Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 430

16/10/2020

Masharti ya Mungu kwa wanadamu siyo tu kuweza kuzungumza kuhusu uhalisi. Je, si hiyo itakuwa rahisi sana? Kwa nini basi Mungu anazungumza kuhusu kuingia katika maisha? Kwa nini Anaongea kuhusu mabadiliko? Kama mtu ana uwezo wa mazungumzo matupu tu kuhusu uhalisi, mabadiliko katika tabia yangeweza kupatikana? Kulifunza kundi la wanajeshi wazuri wa ufalme sio sawa na kuwafunza wanadamu ambao wanaweza tu kuongea kuhusu uhalisi au watu ambao hujigamba tu; badala yake, wanafundishwa kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu wakati wote, ambao ni wagumu bila kujali vikwazo wanavyokumbana navyo, na wanaoishi kwa mujibu wa maneno ya Mungu wakati wote, na hawarudi kwa ulimwengu. Huu ndio uhalisi ambao Mungu anauzungumzia, nayo ni matakwa ya Mungu kwa binadamu. Kwa hiyo, usiuone uhalisi ulionenwa na Mungu kama rahisi sana. Kupata nuru tu kwa Roho Mtakatifu sio sawa na kuumiliki uhalisi: Hiki sicho kimo cha wanadamu, lakini neema ya Mungu, nayo haihusishi mafanikio yoyote ya wanadamu. Kila mwanadamu ni lazima ayavumilie mateso ya Petro, na hata zaidi aumiliki utukufu wa Petro, ambao ndio watu huishi kwa kudhihirisha baada ya kupata kazi ya Mungu. Hii tu ndiyo inaweza kuitwa uhalisi. Usidhani kwamba utamiliki uhalisi kwa sababu unaweza kuzungumza kuhusu uhalisi. Huu ni uongo, huu haulingani na mapenzi ya Mungu, na hauna maana halisi. Usiseme mambo kama haya katika siku zijazo—komesha misemo kama hii! Wale wote walio na uelewa wa uongo wa maneno ya Mungu ni makafiri. Hawana maarifa yoyote halisi, sembuse kimo chochote halisi; wao ni watu wenye kujigamba bila ya uhalisi. Hiyo ni, wale wote wanaoishi nje ya dutu ya maneno ya Mungu ni makafiri. Wale wanaoonekana kuwa makafiri na wanadamu ni wanyama mbele za Mungu, na wale wanaoonekana kuwa makafiri na Mungu ni wale ambao hawana maneno ya Mungu kama maisha yao. Kwa hiyo, wale ambao hawana uhalisi wa maneno ya Mungu nao wanashindwa kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu ni makafiri. Nia ya Mungu ni kufanya iwe kwamba kila mmoja anaishi kwa kudhihirisha uhalisi wa maneno ya Mungu. Sio tu kwamba kila mtu anaweza kuzungumza kuhusu uhalisi, lakini muhimu zaidi, kwamba kila mmoja anaweza kuishi kwa kudhihirisha uhalisi wa maneno ya Mungu. Uhalisi ambao mwanadamu anautambua ni wa juu juu sana, hauna thamani, hauwezi kutimiza mapenzi ya Mungu, ni duni sana, hata haustahili kutajwa, una upungufu sana, na uko mbali sana na kiwango cha mahitaji ya Mungu. Kila mmoja wenu atapitia ukaguzi mkuu ili kuona ni nani kati yenu anayejua tu kuzungumza kuhusu uelewa wake lakini hawezi kuonyesha njia, na kuona ni nani kati yenu ni taka bure. Kumbuka hili katika siku zijazo! Usizungumze kuhusu uelewa mtupu—zungumza tu kuhusu njia ya utendaji, na kuhusu uhalisi. Geuka kutoka maarifa halisi hadi kwenye vitendo halisi, na kisha geuka kutoka kutenda hadi kuishi kwa kudhihirisha uhalisi. Usiwahutubie wengine, na usizungumze kuhusu maarifa ya ukweli. Kama uelewa wako ni njia, basi unaweza kuuachilia; kama si njia, basi tafadhali nyamaza, na uache kuongea. Kile unachosema ni bure. Ni baadhi tu ya maneno ya uelewa ya kumpumbaza Mungu na kuwafanya wengine wakuonee wivu. Si hilo ni lengo lako? Je, hii si kuwachezea wengine kimakusudi? Je, kunayo thamani yoyote katika hili? Zungumza tu kuhusu uelewa baada ya kuwa na uzoefu kuuhusu, na kisha hutakuwa unajisifu tena. La sivyo wewe ni mtu tu ambaye anasema maneno yenye kiburi. Huwezi hata kuyashinda mambo mengi au kuasi dhidi ya mwili wako wenyewe katika uzoefu wako halisi, siku zote ukifanya chochote unachoelekezwa kukifanya kwa tamaa zako, sio kwa kuyaridhisha mapenzi ya Mungu, lakini bado unayo nyongo ya kuzungumzia uelewa wa kinadharia—huna haya! Bado unayo nyongo ya kuzungumza kuhusu uelewa wako wa maneno ya Mungu—wewe ni fidhuli jinsi gani! Kuhutubu na kujisifu kumekuwa asili yako, na umekuwa na desturi ya kufanya hili. Unalijua sana kila wakati unapotaka kuzungumza, unalifanya kwa ustadi na bila kufikiria, nawe unajiingiza katika mapambo inapokuja wakati wa kutenda. Je, si hii ni kuwapumbaza wengine? Unaweza kuwapumbaza wanadamu, lakini Mungu hawezi kupumbazwa. Wanadamu hawajui na hawana utambuzi, lakini Mungu anatilia maanani masuala hayo, naye hatakusaza. Ndugu na dada zako wanaweza kukutetea, wakiusifu uelewa wako, wakipendezwa nawe, lakini ikiwa huna uhalisi, Roho Mtakatifu hatakusaza. Pengine Mungu wa matendo hatazikaripia dosari zako, lakini Roho wa Mungu hataweka makini yoyote kwako, na hiyo itatosha wewe kuvumilia. Je, unaamini hili? Zungumza zaidi kuhusu uhalisi wa utendaji; Je, umeshasahau tayari? Zungumza zaidi kuhusu njia za kiutendaji; Je, ushasahau tayari? “Zungumza kwa uchache kuhusu nadharia za fahari au mazungumzo mazuri yasiyo na maana, na ni bora kuanza mazoezi kuanzia sasa.” Je, umesahau maneno haya? Je, huelewi yoyote haya? Je, hauna uelewa wa mapenzi ya Mungu?

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp