Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 44

Shetani Amjaribu Ayubu Mara Nyingine Tena (Majipu Mabaya Yaupiga Mwili wa Ayubu)

a. Maneno Yaliyotamkwa na Mungu

Ayubu 2:3 Naye Yehova akasema kwa Shetani, je, umemfikiria mtumishi wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu? Na bado anashikilia ukamilifu wake, ingawa ulinichochea dhidi yake, ili mimi nimwangamize bila sababu.

Ayubu 2:6 Naye Yehova akasema kwa Shetani, Tazama, yeye yuko katika mkono wako; lakini uuhifadhi uhai wake.

b. Maneno Yaliyotamkwa na Shetani

Ayubu 2:4-5 Naye Shetani akamjibu Yehova, na akasema, Ngozi kwa ngozi, ndiyo, yote ambayo mtu anayo atayatoa kwa sababu ya uhai wake. Lakini nyosha mbele mkono wako sasa, na uguse mfupa wake na nyama yake, na yeye atakulaani mbele ya uso wako.

Katikati ya Mateso makuu, Ayubu Anatambua kwa kweli Utunzaji wa Mungu wa Wanadamu

Kufuatia maswali ya Yehova Mungu kwa Shetani, Shetani alifurahi kisirisiri. Kwa sababu Shetani alijua kwamba angeweza kwa mara nyingine kuruhusiwa kumshambulia mtu aliyekuwa mtimilifu katika macho ya Mungu—jambo ambalo kwa Shetani lilikuwa fursa ya nadra. Shetani alitaka kutumia fursa hii kudhalilisha kabisa kujitolea kwa Ayubu kumfanya kupoteza imani yake kwa Mungu na hivyo basi kutomcha Mungu tena au kubariki jina la Yehova Mungu. Hali hii ingempa Shetani fursa: Haijalishi ni wapi au ni muda gani, angeweza kumfanya Ayubu kuwa kikaragosi cha kufuata amri zake. Shetani alificha njama zake za maovu bila kuacha alama, lakini hakuweza kudhibiti asili yake ya maovu. Ukweli huu unaashiriwa kupitia kwa majibu yake kwa maneno ya Yehova Mungu, kama yalivyorekodiwa kwenye maandiko. “Naye Shetani akamjibu Yehova, na akasema, Ngozi kwa ngozi, ndiyo, yote ambayo mtu anayo atayatoa kwa sababu ya uhai wake. Lakini nyosha mbele mkono wako sasa, na uguse mfupa wake na nyama yake, na yeye atakulaani mbele ya uso wako” (Ayubu 2:4-5). Haiwezekani kutopata maarifa makuu na hali ya kuonea kijicho ya Shetani kutokana na mabadilishano haya kati ya Mungu na Shetani. Baada ya kusikia uongo huu wa Shetani, wale wote wanaoupenda ukweli na kuchukia uovu bila shaka watakuwa na chuki kubwa zaidi kwa utwezo na kutokuwa na aibu kwa Shetani, watahisi wakiwa wametishika na kusinyika kutokana na uongo wa Shetani, na, wakati huohuo, watatoa maombi yao ya kina na heri zao za dhati kwa Ayubu, wakiomba kwamba binadamu huyu mwenye unyofu ataweza kutimiza utimilifu wake, wakitamani kwamba binadamu huyu anayemcha Mungu na kujiepusha na maovu aweze kushinda milele majaribio ya Shetani, na kuishi kwa mwangaza, na kuishi katikati ya mwongozo na baraka za Mungu, hivyo, pia ndivyo watakavyotaka matendo ya haki ya Ayubu yaweze milele kuenea na kuhimiza wale wanaofuatilia njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Ingawaje nia ya kijicho ya Shetani inaweza kuonekana kupitia kwa tangazo hili, Mungu alikubali kwa urahisi “ombi” la Shetani—lakini alikuwa pia na sharti moja: “yeye yuko katika mkono wako; lakini uuhifadhi uhai wake” (Ayubu 2:6). Kwa sababu, wakati huu, Shetani aliomba kunyosha mbele mkono wake ili kudhuru mwili na mifupa ya Ayubu, Mungu Alisema, “lakini okoa maisha yake.” Maana ya maneno haya ni kwamba alimpa Shetani mwili wa Ayubu, lakini Akabakiza maisha yake. Shetani asingeweza kuyachukua maisha ya Ayubu, lakini isipokuwa haya angeweza kutumia njia au mbinu zozote dhidi ya Ayubu.

Baada ya kupata ruhusa kutoka kwa Mungu, Shetani alimkimbilia Ayubu na kunyosha mbele mkono wake ili kuathiri ngozi yake na akamsababishia majipu mabaya yaliyoupiga mwili wake wote, naye Ayubu akahisi maumivu kwenye ngozi yake. Ayubu aliyasifu maajabu na utakatifu wa Yehova Mungu, jambo ambalo lilimfanya Shetani hata kuwa wazi zaidi katika ufidhuli wake. Kwa sababu alikuwa amehisi furaha ya kumwumiza binadamu, Shetani aliunyosha mkono wake na akakwaruza nyama ya Ayubu, na kusababisha majipu yake mabaya kutunga usaha. Mara moja Ayubu alihisi maumivu na mateso kwenye mwili wake ambayo hayakuwa na kifani, na asingeweza kujisaidia kwa vyovyote vile isipokuwa kujikanda yeye mwenyewe kutoka kwenye kichwa hadi miguu akitumia mikono yake, ni kana kwamba kufanya hivi kungetuliza balaa ile iliyofanyikia roho yake kutokana na maumivu haya ya nyama za mwili wake. Alitambua kwamba Mungu Alikuwa kando yake akimwangalia, na akajaribu kwa njia bora zaidi kujituliza. Kwa mara nyingine alipiga magoti kwenye ardhi, na kusema: Unaangalia ndani ya binadamu, unauona umaskini wake; kwa nini unyonge wake unakuhusu wewe? Jina la Yehova Mungu lisifiwe. Shetani aliyaona yale maumivu yasiyovumilika ya Ayubu, lakini hakumwona Ayubu akiliacha neno la Yehova Mungu. Hivyo aliunyoosha mkono wake haraka mbele ili kudhuru mifupa ya Ayubu, akiwa na tamaa ya kudhuru kila kiungo cha mwili wake. Mara, Ayubu akahisi mateso asiyoyatarajia; ni kana kwamba mwili wake ulikuwa umepasuliwa katikati kutoka kwenye mifupa, na kana kwamba mifupa yake ilikuwa ikipasuliwa kipande hadi kipande. Mateso haya ya kuumiza yalimfanya akafikiria afadhali basi afe…. uwezo wake wa kuvumilia ulikuwa umefikia kilele…. Alitaka kulia kwa sauti, alitaka kuirarua ngozi kwenye mwili wake ili kupunguza maumivu—lakini alishikilia mayowe yake, na hakuirarua ngozi yake kutoka kwenye mwili wake, kwani hakutaka Shetani auone udhaifu wake. Na hivyo alipiga magoti chini kwa mara nyingine, lakini wakati huu hakuhisi uwepo wa Yehova Mungu. Alijua kwamba mara nyingi alikuwa mbele yake, na nyuma yake, na upande wake. Lakini kwenye maumivu haya, Mungu alikuwa hajawahi kuyatazama; Aliufunika uso wake na Akawa Amefichwa, kwa maana uumbaji wake wa binadamu haukuwa wa kumletea mateso binadamu. Wakati huu, Ayubu alikuwa akilia, na akijaribu kwa njia bora zaidi kuvumilia maumivu yake ya kimwili, lakini asingeweza kujizuia tena dhidi ya kutoa shukrani kwa Mungu: Binadamu aanguka kwa mpigo wa kwanza, yeye ni myonge na asiye na nguvu, yeye ni mchanga na asiyejua—kwa nini ukataka kumtunza na kuwa mzuri kwake yeye? Unanipiga, ilhali inakuumiza kufanya hivyo. Ni nini cha binadamu kinastahili utunzaji na kujali Kwako? Maombi ya Ayubu yalifikia masikio ya Mungu, na ya Mungu Alikuwa kimya, Akitazama tu bila kutoa sauti…. Akiwa amejaribu kila ujanja kwenye kitabu bila mafanikio, Shetani aliondoka kimyakimya, lakini haya hayakufikisha hadi tamati majaribio ya Ayubu kutoka kwa Mungu. Kwa sababu nguvu za Mungu zilizokuwa zimefichuliwa ndani ya Ayubu zilikuwa hazijajulikana kwa umma, hadithi ya Ayubu haikuishia pale ambapo Shetani alijiondoa. Huku wahusika wengine wakiingia katika tukio hilo, matukio mengine ya ajabu zaidi yalikuwa yaje.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp