Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake

(Sehemu ya Pili)

Tembea katika Njia ya Mungu: Mche Mungu na Kuepuka Maovu

Kunao msemo ambao mnafaa kutilia maanani. Ninasadiki msemo huu ni muhimu sana, kwa sababu kwangu Mimi unakuja akilini mara nyingi kila siku. Kwa nini hivyo? Kwa sababu kila wakati Ninapokumbana na mtu, kila wakati Ninaposikia hadithi ya mtu, kila wakati Ninaposikia kile alichopitia mtu au ushuhuda wake wa kusadiki Mungu, siku zote Ninatumia msemo huu kuweza kupima kama mtu huyu binafsi ni mtu wa aina ambayo Mungu anataka au la, mtu wa aina ambayo Mungu anapenda. Hivyo msemo huu ni upi, basi? Sasa nyinyi nyote mnasubiri kwa hamu. Nitakapoufichua msemo huu, pengine mtakasirika kwa sababu wapo baadhi yenu ambao mmekuwa mkijifanya kuwa mnakubaliana nao kwa miaka mingi. Lakini Kwangu Mimi, Sijawahi kujifanya kuwa nakubaliana nao. Msemo huu umo moyoni Mwangu. Hivyo basi msemo huu ni upi? Msemo ni “tembea katika njia ya Mungu: mche Mungu na kuepuka maovu.” Je, huoni kwamba kauli hii ni rahisi kupindukia? Ilhali ingawa msemo huu unaweza kuwa rahisi, mtu ambaye anao uelewa wa ndani na wa kweli wa msemo huu atahisi kwamba ni wenye uzito mkubwa; kwamba unao thamani nyingi ya kutenda; kwamba ni lugha ya uzima iliyo na uhalisia wa ukweli; ambayo ni lengo la maishani katika kulenga wale wanaotafuta kutosheleza Mungu; na hiyo ni njia ya maisha marefu itakayofuatwa na mtu yeyote anayejali nia za Mungu. Hivyo basi mnafikiria nini: Je, msemo huu ni ukweli? Je, unao aina hii ya umuhimu? Pengine wapo baadhi ya watu wanaofikiria kuhusu msemo huu, wakijaribu kuuelewa, na wapo baadhi ambao bado wanautilia shaka. Je, msemo huu ni muhimu sana? Je, ni muhimu sana? Unahitajika sana na unastahili kutiliwa mkazo? Pengine wapo baadhi ya watu ambao hawapendi sana msemo huu kwa sababu wanafikiria kwamba kuchukua njia ya Mungu na kuitiririsha ndani ya msemo huu mmoja ni urahisishaji wa kupindukia. Kuyachukua yale yote ambayo Mungu alisema na kuyafanya yawe msemo mmoja—je, hivi si kumfanya Mungu kuwa yule asiyekuwa na umuhimu sana? Hivi ndivyo ilivyo? Inaweza kuwa kwamba wengi wenu nyinyi hamwelewi kabisa maana kuu ya maneno haya. Ingawa mmeyanakili na kuyatilia maanani, hamnuii kuuweka msemo huu katika mioyo yenu; mnaunakili tu, na kuudurusu tu, na kuufikiri katika muda wenu wa ziada. Wapo baadhi ya watu ambao hata hawatashughulika kuutia kwenye kumbukumbu msemo huu, sikuambii hata kujaribu kuutumia vizuri. Lakini kwa nini Nikauzungumzia msemo huu? Licha ya mtazamo wenu, au kile mtakachofikiria, lazima Nizungumzie msemo huu kwa sababu unafaa ajabu namna ambavyo Mungu huasisi matokeo ya binadamu. Bila kujali kama uelewa wenu wa sasa wa msemo huu upo, namna mnavyouchukulia, bado Nitawaeleza: Kama mtu anaweza kuutenda msemo huu kwa njia bora na kutimiza kiwango cha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, basi atahakikishiwa kuishi, kisha atahakikishiwa kuwa mtu mwenye matokeo mazuri. Kama huwezi kutimiza kiwango kilichowekwa wazi katika msemo huu, basi inaweza kusemekana kwamba matokeo yako hayajulikani. Hivyo basi Ninaongea kwenu kuhusu msemo huu kwa matayarisho yenu ya kiakili, na ili mjue ni kiwango aina gani ambacho Mungu anatumia kuwapima. Kama Nilivyozungumza tu muda mfupi uliopita, msemo huu unafaa pakubwa kwa wokovu wa Mungu kwa binadamu na namna ambavyo Aliyaasisi matokeo ya binadamu. Uhusiano huu unapatikana wapi? Mngependa kwa kweli kujua, hivyo basi tutauzungumzia leo.

Mungu Hutumia Majaribio Tofauti ili Kupima Kama Watu Humcha Mungu na Kujiepusha na Maovu

Katika kila enzi, Mungu huwapa binadamu baadhi ya maneno Anapofanya kazi ulimwenguni, huku akimwambia mwanadamu kuhusu baadhi ya ukweli. Ukweli huu unahudumu kama njia ambayo binadamu anafaa kuitii, njia ya kutembelewa na binadamu, njia ambayo humwezesha binadamu kumcha Mungu na kujiepusha na uovu, na njia ambayo watu wanafaa kuweka katika vitendo na kuitii katika maisha yao na kwenye mkondo wa safari zao za maisha. Ni kwa sababu hizi ambapo Mungu anampa binadamu maneno haya. Binadamu anafaa kuyatii maneno haya yanayotoka kwa Mungu, na kuyatii ni kupokea uzima. Kama mtu hataweza kuyatii, na hayatii kwenye matendo, na haishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu katika maisha yake, basi mtu huyo hautilii ukweli katika matendo. Na kama hawatilii ukweli katika matendo, basi hawamchi Mungu na hawaepuki uovu, wala hawawezi kumtosheleza Mungu. Kama mtu hawezi kumtosheleza Mungu, basi hawezi kupokea sifa ya Mungu; mtu wa aina hii hana matokeo. Hivyo basi ni vipi katika mkondo wa kazi ya Mungu ndipo Anapoasisi matokeo ya mtu? Ni mbinu gani anayoitumia Mungu kuasisi matokeo ya binadamu? Pengine nyinyi hamlielewi suala hili sasa hivi, lakini Nitakapowaambia mchakato jambo hili litakuwa wazi kabisa. Hii ni kwa sababu watu wengi tayari wamelipitia suala hili wenyewe.

Katika mkondo wa kazi ya Mungu, kuanzia mwanzo hadi sasa, Mungu Amepanga majaribio kwa kila mtu—au mnaweza kusema, kila mtu anayemfuata Yeye—na majaribio haya yanakuja kwa ukubwa tofauti. Wapo wale ambao wamepitia jaribio la kukataliwa na familia zao; wapo wale ambao wamepitia jaribio la mazingira mabovu; wapo wale ambao wamepitia majaribio ya kukamatwa na kuteswa; wapo wale ambao wamepitia majaribio ya kukumbwa na chaguo; na wapo wale ambao wamekumbwa na majaribio ya pesa na hadhi. Nikizungumza kwa ujumla, kila moja wenu amekabiliwa na aina zote za majaribio. Kwa nini Mungu anafanya kazi hivyo? Kwa nini Mungu Anamtenda hivi kila mtu? Ni matokeo aina gani Anayotaka kuyaona? Hii ndiyo hoja muhimu kuhusu kile Ninachotaka kuwaambia: Mungu anataka kuona kama mtu huyu ni yule anayemcha Mungu na kujiepusha na uovu. Maana ya haya ni kwamba wakati Mungu anakupa jaribio, na kukufanya kukabiliwa na baadhi ya hali, Anataka kukupima na kujua kama wewe ndiye yule mtu anayemcha Mungu, mtu huyo anayejiepusha na uovu au la. Kama mtu amekumbwa na wajibu wa kutunza sadaka, na anakutana na sadaka ya Mungu, basi unadhani kwamba hiki ni kitu ambacho Mungu amepanga? Bila shaka! Kila kitu unachokumbana nacho ni kitu ambacho Mungu amepanga. Unapokumbwa na suala hili, Mungu atakuangalia kwa siri, namna ulivyochagua, namna unavyotenda, na kile unachofikiria. Matokeo yake ya mwisho ndiyo ambayo Mungu anayajali zaidi, sababu ni matokeo ambayo yatamruhusu Yeye kupima kama umetimiza kiwango cha Mungu katika jaribio hilo au la. Hata hivyo, wakati watu wanapokumbwa na baadhi ya masuala haya, mara nyingi hawafikirii kuhusu ni kwa nini wanakumbwa na mambo hayo, au kile kiwango ambacho kinahitajika na Mungu. Hawafikirii kuhusu kile Mungu anachotaka kutoka kwao, kile Anachotaka kupata kutoka kwao. Wakati wanapokumbwa na suala hili, mtu wa aina hii anafikiria tu: “Hili ni jambo ambalo nimekumbwa nalo; lazima niwe makinifu, wala si mzembe! Haijalishi ni nini, hii ni sadaka ya Mungu na siwezi kuigusa.” Mtu huyo anasadiki kwamba anaweza kutimiza jukumu lake kupitia kufikiria huko sahili. Je, Mungu ataweza kutosheka na matokeo ya jaribio hili? Au Hatatosheka? Mnaweza kuzungumzia suala hili. (Kama mtu anamcha Mungu katika moyo wake, kisha anapokumbwa na wajibu unaomruhusu kukutana na sadaka ya Mungu, anaweza kufikiria namna ilivyo rahisi kukosea tabia ya Mungu, ili wawe na hakika ya kuendelea kwa tahadhari.) Mwitikio wako u katika njia sahihi, lakini bado haujafika. Kutembea katika njia ya Mungu hakuhusu kuangalia sheria juujuu. Badala yake, kunamaanisha kwamba unapokabiliwa na suala, kwanza kabisa, unaliangalia kama ni hali ambayo imepangwa na Mungu, wajibu uliopewa wewe na Yeye, au kitu ambacho Amekuaminia wewe, na kwamba unapokabiliana na suala hili, unapaswa kuliona kama jaribio kutoka kwa Mungu. Wakati unapokabiliwa na suala hili, lazima uwe na kiwango, lazima ufikirie kwamba suala hilo limetoka kwa Mungu. Lazima ufikirie ni vipi ambavyo utashughulikia suala hili kiasi cha kwamba unaweza kutimiza wajibu wako, na kuwa mwaminifu kwa Mungu; namna ya kulifanya bila ya kumghadhabisha Mungu; au kukosea tabia Yake. Tumetoka tu kuzungumzia kutunza sadaka. Swala hili linahusu sadaka, na linahusisha pia wajibu wako, jukumu lako. Unahitajika kuwajibikia jukumu hili. Ilhali unapokabiliwa na suala hili, kunalo jaribio lolote? Lipo! Jaribio hilo linatoka wapi? Jaribio hilo linatoka kwa Shetani, na linatoka pia kwa tabia potovu na ya uovu ya binadamu. Kwa sababu kunalo jaribio, hili linahusisha kuwa shahidi; kuwa shahidi ni jukumu na wajibu wako pia. Baadhi ya watu husema: “Hili ni suala dogo; kwa kweli linahitajika kulifanya suala hili dogo kuwa kubwa hivyo?” Ndiyo pana haja! Kwa sababu ili kutembea katika njia ya Mungu, hatuwezi kuwachilia chochote kinachotuhusu sisi wenyewe, au kinachofanyika karibu nasi, hata yale mambo madogo madogo. Haijalishi kama tunafikiria tunafaa kumakinika au la, mradi tu suala lolote linatukabili hatufai kuliacha. Lote linafaa kuonekana kama jaribio la Mungu kwetu. Mwelekeo aina hii uko vipi? Kama unao mwelekeo aina hii, basi unathibitisha hoja moja: Moyo wako unamcha Mungu, na moyo wako uko radhi kujiepusha na maovu. Kama unalo tamanio hili la kumtosheleza Mungu, basi kile unachotia katika matendo hakiko mbali na kiwango cha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

Kunao mara nyingi wale wanaosadiki kwamba masuala ambayo hayatiliwi maanani na watu, masuala ambayo kwa kawaida hayatajwi—haya ni mambo madogo tu, na hayana chochote kuhusiana na kutia ukweli katika matendo. Wakati watu hawa wanakabiliwa na suala kama hilo, hawalifikirii sana na wanaliachilia tu. Lakini ukweli wa mambo ni kwamba, suala hili ni funzo ambalo unafaa kulidadisi, funzo kuhusu namna ya kumcha Mungu, namna ya kujiepusha na maovu. Zaidi, kile unachofaa kujali hata zaidi ni kujua kile Mungu anachofanya wakati suala hili linapoibuka kukabiliana na wewe. Mungu yuko kando yako, anaangalia kila mojawapo ya maneno na vitendo vyako, anaangalia hatua zako, mabadiliko ya akili zako—hii ni kazi ya Mungu. Baadhi ya watu husema: “Basi kwa nini siihisi?” Huihisi kwa sababu namna ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu haijawa ndiyo njia muhimu zaidi kwako kushughulikiwa. Hivyo basi, huwezi kuhisi kazi ngumu ya Mungu katika binadamu, inayojionyesha kulingana na fikira tofauti na vitendo tofauti vya watu. Wewe u makini! Suala kubwa ni lipi? Swala dogo ni lipi? Masuala yote yanayohusu kutembea katika njia ya Mungu hayagawanywi kwa masuala makubwa au madogo. Mnaweza kulikubali hilo? (Tunaweza kulikubali.) Kuhusiana na masuala ya kila siku, kunayo yale ambayo watu wanayaona kuwa makubwa sana na muhimu, na mengine yanaonekana kuwa mambo madogo madogo tu. Mara nyingi watu huyaona masuala haya makubwa kuwa ndiyo muhimu zaidi, na wanayachukulia kwamba yametumwa na Mungu. Hata hivyo, kwenye mkondo wa masuala haya makubwa kujitokeza, kutokana na kimo finyu cha binadamu, na kutokana na kiwango cha binadamu kisichotosha, mara nyingi binadamu haendani sawa na nia za Mungu, hawezi kupata ufunuo wowote, na hawezi kufaidi maarifa yoyote halisi yenye thamani. Kuhusu masuala madogo, haya yanapuuzwa tu na binadamu, kuachwa kuponyoka kidogokidogo. Hivyo basi, wamepoteza fursa nyingi sana za kuchunguzwa mbele ya Mungu, kujaribiwa na Yeye. Je unafaa kuwapuuza watu, masuala na hali hizi siku zote ambazo Mungu anakupangilia wewe, hii itamaanisha nini? Inamaanisha kwamba kila siku, hata kila wakati, siku zote unakana ukamilifu wa Mungu kwako, na uongozi wa Mungu. Kila Mungu anapopanga hali hizi kwako wewe, Yeye anakuangalia kwa siri, Anauangalia moyo wako, Anaziangalia fikira na hali zako, Anaangalia namna unavyofikiria wewe, Anaangalia namna unavyochukua hatua. Kama wewe ni mtu asiyejali—mtu ambaye hajawahi kujali kuhusu njia ya Mungu, neno la Mungu, au ukweli—basi hutajali, hutatilia maanani kile ambacho Mungu anataka kukamilisha, na yale ambayo Mungu anakuhitaji wewe kufanya wakati Anapopanga hali hizi kwako wewe. Hutajua pia namna ambavyo masuala haya ya kila siku yanavyohusiana na ukweli au nia za Mungu. Baada ya kukabiliana na hali nyingi kama hizi na majaribio mengi kama haya, huku naye Mungu haoni mafanikio yoyote kutokana na wewe, ataweza kuendelea vipi? Baada ya kukabiliwa na majaribio mara kwa mara, humkuzi Mungu katika moyo wako, na hushughulikii zile hali ambazo Mungu anakupangia wewe kama zilivyo—kama majaribio ya Mungu au mitihani ya Mungu. Badala yake unakataa fursa ambazo Mungu amekupa wewe moja baada ya nyingine, na unaziacha kutokomea mara kwa mara. Je huu si kutotii kwa kiwango cha juu na binadamu? (Naam, ni kutotii.) Je, Mungu atahuzunika kwa sababu ya haya? (Naam Atahuzunika.) Mungu hatahuzunika! Mkinisikia Nikiongea hivi mnashtuka kwa mara nyingine tena. Kwani umesahau, ilisemekana hapo awali kwamba Mungu huhuzunika siku zote? Mungu hatahuzunika? Ni lini basi Mungu atahuzunika? Usijali, Mungu hatahuzunika na hali hii. Basi mwelekeo wa Mungu kwa aina hii ya tabia iliyoelezwa kwa muhtasari hapo juu ni upi? Wakati watu wanapokataa majaribio, mitihani, ambayo Mungu anawapa, wakati wanapoikwepa, kunao mwelekeo mmoja tu ambao Mungu anao kwa watu kama hawa. Mwelekeo huu ni upi? Mungu husukumia mbali aina hii ya watu kutoka kina cha moyo Wake. Kunazo safu mbili za maana ya kauli “sukumia mbali”. Ninawezaje kuzielezea? Ndani kabisa ya moyo, kauli hii inao mkazo wa kuchukiza, wa chuki. Na je, safu ya pili ya maana? Sasa hiyo ndiyo sehemu inayoashiria kukata tamaa dhidi ya kitu. Nyote mnajua “kukata tamaa” kunamaanisha nini, ni kweli? Kwa ufupi, kusukumia mbali kunamaanisha uamuzi na mwelekeo wa mwisho wa Mungu kwa watu wanaokuwa na mwenendo huu. Ni chuki ya kupindukia dhidi yao, maudhi, na hivyo basi uamuzi wa kuwaacha. Huu ndio uamuzi wa mwisho wa Mungu kwa mtu ambaye hajawahi kutembea katika njia ya Mungu, ambaye hajawahi kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Je, nyote mnaweza kuona sasa umuhimu wa msemo huu Niliouzungumzia?

Sasa mnaelewa mbinu ambayo Mungu hutumia kuasisi matokeo kwa binadamu? (Kupanga hali tofauti kila siku.) Kupangilia hali tofauti—hivi ndivyo watu wanavyoweza kuhisi na kugusa. Basi nia ya Mungu kwa haya yote ni nini? Nia ni kwamba Mungu anataka kumpa kila mmoja wetu majaribio katika njia tofauti, katika nyakati tofauti, na katika sehemu tofauti. Ni dhana zipi za binadamu zinazopimwa katika jaribio? Haijalishi kama wewe ni mtu wa aina ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu katika kila suala unalokabiliwa nalo, unalosikia kuhusu, unaloliona, na unalolipitia wewe binafsi au la. Kila mmoja atakabiliwa na aina ya jaribio, kwa sababu Mungu ni mwenye haki kwa watu wote. Baadhi ya watu husema: “Nimesadiki Mungu kwa miaka mingi; inakuaje kwamba sijawahi kabiliwa na jaribio?” Unahisi hujakabiliwa na jaribio kwa sababu kila wakati Mungu amepanga hali kwako wewe, hujazichukulia hali hizo kwa umakinifu, na hujataka kutembea kwa njia ya Mungu. Hivyo basi huna kamwe hisia zozote za majaribio ya Mungu. Baadhi ya watu husema: “Nimekabiliwa na majaribio machache, lakini sijui njia bora ya kufanya mazoezi. Hata ingawa nilitenda, bado sijajua kama nilisimama imara wakati huo wa majaribio.” Watu walio na aina hii ya hali bila shaka hawamo katika kundi la walio wachache. Hivyo basi ni nini kiwango ambacho Mungu hupimia watu? Ni vile tu Nilivyosema muda mfupi uliopita: Kila kitu unachofanya, kila kitu unachofikiria, na kila kitu unachoelezea—ni kumcha Mungu na kujiepusha na uovu? Hivi ndivyo inavyobainika kama wewe ni mtu unayemcha Mungu na kujiepusha na maovu au la. Hii ni dhana rahisi? Ni rahisi mno kusema, lakini ni rahisi pia kutia katika matendo? (Si rahisi mno.) Kwa nini si rahisi mno? (Kwa sababu watu hawamjui Mungu, hawajui namna ambavyo Mungu humfanya binadamu kuwa mtimilifu, na hivyo basi wanapokabiliwa na masuala hawajui namna ya kutafuta ukweli ili kutatua tatizo lao; watu lazima wapitie majaribio mbalimbali, usafishaji, kuadibu, na hukumu kabla ya kuwa na uhalisia wa kumcha Mungu.) Mnasema hivyo, lakini kulingana na vile mnavyojua, kumcha Mungu na kujiepusha na maovu kunaonekana rahisi kufanywa kwa sasa. Kwa nini Nasema hivi? Kwa sababu mmesikiliza ibada nyingi, na umepokea kiwango kingi cha kunyunyiziwa kwa uhalisia wa ukweli. Hii imewaruhusu kuelewa namna ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu kwa mujibu wa nadharia na kufikiria. Kuhusiana na matendo yenu ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, haya yote yamekuwa yenye manufaa na kuwafanya kuhisi kwamba kitu kama hicho kinaweza kutimizika. Basi ni kwa nini katika uhalisia wa mambo watu hawajawahi kukitimiza? Hii ni kwa sababu kiini halisi cha asili ya binadamu hakimchi Mungu na kinapenda maovu. Hiyo ndiyo sababu halisi.

Kutomcha Mungu na Kutojiepusha na Maovu ni Kumpinga Mungu

Hebu tuanze kuangazia ni wapi ambapo msemo huu “kumcha Mungu na kujiepusha na maovu” ulitokea. (Kitabu cha Ayubu.) Sasa kwa vile mmetaja Ayubu, hebu tumzungumzie. Katika nyakati za Ayubu, Mungu alikuwa akishughulikia kushinda na wokovu wa binadamu? Alikuwa hafanyi hivyo, kweli? Na kuhusiana na Ayubu, ni maarifa kiwango gani alikuwa nayo kumhusu Mungu wakati huo? (Si maarifa mengi.) Na maarifa hayo ya Mungu yanalingana vipi na maarifa mliyo nayo sasa? Inakuwaje kwamba hamthubutu kujibu hili? Maarifa ya Ayubu yalikuwa mengi zaidi au machache kuliko maarifa mliyo nayo sasa? (Machache.) Hili ni swali rahisi sana kujibu. Machache! Hapo nina hakika! Sasa hivi mnaangaliana uso kwa uso na Mungu, uso kwa macho na neno la Mungu. Maarifa yenu ya Mungu ni mengi zaidi kuliko yale ya Ayubu. Kwa nini Naleta suala hili? Kwa nini Ninaongea hivi? Ningependa kuwaelezea hoja moja, lakini kabla Sijafanya hivyo, Ningependa kuwauliza swali: Ayubu alijua machache sana kumhusu Mungu, ilhali angeweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Hivyo basi kwa nini watu siku hizi wanashindwa kufanya hivyo? (Upotoshaji mkubwa.) Upotoshaji mkubwa—hicho ndicho kiini cha swali, lakini Sitawahi kulitazama hivyo. Mara nyingi mnachukua falsafa na barua ambazo mnazungumzia mara kwa mara, kama vile “upotoshaji mkuu,” “kuasi dhidi ya Mungu,” “kutotii Mungu,” “kutotii,” “kutopenda ukweli,” na mnatumia vidahizo kama hivi kuelezea kiini halisi cha kila swali. Hii ni njia isiyofaa ya kufanya mazoezi. Kutumia jibu moja kuelezea maswali yaliyo na asili tofauti mara moja huibua shaka ya kuukufuru ukweli na Mungu. Sipendi kusikia aina hii ya jibu. Hebu fikiria! Hakuna yeyote kati yenu amefikiria kuhusu suala hili, lakini kila siku Mimi Ninaliona, na kila siku Mimi Ninalihisi. Hivyo basi, mnafanya, na Mimi Ninatazama. Wakati mnapolifanya, hamwezi kuhisi kiini halisi cha suala hili. Lakini wakati Ninapoliona, Ninaweza kuona kiini halisi chake, na Ninaweza kuhisi kiini chake halisi vilevile. Hivyo basi kiini hiki ni nini basi? Kwa nini watu siku hizi hawamchi Mungu na hawaambai maovu? Majibu yenu yako mbali na kuweza kueleza kiini halisi cha swali hili, na haziwezi kutatua kiini halisi cha swali hili. Hiyo ni kwa sababu kunacho chanzo hapa ambacho nyinyi hamna habari kukihusu. Chanzo hiki ni kipi? Ninajua mnataka kusikia kukihusu, hivyo basi Nitawaambia kuhusu chanzo cha swali hili.

Hapo mwanzo kabisa wa kazi ya Mungu, Alichukulia vipi binadamu? Mungu alimwokoa binadamu; Alimchukulia binadamu kama mmoja wa familia Yake, kama mlengwa wa kazi Yake, kama kile ambacho Alitaka kukishinda, kuokoa, na kile ambacho Alitaka kufanya kuwa kitimilifu. Huu ndio uliokuwa mwelekeo wa Mungu kwa binadamu mwanzoni mwa kazi Yake. Lakini mwelekeo wa binadamu kwa Mungu wakati huo ulikuwa upi? Mungu alikuwa haeleweki kwa binadamu na binadamu alimchukulia Mungu kuwa mgeni. Inaweza kusemwa kwamba mwelekeo wa binadamu kwa Mungu ulikuwa si sahihi, na binadamu hakuwa na uwazi mzuri wa namna ya kumchukua Mungu. Hivyo basi Alimshughulikia alivyopenda yeye, na akafanya kile alichopenda yeye. Je, binadamu alikuwa na mtazamo kuhusu Mungu? Hapo mwanzoni, binadamu hakuwa na mtazamo wowote kuhusu Mungu. Mtazamo wa binadamu kama ulivyojulikana, ulikuwa tu baadhi ya dhana na fikira kumhusu Mungu. Kile ambacho kiliingiliana na dhana za watu kilikubalika; kile ambacho hakikuingiliana kiliitikiwa juujuu, lakini katika mioyo yao watu waligongana pakubwa nacho na wakakipinga. Huu ndio uliokuwa uhusiano wa binadamu na Mungu hapo mwanzoni: Mungu alimwona binadamu kama mwanachama wa familia, ilhali binadamu alimchukulia Mungu kama mgeni. Lakini baada ya kipindi cha kazi ya Mungu, binadamu alielewa hatimaye kile ambacho Mungu alikuwa akijaribu kutimiza. Watu hatimaye walijua kwamba Mungu ndiye aliyekuwa Mungu wa kweli, na hatimaye wakajua kile ambacho binadamu angepokea kutoka kwa Mungu. Binadamu alimchukulia Mungu wakati huu kuwa nini? Binadamu alichukulia Mungu kuwa tegemeo kuu, akitumai kupokea neema, kupokea baraka, kupokea ahadi. Naye Mungu alimchukulia binadamu wakati huu kuwa nini? Mungu alimchukulia binadamu kuwa mlengwa wa ushindi Wake. Mungu alitaka kuyatumia maneno ili kumhukumu binadamu, kumjaribu binadamu, kumpa majaribio binadamu. Lakini kwa wanadamu wakati huu hasa, Mungu alikuwa kifaa ambacho angetumia kutimiza shabaha zake binafsi. Watu waliona kwamba ukweli uliotolewa na Mungu ungeweza kushinda na kuwaokoa, na kwamba walikuwa na fursa ya kupokea vitu walivyotaka kutoka kwa Mungu, hatima ambayo walikuwa wakitaka. Kwa sababu ya haya, chembechembe ya uaminifu kajitunga katika mioyo yao, na walikuwa radhi kumfuata Mungu huyu. Muda ukapita na watu wakawa na maarifa fulani ya juujuu na ya kifalsafa kuhusu Mungu. Inaweza kusemekana kwamba walikuwa wameanza “kuzoeana” zaidi na zaidi na Mungu. Neno likitamkwa na Mungu, mahubiri Yake, ukweli Aliokuwa ameutoa awali, na kazi Yake—watu walikuwa “wamezoea” zaidi na zaidi. Hivyo basi, watu walidhania kimakosa kwamba Mungu hakuwa tena mgeni, na kwamba tayari walikuwa wakitembea njia ya uwiano na Mungu. Tangu hapo mpaka sasa, watu wamesikiliza mahubiri mengi ya ukweli, na wamepitia kazi nyingi ya Mungu. Ilhali kwenye uingiliaji kati na uzuiaji wa mambo mengi tofauti na hali, watu wengi hawawezi kufikia hali ya kutia ukweli katika matendo, na hawawezi kufikia hali ya kumtosheleza Mungu. Watu wanazidi kuwa goigoi, wanazidi kuikosa imani. Wanazidi kuhisi ni kana kwamba matokeo yao binafsi hayajulikani. Hawathubutu kuwa na mawazo yoyote ya kupita kiasi, na hawatafuti kupiga hatua yoyote ya maendeleo; wanafuata tu shingo upande, wakienda mbele hatua kwa hatua. Kuhusiana na hali ya sasa ya binadamu, mwelekeo wa Mungu kwa binadamu ni upi? Tamanio tu la Mungu ni kuukabidhi ukweli huu kwa binadamu, na kutia moyoni mwa binadamu njia Yake, na kupangilia hali mbalimbali ili kujaribu binadamu katika njia tofauti. Shabaha yake ni kuweza kuchukua maneno haya, ukweli huu, na kazi Yake, na kusababisha matokeo ambapo binadamu anaweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Watu wengi ambao Nimewaona wanalichukua tu neno la Mungu na kuliona kuwa falsafa, kuliona kuwa barua, kuliona kuwa kanuni za kufuatwa. Wanapoendelea na shughuli zao na kuongea au kukabiliwa na majaribio, hawachukulii njia ya Mungu kama njia ambayo wanafaa kuifuata. Hali hii hasa ni kweli wakati watu wanapokabiliwa na majaribio makuu; Sijamwona yeyote ambaye alikuwa anatia katika matendo kwa mwelekeo wa kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kwa sababu ya hili, mwelekeo wa Mungu kwa binadamu umejaa chuki na chukizo ya kupindukia. Baada ya Mungu kuwapa watu majaribio kadhaa, hata mara mia, bado hawana mwelekeo wazi wa kuonyesha bidii yao—ninataka kumcha Mungu na kujiepusha na maovu! Kwa sababu watu hawana bidii hii, na hawaonyeshi ishara kama hii, mwelekeo wa sasa wa Mungu kwao si kama ule wa hapo nyuma, Alipotoa rehema Yake, akatoa uvumilivu wake, akatoa ustahimilivu na subira yake. Badala yake, Amesikitishwa mno na binadamu. Ni nani aliyesababisha masikitiko haya? Aina hii ya mwelekeo ambao Mungu anao kwa binadamu, unamtegemea nani? Unategemea kila mtu anayemfuata Mungu. Kwenye mkondo wa miaka Yake mingi ya kazi, Mungu ametaja mahitaji mengi kwa binadamu, na kupangilia hali nyingi kwa binadamu. Lakini haijalishi ni vipi binadamu ametenda, na haijalishi ni mwelekeo upi ambao binadamu anao kwa Mungu, binadamu hawezi kutenda kwa njia wazi kulingana na shabaha ya kumcha Mungu na kujiepusha na uovu. Hivyo basi, Nitajumlisha yote haya kwa msemo mmoja, na kuweza kutumia msemo huu kuelezea kila kitu ambacho tumeweza kuzungumzia kuhusiana na ni kwa nini watu hawawezi kutembea kwa njia ya Mungu—mche Mungu na kujiepusha na maovu. Msemo huu ni upi? Msemo huu ni: Mungu humchukulia binadamu kama kifaa cha wokovu Wake, kifaa cha kazi Yake; binadamu humchukulia Mungu kama adui wake, kama tabaini yake. Je, unalielewa suala hili sasa? Kile ambacho ndicho mwelekeo wa binadamu; kile ambacho ndicho mwelekeo wa Mungu; kile ambacho ni uhusiano wa binadamu na Mungu—hivi vyote viko wazi sana sasa. Haijalishi ni kiwango kipi cha mahubiri ambayo mmeyasikiliza, yale mambo ambayo mliyoyatolea muhtasari nyinyi wenyewe—kama vile kuwa mwaminifu kwa Mungu, kumtii Mungu, kutafuta njia ya uwiano na Mungu, kutaka kuishi daima dawamu kwa ajili ya Mungu, kuishi kwa ajili ya Mungu—kwangu Mimi mambo hayo hayajumuishi kutembea kwa njia ya Mungu kwa nadhari, ambako ni kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Badala yake, ni njia mbalimbali kupitia kwazo mnaweza kufikia shabaha fulani. Ili kutimiza shabaha hizi, mnaangalia shingo upande baadhi ya taratibu. Na ni taratibu hizi hasa ambazo huwapeleka watu mbali zaidi kutoka katika njia ile ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, na kumweka Mungu katika upinzani na binadamu kwa mara nyingine.

Swali tunalolizungumzia leo ni zito kidogo, lakini licha ya chochote, bado Natumai kwamba mtakapopitia yale yote yajayo, na kwenye nyakati zijazo, mnaweza kufanya kile ambacho Nimewaambia mfanye. Msipuuze Mungu na kumchukulia Yeye kama hewa tupu, kuhisi kwamba Anakuwepo tu nyakati zile Anapokuwa Mwenye manufaa kwako, lakini wakati ule ambao humhitaji unahisi kwamba Yeye hayupo. Unaposhikilia uelewa huu katika bila ufahamu, tayari umemghadhabisha Mungu. Pengine kunao watu wanaosema: “Mimi sichukulii Mungu kama hewa tupu, mimi siku zote humwomba Mungu, siku zote mimi humtosheleza Mungu, na kila kitu ninachokifanya huwa katika ule upana na kiwango na kanuni zinazohitajika na Mungu. Bila shaka siendelei kulingana na mawazo yangu binafsi.” Ndiyo, namna ambayo unafanya mambo ni sahihi. Lakini unafikiria vipi wakati unakumbana macho kwa macho na suala? Unakuwa na matendo gani unapokabiliwa na suala? Baadhi ya watu huhisi kwamba Mungu yupo wakati wanapomwomba Yeye, na Kumsihi kuwasikiliza. Lakini wakati wanapokabiliwa na suala wanakuja na fikira zao binafsi na wanataka kuzitii. Hapa Mungu huchukuliwa kama hewa tupu. Aina hii ya hali humfanya Mungu kutokuwepo. Watu hufikiria kwamba Mungu anafaa kuwepo wakati wanapomhitaji Yeye, na wakati hawamhitaji Mungu Hafai kuwepo. Watu hufikiria kwamba kufanya mambo kulingana na mawazo yao katika matendo ya maisha ni tosha. Wanasadiki wanaweza kufanya mambo vyovyote vile wapendavyo. Wanafikiria tu kwamba hawahitaji kutafuta njia ya Mungu. Watu ambao kwa sasa wamo katika aina hii ya hali, hali hii ya namna—huoni kwamba karibu wataingia hatarini? Baadhi ya watu husema: “Haijalishi kama karibu nitaingia hatarini au la, nimesadiki kwa miaka mingi sana, na ninasadiki kwamba Mungu hataniacha kwa sababu Asingeweza kustahimili kuniacha mimi.” Watu wengine husema: “Hata tangu nilipokuwa kwenye tumbo la mama yangu, nilimsadiki Bwana, tangu hapo mpaka sasa, jumla ya miaka arubaini au hamsini hivi. Kwa mujibu wa muda, mimi ndimi nimefuzu zaidi kuokolewa na Mungu; mimi ndimi nimefuzu zaidi kuwepo. Kwenye kipindi hiki cha muda cha miongo minne au mitano, niliiacha familia yangu na kazi yangu. Nilijitolea kila kitu nilichokuwa nacho kwa Mungu, kama pesa, ardhi, anasa na muda wa familia; sijala vyakula vingi vitamu; sijafurahia vitu vingi vya kusisimua; sijatembelea sehemu nyingi za kuvutia; nimeweza hata kupitia mateso ambayo hata watu wa kawaida wasingevumilia. Kama Mungu hawezi kuniokoa mimi kwa sababu ya haya yote, basi mimi nashughulikiwa kwa njia isiyo ya haki na siwezi kuamini kwa aina hii ya Mungu.” Je, kunao watu wengi walio na aina hii ya mtazamo? (Kunao wengi sana.) Basi leo Nitawasaidia kuelewa hoja moja: Kila mmoja wa hao anayeshikilia aina hii ya maoni anachukua hatua zitakazomdhuru mwenyewe. Hii ni kwa sababu wanatumia maoni yao binafsi katika kuyafunika macho yao. Ni kufikiria kwao hasa, na hitimisho yao binafsi zinazochukua nafasi ya kiwango cha kile Mungu anahitaji kutoka kwa binadamu, ndizo zinazowashikilia dhidi ya kukubali nia za kweli za Mungu, na kuwafanya kutoweza kuhisi uwepo wa kweli wa Mungu, na kuwafanya pia kupoteza fursa yao kufanywa kuwa watimilifu na Mungu na kutokuwa na sehemu au mgao katika ahadi ya Mungu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp