Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 31

Baada tu ya kuumba binadamu, Mungu Alianza kujihusisha na binadamu na kuzungumza na binadamu, na tabia yake ikaanza kuonyeshwa kwa binadamu. Kwa maneno mengine, tangu Mungu alipojihusisha kwanza na wanadamu, Alianza kuweka wazi kwa mwanadamu, bila kusita, kiini Chake halisi na kile Anacho na alicho. Licha ya kama watu wa awali au watu wa leo wanaweza kuona au kuelewa kiini hicho, kwa ufupi Mungu anamzungumzia mwanadamu na kufanya kazi miongoni mwa binadamu, Akifichua tabia Yake na Akionyesha kiini Chake—jambo ambalo ni ukweli, na lisilopingika na mtu yeyote. Hii inamaanisha pia kwamba tabia ya Mungu, kiini cha Mungu, na kile Anacho na alicho vyote vinatolewa daima na kufichuliwa huku naye Akifanya kazi na kujihusisha na binadamu. Hajawahi kusetiri au kumfichia binadamu chochote, lakini badala yake anatangaza kwa umma na kuachilia tabia Yake binafsi bila ya kuficha chochote. Hivyo basi, Mungu anatumai kwamba binadamu anaweza kumjua Yeye na kuielewa tabia Yake na kiini chake. Hapendi binadamu kuchukulia tabia Yake na kiini Chake kuwa mafumbo ya milele, wala Hataki wanadamu kumchukulia Mungu kama fumbo lisiloweza kutatuliwa. Mpaka tu pale ambapo wanadamu watakapomjua Mungu ndipo binadamu atakapojua njia ya kufuata na kuweza kuukubali mwongozo wa Mungu, na wanadamu tu kama hawa ndio wanaoweza kuishi kwa kweli katika utawala wa Mungu, na kuishi katika mwangaza, na kuishi katikati ya baraka za Mungu.

Maneno na tabia iliyowasilishwa mbele na kufichuliwa na Mungu inawakilisha mapenzi Yake, na pia inawakilisha kiini Chake halisi. Wakati Mungu anapojihusisha na binadamu, haijalishi ni nini Anachosema au kufanya, au tabia gani Anayofichua, na haijalishi ni nini binadamu anaona kuhusu kiini cha Mungu na kile Anacho na alicho, vyote vinawasilisha mapenzi ya Mungu kwa binadamu. Licha ya kiwango ambacho binadamu anaweza kutambua, kufahamu, au kuelewa, vyote hivi vinawakilisha mapenzi ya Mungu—mapenzi ya Mungu kwa binadamu. Hili ni bila shaka! Mapenzi ya Mungu kwa binadamu ni vile Anavyohitaji watu kuwa, kile Anachohitaji wao kufanya, namna Anavyohitaji wao kuishi, na vile Anavyowahitaji kuweza kukamilisha kutimia kwa mapenzi ya Mungu. Je, mambo haya hayawezi kutenganishwa na kiini cha Mungu? Kwa maneno mengine, Mungu huwasilisha mbele tabia Yake na chote Alicho nacho na alicho wakati huohuo Akimtolea madai binadamu. Hakuna uongo, hakuna kusingizia, hakuna ufichaji, na wala hakuna kupiga chuku. Ilhali kwa nini binadamu hawezi kujua na kwa nini hajawahi kuweza kutambua waziwazi tabia ya Mungu? Na kwa nini hajawahi kutambua mapenzi ya Mungu? Kile ambacho kimefichuliwa na kuwasilishwa mbele na Mungu ndicho kile Mungu anacho Mwenyewe na maana yake, na kinaonyesha kila kipengele cha tabia Yake ya kweli—hivyo kwa nini binadamu hawezi kuona? Kwa nini binadamu hana uwezo wa kuwa na maarifa ya kina? Kunayo sababu muhimu ya haya. Na sababu yenyewe ni ipi? Tangu wakati wa uumbaji, binadamu hajawahi kumchukulia Mungu kama Mungu. Kwenye nyakati zile za mwanzo kabisa, haikujalisha ni nini Mungu alifanya kuhusiana na binadamu, yule binadamu ambaye ndiye tu alikuwa ameumbwa, binadamu alimchukulia yeye kuwa mwandani wake tu na wala si zaidi ya hapo, kama mtu wa kutegemewa, na hakuwa na maarifa yoyote wala uelewa wa Mungu. Hivi ni kusema, hakujua kwamba kile kilichowasilishwa mbele na Kiumbe huyu—Kiumbe huyu ambaye yeye alitegemea na kumwona kuwa mwandani wake—alikuwa kiini cha Mungu, na wala hakujua kwamba Kiumbe huyu ndiye anayetawala viumbe wote. Nikisema kwa urahisi, watu wa wakati huo hawakuwa na maarifa hata kidogo kumhusu Mungu. Hawakujua kwamba mbingu na nchi na mambo yote yalikuwa yameumbwa na Yeye na wala hawakujua ni wapi Alipotokea, na, zaidi hawakujua Yeye Alikuwa nani. Bila shaka, wakati huo Mungu hakumhitaji binadamu kumjua Yeye au kumfahamu Yeye au kuelewa kila kitu Alichofanya, au kufahamishwa kuhusu mapenzi Yake, kwani hizi zilikuwa nyakati za mapema zaidi baada ya uumbwaji wa wanadamu. Wakati Mungu alipoanza matayarisho ya kazi ya Enzi ya Sheria, Mungu alifanya mambo fulani kwa binadamu na pia Akaanza kutolea binadamu madai fulani, Akimwambia namna ya kutolea Mungu sadaka na namna ya kumwabudu. Ni wakati huo ndipo binadamu alipopata mawazo machache mepesi kuhusu Mungu, ni hapo tu ndipo alipojua tofauti kati ya binadamu na Mungu na kwamba Mungu Ndiye aliyewaumba wanadamu. Wakati binadamu alipojua kwamba Mungu alikuwa Mungu na binadamu alikuwa binadamu kukawa umbali fulani kati ya Yeye na Mungu, bado Mungu hakuhitaji kwamba binadamu awe na maarifa makuu au uelewa wa kina kumhusu Yeye. Hivyo basi, Mungu anayatoa mahitaji tofauti kwa binadamu kutokana na awamu na hali za kazi Yake. Mnaona nini katika haya? Ni kipengele kipi cha tabia ya Mungu unayoitambua? Je, Mungu ni wa kweli? Yale mahitaji ambayo Mungu anampa binadamu yanastahili? Kwenye nyakati za mapema kabisa kufuatia uumbaji wa wanadamu na Mungu, wakati ambao Mungu alikuwa bado hajatekeleza kazi ya ushindi na utimilifu wa binadamu, na Alikuwa hata bado hajaongea yale maneno mengi sana kwake, Alihitaji kidogo sana kutoka kwa binadamu. Licha ya kile ambacho binadamu alifanya na namna alivyotenda—hata kama alifanya mambo fulani yaliyomkosea Mungu—Mungu alimsamehe hayo yote, na akayapuuza. Kwa sababu Mungu Alijua kile Alichokuwa Amempa binadamu, na Alijua kile kilichokuwa ndani ya binadamu, basi Alijua kiwango cha mahitaji ambayo anafaa kudai kutoka kwa binadamu. Ingawaje kiwango cha mahitaji Yake kilikuwa cha chini sana wakati huo, hii haimaanishi kwamba tabia Yake haikuwa kuu, au kwamba hekima na uweza Wake yalikuwa si yoyote ila maneno matupu. Kwa binadamu, kunayo njia moja tu ya kujua tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe: kwa kufuata hatua za kazi ya usimamizi ya Mungu na wokovu wa wanadamu, na kuyakubali maneno ambayo Mungu anaongea akiyaelekeza kwa wanadamu. Kujua kile Mungu anacho na alicho, na kujua tabia ya Mungu, bado binadamu angemuuliza Mungu kumwonyesha nafsi Yake halisi? Binadamu hatafanya hivyo, na hathubutu kufanya hivyo, kwa kuweza kuifahamu tabia ya Mungu na kile Anacho na alicho, tayari binadamu atakuwa amemwona Mungu Mwenyewe wa kweli, na atakuwa tayari ameona nafsi Yake halisi. Haya ndiyo matokeo yasiyoepukika.

Kazi na mpango wa Mungu ulipokuwa ukiendelea mbele bila kusia, na baada ya Mungu kuanzisha agano la upinde wa mvua na binadamu kama ishara kwamba Hangewahi tena kuuangamiza ulimwengu kwa kutumia gharika, Mungu alikuwa na tamanio lililokuwa likiongezeka na kumsukuma kuwapata wale ambao wangeweza kuwa katika akili moja na Yeye. Hivyo, pia, Alikuwa na tamanio la haraka zaidi la kupata wale waliokuwa na uwezo wa kufanya mapenzi Yake duniani, na, isitoshe, kupata kundi la watu ambao wangeweza kuwa huru dhidi ya nguvu za giza, na kutoweza kuwa watumwa wa Shetani, na kuweza kuwa na ushuhuda kwake Yeye duniani. Kupata kundi la watu kama hawa kulikuwa ni tamanio la Mungu kwa muda mrefu, Alichokuwa akisubiria tangu wakati wa uumbaji. Hivyo basi, licha ya matumizi ya gharika na Mungu ili kuuangamiza ulimwengu, au agano Lake na binadamu, mapenzi ya Mungu, hali yake ya akili, mpango, na matumaini yote yalibakia yaleyale. Kile Alichotaka kufanya, ambacho Alikuwa ametamani kwa muda mrefu kabla ya uumbaji, kilikuwa kupata wale walio miongoni mwa wanadamu ambao Alitamani kuwapata—Kupata watu wa kundi hili ambao walioweza kufahamu na kujua tabia Yake, na kuyaelewa mapenzi Yake, kundi ambalo lingeweza kumwabudu Yeye. Watu kwenye kundi kama hili wanaweza kweli kuwa na ushuhuda kwake, na wao ndio, yaweza kusemekana, wasiri Wake.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp