Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 83

Mungu Hutumia Maneno ili Kuumba Viumbe Vyote

Mwa 1:3-5 Na Mungu akasema, Na kuwe na mwanga; kukawa na mwanga. Mungu akauona mwanga, na kuwa ulikuwa mzuri: na Mungu akautenga mwanga na kiza. Naye Mungu akauita mwanga Mchana, na kiza akaliita Usiku. Na jioni na asubuhi yalikuwa siku ya kwanza.

Mwa 1:6-7 Na Mungu alisema, Na kuwe na mbingu katikati ya maji, na uigawanye maji kutoka kwa maji. Na Mungu akaitengeneza mbingu, na akayagawanya yale maji yaliyokuwa chini ya mbingu kutoka kwa yale maji yaliyokuwa juu ya mbingu: na kukawa vivyo hivyo.

Mwa 1:9-11 Naye Mungu akasema, Nayo maji yaliyo chini ya mbingu yakonge pahali pamoja, na ardhi kavu ionekane; na kukawa vivyo hivyo. Naye Mungu akaiita nchi kavu Dunia: na kukonga kwa maji akakuita Bahari: naye Mungu akaona kwamba ni vyema. Naye Mungu akasema, Na dunia izae majani, mche ambao unatoa mbegu, na mti wa matunda ambao unazaa tunda kwa aina yake, ambao mbegu zake ziko ndani yake, juu ya dunia: na kukawa vivyo hivyo.

Mwa 1:14-15 Naye Mungu akasema, Kuwe na mwangaza katika anga la mbingu kwa minajili ya kutenga mchana na usiku; na uwe ndio ishara; na majira, na siku na miaka: Na tena uwe ndio mwangaza katika anga la mbingu kwa minajili ya kupa nchi nuru; na ikawa vile.

Mwa 1:20-21 Na Mungu akasema, Na maji yalete kwa wingi kiumbe asongaye aliye na uhai, na ndege wanaoweza kuruka juu ya nchi katika anga wazi la mbingu. Naye Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na viumbe wote walio na uhai wasongao, ambao maji yalileta kwa wingi, kwa aina yao, na kila ndege anayeruka kwa aina yake: na Mungu akaona kuwa ilikuwa vizuri.

Mwa 1:24-25 Naye Mungu aksema, Dunia na ilete kiumbe kilicho hai kwa namna yake, mifugo, na kitu kinachotambaa, na wanyama wa mwituni kwa namna yake: na ikafanyika. Naye Mungu akaumba wanyawa wa mwituni kwa namna yake, na mifugo kwa namna yake, na chote kinachotambaa duniani kwa namna yake: na Mungu akaona kwamba ni vizuri.

Kwenye Siku ya Kwanza, Mchana na Usiku wa Mwanadamu Vinazaliwa na Kujitokeza Waziwazi kwa Msaada wa Mamlaka ya Mungu

Hebu na tuweze kuangalia fungu la kwanza: “Na Mungu akasema, Na kuwe na mwanga; kukawa na mwanga. Mungu akauona mwanga, na kuwa ulikuwa mzuri: na Mungu akautenga mwanga na kiza. Naye Mungu akauita mwanga Mchana, na kiza akaliita Usiku. Na jioni na asubuhi yalikuwa siku ya kwanza” (Mwa 1:3-5). Fungu hili linafafanua kitendo cha kwanza cha Mungu wakati wa mwanzo wa uumbaji, na siku ya kwanza ambayo Mungu alipitisha ambapo kulikuwa na jioni na asubuhi. Lakini ilikuwa siku ya kipekee: Mungu alianza kutayarisha nuru ya viumbe vyote, na, vilevile, Akagawa nuru kutoka kwa giza. Kwenye siku hii, Mungu alianza kunena, na matamshi na mamlaka Yake vyote vilikuwa pamoja. Mamlaka Yake yalianza kujitokeza miongoni mwa viumbe vyote, na nguvu Zake zikaenea miongoni mwa viumbe vyote kutokana na maneno Yake. Kuanzia siku hii kuendelea mbele, viumbe vyote viliumbwa na vikawa viko tayari kwa sababu ya maneno ya Mungu, mamlaka ya Mungu na nguvu za Mungu, na vikaanza kufanya kazi kwa msaada wa maneno ya Mungu, mamlaka ya Mungu na nguvu za Mungu. Wakati Mungu aliposema maneno haya “Na kuwe na mwanga,” kulikuwepo na nuru. Mungu hakuanza kushughulikia shughuli yoyote; nuru ilikuwa imeonekana kama matokeo ya maneno Yake. Hii ilikuwa nuru ambayo Mungu aliita mchana, na ambayo binadamu angali anaitegemea kwa minajili ya kuwepo kwake leo. Kwa amri ya Mungu, hali yake halisi na thamani havijawahi kubadilika na havijawahi kutoweka. Uwepo wake unaonyesha mamlaka na nguvu za Mungu, na unatangaza uwepo wa Mungu, na unathibitisha, tena na tena, utambulisho na hadhi ya Muumba. Haiwezi kushikika, au kuonekana, lakini ni nuru halisi inayoweza kuonekana na binadamu. Kuanzia wakati huo kusonga mbele, kwenye ulimwengu huu mtupu ambao “nchi ilikuwa ya ukiwa na tupu; na kulikuwa na giza sehemu ya juu ya vilindi,” kulikuwepo kiumbe kile cha kwanza cha kushikika. Kiumbe hiki kilitokana na maneno ya kinywa cha Mungu na kikaonekana kwenye tukio la kwanza la kuumbwa kwa viumbe vyote kwa sababu ya mamlaka na matamshi ya Mungu. Muda mfupi baadaye, Mungu aliamuru nuru na giza kutengana… Kila kitu kilibadilika na kilikamilishwa kwa sababu ya maneno ya Mungu… Mungu akaiita nuru hii “Mchana,” na giza hili Akaliita “Usiku.” Kuanzia wakati huo, jioni ya kwanza na asubuhi ya kwanza ziliweza kuumbwa katika ulimwengu ambao Mungu alinuia kuumba, na Mungu akasema hii ndiyo iliyokuwa siku ya kwanza. Siku hii ilikuwa siku ya kwanza ya vile vilivyoumbwa na Muumba wa viumbe vyote, na ilikuwa mwanzo wa kuumbwa kwa viumbe vyote, na ndio wakati wa kwanza ambao mamlaka na nguvu za Muumba vilikuwa vimeonyeshwa katika ulimwengu huu ambao Alikuwa ameumba.

Kupitia maneno haya, binadamu anaweza kutazama mamlaka ya Mungu, na mamlaka ya maneno ya Mungu, na nguvu za Mungu. Kwa sababu Mungu tu ndiye anayemiliki nguvu kama hizo, na kwa hivyo Mungu pekee ndiye aliye na mamlaka, na kwa sababu Mungu ndiye anayemiliki mamlaka kama hayo, kwa hivyo Mungu pekee ndiye aliye na nguvu kama hizo. Je, binadamu au kifaa chochote kingeweza kumiliki mamlaka na nguvu kama hizi? Je, kunalo jibu katika moyo wako? Mbali na Mungu, je, kuna kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa kinachomiliki mamlaka kama hayo? Umewahi kuona mfano wa kiumbe kama hiki kwenye vitabu vingine vyovyote au machapisho? Kunayo rekodi yoyote kwamba mtu aliumba mbingu na ulimwengu na viumbe vyote? Jambo hili halionekani katika vitabu au rekodi nyingine zozote; haya ndiyo, bila shaka, maneno ya kipekee yenye mamlaka na nguvu kuhusu uumbaji wa kupendeza wa Mungu wa ulimwengu, yaliyorekodiwa kwenye Biblia, na maneno haya yanazungumzia mamlaka ya kipekee ya Mungu, na utambulisho wa kipekee wa Mungu. Je, mamlaka na nguvu kama hizi zinaweza kusemekana kuwa zinaashiria utambulisho wa kipekee wa Mungu? Yanaweza kusemwa yanamilikiwa na Mungu, na Mungu pekee? Bila shaka, Mungu Mwenyewe pekee ndiye anayemiliki mamlaka na nguvu kama hizi! Mamlaka na nguvu hizi vyote haviwezi kumilikiwa au kubadilishwa na kiumbe chochote kingine kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa! Je, hii ni mojawapo ya sifa za Mungu Mwenyewe wa kipekee? Je, umewahi kuishuhudia? Maneno haya yanaruhusu watu kuelewa kwa haraka na waziwazi hoja hii kwamba Mungu anamiliki mamlaka ya kipekee, na nguvu za kipekee, na Anamiliki utambulisho na hadhi isiyo ya kawaida. Kutokana na ushirika wa hapa juu, je, unaweza kusema kwamba Mungu unayemsadiki ndiye Mungu Mwenyewe wa kipekee?

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp