Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 14

Ni Nani Hupanga Matokeo ya Binadamu

Kunalo jambo jingine muhimu zaidi, na hilo ni mwelekeo wenu kwa Mungu. Mwelekeo huu ni muhimu sana! Huamua kama hatimaye mtatembea kuelekea katika maangamizo, au kwenye hatima nzuri na ya kupendeza ambayo Mungu amewatayarishia. Katika Enzi ya Ufalme, Mungu tayari amefanya kazi kwa zaidi ya miaka 20 na kwenye kipindi cha miaka hii 20 pengine mioyo yenu imekuwa na tashwishi kuhusu utendakazi wenu. Hata hivyo, katika moyo wa Mungu, Ameweka rekodi halisi na ya kweli kwa kila mmoja wenu. Kuanzia wakati ule ambao kila mtu anaanza kumfuata Yeye na kusikiliza mahubiri Yake, kuelewa zaidi na zaidi kuhusu ukweli, hadi pale ambapo wanatekeleza wajibu wao—Mungu anayo rekodi ya kila mojawapo ya maonyesho haya. Wakati mtu anapofanya wajibu wake, wakati anapokabiliwa na kila aina ya hali, kila aina ya majaribio, mwelekeo wa mtu huyo ni upi? Wanatenda kazi vipi? Wanahisi vipi kwa Mungu katika mioyo yao? … Mungu ameweka rekodi ya yote haya, rekodi yote kwa hakika. Pengine kutokana na mtazamo wenu, masuala haya yanakanganya. Hata hivyo, kutoka pale ambapo Mungu yupo, yote yako wazi kabisa, na hakuna hata dalili yoyote ya kutokuwa wazi. Hili ni suala linalohusisha matokeo ya kila mmoja, na majaliwa yao na matarajio yao ya siku za baadaye vilevile. Hata zaidi, hapa ndipo ambapo Mungu anatumia jitihada Zake zote alizomakinikia. Hivyo basi Mungu hathubutu kuipuuza hata kidogo, na hatavumilia kutomakinika kokote. Mungu anarekodi haya yote kuhusu wanadamu, anarekodi mambo kuhusu mkondo mzima wa binadamu anayefuata Mungu, kuanzia mwanzo hadi mwisho. Mwelekeo wako kwa Mungu wakati huu utaamua hatima yako. Je, haya si kweli? Kutoka hapo mpaka sasa, mnasadiki kwamba Mungu ni mwenye haki? Vitendo vya Mungu vinafaa? Bado mnayo picha yoyote ya Mungu vichwani mwenu? (La.) Basi mnasema kwamba matokeo ya binadamu ni kwa ajili ya Mungu kuweza kupanga au kwa ajili ya binadamu mwenyewe kupanga? (Ni kwa Mungu kupanga.) Ni nani basi anayeyapanga? (Mungu.) Hamna hakika, sivyo? Ndugu wa makanisa ya Hong Kong, ongeeni—ni nani anayeyapanga? (Binadamu anayapanga mwenyewe.) Mwanadamu anayapanga? Hivyo basi haimaanishi kwamba haina chochote kuhusu Mungu? Ni nani anayetaka kuongea kutoka kwenye makanisa ya Korea? (Mungu huanzisha matokeo ya binadamu kutokana na hatua na vitendo vyake vyote na kutokana pia na njia wanayotembelea.) Hili ni jibu halisi sana. Kunayo hoja hapa ambayo lazima Niwafahamishe nyinyi: Kwenye mkondo wa kazi ya wokovu wa Mungu, Yeye huweka kiwango kwa binadamu. Kiwango hiki ni kwamba binadamu anaweza kutii neno la Mungu, na kutembea kwa njia ya Mungu. Ndicho kiwango kinachotumika kupima matokeo ya binadamu. Kama utafanya mazoezi kwa mujibu wa kiwango hiki cha Mungu, basi unaweza kupata matokeo mazuri; kama hutafanya hivyo, basi huwezi kupokea matokeo mazuri. Basi ni nani unayesema kwamba anayapanga matokeo haya? Si Mungu pekee anayeyapanga, lakini badala yake Mungu na binadamu pamoja. Hiyo ni sahihi? (Ndiyo.) Kwa nini hivyo? Kwa sababu ni Mungu ambaye anataka kujishughulisha na kujihusisha katika kazi ya wokovu wa wanadamu, na kutayarisha hatima nzuri kwa ajili ya binadamu; binadamu ndiye mlengwa wa kazi ya Mungu, na matokeo haya, hatima hii, ndiyo ambayo Mungu humtayarishia binadamu. Kama kusingekuwa na kilengwa cha kazi Yake, basi Mungu asingehitaji kazi hii; kama Mungu asingefanya kazi hii, basi binadamu asingekuwa na fursa ya wokovu. Binadamu ndiye mlengwa wa wokovu, na ingawa binadamu yumo kwenye upande wa kimya katika mchakato huu, ni mwelekeo wa upande huu ambao unaamua kama Mungu atafanikiwa katika kazi Yake ya kuwaokoa wanadamu au la. Kama si mwongozo ambao Mungu anakupa wewe, basi usingejua kiwango Chake, na usingekuwa na lengo lolote. Kama unacho kiwango hiki, lengo hili, ilhali hushirikiani, hulitilii kwenye matendo, hulipii gharama, basi bado hutapokea matokeo haya. Hii ndiyo maana tunasema kwamba matokeo haya hayawezi kutenganishwa na Mungu, na pia hayawezi kutenganishwa na binadamu. Na sasa unaweza kujua ni nani anayepanga matokeo ya binadamu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp