Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 32

Mungu Amwahidi Ibrahimu Mwana

Mwa 17:15-17 Naye Mungu akasema kwake Ibrahimu, na kuhusu Sarai mke wako, hutamwita kwa jina lake la Sarai, kwa maana sara ndilo litakuwa jina lake. Na mimi nitambariki yeye, na pia nitakupa mwana kutoka kwake: ndiyo, nitambariki yeye, na yeye atakuwa mama yao mataifa; wafalme wa watu watatoka kwa yeye. Kisha Ibrahimu akaanguka chini kifudifudi, na kucheka, na akasema moyoni, Je, mtoto atazaliwa kwa mtu mwenye umri wa miaka mia moja? naye Sara, aliye na umri wa miaka tisini, atazaa?

Mwa 17:21-22 Lakini nitaliimarisha agano langu na Isaka, ambaye Sara atakuzalia wewe wakati kama huu mwaka ujao. Naye akakoma kuzungumza na yeye, na Mungu akapanda juu kutoka kwa Ibrahimu.

Hakuna Awezaye Kuzuia Kazi Ambayo Mungu Anaamua Kufanya

Hivyo, muda mfupi uliopita nyote mmesikia hadithi ya Ibrahimu. Alichaguliwa na Mungu baada ya gharika kuuangamiza ulimwengu, jina lake lilikuwa Ibrahimu, na alipokuwa na miaka mia moja, na mke wake Sara akiwa na umri wa miaka tisini, ahadi ya Mungu ilimjia. Mungu alimwahidi nini? Mungu alimwahidi kile ambacho kinarejelewa katika Maandiko: “Na mimi nitambariki yeye, na pia nitakupa mwana kutoka kwake.” Ni maelezo yapi yalitangulia ahadi ya Mungu ya kumpa mtoto? Maandiko yanaelezea yafuatayo: “Kisha Ibrahimu akaanguka chini kifudifudi, na kucheka, na akasema moyoni, Je, mtoto atazaliwa kwa mtu mwenye umri wa miaka mia moja? naye Sara, aliye na umri wa miaka tisini, atazaa?” Kwa maneno mengine wanandoa hawa wazee walikuwa na umri mwingi sana wa kupata watoto. Naye Ibrahimu alifanya nini baada ya Mungu Kumwahidi? Aliuangukia uso wake akicheka, na kujiambia, “Je, mtoto atazaliwa kwa mtu mwenye umri wa miaka mia moja?” Ibrahimu aliamini kwamba haikuwezekana—hivi alimaanisha kwamba alisadiki ahadi ya Mungu kwake haikuwa chochote ila mzaha. Kutoka mtazamo wa binadamu, ahadi isingeweza kutimizika na binadamu, na vilevile isingeweza kutimizika na Mungu na ilikuwa haiwezekani kwa Mungu. Pengine, kwa Ibrahimu, ahadi hii ilikuwa ya kuchekesha. Mungu alimuumba binadamu, lakini yaonekana kwamba hajui kwamba mtu aliyezeeka sana hawezi kupata watoto; Anafikiria kwamba Anaweza kuniruhusu kupata mtoto, Anasema kwamba atanipa mtoto—kwa kweli hilo haliwezekani! Na hivyo, Ibrahimu akaangukia uso wake na kucheka, akijifikiria yeye mwenyewe: Haiwezekani—Mungu anafanya mzaha na mimi, hili haliwezi kuwa kweli. Hakutilia maanani maneno yake Mungu. Hivyo, katika macho ya Mungu, Ibrahimu alikuwa binadamu wa aina gani? (Mwenye haki.) Ni wapi ulipojifunza kwamba alikuwa mwenye haki? Ninyi mnafikiria kwamba wale wote ambao Mungu anawaita ni wenye haki, na watimilifu, na watu wanaotembea na Mungu. Wewe unashikilia mafundisho ya dini! Lazima uone waziwazi kwamba wakati Mungu anapomfasili mtu, Hafanyi hivyo kiholela. Hapa, Mungu hakusema kwamba Ibrahimu alikuwa mwenye haki. Katika moyo Wake, Mungu anavyo viwango vya kupima kila mtu. Ingawaje Mungu hakusema ni mtu wa aina gani ambaye Ibrahimu alikuwa, kwa mujibu wa mwenendo wake, Ibrahimu alikuwa na imani ya aina gani kwake Mungu? Ilikuwa ya kidhahania kidogo? Au alikuwa mwenye imani kuu? La, hakuwa! Kicheko na fikira zake zilionyesha yeye alikuwa nani, hivyo imani yenu kwamba alikuwa mwenye haki ni ndoto ya kufikiria kwenu, ni matumizi yasiyo na mwelekeo ya mafundisho ya dini, usiopaswa. Je, Mungu alikiona kicheko cha Ibrahimu na maonyesho yake madogo, Alijua kuyahusu? Mungu alijua. Lakini Mungu angebadilisha kile Alichokuwa ameamua kufanya? La! Wakati Mungu alipopangilia na kuamua kwamba Angemchagua binadamu huyu, suala hilo lilikuwa tayari limekamilishwa. Si fikira za binadamu wala mwenendo wake ungemshawishi au kuhitilafiana na Mungu hata chembe; Mungu Asingebadilisha kiholela mpango Wake, wala Asingebadilisha au kuharibu mpango Wake kwa sababu ya mwenendo wa binadamu, hali ambayo ingekuwa ujinga. Nini, basi, kimeandikwa katika Mwanzo 17:21-22? “Lakini nitaliimarisha agano langu na Isaka, ambaye Sara atakuzalia wewe wakati kama huu mwaka ujao. Naye akakoma kuzungumza na yeye, na Mungu akapanda juu kutoka kwa Ibrahimu.” Mungu hakutilia maanani hata chembe kile Ibrahimu alichofikiria au kusema. Na sababu ya kutotilia maanani Kwake ni gani? Kutotilia maanani kwake kulikuwa kwa sababu, wakati huo Mungu hakuhitaji kwamba mwanadamu awe mwenye imani kuu au kwamba aweze kuwa na maarifa makuu kuhusu Mungu, au, vilevile, aweze kuelewa kile kilichofanywa na kusemwa na Mungu. Hivyo, hakuhitaji kwamba binadamu aelewe kabisa kile Alichoamua kufanya, au watu Alioamua kuchagua, au kanuni za vitendo Vyake, kwani kimo cha binadamu hakikutosha tu. Wakati huo, Mungu alichukulia kile ambacho Ibrahimu alifanya na vyovyote alivyojiendesha yeye mwenyewe kuwa kawaida. Hakushutumu, au kukemea, lakini alisema tu: “Sara atakuzalia Isaka wakati huu uliopangwa mwaka ujao.” Kwa Mungu, baada Yake kuyatangaza maneno haya, suala hili hatimaye lilikuwa kweli hatua kwa hatua; katika macho ya Mungu, kile ambacho kilikuwa kikamilishwe na mpango Wake kilikuwa tayari kimetimizwa. Baada ya kuikamilisha mipangilio ya hayo, Mungu aliondoka. Kile binadamu hufanya au kufikiria, kile binadamu huelewa, mipango ya binadamu—hakuna chochote kati ya hivi vyote kinacho uhusiano wowote na Mungu. Kila kitu hufanyika kulingana na mpango wa Mungu, kikiendana na nyakati na awamu zilizowekwa na Mungu. Hivyo ndivyo kanuni ya kazi ya Mungu inavyoenda. Mungu haingilii kati chochote kile binadamu anafikiria au kujua, ilhali Haachi mpango Wake, wala kuacha kazi Yake kwa sababu binadamu hasadiki wala kuelewa. Kweli hizi hivyo basi zinakamilishwa kulingana na mpango na fikira za Mungu. Hivi ndivyo hasa tunavyoona kwenye Bibilia: Mungu Alisababisha Isaka kuzaliwa wakati ule Aliokuwa amepanga. Je, kweli zinathibitisha kwamba tabia na mwenendo wa binadamu vilizuia kazi ya Mungu? Havikuzuia kazi ya Mungu! Je, imani ndogo ya binadamu kwa Mungu, na dhana zake na fikira kumhusu Mungu viliweza kuathiri kazi ya Mungu? La, havikuathiri! Hata kidogo! Mpango wa usimamizi wa Mungu hauathiriwi na binadamu, suala, au mazingira yoyote. Kila kitu Anachoamua kufanya kitakamilika na kukamilishwa kwa wakati na kulingana na mpango Wake, na kazi Yake haiwezi kutatizwa na binadamu yeyote. Mungu hupuuza vipengele fulani vya ujinga na kutojua kwa binadamu, na hata upinzani na dhana fulani za binadamu Kwake, Akifanya kazi ambayo lazima Afanye bila ya kujali. Hii ni tabia ya Mungu na ni onyesho la kudura Yake.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp