Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 49

Katika Maisha ya Kila Siku ya Ayubu Tunaona Utimilifu, Unyofu, Kumcha Mungu, na Kujiepusha na Maovu Kwake

Kama tutazungumzia Ayubu, basi lazima tuanze na namna ambavyo alitathminiwa kwa mujibu wa matamshi kutoka kwa kinywa cha Mungu mwenyewe: “hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu.”

Hebu kwanza tujifunze kuhusu utimilifu na unyofu wa Ayubu.

Unaelewa vipi maneno haya “utimilifu” na “unyofu”? Unasadiki kwamba Ayubu hakuwa na lawama, na kwamba aliheshimika? Hili, bila shaka, litakuwa ni ufasiri wa moja kwa moja na uelewa wa “mtimilifu” na “mnyofu.” Muhimu katika uelewa wa kweli wa Ayubu ni maisha halisi—maneno, vitabu, na nadharia pekee haviwezi kutupa majibu yoyote. Tutaanza na kuyaangalia maisha ya Ayubu ya nyumbani, kuangalia namna mwenendo wake wa kawaida ulivyokuwa maishani mwake. Kufanya hivi kutatwambia kuhusu kanuni na malengo yake maishani, pamoja na hulka yake na mambo yale aliyoyafuatilia. Sasa, hebu tuyasome maneno ya mwisho katika Ayubu 1:3: “mtu huyo alikuwa mkubwa zaidi kuwaliko watu wengine wote wa mashariki.” Kile ambacho maneno haya yanasema ni kwamba hadhi na heshima ya Ayubu ilikuwa ya juu sana, na ingawaje hatuambiwi kama alikuwa ndiye mkubwa zaidi kati ya wanaume wote wa mashariki kwa sababu ya wingi wa rasilimali zake au kwa sababu alikuwa mtimilifu na mnyofu, na kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu, kwa ujumla tunajua kwamba hadhi na heshima ya Ayubu vyote vilithaminiwa sana. Kama ilivyorekodiwa kwenye Biblia, picha za kwanza za Ayubu kwa watu zilikuwa kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu, kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu na kwamba alimiliki utajiri mkubwa na alikuwa na hadhi ya kuheshimika. Kwa mtu wa kawaida anayeishi katika mazingira kama haya na hali kama hizo, mlo wa Ayubu, ubora wa maisha, na vipengele mbalimbali vya maisha yake ya kibinafsi vyote vingekuwa malengo ya umakinifu wa watu wengi; hivyo lazima tuendelee kuyasoma maandiko: “Nao wana wake walienda na kufurahia karamu katika nyumba zao, kila kwa siku yake; na wao wakatuma na kuwaita ndugu zao wa kike watatu ili wakule na kunywa pamoja na wao. Na ilikuwa hivyo, wakati hizo siku zao za karamu ziliisha, Ayubu aliwatuma na kuwatakasa, na akaamka asubuhi mapema, na kutoa sadaka za kuteketezwa kulingana na hesabu yao wote; kwa sababu Ayubu alisema, Inaweza kuwa kwamba wana wangu wametenda dhambi, na kumlaani Mungu mioyoni mwao. Hivyo ndivyo Ayubu alivyofanya kila siku” (Ayubu 1:4-5). Kifungu hiki kinatuambia mambo mawili: Jambo la kwanza ni kwamba watoto wa kiume na wa kike wa Ayubu walishiriki kwenye karamu mara kwa mara, wakila na wakinywa; pili ni kwamba Ayubu mara kwa mara alitoa sadaka za kuteketezwa kwa sababu alikuwa na wasiwasi na wao, akiogopa kwamba walikuwa wakitenda dhambi, kwamba katika mioyo yao walikuwa wamemlaani Mungu. Katika maandiko haya maisha ya watu wa aina mbili tofauti yanafafanuliwa. Maisha ya kwanza, watoto wa kiume na kike wa Ayubu, mara nyingi walishiriki kwenye karamu kwa sababu ya ukwasi wao, waliishi kwa ubadhirifu, wakinywa na wakila hadi mioyo yao kutosheka, wakifurahia maisha ya kiwango cha juu yaliyoletwa na utajiri wa anasa. Wakiishi maisha kama haya, ilikuwa lazima kwamba mara kwa mara wangetenda dhambi na kumkosea Mungu—ilihali hawakujitakasa wala kutoa sadaka za kuteketezwa kutokana na hayo yote. Waona, basi, kwamba Mungu hakuwa na nafasi katika mioyo yao, kwamba hawakufikiria kuhusu neema za Mungu, wala kuogopa kumkosea Mungu, isitoshe hawakuogopa kumuacha Mungu katika mioyo yao. Bila shaka zingatio letu si watoto wa Ayubu, lakini ni kwa kile ambacho Ayubu alifanya alipokabiliwa na mambo kama haya; hili ndilo suala lile jingine lililofafanuliwa katika kifungu, na ambalo linahusisha maisha ya kila siku ya Ayubu na kiini cha ubinadamu wake. Wakati Biblia inapofafanua kushiriki kwa watoto wa kike na kiume katika karamu mbalimbali hakuna mahali ambapo Ayubu anatajwa; yasemekana tu kuwa ni watoto wake wa kiume na wa kike walio kula na kunywa pamoja. Kwa maneno mengine, hakuandaa karamu, wala hakujiunga na watoto wake wa kiume na kike katika karamu hizo ili kuendeleza ubadhirifu. Ingawaje alikuwa tajiri, na alimiliki raslimali nyingi na watumishi wengi, maisha ya Ayubu hayakuwa ya anasa. Hakudanganywa na mazingira yake ya juu kabisa aliyoyaishi na wala hakujawa na ulafi wa anasa za mwili au kusahau kutoa sadaka za kuteketezwa kwa sababu za utajiri wake, isitoshe pia haya yote hayakumsababisha kuanza kujiepusha na Mungu ndani ya moyo wake kwa utaratibu. Ni dhahiri shairi, hivyo basi, kwamba Ayubu alikuwa na nidhamu katika hali ya maisha yake, na wala hakuwa mlafi au na imani ya kuwa anasa ni kitu muhimu katika maisha, wala hakushikilia na kupumbazwa na ubora wa maisha, kutoka na baraka za Mungu kwake. Badala yake, alinyenyekea na akawa asiye na majivuno, na kuwa mtulivu na makini mbele ya Mungu, mara nyingi alifikiria kuhusu neema na baraka za Mungu, na siku zote alimcha Mungu. Katika maisha yake ya kila siku, Ayubu mara nyingi alirauka mapema ili kutoa sadaka zilizoteketezwa kwa niaba ya watoto wake wa kiume na kike. Kwa maneno mengine, Ayubu mwenyewe alimcha Mungu na pia alitumaini kwamba watoto wake wangeweza vilevile kumcha Mungu na kutotenda dhambi dhidi ya Mungu. Utajiri wa anasa wa Ayubu haukuwa na mahali popote ndani ya moyo wake, wala haukusawazisha ile nafasi iliyoshikiliwa na Mungu; haijalishi kama ilikuwa ni kwa ajili yake mwenyewe au watoto wake, vitendo vyote vya kila siku vya Ayubu viliunganishwa katika kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kumcha Yehova Mungu kwake hakukuishia kwenye kinywa chake lakini kulitiwa katika vitendo, na kukajionyesha katika kila sehemu ya maisha yake. Mwenendo huu halisi wa Ayubu unatuonyesha kwamba alikuwa mwaminifu, na alimiliki kiini kilichopenda haki na mambo yaliyokuwa mazuri. Kwamba Ayubu mara nyingi alituma sadaka ya kuwateketeza na kwa niaba ya watoto wake wa kiume na kike na kuwatakasa kunamaanisha kwamba hakuruhusu wala kuidhinisha tabia ya watoto wake; badala yake katika moyo wake alichoshwa na tabia yao, na akawashutumu vikali. Alikuwa amethibitisha kwamba tabia ya watoto wake wa kike na kiume haikupendeza Yehova Mungu na hivyo basi mara nyingi aliwaita kwenda mbele ya Yehova Mungu na kutubu dhambi zao. Vitendo vya Ayubu vinatuonyesha upande mwingine wa ubinadamu wake: ule ambao unaonyesha kwamba hakuwahi kutembea na wale ambao mara nyingi walitenda dhambi na kumkosea Mungu, lakini badala yake alijiepusha na kutotaka kuwa nao. Hata ingawaje watu hawa walikuwa watoto wake wa kike na kiume, hakuziacha kanuni zake za kibinafsi kwa sababu walikuwa ukoo wake binafsi wala hakujihusisha kwa dhambi zao kwa sababu ya hisia zake binafsi za moyoni. Badala yake aliwasihi kutubu na kupata ustahimilivu wa Yehova Mungu na akawaonya kutomwacha Mungu kwa ajili ya kujifurahisha kwao kwa ulafi. Kanuni za namna ambavyo Ayubu aliwashughulikia wengine haziwezi kutenganishwa na zile kanuni za kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Alipenda kile kilichokubalika na Mungu na kuchukia kile Alichokiona Mungu kuwa mbaya, na akawapenda wale waliomcha Mungu katika mioyo yao, na kuchukia wale waliotenda maovu au kutenda dhambi dhidi ya Mungu. Upendo na chuki kama hiyo zilionyeshwa katika maisha yake ya kila siku, na ndio uliokuwa unyofu wenyewe wa Ayubu ulioonekana katika macho ya Mungu. Kiasili, haya pia ndiyo maonyesho na kuishi kulingana na ubinadamu wa kweli wa Ayubu katika mahusiano yake na wengine katika maisha yake ya kila siku ambao lazima tujifunze kuhusu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp