Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 353

17/08/2020

Kila siku, fikira na matendo ya kila mmoja yanachunguzwa na Yeye na, katika wakati uo huo, wamo katika matayarisho ya siku zao zinazofuata. Hii ni njia ambayo lazima kila mtu aliye hai aipitie na ambayo Nimeamulia kabla kila mmoja. Hakuna anayeweza kuepuka hili na hakuna atakayepata upendeleo. Nimezungumza maneno yasiyohesabika na zaidi ya yote Nimefanya kazi kubwa mno. Kila siku, Ninatazama vile kila mwanadamu kiasili anafanya yote ambayo anafaa kufanya kulingana na asili yake na vile inavyoendelea. Bila kujua, wengi tayari wamo katika “njia sahihi”, ambayo Niliiweka kwa ufunuo wa mwanadamu wa kila aina. Tayari Nimemweka kila aina ya mwanadamu katika mazingira tofauti tofauti, na katika sehemu zao, kila mmoja amekuwa akionyesha tabia zake za asili. Hakuna mtu wa kuwafunga, hakuna mtu wa kuwatongoza. Wako huru katika nafsi yao yote na lile wanalolieleza linakuja kwa wepesi. Kuna kitu kimoja tu ambacho huwaweka katika nidhamu, na hayo ni maneno Yangu. Kwa hivyo, kuna idadi ya wanadamu husoma tu maneno Yangu shingo upande ili mwisho wao usiwe ule wa mauti, lakini kamwe hawaweki maneno Yangu katika matendo. Kwa upande mwingine, wanadamu wengine huona ugumu kuvumilia siku bila maneno Yangu kuwaelekeza na kuwapa, kwa hivyo wao hushikilia maneno Yangu kiasili wakati wote. Muda unavyopita, wao basi hugundua siri ya maisha ya mwanadamu, hatima ya mwanadamu na thamani ya kuwa na utu. Mwanadamu si zaidi ya haya katika uwepo wa maneno Yangu, na Mimi huruhusu tu mambo yachukue mkondo wake. Sifanyi chochote kinachomlazimisha mwanadamu kuishi kulingana na maneno Yangu kama msingi wa kuwepo kwake. Na kwa hivyo wale wasiokuwa na dhamiri au thamani katika kuwepo kwao hutazama kwa kimya mambo yanavyoenda kisha wanayatupa maneno Yangu kando kwa ujasiri na kufanya vile wanavyopenda. Wanaanza kuchoshwa na ukweli na mambo yote yatokayo Kwangu. Isitoshe, wao huchoka kukaa katika nyumba Yangu. Wanadamu hawa hukaa katika nyumba Yangu kwa ufupi tu kwa ajili ya hatima zao na kuepuka adhabu, hata kama wanafanya huduma. Lakini nia zao huwa hazibadiliki, wala matendo yao. Hii huendeleza zaidi hamu zao za Baraka, hamu za njia moja kwenda katika ufalme ambako wanaweza kubakia milele, na pia njia ya kuingia mbingu ya milele. Jinsi wanavyotamani zaidi siku Yangu ije hivi karibuni, ndivyo wanavyohisi zaidi kuwa ukweli umekuwa kizingiti, kizuizi njiani mwao. Wanangoja kwa hamu kuingia katika ufalme ili wafurahie daima baraka za ufalme wa mbinguni, bila kutaka kuufuata ukweli ama kukubali hukumu na kuadibu, na zaidi ya yote, bila kuhitaji kuishi kwa utumishi katika nyumba Yangu na kufanya vile Ninavyoamuru. Wanadamu hawa hawaingii katika nyumba Yangu kuukamilisha moyo unaotaka kujua ukweli wala kufanya kazi pamoja na uongozi Wangu. Lengo lao tu ni wawe miongoni mwa wale ambao hawataangamizwa katika enzi inayofuata. Kwa hivyo nyoyo zao hazijawahi kuujua ukweli wala kujua jinsi ya kuukubali ukweli. Hii ndiyo sababu wanadamu wa aina hii hawajawahi kutia vitendoni ukweli au kujua undani wa ufisadi wao, ilhali wameishi katika nyumba yangu kama “wajakazi” mpaka mwisho. Wanangoja “kwa uvumilivu” kuja kwa siku Yangu, na hawachoki wanaporushwa huku na kule na hali ya kazi Yangu. Haijalishi bidii zao ni kubwa namna gani au ni gharama gani wamelipa, hakuna atakayeona kuwa wameteseka kwa ajili ya ukweli ama kujitoa kwa ajili Yangu. Katika mioyo yao, wanangoja kwa hamu siku ambayo Nitakomesha enzi nzee, na zaidi ya hayo, wanangoja kwa hamu kujua jinsi nguvu na mamlaka Yangu ni kuu. Kile hawajawahi kimbilia kufanya ni kujibadilisha na kufuata ukweli. Wanapenda kile kinachonichosha na kuchoshwa na kile ninachopenda. Wanangoja kwa hamu kile Ninachokuwa na kinyongo nacho lakini wakati uo huo wanaogopa kupoteza kile Ninachochukia. Wanaishi katika dunia hii yenye maovu ila hawajawahi kuwa na chuki nayo na wana hofu sana kuwa Nitaiangamiza dunia hii. Nia walizo nazo zinakanganya: Wanapendezwa na dunia hii Ninayochukia, na kwa wakati uo huo wanangoja kwa hamu Niiharibu dunia hii hivi karibuni. Kwa njia hii, wataepuka mateso ya uharibifu na wabadilishwe kuwa watawala wa enzi mpya kabla hawajapotoshwa kutoka katika njia ya kweli. Hii ni kwa sababu hawapendi ukweli na wanahofia kila kitu kitokacho Kwangu. Huenda ikawa watakuwa “watu watiifu” kwa muda mfupi kwa minajili ya kutopoteza baraka, lakini fikira zao za kungoja baraka kwa hamu na woga wao wa kuangamia na kuingia katika ziwa la moto haziwezi kukingwa kuonekana. Siku Yangu inapokaribia, hamu zao zinazidi kuimarika. Na vile janga lilivyo kubwa, ndivyo wanavyopoteza tumaini wasijue watakapoanzia ili kunifanya Nifurahi na kuzuia wasipoteze baraka ambazo wamezingoja kwa muda mrefu. Pindi mkono Wangu unapoanza kazi yake, wanadamu hawa wana hamu kuchukua hatua kuhudumu kama watangulizi. Wanafikiri tu kusonga kwa nguvu mpaka mstari wa mbele wa majeshi, wakiwa na woga mwingi kuwa Sitawaona. Wanafanya na kusema kile wanachodhani ni ukweli, bila kujua kuwa vitendo na matendo yao hayajawahi na umuhimu kwa ukweli, na kuwa hutatiza na kuingilia tu mipango Yangu. Hata ingawa wanaweza kuwa wameweka juhudi nyingi na wanaweza kuwa wa kweli katika ridhaa na nia zao kustahimili ugumu, kila wanachokifanya hakihusiani na Mimi, kwa maana Sijaona hata mara moja kwamba matendo yao yametoka kwa nia njema, na zaidi ya hayo, Sijawaona kama wameweka kitu chochote kwenye madhabahu Yangu. Hayo ndiyo matendo yao mbele Yangu kwa miaka hii mingi.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp