Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 45

Maonyesho Mengine ya Kumcha Mungu na Kujiepusha na Maovu kwa Ayubu ni Kutukuza Kwake Jina la Mungu Katika Mambo Yote

Ayubu alikuwa ameteseka kutokana na maudhi ya Shetani, lakini bado hakuliacha jina la Yehova Mungu. Mke wake ndiye aliyekuwa wa kwanza kujiondoa na kuendeleza wajibu wa Shetani unaoweza kuonekana kwa kumshambulia Ayubu. Maandishi asilia yanafafanua hali hii hivyo basi: “Kisha mkewe akasema kwake, Je, Wewe bado unabaki na ukamilifu wako? mlaani Mungu, ufe” (Ayubu 2:9). Haya yalikuwa maneno yaliyozungumzwa na Shetani akisingizia kuwa binadamu. Yalikuwa ni shambulizi, na shtaka, pamoja na kichocheo, jaribio, na matusi. Baada ya kushindwa kushambulia mwili wa Ayubu, Shetani sasa alishambulia moja kwa moja uadilifu wa Ayubu, akitaka kutumia jambo hili kumfanya Ayubu kutupilia mbali uadilifu wake, kumwacha Mungu, na kusita kuishi. Hivyo, pia, ndivyo Shetani alivyotaka kutumia maneno kama hayo kumjaribu Ayubu: Kama Ayubu angeacha jina la Yehova Mungu, asingelazimika kuvumilia mateso kama hayo, angejiondolea mateso ya mwili. Akiwa amekabiliwa na ushauri wa mke wake, Ayubu alimkosoa kwa kusema, “Wewe unazungumza mithili ya mmoja wa wanawake walio wapumbavu wanavyozungumza. Ati? tupokee mema kutoka mkononi mwa Mungu, nasi tusipokee mabaya?” (Ayubu 2:10). Ayubu alikuwa amejua kwa muda mrefu maneno haya, lakini wakati huu ukweli wa maarifa ya Ayubu kuhusu maneno haya ulikuwa umethibitishwa.

Wakati mke wake alimshauri kulaani Mungu na kufa, maana yake ilikuwa: Mungu wako anakushughulikia hivi, kwa hivyo kwa nini usimlaani yeye? Kama ungali hai unafanya nini? Mungu wako hakufanyii haki, na ilhali ungali unabariki jina la Yehova Mungu. Angekuleteaje janga hili huku unabariki jina Lake? Harakisha na uliache jina la Mungu, na usimfuate yeye tena. Kwa njia hii matatizo yako yataisha. Kwa wakati huu, ushuhuda ulitolewa ambao Mungu alitaka kuuona kwa Ayubu. Hakuna mtu yeyote wa kawaida ambaye angeweza kuwa na ushuhuda huu, wala hatuusomi katika mojawapo ya hadithi za Biblia—lakini Mungu Alikuwa ameuona kabla hata Ayubu kuongea maneno haya. Mungu Alitaka tu kutumia fursa hii kumruhusu Ayubu kuthibitisha kwa wote kwamba Mungu alikuwa sahihi. Akiwa amekabiliwa na ushauri wa mke wake, Ayubu hakutupilia tu mbali uadilifu wake au kumuacha Mungu, bali pia alimwambia mke wake: “Tupokee mema kutoka mkononi mwa Mungu, nasi tusipokee mabaya?” Je, maneno haya yanao uzito mkuu? Hapa, kunayo ukweli mmoja tu unaoweza kuthibitisha uzito wa maneno haya. Uzito wa maneno haya ni kwamba yameidhinishwa na Mungu ndani ya moyo Wake, ndiyo yale yaliyotamaniwa na Mungu, ndiyo yale Mungu Alitaka kusikia, na ndiyo matokeo ambayo Mungu Alitamani kuona; maneno haya ndiyo pia kiini cha ushuhuda wa Ayubu. Katika haya, utimilifu, unyofu, kumcha Mungu, kujiepusha na maovu kwa Ayubu kulithibitishwa. Thamani ya Ayubu ilikuwa namna ambavyo, alipojaribiwa, na hata wakati mwili wake mzima ulikuwa umefunikwa na majipu mabaya, alipovumilia mateso ya kiwango cha juu zaidi, na wakati mke na watu wake wa ukoo walipomshauri, bado aliyatamka maneno hayo. Ili niweze kuiweka kwa njia nyingine, ndani ya moyo wake alisadiki kwamba, haijalishi ni kiasi kipi cha majaribio, au ni vipi ambavyo masaibu au mateso yalivyokuwa, hata kama kifo kingemjia, hangemuacha Mungu au kugeuka na kuacha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Unaona, basi, kwamba Mungu Alishikilia sehemu muhimu sana ndani ya moyo wake, na kwamba kulikuwa tu na Mungu moyoni mwake. Ni kwa sababu ya haya ndipo tunasoma ufafanuzi kama huo kuhusu yeye katika maandiko kama: Katika yote haya Ayubu hakutenda dhambi na midomo yake. Hakutenda dhambi kwa kutumia mdomo wake tu, lakini ndani ya moyo wake hakulalamika katu kuhusu Mungu. Hakusema maneno mabaya kuhusu Mungu, wala hakutenda dhambi dhidi ya Mungu. Kinywa chake hakikubariki tu jina la Mungu, lakini ndani ya moyo wake alibariki pia jina la Mungu; mdomo na moyo wake ulikuwa kitu kimoja. Huyu ndiye aliyekuwa Ayubu wa kweli aliyeonekana na Mungu, na hii ndiyo iliyokuwa sababu ya kweli kwa nini Mungu alimthamini sana Ayubu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp