Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 332

11/08/2020

Kila siku mnayoiishi sasa ni ya maana sana na muhimu sana kwa hatima yenu na majaliwa yenu, kwa hivyo mnapaswa kufurahia kila mlicho nacho na kila dakika inayopita. Mnapaswa kutumia muda wenu vizuri ili muweze kujinufaisha, ili msije kuishi maisha haya bure. Pengine mnajihisi kukanganyikiwa mnaojiuliza ni kwa nini Ninazungumza maneno haya. Kwa kweli, Sijapendezwa na matendo ya yeyote kati yenu. Kwa maana matumaini ambayo Nimekuwa nayo juu yenu si vile tu mlivyo sasa. Kwa hivyo, Naweza kuelezea hivi: Nyinyi nyote mko hatarini kabisa. Vilio vyenu vya kwanza kwa ajili ya wokovu na matamanio yako ya kwanza ya kufuatilia ukweli na kutafuta nuru vinakaribia mwisho. Hivi ndivyo mtakavyonifidia mwishowe, ambacho ni kitu ambacho Sikukitumainia. Sitamani kuzungumza kinyume cha ukweli, kwa maana mmenivunja moyo sana. Pengine hampendi kuiachia mada hapo na hutaki kuukabili ukweli, lakini ni lazima niwaulize swali hili: Kwa miaka hii yote, mioyo yenu imejawa na nini? Mioyo yenu inamwamini nani? Usiseme kwamba swali Langu limekuja ghafla sana, na usiniulize kwa nini Nauliza swali kama hilo. Mnapaswa kujua hili: Ni kwa sababu Ninawafahamu vizuri, ninawajali sana, na Ninajitolea moyo Wangu sana kwa kile mnachofanya, ndio maana Ninawauliza kwa kurudiarudia na kubeba taabu isiyoelezeka. Hata hivyo, malipo Yangu yamekuwa ni kupuuzwa na kukataliwa kusikostahimilika. Hivyo mmekuwa na ajizi sana juu Yangu; Ninawezaje kutojua kitu kuhusu hilo? Kama mnaamini kwamba hili linawezekana, inathibitisha ukweli zaidi kwamba hamunitendei wema kabisa. Kisha Ninawaambia kwamba mnajidanganya nyinyi wenyewe. Nyinyi nyote ni werevu sana kiasi kwamba hamjui kile mnachofanya; sasa mtatumia nini ili kunipatia ufafanuzi?

Swali muhimu sana kwangu ni mioyo yenu inawamini nani. Pia Ningependa kila mmoja wenu afikiri vizuri na kisha ajiulize uaminifu wake uko kwa nani na anaishi kwa ajili ya nani? Pengine hamjawahi kuliangalia swali hili kwa makini, hivyo nitawapatia jibu lake.

Wale wenye kumbukumbu nzuri wataukubali ukweli huu: Mwanadamu anaishi kwa ajili yake mwenyewe na ni mwaminifu kwake mwenyewe. Siamini kwamba jibu lenu ni sahihi kabisa, kwa maana kila mmoja wenu anaishi maisha yake, kila mmoja wenu anapambana katika dhiki yake. Kwa hivyo, kile mnachokuwa waaminifu kwacho ni watu mnaowapenda, na vitu vinavyowapendeza, na wala nyinyi si waaminifu kwa nafsi zenu wenyewe. Kwa sababu kila mmoja wenu anaathiriwa na watu, matukio, na vitu vinavyowazunguka, kimsingi nyinyi si waaminifu kwa nafsi zenu. Sisemi maneno haya kwa kuwataka muwe waaminifu kwa nafsi zenu bali Nasema ili kufichua uaminifu wenu kwa kitu chochote kile. Maana kwa miaka yote hii Sijawahi kupokea uaminifu kutoka kwa mtu yeyote kati yenu. Mmekuwa wafuasi Wangu kwa miaka mingi sana, lakini hamjawahi kunionesha hata chembe ya uaminifu. Badala yake mmekuwa mkizunguka kwa watu mnaowapenda na vitu vinavyowapendeza sana, na kuviweka karibu na mioyo yenu na havijawahi kuachwa, wakati wowote, mahali popote. Mnapokuwa na hamu ama shauku na kitu chochote kile Mnachokipenda, siku zote mnakuwa ni wakati ambapo mnanifuata, au hata wakati mnaposikiliza maneno Yangu. Hivyo nasema, mnatumia uaminifu ninaowataka muonyeshe, kwa kufurahia matamanio yenu wenyewe. Ingawa mnaweza kutoa sadaka ya kitu kimoja au vitu viwili kwa ajili Yangu, hakuwakilishi vitu vyenu vyote, na haionyeshi kwamba ni Kwangu ambako uaminifu wako uko kwa kweli. Mnajiweka wenyewe katika shughuli ambazo mnazipenda: Wengine ni waaminifu kwa watoto, wengine kwa waume, wake, utajiri, kazi, wenye vyeo, umaarufu, au wanawake. Kwa maana kile ambacho mnakuwa waaminifu kwacho, hujawahi kuhisi kuchoshwa au kukerwa nacho, badala yake, mnatamani kuwa na kiasi kikubwa zaidi na ubora wa vitu ambavyo mu waaminifu kwavyo na hamjawahi kukata tamaa. Mimi mwenyewe na maneno Yangu daima hutupwa pembeni katika masuala ya vitu mnavyovipenda. Na hamna namna isipokuwa kuyaweka mwisho; wengi hata wanaondoka sehemu ya mwisho kwa ajili ya kuwa waaminifu kwa kitu ambacho hawajakigundua bado. Hawajawahi kuniweka mioyoni mwao kwa kiwango chochote kile. Pengine mtafikiri kwamba ninahitaji mambo mengi sana kutoka kwenu au Ninawahukumu kimakosa, lakini je, mmeshawahi kufikiri kuhusu ukweli huu kwamba mnapotumia muda kwa furaha pamoja na familia yenu, hujawahi kuwa mwaminifu kwangu hata mara moja? Wakati kama huu, hii haiwaumizi? Mioyo yenu inapojawa na furaha kwa kupokea malipo kwa kazi zenu, haiwavunji moyo kwamba hamjajitweka kwa ukweli wa kutosha? Ni lini mmewahi kulia kwa kukosa idhinisho langu? Mnaitesa akili yenu na kupata maumivu makubwa kwa ajili ya watoto wenu, lakini bado hamjaridhika, bado mnaamini kwamba hamjaweka jitihada za kutosha kwao, kwamba hamjatumia nguvu zenu zote. Lakini Kwangu, mmekuwa ajizi na wa kutojali, mkiniweka tu katika kumbukumbu zenu na wala Sidumu ndani ya mioyo yenu. Kujitolea Kwangu na jitihada zangu daima hupita bila nyinyi kuzihisi, na wala hamjawahi kuweka jitihada ili muweze kuelewa. Nyinyi hutafakari kidogo tu na kuamini kwamba hiyo itatosha. “Uaminifu” wa aina hii sio ule ambao Nimekuwa nikiutazamia, bali ni ule ambao umekuwa machukizo Kwangu kwa muda mrefu. Hata hivyo, licha ya kile Ninachokisema, mtaendelea kukubali kitu kimoja tu au vitu viwili na kushindwa kukikubali kwa ukamilifu, kwa maana nyote mnajiamini sana, na siku zote mnachagua kipi mtakachokikubali kutoka katika maneno Niliyoyasema. Kama bado mko hivi, Nina njia katika akiba za kukabiliana na kujiamini kwenu, na Nitazitumia ili muweze kuyatambua maneno Yangu yote kuwa ni kweli na sio upotoshaji wa ukweli.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Where Are Your Expressions of Loyalty to God?

I

You have followed God for all these years without one iota of loyalty. Instead, you’ve revolved around the people that you love and all the things that please you. You always keep them close to your hearts, and you have never once abandoned them. When you become eager or passionate about any one thing that you love, it happens while you are following God, or even while you’re listening to His words. Therefore, God says you are using the loyalty He asks of you to instead be loyal to and cherish your “pets.” You sacrifice a thing or two for God, but that is not your all. It doesn’t show your true loyalty is with Him. God and His words are always being pushed back behind the things that you are passionate about. And you have no choice but to rank them last. There are even those who save this last place for things they’re loyal to that they have yet to discover. Never has there been a slightest trace of God in their hearts.

II

You involve yourselves in undertakings about which you are truly passionate. Some people are loyal to sons and daughters, others to husbands, wives, work, and riches, or superiors, status, or women. Toward all those things you’re loyal to, you never feel weary, never annoyed. Rather you grow more eager to have these things, to have them in even greater numbers and higher quality, never giving up. Therefore, God says you are using the loyalty He asks of you to instead be loyal to and cherish your “pets.” You sacrifice a thing or two for God, but that is not your all. It doesn’t show your true loyalty is with Him. God and His words are always being pushed back behind the things that you are passionate about. And you have no choice but to rank them last. There are even those who save this last place for things they’re loyal to that they have yet to discover. Never has there been a slightest trace of God in their hearts.

from Follow the Lamb and Sing New Songs

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp