Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 96

Hoja ya Udhibiti wa Muumba na Utawala Juu ya Vitu Vyote na Viumbe Vilivyo Hai Inazungumzia Uwepo wa Kweli wa Mamlaka ya Muumba

Baraka za Yehova Mungu kwa Ayubu zimerekodiwa katika Kitabu cha Ayubu. Ni nini ambacho Mungu alimpa Ayubu? “Kwa hivyo Yehova akabariki mwisho wa baadaye wa Ayubu zaidi kuliko mwanzo wake: kwa sababu alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na elfu moja ya jozi za ng’ombe, na elfu moja ya punda wa kike” (Ayubu 42:12). Kutoka kwenye mtazamo wa binadamu, ni vitu gani alivyopewa Ayubu? Je, vilikuwa rasilimali ya binadamu? Akiwa na rasilimali hizi, je, Ayubu angeweza kuwa tajiri sana kwenye kipindi hicho? Na aliwezaje kumiliki rasilimali kama hizo? Ni nini kilisababisha utajiri wake? Bila shaka ilikuwa ni shukrani kwa baraka ya Mungu ambapo Ayubu alifanikiwa kumiliki. Namna ambavyo Ayubu alitazama rasilimali hizi, na vipi alivyochukulia baraka za Mungu, si jambo ambalo tutalizungumzia hapa. Tunapokuja katika baraka za Mungu watu wote hutamani, mchana na usiku, kubarikiwa na Mungu, ilhali binadamu hana udhibiti wowote kuhusiana na idadi ngapi ya rasilimali anaweza kufaidi katika maisha yake yote, au kama anaweza kupokea baraka kutoka kwa Mungu—na hii ni hoja isiyopingika! Mungu anayo mamlaka, na nguvu za kumpatia mwanadamu rasilimali yoyote, kumruhusu binadamu kupata tamko lolote la baraka, ilhali kuna kanuni ya baraka za Mungu. Ni aina gani ya watu ambao Mungu hubariki? Watu Anaowapenda, bila shaka! Ibrahimu na Ayubu walibarikiwa wote na Mungu, ilhali baraka walizopokea hazikuwa sawa. Mungu alibariki Ibrahimu kwa vizazi vingi kama mchanga na nyota. Wakati Mungu alipombariki Ibrahimu, Alisababisha vizazi vya mtu mmoja, taifa moja, kuwa na nguvu na ufanisi. Katika haya mamlaka ya Mungu yalitawala mwanadamu, ambaye alipumua pumzi za Mungu miongoni mwa viumbe vyote na viumbe vyenye uhai. Chini ya ukuu wa mamlaka ya Mungu, huyu mwanadamu aliweza kupenyeza na kuwepo kwa kasi, na ndani ya upana, ulioamuliwa na Mungu. Haswa, uwezo wa taifa hili, kima cha upanuzi, na matarajio ya maisha vyote vilikuwa sehemu ya mipangilio ya Mungu, na kanuni ya haya yote ilitokana kwa ujumla kwa ahadi ambazo Mungu alimpa Ibrahimu. Hivi ni kusema kwamba, licha ya hali zozote zile, ahadi za Mungu zingeendelea mbele bila kizuizi na kuweza kutambuliwa kulingana na uwepo wa mamlaka ya Mungu. Katika ahadi ambayo Mungu alimpa Ibrahimu, licha ya misukosuko ya ulimwengu, licha ya umri, licha ya majanga yanayovumiliwa na mwanadamu, vizazi vya Ibrahimu visingeweza kukabiliwa na hatari ya maangamizo, na taifa lao lisingefifia na kutokomea. Baraka ya Mungu kwa Ayubu, hata hivyo, ilimfanya kuwa tajiri wa kupindukia. Kile Mungu alichompa kilikuwa mseto wa viumbe hai, vinavyopumua, maelezo yake yalikuwa—idadi yao, kasi yao ya kuzaa, kima cha kuishi, kiwango cha mafuta kwenye viumbe hivyo, na kadhalika—vilidhibitiwa pia na Mungu. Ingawaje viumbe hivi hai havikumiliki uwezo wa kuongea, navyo pia vilikuwa sehemu ya mipangilio ya Muumba, na kanuni za mipangilio ya Mungu zilikuwa kulingana na baraka ambayo Mungu aliahidi Ayubu. Katika baraka ambazo Mungu alimpa Ibrahimu na Ayubu, ingawaje kile kilichokuwa kimeahidiwa kilikuwa tofauti, mamlaka ambayo Muumba alitumia kutawala viumbe vyote na viumbe vilivyo na uhai yalikuwa yale yale. Kila maelezo ya mamlaka na Nguvu za Mungu yameonyeshwa kwenye ahadi Zake tofauti na baraka zake kwa Ibrahimu na Ayubu, kwa mara nyingine zaonyesha binadamu kwamba mamlaka ya Mungu ni zaidi ya kufikiria kwa binadamu. Maelezo haya yanamwambia binadamu kwa mara nyingine kwamba kama angetaka kujua mamlaka ya Mungu, basi hii itawezekana tu kupitia kwa maneno ya Mungu na kuweza kupitia kazi ya Mungu.

Mamlaka ya Mungu ya ukuu juu ya viumbe vyote huruhusu binadamu kuweza kuona ukweli kwamba: Mamlaka ya Mungu hayapo tu katika matamshi “Mungu akasema, na Kuwepo na nuru, na kukawa na nuru, na, Kuwepo na anga, na kukawa na anga, na, Kuwepo na ardhi, na kukawa na ardhi,” lakini, vilevile namna Alivyofanya nuru ile kuendelea kuwepo, kulizuia anga dhidi ya kutoweka na Akaiweka ardhi milele ikiwa kando na maji, pamoja na maelezo ya namna Alivyotawala na kusimamia viumbe: nuru, anga, na ardhi. Nini kingine unachoona katika baraka za Mungu kwa mwanadamu? Ni wazi, kwamba baada ya Mungu kuwabariki Ibrahimu na Ayubu, nyayo za Mungu hazikusita, kwani Alikuwa tu ameanza kuonyesha mamlaka Yake, na Alinuia kuhakikisha kwamba kila mojawapo ya matamshi Yake yangekuwa uhalisia, na kuhakikisha kuwa kila mojawapo ya maelezo ambayo Alizungumza yanatokea kuwa kweli, na kwa hivyo kwenye miaka iliyofuata, Aliendelea kufanya kila kitu Alichonuia. Kwa sababu Mungu anayo mamlaka, pengine inaonekana kwa binadamu kwamba Mungu huongea tu, na Hahitaji kuinua hata kidole chake ili mambo yote yaweze kutimizwa. Kufikiria hivyo, ni, lazima Niseme, mzaha! Kama utachukua mtazamo wa upande mmoja wa Mungu kuanzisha agano na binadamu kwa kutumia maneno, na ukamilishaji wa kila kitu na Mungu kwa kutumia maneno, na huwezi kuona ishara na hoja mbalimbali ambazo mamlaka ya Mungu yanatawala juu ya kila kitu, basi ufahamu wako kuhusiana na mamlaka ya Mungu ni mdogo mno na wa mzaha! Kama binadamu anafikiria Mungu kuwa hivyo, basi, lazima isemwe, maarifa ya binadamu kuhusu Mungu yameendeshwa hadi kwenye shimo la mwisho, na sasa yamefika mwisho wenyewe, kwani Yule Mungu ambaye binadamu anafikiria kuhusu ni mashine tu ya kutoa amri, na si Mungu anayemiliki mamlaka. Je, umeona nini kupitia kwenye mifano ya Ibrahimu na Ayubu? Je, umeuona upande halisia wa mamlaka na nguvu za Mungu? Baada ya Mungu kuwabariki Ibrahimu na Ayubu, Mungu hakubakia mahali Alipokuwa, wala Yeye kuwaweka wajumbe Wake kazini huku Akisubiri kuona matokeo yake yatakuwa yapi. Kinyume cha mambo ni kuwa, pindi Mungu alipotamka maneno Yake, akiongozwa na mamlaka ya Mungu, mambo yote yalianza kukubaliana na kazi ambayo Mungu alinuia kufanya, na kulikuwepo na watu waliokuwa wamejitayarisha, vitu, na vifaa ambavyo Mungu alihitaji. Hivi ni kusema kwamba, punde tu maneno hayo yalipotamkwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu, mamlaka ya Mungu yalianza kutumika kotekote kwenye ardhi nzima, na Akaweka wazi mkondo ili kuweza kukamilisha na kutimiza ahadi Alizotoa kwa Ibrahimu na Ayubu, huku Akifanya pia mipango na matayarisho yote kuhusiana na kila kitu kilichohitajika kwa kila awamu Aliyopanga kutekeleza. Kwa wakati huu, hakuwashawishi tu wafanyakazi Wake, lakini pia na viumbe vyote vilivyokuwa vimeumbwa na Yeye. Hivyo ni kusema kwamba upana ambao mamlaka ya Mungu yalitiliwa maanani haukujumuisha tu wajumbe, lakini, vilevile, vitu vyote, vilivyoshawishiwa ili kutii ile kazi ambayo Alinuia kukamilisha; hizi ndizo zilizokuwa tabia mahususi ambazo mamlaka ya Mungu yalitumiwa. Katika kufikiria kwako, baadhi ya watu wanaweza kuwa na ufahamu ufuatao kuhusiana na mamlaka ya Mungu: Mungu anayo mamlaka, na Mungu anao uwezo, na hivyo basi Mungu anahitaji kubaki katika mbingu ya tatu, au Anahitajika tu kubakia mahali maalum, na hahitajiki kufanya kazi yoyote fulani, na uzima wa kazi ya Mungu unakamilishwa katika fikira Zake. Baadhi wanaweza kusadiki kuwa, ingawaje Mungu alibariki Ibrahimu, Mungu hakuhitajika kufanya kitu chochote, na ilitosha kwake Yeye kutamka tu matamshi Yake. Je, hivi ndivyo ilivyofanyika kweli? Bila shaka la! Ingawaje Mungu anamiliki mamlaka na nguvu, mamlaka Yake ni ya kweli na halisia, si matupu. Uhalisi na ukweli wa mamlaka ya Mungu na nguvu hufichuliwa kwa utaratibu, kuwekwa ndani ya uumbaji Wake wa vitu vyote, na udhibiti wa vitu vyote, na katika mchakato ambao Anaongoza na kusimamia wanadamu. Kila mbinu, kila mtazamo na kila maelezo ya ukuu wa Mungu juu ya wanadamu na vitu vyote, na kazi yote ambayo Amekamilisha, vilevile ufahamu Wake kuhusu vitu vyovyote—vinathibitisha kwa kweli kwamba mamlaka na nguvu za Mungu si maneno matupu. Mamlaka na nguvu Zake vyote vinaonyeshwa na kufichuliwa kila mara, na katika mambo yote. Maonyesho haya na ufunuo vyote vinazungumzia uwepo wa kihalisia wa mamlaka ya Mungu, kwani Yeye ndiye anayetumia mamlaka na nguvu Zake kuendeleza kazi Yake, na kuamuru vitu vyote, na kutawala vitu vyote kila wakati, na nguvu na mamlaka Yake, vyote haviwezi kubadilishwa na malaika, au wajumbe wa Mungu. Mungu aliamua ni baraka gani Angempa Ibrahimu na Ayubu—uamuzi ulikuwa wa Mungu. Hata ingawaje wajumbe wa Mungu waliweza kumtembelea Ibrahimu na Ayubu wao binafsi, vitendo vyao vilikuwa kulingana na amri za Mungu, na kulingana na mamlaka ya Mungu, na pia walikuwa wakifuata ukuu wa Mungu. Ingawaje binadamu anawaona wajumbe wa Mungu wakimtembelea Ibrahimu, na hashuhudii Yehova Mungu binafsi akifanya chochote kwenye rekodi za Biblia, kwa hakika Yule Mmoja tu ambaye anatilia mkazo nguvu na mamlaka ni Mungu Mwenyewe, na hali hii haivumilii shaka yoyote kutoka kwa binadamu yeyote! Ingawaje umewaona malaika na wajumbe wakimiliki nguvu nyingi, na wametenda miujiza, au wamefanya baadhi ya mambo yaliyoagizwa na Mungu, vitendo vyao ni kwa minajili tu ya kukamilisha agizo la Mungu, na wala si tu kuonyesha mamlaka ya Mungu—kwani hakuna binadamu au kifaa kilicho na, au kinachomiliki, mamlaka ya Muumba ya kuumba vitu vyote na kutawala vitu vyote. Na kwa hivyo hakuna binadamu au kifaa chochote kinaweza kutumia au kuonyesha mamlaka ya Muumba.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp