Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 30

Mwa 9:11-13 Na nitaweka agano langu na ninyi, wala miili yote haitaondolewa tena na maji ya gharika; wala hakutakuwa na gharika tena kuiharibu dunia. Naye Mungu akasema, Hii ni alama ya agano ambayo naifanya kati ya Mimi na ninyi na viumbe vyote vyenye uhai vilivyo nanyi, kwa vizazi vya kudumu: naweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa alama ya agano kati ya Mimi na dunia.

Mwishoni mwa hadithi ya Nuhu, tunaona kwamba Mungu alitumia mbinu isiyo ya kawaida kuelezea hisia Zake wakati huo. Mbinu hii ni maalumu sana, na ni kuweka agano na binadamu. Ni mbinu inayotangaza mwisho wa matumizi ya gharika na Mungu katika kuangamiza ulimwengu. Kutoka nje, kuweka agano kunaonekana kuwa jambo lililo la kawaida sana. Si jambo lolote zaidi ya kutumia maneno kufunga wahusika ili wasitende vitendo vitakavyokiuka agano, ili kusaidia kutimiza kusudio la kulinda maslahi ya pande zote mbili. Kwa umbo, ni jambo la kawaida sana, lakini kutoka kwa motisha zilizopo na maana ya Mungu kufanya kitu hiki, ni ufunuo wa kweli wa tabia ya Mungu na hali Yake ya akili. Endapo utayaweka maneno haya kando na kuyapuuza, kama Sitawahi kukuambia ukweli wa mambo, basi binadamu hawatawahi kwa hakika kujua kufikiria kwa Mungu. Pengine katika kufikiria kwako Mungu anatabasamu wakati anapofanya agano hili, au pengine maonyesho Yake ni ya kumakinika, lakini haijalishi ni aina gani iliyo maarufu zaidi ya maonyesho Aliyonayo Mungu katika kufikiria kwa watu, hakuna mtu anayeweza kuona moyo wa Mungu au maumivu Yake, na hata upweke Wake. Hakuna mtu anayeweza kumfanya Mungu kumwamini au anayestahili kuaminiwa na Mungu, au kuwa mtu Anayeweza kueleza fikira Zake au kuwa mwandani Wake wa kuambia maumivu Yake. Ndiyo maana Mungu hakuwa na chaguo ila kufanya kitu kama hicho. Kwa juujuu, Mungu alifanya jambo rahisi la kuwaaga binadamu wale wa awali, kuhitimisha hali ya kale ilivyokuwa na kufikia hitimisho halisi katika kuangamiza Kwake kwa ulimwengu akitumia gharika. Hata hivyo, Mungu alikuwa ameyazika maumivu kutoka muda huu ndani kabisa ya moyo Wake. Kwa wakati ambao Mungu hakuwa na yeyote wa kuita mwandani, aliunda agano na wanadamu, akiwaambia kwamba asingeuangamiza ulimwengu kwa gharika tena. Wakati upinde wa mvua unapojitokeza ni kukumbusha watu kwamba, kitu kama hicho kiliwahi kufanyika, kuwapa onyo watu dhidi ya kufanya maovu. Hata katika hali hiyo ya maumivu, Mungu hakusahau kuwahusu wanadamu na bado akaonyesha kujali kwingi sana kwao. Je, huu si upendo na kutokuwa na nafsi kwa Mungu? Lakini nao watu wanafikiria nini wakati wanapoteseka? Kwani huu si wakati ambao wanamhitaji Mungu zaidi? Katika nyakati kama hizi, siku zote watu humkokota Mungu katika mambo yao ili Mungu aweze kuwapa tulizo. Haijalishi ni lini, Mungu hatawahi kuwavunja moyo watu wake, na siku zote Atawaruhusu watu kutoka katika changamoto zao na kuishi katika mwangaza. Ingawaje Mungu anawakimu wanadamu, ndani wa moyo wa binadamu, Mungu si chochote wala lolote ila tembe ya kumhakikishia tu mambo, dawa ya tulizo. Wakati Mungu anateseka, wakati moyo Wake una majeraha, kuwa na kiumbe aliyeumba au mtu yeyote wa kuwa mwandani wake au wa kumtuliza Yeye kwa kweli kwake Mungu ni tamanio tu la kibadhirifu asiloweza kutegemea. Siku zote binadamu hatilii maanani hisia za Mungu, hivyo Mungu siku zote haulizii wala hatarajii kuwa kuna mtu anayeweza kumtuliza Yeye. Anatumia mbinu Zake mwenyewe kueleza hali Yake. Watu hawafikirii kwamba ni jambo kubwa kwa Mungu kupitia mateso fulani, lakini unapojaribu tu kuelewa Mungu kwa kweli, unapoweza kushukuru kwa dhati, nia nzuri za Mungu katika kila kitu anachofanya, ndipo unapoweza kuhisi ukubwa wa Mungu na kutokuwa na nafsi kwake. Ingawaje Mungu aliunda agano na wanadamu kutumia upinde wa mvua, hakuwahi kuambia yeyote kwa nini alifanya hivi, kwa nini alianzisha agano hili, kumaanisha hakuwahi kuambia mtu fikira Zake halisi. Hii ni kwa sababu hakuna mtu anayeweza kufahamu kina cha upendo ambao Mungu anao kwa wanadamu Aliowaumba kwa mikono Yake mwenyewe, na hakuna pia mtu anayeweza kutambua ni kiasi kipi cha maumivu moyo Wake uliteseka wakati Alipoangamiza binadamu. Hivyo basi, hata kama Angeambia watu namna Anavyohisi, hawawezi kumwamini. Licha ya kuwa katika maumivu, angali Anaendelea na hatua inayofuata ya kazi Yake. Siku zote Mungu Anautoa upande wake bora zaidi na mambo bora zaidi kwa wanadamu huku yeye Mwenyewe Akistahimili kimyakimya mateso yote. Mungu kamwe hafichui mateso haya. Badala yake, Anayavumilia na kusubiri kwa kimya. Ustahimilivu wa Mungu si wa kimya tu, usio na hisia, au usio na suluhu, wala si ishara ya unyonge. Ni kwamba upendo na kiini cha Mungu siku zote yamekuwa bila nafsi. Huu ni ufunuo wa kiasili wa kiini na tabia Yake na maonyesho halisi wa utambulisho wa Mungu kama Muumba wa kweli.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp