Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatua Tatu za Kazi | Dondoo 43

06/10/2020

Wakati Yesu Alikuja kufanya kazi yake, ilikuwa ni kwa uongozi wa Roho Mtakatifu; Yeye Alitenda vile ambavyo Roho Mtakatifu Alitaka, na haikuwa kwa mujibu wa Enzi ya sheria ya Agano la Kale ama kwa mujibu wa kazi ya Yehova. Ingawa kazi ambayo Yesu Alikuja kufanya haikuambatana na sheria za Yehova ama amri za Yehova, chanzo chao kilikuwa sawa. Kazi ambayo Yesu Alifanya iliwakilisha jina la Yesu, na iliwakilisha Enzi ya Neema; kazi iliyofanywa na Yehova, iliwakilisha Yehova, na iliwakilisha Enzi ya Sheria. Kazi yao ilikuwa kazi ya Roho mmoja katika enzi tofauti. Kazi ambayo Yesu Alifanya ingeweza tu kuwakilisha Enzi ya Neema, na kazi ambayo Yehova Alifanya ingeweza tu kuwakilisha Enzi ya Sheria ya Agano la Kale. Yehova Aliwaongoza tu watu wa Israeli na Misri, na mataifa yote nje ya Israeli. Kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema ya Agano Jipya ilikuwa kazi ya Mungu katika jina la Yesu kwa kuwa Yesu ndiye Aliongoza enzi hii. Iwapo utasema kuwa kazi ya Yesu ilikuwa kwa msingi wa kazi ya Yehova, na kuwa hakufanya kazi yoyote mpya, na kuwa yote Aliyofanya ilikuwa kwa mujibu wa maneno ya Yehova, kulingana na kazi ya Yehova na unabii wa Isaya, basi Yesu hakuwa Mungu Aliyekuwa katika mwili. Kama Alitekeleza kazi yake kwa njia hii, basi Yeye Alikuwa mtume au mfanyikazi wa Enzi ya Sheria. Iwapo ni kama unavyosema, basi Yesu hangeweza kuzindua enzi, wala hangeweza kufanya kazi nyingine. Kwa njia hiyo hiyo, Roho Mtakatifu ni sharti afanye kazi Yake hasa kupitia kwa Yehova, na isipokuwa kupitia kwa Yehova Roho Mtakatifu hangeweza kufanya kazi yoyote mpya. Mwanadamu amekosea kwa kuona kazi ya Yesu kwa njia hii. Kama mwanadamu anaamini kwamba kazi iliyofanywa na Yesu ilifanywa inaambatana na maneno ya Yehova na unabii wa Isaya, basi, je, Yesu Alikuwa Mungu Aliyepata mwili, au Yeye Alikuwa nabii? Kwa mujibu wa mtazamo huu, hakukuwa na Enzi ya Neema, na Yesu hakuwa Mungu Aliyepata mwili, kwa kuwa kazi ambayo Alifanya haingeweza kuwakilisha Enzi ya Neema na ingewakilisha tu Enzi ya Sheria ya Agano la Kale. Kungekuwepo tu na enzi mpya wakati Yesu Alikuja kufanya kazi mpya, Alipozindua enzi mpya, na kupenya katika kazi iliyokuwa imefanyika hapo awali katika nchi ya Israeli, na hakufanya kazi yake kwa mujibu wa kazi iliyofanywa na Yehova huko Israeli, hakuzingatia sheria Yake ya zamani, na hakufuata kanuni zozote, na Alifanya kazi mpya ambayo Alitakiwa kufanya. Mungu Mwenyewe anakuja kuzindua enzi, na Mungu mwenyewe huja kuleta enzi kwenye kikomo. Mwanadamu hana uwezo wa kufanya kazi ya kuanzisha enzi hiyo na kuhitimisha enzi. Kama Yesu hakuleta kazi ya Yehova kwenye kikomo baada ya Yeye kuja, basi hio inadhihirisha ya kwamba Yeye Alikuwa tu mwanadamu, na hakuwakilisha Mungu. Kwa usahihi kwa sababu Yesu Alikuja na kuhitimisha kazi ya Yehova, Akaendeleza kazi ya Yehova na, aidha, Akatekeleza kazi Yake, kazi mpya, inathibitisha kuwa hii ilikuwa enzi mpya, na kwamba Yesu alikuwa Mungu Mwenyewe. Walifanya kazi katika awamu mbili zinazotofautiana. Awamu moja ilifanyika katika hekalu, na hiyo nyingine ilifanyika nje ya hekalu. Awamu moja ilikuwa ya kuongoza maisha ya mwanadamu kwa mujibu wa sheria, na awamu nyingine ilikuwa ya kutoa kafara ya dhambi. Awamu hizi mbili za kazi bila shaka zilikuwa tofauti; huu ni mgawanyiko wa enzi ya zamani na enzi mpya, na hakuna kosa kusema kuwa hizo ni enzi mbili! Maeneo ya kazi yao yalikuwa tofauti, na kiini cha kazi yao kilikuwa tofauti, na lengo la kazi yao lilikuwa tofauti. Kwa hivyo, enzi hizi zinaweza kugawanywa kwa awamu mbili: Agano la Kale na Jipya, ambayo ni kusema, enzi mpya na ya zamani. Yesu alipokuja hakuenda katika hekalu, ambayo inathibitisha kwamba enzi ya Yehova ilikuwa imeisha. Hakuingia hekaluni kwa sababu kazi ya Yehova katika hekalu ilikuwa imekamilika, na haikuhitajika kufanywa tena, na kwa hiyo kuifanya tena kungekuwa kuirudia. Kwa kuondoka tu hekaluni, kuanza kazi mpya na kuzindua njia mpya nje ya hekalu, ndio Aliweza kuifikisha kazi ya Mungu kwa upeo wake. Kama Hangeenda nje ya hekalu kufanya kazi Yake, kazi ya Mungu haingeweza kamwe kuendelea mbele kupita hekalu, na hakungekuwa na mabadiliko yoyote mapya. Na kwa hiyo, Yesu Alipokuja, Hakuingia hekaluni, na Hakufanya kazi Yake hekaluni. Alifanya kazi Yake nje ya hekalu, na Akafanya kazi Yake kwa uhuru Akiandamana na wanafunzi. Kuondoka kwa Mungu katika hekalu kufanya kazi Yake kulikuwa na maana kwamba Mungu alikuwa na mpango mpya. Kazi Yake ilikuwa ifanyike nje ya hekalu, na ilikuwa iwe kazi mpya ambayo haingezuiliwa kwa njia ya utekelezaji wake. Kuwasili kwa Yesu kulimaliza kazi ya Yehova ya wakati wa Agano la Kale. Ingawa ziliitwa kwa majina mawili tofauti, awamu zote mbili za kazi zilifanywa na Roho mmoja, na kazi ya pili ilikuwa mwendelezo wa kazi ya kwanza. Kwa kuwa jina lilikuwa tofauti, na kiini cha kazi kilikuwa tofauti, basi enzi ilikuwa tofauti. Wakati Yehova Alikuja, hiyo ilikuwa enzi ya Yehova, na wakati Yesu Alikuja, hiyo ilikuwa enzi ya Yesu. Na kwa hivyo, kila wakati Mungu Anapokuja, anaitwa kwa jina moja, Yeye anawakilisha enzi moja, na Yeye anazindua njia mpya; na kwa kila njia mpya, Yeye huchukua jina jipya, ambalo inaonyesha kuwa Mungu daima ni mpya na wala si wa zamani, na ya kwamba kazi yake daima inasonga mbele. Historia inasonga mbele daima, na kazi ya Mungu inasonga mbele daima. Ili mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita ufike upeo wake, lazima uendelee kusonga mbele. Kila siku ni sharti Yeye afanye kazi mpya, kila mwaka lazima Yeye afanye kazi mpya, ni sharti Yeye azindue njia mpya, azindue enzi mpya, aanzishe kazi mpya na kubwa zaidi, na ni sharti alete majina mapya na kazi mpya.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp