Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 24

Mungu Amuumba Hawa

Mwa 2:18-20 Yehova Mungu akasema, Si vizuri kuwa mtu huyo akuwe peke yake; nitamuumbia msaidizi anayefanana na yeye. Na kutoka kwa ardhi Yehova Mungu akaumba wanyama wote wa msituni, na ndege wote wa angani; na akawaletea kwa Adamu ndiyo aone majina ambayo angewapa: na chochote ambacho Adamu alikiita kiumbe hai, hilo ndilo likawa jina lake kuanzia hapo. Naye Adamu akawapa wanyama wote wa kufugwa majina, na ndege wa hewani, na wanyama wote wa mwituni; lakini kwa Adamu hakupatikana msaidizi ambaye alifanana na yeye.

Mwa 2:22-23 Nao ubavu, ambao Yehova Mungu aliuchukua kutoka kwa Adamu, yeye akaufanya uwe mwanamke, na akampeleka kwa Adamu. Naye Adamu akasema, Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu, na nyama ya nyama zangu: ataitwa Mwanamke, kwa kuwa amechukuliwa kutoka kwa Mwanamume.

Kunazo kauli kuu chache kwenye sehemu hii ya maandiko. Tafadhali zichoree mstari chini: “chochote ambacho Adamu alikiita kiumbe hai, hilo ndilo likawa jina lake kuanzia hapo.” Kwa hivyo ni nani aliyepatia viumbe wote haya majina yao? Alikuwa Adamu, si Mungu. Kauli hii inamwambia mwanadamu ukweli: Mungu alimpa binadamu werevu alipomuumba Yeye. Hivi ni kusema kwamba, werevu wa binadamu ulitoka kwa Mungu. Hili ni kweli. Lakini kwa nini? Baada ya Mungu kumuumba Adamu, Adamu alienda shuleni? Je, alijua namna ya kusoma? Baada ya Mungu kuwaumba viumbe hai mbalimbali, je Adamu aliwatambua wanyama hawa wote? Je, Mungu alimwambia majina ya viumbe hao? Bila shaka, Mungu pia hakumfunza namna ya kutunga yale majina ya viumbe hawa. Huo ndio ukweli! Basi alijua vipi namna ya kupatia viumbe hawa hai majina yao na aina gani ya majina ya kuwapatia? Haya yote yanahusiana na swali kuhusu ni nini ambacho Mungu aliongezea kwa Adamu alipomuumba yeye. Ukweli unathibitisha kwamba wakati Mungu alipomuumba binadamu Alikuwa ameongezea werevu kwake. Huu ni ukweli muhimu sana. Je, nyinyi nyote mmesikiliza kwa makini? Kunao ukweli mwingine muhimu ambao unafaa kuwa wazi kwenu? Baada ya Adamu kuwapatia viumbe hai majina yao, majina haya yalipangwa kwenye msamiati wa Mungu. Kwa nini Ninasema hivyo? Hii pia inahusisha tabia ya Mungu, na lazima Niielezee.

Mungu alimuumba binadamu, Akapumua maisha ndani yake, na pia Akampa baadhi ya werevu Wake, uwezo Wake, na kile Anacho na alicho. Baada ya Mungu kumpa binadamu mambo haya yote, binadamu aliweza kufanya baadhi ya mambo haya kwa uhuru na kufikiria pekee yake. Kama kile binadamu anaunda na kufanya ni kizuri machoni mwa Mungu, basi Mungu anakikubali na haingilii kati. Kama kile binadamu anafanya ni sahihi, basi Mungu atakiacha tu kiwe hivyo milele. Kwa hivyo kauli hii “chochote ambacho Adamu alikiita kiumbe hai, hilo ndilo likawa jina lake kuanzia hapo” inaonyesha nini? Inaopendekeza kwamba Mungu hakufanya marekebisho yoyote kwa majina ya wale viumbe mbalimbali hai. Jina lolote lile ambalo Adamu alimwita, Mungu alisema “Ndiyo” na akasajili jina hilo hivyo. Je, Mungu alionyesha maoni yoyote? La, hilo ni hakika. Kwa hivyo, mnaona nini hapa? Mungu Alimpa binadamu werevu naye binadamu akautumia werevu wake aliopewa na Mungu kufanya mambo. Kama kile binadamu anafanya ni kizuri machoni mwa Mungu, basi kinathibitishwa, kutambulika, na kukubalika na Mungu bila ya utathmini au upinzani wowote. Hili ni jambo ambalo hakuna mtu wala roho wa maovu, wala Shetani, anaweza kufanya. Je, mnauona ufunuo wa tabia ya Mungu hapa. Je, mwanadamu, mwanadamu aliyepotoshwa, au Shetani anaweza kuwakubali wengine kuwawakilisha katika kufanya mambo huku wakitazama? Bila shaka la! Je, wanaweza kupigania cheo na yule mtu mwingine au nguvu nyingine ambayo ni tofauti na wao? Bila shaka wangefanya hivyo! Na kwa muda huo, kama angekuwa ni mtu aliyepotoshwa au Shetani aliyekuwa na Adamu, bila shaka wangekataa kile ambacho Adamu alikuwa akifanya. Ili kuthibitisha kwamba wanao uwezo wa kufikiria kwa uhuru na wanayo maono yao binafsi na ya kipekee, wangekataa kabisa kila kitu alichofanya Adamu: “Unataka kukiita hivyo? Kwa kweli, sitakiita hivyo, nitakiita hivi; ulikiita Tom lakini mimi nitakiita Harry. Lazima nionyeshe ustadi wangu.” Haya ni aina gani ya asili? Hii ni asili ya kiburi kisicho na mipaka? Lakini Mungu anayo tabia kama hii? Je, Mungu alikuwa na upinzani wowote usiokuwa wa kawaida kwa mambo haya ambayo Adamu alifanya? Jibu ni bila shaka la! Kati ya tabia ambayo Mungu anafichua, hakuna hata chembe ya ubishi, ya kiburi, au kujigamba kwa nafsi. Hilo liko wazi kabisa hapa. Hili ni jambo dogo tu, lakini kama huelewi kiini cha Mungu, kama moyo wako hautajaribu kujua namna ambavyo Mungu anatenda na mwelekeo wa Mungu ni ipi, basi hutajua tabia ya Mungu au kuyaona maonyesho na ufunuo wa tabia ya Mungu. Je, hayo si kweli? Je, unakubali kile Nimetoka tu kukuelezea? Kwa kujibu matendo ya Adamu, Mungu hakutangaza kwa sauti kwamba, “Umefanya vyema. Umefanya sahihi Ninakubali.” Katika Moyo Wake, hata hivyo, Mungu aliidhinisha, akathamini, akashangilia kile Adamu alikuwa amefanya. Hili ndilo jambo la kwanza tangu uumbaji ambalo binadamu alikuwa amemfanyia Mungu akifuata maagizo Yake. Ni jambo ambalo binadamu alifanya badala ya Mungu na kwa niaba ya Mungu. Mbele ya macho yake, hili lilitokana na werevu Aliokuwa amempa binadamu. Mungu aliliona kama jambo zuri, kitu kizuri. Kile ambacho Adamu alifanya wakati huo kilikuwa maonyesho ya kwanza ya werevu wa Mungu kwa binadamu. Hili lilikuwa onyesho zuri kutoka kwa maoni ya Mungu. Kile Ninachotaka kuwaambia nyinyi hapa ni kwamba nia ya Mungu katika kuongezea sehemu ya kile Anacho na alicho na werevu wake kwa binadamu ilikuwa ili mwanadamu aweze kuwa kiumbe hai anayemwonyesha Yeye. Kwa kiumbe hai kama huyo kufanya mambo hayo kwa niaba yake, ilikuwa ndicho hasa kile Mungu alikuwa akitamani kuona.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp