Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 199

01/08/2020

Mielekeo Mbalimbali ya Wanadamu kwa Mungu

Jinsi watu wamtendeavyo Mungu huamua hatima yao, na huamua jinsi Mungu anavyowatendea na kuwashughulikia. Kufikia sasa nitawapa mifano kadhaa ya jinsi watu wanavyotenda mbele za Mungu. Hebu tusikie kitu kuhusu ama mienendo na tabia ambazo kwazo wanamtendea Mungu ni sahihi au la. Hebu tuangalie mwenendo wa aina saba za watu wafuatao:

1) Kuna aina moja ya watu ambao mwelekeo wao kwa Mungu haswa ni wa kipuuzi. Wanafikiria kuwa Mungu ni kama Bodhisattva au kiumbe takatifu wa masimulizi ya kibinadamu, na kuwataka watu kusujudu mara tatu wanapokutana na kuchoma ubani baada ya kula. Kwa hivyo, katika mioyo yao, wanapomshukuru Mungu kwa neema Yake, na kuwa wenye shukrani kwa Mungu, mara nyingi wana msukumo kama huo. Hivyo wanatamani Mungu wanaomwamini leo, kama kiumbe takatifu wanayemtamania ndani ya mioyo yao, anaweza kukubali mienendo yao Kwake ambapo wanasujudu mara tatu wanapokutana, na kuchoma ubani baada ya kula.

2) Watu wengine wanamwona Mungu kama Budha anayeishi, mwenye uwezo wa kutoa wanaoishi wote kutoka kwenye mateso, na kuwaokoa; wanaona Mungu kama Budha anayeishi mwenye uwezo wa kuwatoa kwenye mateso mengi. Imani ya watu hawa kwa Mungu ni kumwabudu Mungu kama Buddha. Ijapokuwa hawachomi ubani, kusujudu, au kutoa sadaka, katika nyoyo zao Mungu ni kama tu Buddha, na huwataka tu wawe wema na wenye huruma, kuwa wasiue chochote kilicho hai, wasiwaapie wengine, waishi maisha yanayoonekana kuwa manyoofu, na wasifanye chochote kibaya—vitu hivi tu. Huyu ndiye Mungu mioyoni mwao.

3) Watu wengine humwabudu Mungu kama mtu mkubwa au maarufu. Kwa mfano, kwa namna yoyote mtu huyu mkubwa hupenda kuongea, kwa kiimbo chochote huongea, maneno na msamiati anaotumia, kiimbo chake, ishara zake za mikono, maoni na matendo yake, ukali wake—wanaiga yote, na hivi ndivyo vitu ambavyo ni lazima watavisababisha katika mwendo wa imani yao kwa Mungu.

4) Watu wengine wanamwona Mungu kama mfalme, wanahisi kuwa Yuko juu ya vitu vyote vingine, na hakuna anayejaribu kumkosea—na wakifanya hivyo, wataadhibiwa. Wanaabudu mfalme kama huyo kwa sababu wafalme huwa wanashikilia sehemu fulani kwenye mioyo yao. Mawazo, tabia, mamlaka, na asili ya wafalme—hata na maslahi na maisha yao ya kibinafsi—yote huwa kitu ambacho watu hawa lazima waelewe, masuala na mambo ambayo wanashughulika nayo, na hivyo wanamwabudu Mungu kama mfalme. Imani ya namna hiyo inachekesha.

5) Watu wengine wana imani fulani katika uwepo wa Mungu, ambayo ni kubwa na isiyotingishika. Kwa sababu ufahamu wa Mungu kwao ni wa juujuu mno na hawana mazoea ya maneno ya Mungu, wanamwabudu kama sanamu. Sanamu hii ni Mungu aliye ndani ya mioyo yao, ni kitu ambacho wanafaa kuogopa na kusujudia, na ambayo wanalazimika kufuata na kuiga. Wanamwona Mungu kama sanamu, ambayo wanafaa kufuata maisha yao yote. Wanaiga sauti ambayo kwayo Mungu huzungumza, na kwa nje wanaiga wale ambao Mungu anapenda. Aghalabu wanafanya mambo ambayo yanaonekana kuwa manyoofu, safi, na ya kweli, na wanafuata hii sanamu kama mwenzao au mwandani wao ambaye wanaweza kushirikiana. Hiyo ndiyo aina ya imani yao.

6) Kuna watu ambao, kando na kusoma maneno mengi ya Mungu na kuwa wameyasikia mahubiri mengi, wanahisi ndani ya nyoyo zao kuwa msimamo tu wa mienendo yao kwa Mungu ni kuwa kila wakati wanafaa wawe watiifu na kujipendekeza, la sivyo wanafaa kumsifu Mungu na kumwabudu kwa njia isiyo halisi. Wanaamini kuwa Mungu ni Mungu anayewahitaji kutenda hivyo, na wanaamini kuwa wasipofanya hivyo, basi wakati wowote wanaweza kuchochea hasira Yake au kumtenda dhambi, na kwamba kwa sababu ya kutenda dhambi Mungu atawaadhibu. Huyo ndiye Mungu mioyoni mwao.

7) Kisha kuna watu wengi, wanaotafuta riziki ya kiroho katika Mungu. Kwa sababu wanaishi katika ulimwengu huu, hawana amani au furaha, na hakuna wanapopata faraja. Baada ya kumpata Mungu, wanapokuwa wameona na kusikia maneno Yake, ndani ya mioyo yao wanafurahi na kusisimka kisiri. Na kwa nini hivyo? Wanaamini kuwa tayari wamepata mahali ambapo patawapa furaha, kwamba hatimaye wamepata Mungu ambaye atawapa riziki ya kiroho. Hii ni kwa sababu, baada ya kukubali Mungu na kuanza kumfuata, wanakuwa wenye furaha, maisha yao yanakamilishwa, hawako kama wengine wasioamini tena, wanaotembea usingizini maishani mwao kama wanyama, na wanahisi kuwa kuna kitu cha kutamania katika maisha. Kwa hivyo, wanafikiri kuwa huyu Mungu anaweza kuwatimizia mahitaji yao ya kiroho na kuleta furaha kubwa katika mawazo na Roho. Bila ya kujua, wanakuwa hawawezi kumwacha huyu Mungu anayewapa riziki ya kiroho, Anayeleta furaha katika Roho na familia zao. Wanaamini kuwa imani katika Mungu haihitaji zaidi ya kuwapa riziki ya kiroho.

Je, mielekeo kumwelekea Mungu ya watu hawa wa aina mbalimbali waliotajwa hapo juu ipo miongoni mwenu? (Ipo.) Kama, katika imani yao katika Mungu, moyo wa mtu una mwelekeo wowote kati ya hii, je, kweli wanaweza kuja mbele za Mungu? Kama watu wana mwelekeo wowote kati ya hii katika mioyo yao, je, wanamwamini Mungu? Je, wanamwamini Mungu Mwenyewe yule wa kipekee? (La.) Kwa kuwa humwamini Mungu wa kipekee Mwenyewe, unamwamini nani? Kama unachoamini si Mungu Mwenyewe wa kipekee, kuna uwezekano unaamini katika sanamu, mtu maarufu, au Bodhisattva, kuwa unamwabudu Budha moyoni mwako. Zaidi ya hayo, kuna uwezekano unaamini katika mtu wa kawaida. Kwa muhtasari, kwa sababu ya aina tofautitofauti za imani za watu na mielekeo kwa Mungu, watu humweka Mungu wa utambuzi wao wenyewe katika nyoyo zao, wanamlazimishia Mungu fikira zao, wanaweka fikira na mielekeo yao kuhusu Mungu sambamba na Mungu Mwenyewe wa kipekee, na kisha wanayanyanyua juu kuyashangilia. Ina maana gani watu wakiwa na mielekeo hiyo isiyofaa kwa Mungu? Ina maana kuwa wamemkataa Mungu wa kweli Mwenyewe na kuabudu Mungu bandia, na ina maana kuwa wakati uleule wanapomwamini Mungu, wanamkataa Mungu, wanampinga, na kuwa wanakana uwepo wa Mungu wa kweli. Kama watu watazidi kushikilia imani za aina hiyo, matokeo yao yatakuwa gani? Kwa aina hiyo ya imani, je, wanaweza kufikia karibu na kutimiza matakwa ya Mungu? (La, hawawezi.) Kinyume cha hayo, kwa sababu ya dhana na fikira zao, watu watazidi kuwa mbali na njia ya Mungu, kwa kuwa njia wanayoifuata ni kinyume cha njia ambayo Mungu anawahitaji waifuate. Umekwisha kusikia hadithi ya “kwenda kusini kwa kuendesha gari la farasi kuelekea kaskazini”? Hii yaweza kuwa ni mfano wa kwenda kusini kwa kuendesha gari la farasi kuelekea kaskazini. Watu wakimwamini Mungu kwa njia hii ya kipumbavu, basi kadiri unavyojaribu kwa nguvu, ndivyo utakavyokuwa mbali zaidi na Mungu. Na kwa hiyo nakuonya hivi: Kabla ya kufunga safari, ni lazima kwanza ujue kama unaenda njia iliyo sawa. Lenga katika juhudi zako, kuwa na uhakika na kujiuliza, “Je, Mungu ninayemwamini ni Mtawala wa vitu vyote? Je, huyu Mungu ninayemwamini ni mtu tu wa kunipa riziki ya kiroho? Ni sanamu yangu? Je, huyu Mungu ninayemwamini anataka nini kutoka kwangu? Mungu huwa anakubali chochote ninachokifanya? Je, kila kitu ninachokifanya na kutafuta kinalingana na kazi ya kumjua Mungu? Je, kinalingana na mahitaji ya Mungu kwangu? Je, njia ninayoifuata inajulikana na kukubaliwa na Mungu? Je, Mungu anaridhishwa na imani yangu?” Aghalabu na mara kwa mara unafaa ujiulize haya maswali. Kama ungetaka kuutafuta ufahamu wa Mungu, basi lazima uwe na dhamiri safi na malengo wazi ndipo uweze kumridhisha Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp