Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 408

02/10/2020

Ikiwa unataka kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu, basi lazima moyo wako umgeukie Mungu. Hili likiwa msingi, pia utakuwa na uhusiano wa kawaida na watu wengine. Iwapo huna uhusiano wa kawaida na Mungu, basi haijalishi unachofanya kudumisha uhusiano wako na watu wengine, haijalishi jinsi gani unafanya kazi kwa bidii au ni nguvu kiasi gani unaweka ndani yake, bado ni ya falsafa ya mwanadamu ya maisha. Unadumisha nafasi yako miongoni mwa watu kupitia mtazamo wa mwanadamu na falsafa ya mwanadamu ili kwamba watu wakupe wewe sifa, lakini hufuati neno la Mungu ili kuanzisha uhusiano wa kawaida na watu. Iwapo huzingatii uhusiano wako na watu lakini unadumisha uhusiano wa kawaida na Mungu, ikiwa uko tayari kumpa Mungu moyo wako na ujifunze kumtii, basi kwa kawaida sana, uhusiano wako na watu wote utakuwa wa kawaida. Kwa njia hii, uhusiano huu haujengwi kwa mwili, bali juu ya msingi wa upendo wa Mungu. Kwa kiasi kikubwa hakuna ushirikiano uliojengwa juu ya mwili, lakini katika roho kuna ushirikiano na vilevile upendo, starehe, na kutoleana kwa wenza. Haya yote yanafanywa kwa msingi wa moyo unaomridhisha Mungu. Uhusiano huu haudumishwi kwa kutegemea falsafa ya mwanadamu ya maisha, bali unaundwa kwa kawaida kupitia mzigo wa Mungu. Hauhitaji jitihada zilizofanywa na binadamu. Unahitaji tu kutenda kulingana na maadili ya neno la Mungu. Je, unayo hiari ya kuwa mwenye kufikiria mapenzi ya Mungu? Je, uko tayari kuwa mtu “bila mantiki” mbele za Mungu? Je, uko tayari kuutoa moyo wako kwa Mungu kabisa, na kutofikiri kuhusu msimamo wako kati ya watu? Kati ya watu wote ambao una mawasiliano nao, ni gani ambao kati yao unayo mahusiano bora zaidi? Wepi kati yao ambao unayo mahusiano mabaya zaidi nao? Je, mahusiano yako na watu ni ya kawaida? Je, unawachukulia watu wote kwa usawa? Je, uhusiano wako na wengine umeimarishwa kwa mujibu wa falsafa yako ya maisha, ama umejengwa kwenye msingi wa upendo wa Mungu? Wakati mtu hautoi moyo wake kwa Mungu, basi roho yake inakuwa butu, inakufa ganzi na kutofahamu. Mtu wa aina hii kamwe hataelewa maneno ya Mungu na kamwe hatakuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu; tabia ya mtu wa aina hiikamwe haitabadilika. Kubadilisha tabia ya mtu ni mchakato wa mtu kuutoa kabisa moyo wake kwa Mungu, na wa kupokea nuru na mwangaza kutoka kwa maneno ya Mungu. Kazi ya Mungu inaweza, kumruhusu mtu kuingia kwa utendaji, na pia kumwezesha kuepuka masuala yake hasi baada ya kupata maarifa. Unapoweza kuutoa moyo wako kwa Mungu, utaweza kuhisi kila harakati yenye hila ndani ya roho yako, nawe utajua kila nuru na mwangaza upokelewao kutoka kwa Mungu. Shikilia hili, nawe utaingia katika njia ya kukamilishwa na Roho Mtakatifu hatua kwa hatua. Kadri moyo wako unavyoweza kuwa mtulivu mbele za Mungu, ndivyo roho yako itakavyokuwa makini zaidi na wa kutaka uangalifu mkubwa, na kadri roho yako itakavyoweza kutambua kuchochewa na Roho Mtakatifu, kisha uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida zaidi na zaidi. Uhusiano wa kawaida kati ya watu huundwa juu ya msingi wa kumpa Mungu mioyo yao haufanikishwi kupitia jitihada za binadamu. Bila Mungu mioyoni mwao, uhusiano kati ya watu ni uhusiano wa mwili tu. Sio uhusiano wa kawaida, lakini badala yake, ni utelekezaji kwa ajili ya tamaa za mwili. Ni uhusiano ambao Mungu anachukia, Asioupenda. Ukisema kuwa roho yako imeguzwa, lakini daima unataka kuwa na ushirika na watu wanaokupendeza, na wale unaowachukulia kwa hali ya juu, na iwapo kuna mtafutaji mwingine ambaye hakupendezi, ambaye huna upendeleo kwake na huwezi kujihusisha naye, huu ni ushahidi zaidi kuwa wewe uko chini ya hisia zako na kuwa huna uhusiano wa kawaida na Mungu kamwe. Unajaribu kumdanganya Mungu na kuficha ubaya wako mwenyewe. Hata ingawa unaweza kushirikisha uelewano kiasi lakini unabeba ubaya moyoni mwako, kila kitu unachofanya ni kizuri tu kwa kiwango cha mwanadamu. Mungu hatakusifu—unatenda kulingana na mwili, sio kulingana na mzigo wa Mungu. Iwapo unaweza kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu na kuwa na ushirikiano wa kawaida na wale wote wanaompenda Mungu, ni hapo tu ndipo utakuwa uko tayari kwa matumizi ya Mungu. Kwa njia hii, haijalishi jinsi unavyopatana na wengine, haitakuwa kulingana na falsafa ya maisha, lakini itakuwa kuishi mbele ya Mungu, kuufikiria mzigo Wake. Je, ni watu wangapi wa aina hii wapo miongoni mwenu? Je, mahusiano yako na watu wengine ni ya kawaida kweli? Yamejengwa katika msingi upi? Je, ni falsafa ngapi za maisha zimo ndani mwako? Je, zimetupiliwa mbali? Ikiwa moyo wako hauwezi kumgeukia Mungu kabisa, basi wewe si wa Mungu—unatoka kwa Shetani, na mwishowe utarudishwa kwa Shetani. Wewe hustahili kuwa mmoja wa watu wa Mungu. Yote haya yanahitaji kufikiria kwako kwa makini.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida na Mungu

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp