtu wa aina hii kila pahali: Baada ya kuwa na hakika kuhusu njia ya Mungu, kwa sababu mbalimbali, wanaondoka kimyakimya bila ya neno la kwaheri na kufanya chochote kile ambacho moyo wao unatamani. Huku haya yakiendelea, hatutaingilia kwa nini mtu huyu anaondoka. Kwanza tutaangalia mwelekeo wa Mungu ni upi kwa mtu wa aina hii. Iko wazi sana! Tangu muda ule ambao mtu huyu huondoka, machoni mwa Mungu, kile kipindi cha imani yao kimekwisha. Si mtu huyu aliyekimaliza, bali ni Mungu. Kwamba mtu huyu alimwacha Mungu inamaanisha kwamba tayari amemkataa Mungu, kwamba tayari hamtaki Mungu. Inamaanisha kwamba tayari hakubali wokovu wa Mungu. Kwa sababu mtu huyu hamtaki Mungu, Mungu naye anaweza bado kumtaka? Aidha wakati mtu huyu anao mwelekeo huu, mtazamo huu, na anayo azma ya kumwacha Mungu, tayari ameikera tabia ya Mungu. Hata ingawa hawakujipata wakiwa na hasira na wakalaani Mungu, hata ingawa hawakujihusisha katika uovu wowote au tabia au utovu wa nidhamu, na hata ingawa mtu huyu hafikirii: Kama kutawahi kuwepo na siku nitakapokuwa nimeshiba anasa zangu kwa nje, au nitakapokuwa bado nahitaji kitu kutoka kwa Mungu, nitarudi. Au kama Mungu ataniita, nitarudi. Au wanasema: Kama nitajeruhiwa kwa nje, nikiuona ulimwengu wa nje una giza sana na una maovu sana na sitaki tena kujishirikisha nao, nitarudi kwa Mungu. Hata ingawa mtu huyu amepiga hesabu katika akili zake ni wakati gani anarudi, hata ingawa wanauacha mlango ukiwa wazi wa kurudi kwao, hawatambui kwamba bila kujali ni namna gani wanavyofikiria na namna gani wanavyopanga, hii ni ndoto tu. Kosa lao kubwa zaidi ni kutokuwa wazi kuhusu namna ambavyo Mungu anahisi wakati wanapotaka kuondoka. Kuanzia muda ule ambao mtu huyu anaamua kumwacha Mungu, Mungu amemwacha kabisa; tayari Mungu ameanzisha matokeo katika moyo Wake. Matokeo hayo ni yapi? Kwamba mtu huyu ni mmoja wa buku, na ataangamia pamoja nao. Hivyo basi, watu mara nyingi huona aina hii ya hali: Mtu anamwacha Mungu, lakini hapokei adhabu yoyote. Mungu hufanya kazi kulingana na kanuni Zake binafsi. Watu wanaweza kuona baadhi ya mambo, na baadhi ya mambo yanahitimishwa tu katika moyo wa Mungu, kwa hivyo watu hawawezi kuyaona matokeo. Kile ambacho watu huona si lazima kiwe ndio upande wa ukweli wa mambo; lakini upande ule mwingine, ule upande usiouona—hizi ndizo fikira na hitimisho la kweli kuhusu moyo wa Mungu.

Watu Wanaotoroka Wakati wa Kazi ya Mungu ni Wale Wanaoiacha Njia ya Kweli

Hivyo basi kwa nini Mungu ampe mtu wa aina hii adhabu kali kama hiyo? Kwa nini Mungu anakuwa na hasira kali kwao? Kwanza kabisa tunajua kwamba tabia ya Mungu ni adhama, ni hasira. Yeye si kondoo ili achinjwe na yeyote; na hata zaidi Yeye si kikaragosi ili adhibitiwe na watu vyovyote vile wanavyotaka. Yeye pia si hewa tupu ili kuamrishwa huku na kule na watu. Kama kweli unasadiki kwamba Mungu yupo, unafaa kuwa na moyo unaomcha Mungu, na unafaa kujua kwamba kiini halisi cha Mungu hakifai kughadhabishwa. Ghadhabu hii inaweza kusababishwa na neno; pengine fikira; pengine aina fulani ya tabia bovu; pengine tabia ya upole tabia inayoweza kuruhusiwa kwenye macho na maadili ya binadamu; au pengine inasababishwa na falsafa, nadharia. Hata hivyo, punde unapomghadhabisha Mungu, fursa yako inapotea na siku zako za mwisho zinakuwa zimewasili. Hili ni jambo baya! Kama huelewi kwamba Mungu hawezi kukosewa, basi pengine humchi Mungu, na pengine unamkosea Yeye kila wakati. Kama hujui namna ya kumcha Mungu, basi huwezi kumcha Mungu, na hujui namna ya kujiweka kwenye njia ya kutembelea kwa njia ya Mungu—kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Punde unapokuwa na habari, unaweza kuwa na ufahamu kwamba Mungu hawezi kukosewa, kisha utajua ni nini maana ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

Kutembea katika njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu si lazima kuumaanishe ni kiwango kipi cha ukweli unachojua, ni majaribio mangapi ambayo umepitia, au ni mitihani mingapi ambayo umepitia na kutiwa adabu. Badala yake, kunategemea na kiini halisi cha moyo wako kumhusu Mungu, na mwelekeo wako kwa Mungu pia. Kiini halisi cha watu na mielekeo yao ya kibinafsi—mambo haya ni muhimu sana, muhimu kabisa. Kuhusiana na wale watu ambao wamemkana na kumwacha Mungu, mwelekeo wao wa dharau kwa Mungu na mioyo yao inayodharau ukweli ulikera tabia ya Mungu, hivyo basi kulingana na Mungu hawatawahi kusamehewa. Wamejua kuhusu uwepo wa Mungu, wamekuwa na taarifa kwamba Mungu tayari amewasili, wameweza hata kupitia kazi mpya ya Mungu. Kuondoka kwao si kutokana na kudanganywa, wala si suala kwamba wao wamechanganyikiwa kulihusu. Hata si suala hata kidogo la wao kulazimishwa kuondoka. Lakini kwa nadhari yao, na kwa akili iliyo wazi, wamechagua kumwacha Mungu. Kuondoka kwao si kupotea kwao; si hata kutupwa kwao nje. Hivyo basi, katika macho ya Mungu, wao si kondoo aliyepotea njia kutoka kwenye kondoo wale wengine, sikuambii hata mtoto wa kiume mbadhirifu aliyepotea njia yake. Waliondoka bila hofu ya kuadhibiwa, na hali kama hiyo, mfano kama huo unaikera tabia ya Mungu na ni kutokana na kero hili ambapo Yeye huwapa matokeo yasiyo na matumaini. Je, huoni kwamba matokeo kama haya yanatisha? Hivyo basi kama watu hawamjui Mungu, wanaweza kumkosea Mungu. Hilo ni suala dogo! Kama mtu hatachukulia mwelekeo wa Mungu kwa umakinifu, na bado anasadiki kwamba Mungu angali anatarajia kurudi kwake—kwa sababu wao ni mojawapo wa kondoo wa Mungu waliopotea na kwamba Mungu angali anawasubiria kubadilisha moyo wao—basi mtu huyu hayupo mbali sana na kuweza kuondolewa kwenye siku yake ya adhabu. Mungu hatakataa tu kumkaribisha. Hii ndiyo mara yake ya pili ya kuikera tabia ya Mungu; hivyo basi suala hili ni baya zaidi! Mwelekeo wa mtu huyu usioheshimu vitu vitakatifu tayari umekosea agizo la kiutawala la Mungu. Bado Mungu atawakaribisha? Kanuni za Mungu kuhusiana na suala hili ni: Kama mtu amekuwa na hakika kuhusu njia ya kweli ilhali anaweza bado kwa nadhari yake na kwa akili wazi kumkataa Mungu, na kuwa mbali na Mungu, basi Mungu atazuia kabisa barabara iendayo katika wokovu wake, na hata lango la kuingia kwenye ufalme watafungiwa. Wakati mtu huyu atakapokuja kubisha kwa mara nyingine, Mungu hatamfungulia lango. Mtu huyu atafungiwa milele. Pengine baadhi yenu mmeisoma hadithi hii ya Musa kwenye Biblia. Baada ya Musa kupakwa mafuta na Mungu, viongozi 250 hawakutosheka na Musa kwa sababu ya hatua zake na sababu zingine mbalimbali. Ni nani waliyekataa kumtii? Hakuwa Musa. Walikataa kutii mipango ya Mungu; walikataa kutii kazi ya Mungu katika suala hili. Walisema yafuatayo: “Ninyi mnachukua mengi kwenu, kwa sababu mkusanyiko wote ni mtakatifu, kila mmoja wao, naye Yehova yuko miongoni mwao….” Katika macho yenu, maneno haya ni mazito? Si mazito! Angaa maana ya moja kwa moja ya maneno haya si mazito. Katika mkondo wa kisheria, hawavunji sheria zozote, kwa sababu kwenye sehemu ya juu kabisa si lugha katili, au msamiati, isitoshe, hayana maana yoyote ya kukufuru. Sentensi ya kawaida ndiyo iliyo hapo, hamna cha ziada. Ilhali inakuwaje kwamba maneno haya yanaweza kuanzisha hasira kali kama hiyo kutoka kwa Mungu? Ni kwa sababu hayasemwi kwa watu, mbali kwa Mungu. Mwelekeo na tabia iliyoelezewa na wao ndicho hasa kinachoikera tabia ya Mungu, hasa ile tabia ya Mungu ambayo haiwezi kukosewa. Sote tunajua matokeo yao hatimaye yalikuwa yapi. Kuhusiana na wale waliomwacha Mungu, mtazamo wao ni upi? Mwelekeo wao ni upi? Na ni kwa nini mtazamo na mwelekeo wao unasababisha Mungu kuwashughulikia kwa njia hiyo? Sababu ni kwamba wanajua waziwazi Yeye ni Mungu ilhali bado wanachagua kumsaliti Yeye. Na ndiyo maana wanaondolewa kabisa fursa yao ya wokovu. Kama vile Biblia inavyosema: “Kwa sababu tukitenda dhambi makusudi baada ya sisi kupokea maarifa ya ukweli, hakuna tena dhabihu ya dhambi.” Je, mmelielewa suala hili sasa?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp