Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 71

Samehe Sabini Mara Saba

Mat 18:21-22 Kisha Petro akakuja kwake, na kusema, Bwana, ni mara ngapi ndugu yangu atanikosea, nami nimsamehe? Hadi mara saba? Yesu akasema kwake, sikuambii, hadi mara saba: ila, hadi sabini mara saba.

Upendo wa Bwana

Mat 22:37-39 Yesu akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako mzima, na roho yako nzima, na akili yako nzima. Hii ni amri ya kwanza na kubwa. Na ya pili ni kama hiyo, Mpende jirani yako kama unavyojipenda.

Kati ya dondoo hizi mbili, moja yazungumzia msamaha na nyingine inazungumzia upendo. Mada hizi mbili zinaangazia kwa kweli kazi ambayo Bwana Yesu alitaka kutekeleza katika Enzi ya Neema.

Wakati Mungu alipokuwa mwili, Alileta pamoja naye hatua ya kazi Yake—Alileta pamoja naye kazi mahususi na tabia Aliyotaka kuonyesha katika enzi hii. Katika kipindi hicho, kila kitu ambacho Mwana wa Adamu alifanya kilizungukia kazi ambayo Mungu alitaka kutekeleza katika enzi hii. Asingeweza kufanya zaidi au kufanya kidogo zaidi. Kila kitu Alichosema na kila aina ya kazi Aliyotekeleza ilihusiana yote na enzi hii. Haijalishi kama Alionyesha kwa njia ya kibinadamu Akitumia lugha ya kibinadamu au kupitia kwa lugha ya kiungu—haijalishi ni njia gani, au kutoka kwa mtazamo gani—lengo Lake lilikuwa ni kuwasaidia watu kuelewa kile Alichotaka kufanya, mapenzi Yake yalikuwa nini, na mahitaji Yake yalikuwa yapi kutoka kwa watu. Anaweza kutumia mbinu mbalimbali kutoka mitazamo mbalimbali ili kuwasaidia watu kuelewa na kujua mapenzi Yake, kuelewa kazi Yake ya kuwaokoa binadamu. Hivyo basi katika Enzi ya Neema tunamwona Bwana Yesu akitumia lugha ya kibinadamu mara kwa mara kuonyesha kile Alichotaka kuwasilisha kwa mwanadamu. Hata zaidi, tunamwona kutoka katika mtazamo wa mwelekezi wa kawaida Akiongea na watu, Akiwaruzuku mahitaji yao, Akiwasaidia na kile walichoomba. Njia hii ya kufanya kazi haikuonekana katika Enzi ya Sheria iliyokuja kabla ya Enzi ya Neema. Aligeuka na kuwa karibu zaidi na mwenye huruma zaidi kwa binadamu, pamoja na kuweza kutimiza zaidi matokeo ya kimatendo katika umbo Lake na tabia Yake. Usemi kusamehe watu sabini mara saba unafafanua zaidi hoja hii. Kusudio lililotimizwa kupitia kwa nambari katika usemi huu ni kuwaruhusu watu kuelewa nia ya Bwana Yesu wakati huo aliposema hayo. Nia Yake ilikuwa kwamba watu wanafaa kuwasamehe wengine—si mara moja wala mara mbili na wala si hata mara saba, lakini sabini mara saba. Hili wazo la “sabini mara saba” ni la aina gani? Ni la kuwafanya watu kufanya msamaha kuwa wajibu wao wa kibinafsi, kitu ambacho lazima wajifunze, na njia ambayo lazima waendeleze. Hata ingawa huu ulikuwa usemi tu, ulikuwa hoja muhimu. Uliwasaidia watu kufahamu kwa kina kile Alichomaanisha na kugundua njia bora za kufanyia mazoezi na kanuni na viwango katika utendaji. Usemi huu uliwasaidia watu kuelewa waziwazi na ukawapa dhana sahihi kwamba wanafaa kujifunza kusamehe—kusamehe bila ya masharti na bila ya upungufu wowote, lakini kwa mtazamo wa uvumilivu na ufahamu kwa wengine. Bwana Yesu aliposema haya, ni nini kilichokuwa moyoni Mwake? Alikuwa akifikiria kwa kweli kuhusu sabini mara saba? Hakuwa akifikiri kuhusu hilo. Ipo idadi ya mara ambazo Mungu atawasamehe binadamu? Kunao watu wengi walio na shauku katika “idadi” iliyotajwa, wanaotaka kwa kweli kuelewa asili na maana ya nambari hii. Wanataka kuelewa kwa nini nambari hii ilitoka kinywani mwa Bwana Yesu; wanaamini kwamba kuna uhusisho wa kina zaidi katika nambari hii. Kwa hakika, huu ulikuwa ni usemi tu wa Mungu katika ubinadamu. Uhusisho au maana yoyote lazima ichukuliwe pamoja na mahitaji ya Bwana Yesu kwa mwanadamu. Wakati Mungu alikuwa bado hajawa mwili, watu hawakuelewa mengi ya Alichosema kwa sababu kilitoka katika uungu kamilifu. Mtazamo na muktadha wa kile Alichosema ulikuwa hauonekani na haufikiwi na mwanadamu; ulionyeshwa kutoka katika ulimwengu wa kiroho ambayo watu wasingeweza kuiona. Kwa watu walioishi katika mwili, wasingeweza kupita katika ulimwengu wa kiroho. Lakini baada ya Mungu kuwa mwili, Aliongea na mwanadamu kutoka katika mtazamo wa ubinadamu, na Alitoka kwa na, na akazidi mawanda ya ulimwengu wa kiroho. Angeweza kuonyesha tabia Yake ya uungu, mapenzi, na mtazamo, kupitia mambo yale ambayo binadamu wangeweza kufikiria na mambo yale wangeweza kuona na kukumbana nayo katika maisha yao, kwa kutumia mbinu ambazo binadamu wangeweza kukubali, kwa lugha ambayo wangeweza kuelewa, na maarifa ambayo wangeweza kuelewa, ili kuruhusu mwanadamu kumwelewa na kumjua Mungu, kufahamu nia Yake na viwango Vyake hitajika ndani ya mawanda ya uwezo wao; hadi kufikia kiwango ambacho wangeweza. Hii ndiyo iliyokuwa mbinu na kanuni ya kazi ya Mungu kwa ubinadamu. Ingawa njia za Mungu na kanuni Zake za kufanya kazi katika mwili ziliweza kutimizwa sana kwa, au kupitia kwa ubinadamu, ziliweza kwa kweli kutimiza matokeo ambayo yasingeweza kutimizwa kwa kufanya kazi moja kwa moja katika uungu. Kazi ya Mungu katika ubinadamu ilikuwa thabiti zaidi, halisi, na yenye malengo, mbinu zilikuwa zaweza kubadilika kwa urahisi zaidi, na kwa umbo iliweza kupita Enzi ya Sheria.

Hapa chini, hebu tuzungumzie kumpenda Bwana na kumpenda jirani yako kama unavyojipenda. Je, hili ni jambo linaloelezewa moja kwa moja kupitia uungu? Bila shaka silo! Haya yalikuwa mambo yote ambayo Mwana wa Adamu alisema kwa ubinadamu; watu tu ndio wangeweza kusema kauli kama “Mpende jirani yako kama unavyojipenda. Kuwapenda wengine ni sawa na kuyatunza maisha yako binafsi,” na watu tu ndio wangeweza kuongea kwa njia hii. Mungu hajawahi kuongea kwa njia hiyo. Kwa kiwango cha chini zaidi, Mungu hana aina hii ya lugha katika uungu Wake kwa sababu Hahitaji aina hii ya imani, “Mpende jirani yako kama unavyojipenda” ili kudhibiti upendo Wake kwa mwanadamu, kwa sababu upendo wa Mungu kwa mwanadamu ni ufichuzi wa kiasili wa kile Alicho nacho na kile Alicho. Ni lini mmewahi kusikia kwamba Mungu alisema kitu kama “Nampenda binadamu kama Ninavyojipenda”? Kwa sababu upendo umo katika kiini cha Mungu, na ndani ya kile Alicho nacho na kile Alicho. Upendo wa Mungu kwa binadamu na jinsi Anavyowashughulikia watu na mtazamo Wake ni maonyesho ya kiasili na ufichuzi wa tabia Yake. Hahitaji kufanya hili kwa njia fulani kimakusudi, au kufuata mbinu fulani au mfumo wa maadili kimakusudi ili kutimiza kumpenda jirani Yake kama Anavyojipenda—tayari Anamiliki aina hii ya kiini. Unaona nini katika haya? Wakati Mungu alipofanya kazi katika ubinadamu, mbinu, maneno, na ukweli Wake mwingi vyote vilionyeshwa kwa njia ya kibinadamu. Lakini wakati uo huo tabia ya Mungu, kile Alicho nacho na kile Alicho, na mapenzi Yake vyote vilionyeshwa kwa watu kuweza kujua na kuvielewa. Kile walichojua na kuelewa kilikuwa hasa kiini Chake na Alicho nacho na kile Alicho, vyote ambavyo vinawakilisha utambulisho na hadhi ya asili ya Mungu Mwenyewe. Hivyo ni kusema kwamba, Mwana wa Adamu kwa mwili Alionyesha tabia ya asili na kiini cha Mungu Mwenyewe kwa kiwango kikubwa zaidi kinachowezekana na kwa usahihi zaidi unaowezekana. Ubinadamu wa Mwana wa Adamu haukuwa pingamizi au kizuizi cha mawasiliano na kuingiliana kwa binadamu na Mungu mbinguni tu, bali kwa hakika ilikuwa ndio njia ya pekee na daraja la pekee la mwanadamu kuungana na Bwana wa uumbaji. Wakati huu, je, hamhisi kwamba kunayo mifanano mingi kati ya asili na mbinu za kazi iliyofanywa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema na awamu ya sasa ya kazi? Hatua ya sasa ya kazi inatumia pia lugha nyingi za kibinadamu kueleza tabia ya Mungu, na inatumia lugha na mbinu nyingi kutoka katika maisha ya kila siku ya binadamu na maarifa ya kibinadamu ili kuonyesha mapenzi binafsi ya Mungu. Punde Mungu anapokuwa mwili, haijalishi kama Anaongea kutoka kwa mtazamo wa kibinadamu au mtazamo wa kiungu, wingi wa lugha na mbinu Zake za maonyesho yote ni kupitia katika njia ya lugha na mbinu za kibinadamu. Yaani, wakati Mungu anapokuwa mwili, ndiyo fursa bora zaidi ya wewe kuweza kuona kudura ya Mungu na hekima Yake, na kujua kila kipengele halisi cha Mungu. Mungu alipogeuka na kuwa mwili, wakati Alikuwa Akikua, Alipata kuelewa, kujifunza, na kuelewa baadhi ya maarifa ya binadamu, maarifa ya kawaida, lugha, na mbinu za maonyesho katika ubinadamu. Mungu mwenye mwili alimiliki mambo haya yaliyotokana na binadamu Aliyekuwa ameumba. Waligeuka na kuwa zana za Mungu katika mwili za kueleza tabia Yake na uungu Wake, na wakamruhusu kuifanya kazi Yake ya kufaa zaidi, halisi zaidi, na sahihi zaidi Alipokuwa akifanya kazi katikati ya mwanadamu, kutoka katika mtazamo wa kibinadamu na kwa kutumia lugha ya kibinadamu. Iliiwezesha kufikiwa zaidi na kueleweka kwa urahisi zaidi na watu, hivyo basi kutimiza matokeo ya kile Mungu Alichotaka. Je, si jambo la busara zaidi kwa Mungu kufanya kazi kupitia kwa mwili kwa njia hii? Je, hii sio hekima ya Mungu? Wakati Mungu alipogeuka na kuwa mwili, wakati mwili wa Mungu uliweza kuchukua kazi Aliyotaka kutekeleza, ndipo Angeonyesha tabia Yake na kazi Yake kwa utendaji, na huu ndio wakati pia ambao Angeanza rasmi huduma Yake kama Mwana wa Adamu. Hii ilimaanisha kwamba hakukuwepo tena na ghuba kati ya Mungu na binadamu, kwamba Mungu angesitisha karibuni kazi Yake ya kuwasiliana kupitia kwa wajumbe, na kwamba Mungu Mwenyewe binafsi angeweza kuonyesha maneno na kazi zote Alizotaka kufanya katika mwili. Hii ilimaanisha pia kwamba watu ambao Mungu huokoa walikuwa karibu na Yeye, na kwamba kazi Yake ya usimamizi ilikuwa imeingia eneo jipya, na kwamba binadamu wote walikuwa karibu kukumbwa na enzi mpya.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp