Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 63

Hata ingawa kile watu wanachosikia kuhusu au kupata ufahamu huo ni tabia ya Mungu, kile Alicho nacho na kile Alicho, kile wanachofaidi ni maisha yanayotoka kwa Mungu. Baada ya maisha haya kuhemshwa ndani yako, uchaji wako wa Mungu utakuwa mkubwa zaidi na zaidi, na kuvuna mavuno haya kunafanyika kwa kawaida sana. Kama hutaki kuelewa au kujua kuhusu tabia ya Mungu au kiini Chake, kama hutaki hata kutafakari juu ya mambo haya au kuyazingatia, Naweza kukuambia kwa hakika kwamba hiyo njia unayoifuatilia katika imani yako kwa Mungu haitawahi kukuruhusu kuyaridhisha mapenzi Yake au kupata sifa Zake. Zaidi ya hayo, huwezi kamwe kufikia wokovu—hizi ndizo athari za mwisho. Wakati watu hawamwelewi Mungu na hawajui tabia Yake, mioyo yao haiwezi kamwe kuwa wazi Kwake. Punde wanapomwelewa Mungu, wataanza kuelewa na kufurahia kile kilicho moyoni Mwake kwa kivutio na imani. Unapoelewa na kufurahia kile kilichomo ndani ya moyo wa Mungu, moyo wako utaanza kwa utaratibu, kidogokidogo, kuwa wazi Kwake. Wakati moyo wako unakuwa wazi Kwake, utahisi namna ambavyo mabadilishano yako na Mungu yatakavyokuwa ya aibu na duni, madai yako kutoka kwa Mungu na matamanio yako mengi binafsi. Moyo wako unapofunguka kwa kweli kwa Mungu, utaona kwamba moyo Wake ni ulimwengu usio na mwisho, na utaingia katika ulimwengu ambao hujawahi kuupitia awali. Katika ulimwengu huu hakuna kudanganya, hakuna udanganyifu, hakuna giza, hakuna maovu. Kunao ukweli wa dhati na uaminifu; kunayo nuru na uadilifu tu; kunayo haki na huruma. Umejaa upendo na utunzaji, umejaa rehema na uvumilivu, na kupitia katika ulimwengu huu utahisi shangwe na furaha ya kuwa hai. Mambo haya ndiyo ambayo Atakufichulia utakapoufungua moyo wako kwa Mungu. Hii dunia isiyo na kikomo imejaa hekima ya Mungu, na imejaa kudura Yake; umejaa pia upendo Wake na mamlaka Yake. Hapa unaweza kuona kila kipengele cha kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho, ni nini kinachomletea Yeye shangwe, kwa nini Anakuwa na wasiwasi na kwa nini Anakuwa na huzuni, kwa nini Anakuwa na hasira…. Haya ndiyo ambayo kila mmoja anayeufungua moyo wake na kumruhusu Mungu kuingia ndani anaweza kuona. Mungu anaweza tu kuingia katika moyo wako kama utaufungua kwa ajili Yake. Unaweza kuona tu kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho, na unaweza kuona tu mapenzi Yake kwako, kama Ameingia katika moyo wako. Wakati huo, utagundua kwamba kila kitu kuhusu Mungu ni chenye thamani, kwamba kile Alicho nacho na kile Alicho kina thamani sana ya kuthaminiwa. Ukilinganisha na hayo, watu wanaokuzunguka, vifaa na matukio katika maisha yako, hata wapendwa wako, mwandani wako, na mambo unayopenda, si muhimu sana. Ni madogo mno, na ni ya kiwango cha chini; utahisi kwamba hakuna chombo chochote cha anasa ambacho kitaweza kukuvutia tena, na vitu hivi haviwezi kukufanya kuvilipia gharama yoyote tena. Kwa unyenyekevu wa Mungu utaona ukubwa Wake na mamlaka Yake ya juu; aidha, katika jambo Alilofanya uliloliamini kuwa dogo mno, utaweza kuiona hekima Yake na uvumilivu Wake usio na mwisho, na utaiona subira Yake, uvumilivu Wake na ufahamu Wake kwako. Hili litazaa ndani yako upendo Kwake. Siku hiyo, utahisi kwamba mwanadamu anaishi katika ulimwengu mchafu, kwamba watu walio upande wako na mambo yanayokufanyikia katika maisha yako, na hata kwa wale unaopenda, upendo wao kwako, na ulinzi wao kama ulivyojulikana au kujali kwao kwako havistahili hata kutajwa—Mungu tu ndiye mpendwa wako na ni Mungu tu unayethamini zaidi. Wakati siku hiyo itawadia, Naamini kwamba kutakuwa na baadhi ya watu watakaosema: Upendo wa Mungu ni mkubwa na kiini Chake ni kitakatifu mno—ndani ya Mungu hakuna udanganyifu, hakuna uovu, hakuna wivu, na hakuna mabishano, lakini ni haki tu na uhalisi, na kila kitu Alicho nacho Mungu na kile Alicho vyote vinafaa kutamaniwa na binadamu. Binadamu wanafaa kujitahidi na kuwa na hamu ya kuvipata. Ni kwa msingi gani ndipo uwezo wa mwanadamu wa kutimiza haya umejengwa? Unajengwa kwa msingi wa ufahamu wa binadamu wa tabia ya Mungu, na ufahamu wao kuhusu kiini cha Mungu. Hivyo basi kuelewa tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho, ni funzo la maisha yote kwa kila mtu na ni lengo la maisha yote linalofuatiliwa na kila mtu anayelenga kubadilisha tabia yake, na kutamani kumjua Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp