Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 100

Mamlaka yenyewe yanaweza kufafanuliwa kama nguvu za Mungu. Kwanza, inaweza kusemekana kwa uhakika kwamba mamlaka na nguvu vyote ni vizuri. Havina uunganisho wowote na kitu chochote kibaya, na havina uhusiano wowote na viumbe vyovyote vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa. Nguvu za Mungu zinaweza kuumba viumbe vya mfumo wowote ulio na uzima na nguvu, na haya yote yanaamuliwa na uzima wa Mungu. Mungu ni uzima, kwa hivyo Yeye ndiye chanzo cha viumbe hai vyote. Vilevile, mamlaka ya Mungu yanaweza kufanya viumbe vyote kutii kila neno la Mungu, yaani kuumbika kulingana na matamshi yanayotoka kwenye kinywa cha Mungu, na kuishi na kuzaana kwa amri ya Mungu, ambapo baadaye Mungu anatawala na kuamuru viumbe vyote hai, na hakutakuwa na kupotoka kokote, daima dawamu. Hakuna mtu au kifaa kilicho na mambo haya; Muumba tu ndiye anayemiliki na aliye na nguvu kama hizo, na hivyo basi yanaitwa mamlaka. Huu ndio upekee wa Muumba. Kwa hivyo, haijalishi kama ni neno lenyewe “mamlaka” au hali halisi ya mamlaka haya, kila mojawapo linaweza tu kuhusishwa na Muumba kwa sababu ni ishara ya utambulisho na hali halisi ya kipekee ya Muumba; na inawakilisha utambulisho na hadhi ya Muumba, mbali na Muumba, hakuna mtu au kifaa kinachoweza kuhusishwa na neno “mamlaka” Huu ni ufasiri wa mamlaka ya kipekee ya Muumba.

Ingawaje Shetani alimwaangalia Ayubu kwa macho ya kutamani mali yake, bila ya ruhusa ya Mungu hakuthubutu kugusa hata unywele mmoja wa mwili wa Ayubu. Ingawaje ni mwenye uovu na unyama wa ndani, baada ya Mungu kutoa shurutisho Lake kwake, Shetani hakuwa na chaguo lakini kutii shurutisho la Mungu. Na kwa hivyo, hata ingawaje Shetani alionekana kana kwamba ameshikwa na kichaa sawa na mbwamwitu miongoni mwa kondoo alipomjia Ayubu, hakuthubutu kusahau mipaka aliyowekewa wazi na Mungu, hakuthubutu kukiuka shurutisho za Mungu, na kwa hayo yote, Shetani hakuthubutu kutoka kwenye kanuni ya maneno ya Mungu—je, hii si kweli? Kutokana na mtazamo huu wa maisha, tunaona kwamba Shetani hathubutu kuvunja matamshi yoyote yale ya Yehova Mungu. Kwake Shetani, kila neno kutoka kwenye kinywa cha Mungu ni shurutisho, na sheria ya kimbinguni, na maonyesho ya mamlaka ya Mungu—kwani nyuma ya kila neno la Mungu kunadokezwa adhabu ya Mungu kwa wale wanaokiuka maagizo ya Mungu, na wale wasiotii na wanaopinga sheria za kimbinguni. Shetani anajua wazi kwamba kama atakiuka shurutisho za Mungu, basi lazima akubali athari za kukiuka mamlaka ya Mungu na kupinga sheria za kimbinguni. Na sasa athari hizi ni zipi? Sina haja ya kusema kwamba, athari hizi bila shaka, ni adhabu kutoka kwa Mungu. Vitendo vya Shetani kwake Ayubu vilikuwa tu mfano mdogo wa yeye kumpotosha binadamu, na wakati ambapo Shetani alipokuwa akitekeleza vitendo hivi, ile mipaka ambayo Mungu Aliweka na amri Alizotoa kwake Shetani vilikuwa tu mfano mdogo wa kanuni zinazotokana na kila kitu anachofanya. Aidha, wajibu na nafasi ya Shetani katika suala hili ulikuwa tu mfano mdogo wa wajibu na nafasi yake katika kazi ya usimamizi wa Mungu, na utiifu kamili wa shetani kwa Mungu wakati alipomjaribu Ayubu, ulikuwa tu mfano mdogo wa namna ambavyo Shetani hakuthubutu kuweka hata upinzani mdogo kwa Mungu katika kazi ya usimamizi wa Mungu. Ni onyo gani ambalo mifano hii midogo inakupa? Miongoni mwa mambo yote, akiwemo Shetani, hakuna mtu au kitu kinachoweza kukiuka sheria na kanuni za mbinguni zilizowekwa wazi na Muumba, na hakuna mtu au kitu kinachothubutu kukiuka sheria na kanuni hizi za mbinguni, kwani hakuna mtu au kifaa kinaweza kubadilisha au kuepuka adhabu ambayo Mungu anawawekea wale wanaokosa kumtii. Ni Muumba tu anayeweza kuanzisha sheria na kanuni za kimbinguni, ni Muumba tu aliye na nguvu za kuanza kuzitekeleza na nguvu za Muumba ndizo haziwezi kukiukwa na mtu au kitu chochote. Haya ndiyo mamlaka ya kipekee ya Muumba, mamlaka haya yako juu zaidi miongoni mwa mambo yote, na kwa hivyo haiwezekani kusema kwamba “Mungu ndiye mkubwa zaidi naye Shetani ni nambari mbili.” Isipokuwa Muumba anayemiliki mamlaka ya kipekee, hakuna Mungu mwengine.

Je, sasa unayo maarifa mapya kuhusu mamlaka ya Mungu? Kwanza, kunayo tofauti kati ya mamlaka ya Mungu yaliyotajwa hivi punde na nguvu za binadamu? Na tofauti ni nini? Baadhi ya wanadamu husema kwamba hakuna ulinganifu wowote kati ya haya mawili. Hayo ni kweli! Ingawaje watu husema kwamba hakuna ulinganisho kati ya haya mawili, kwenye fikira na dhana za binadamu, nguvu za binadamu mara nyingi zinadhaniwa kuwa mamlaka, huku haya mawili yakilinganishwa mara nyingi sako kwa bako. Ni nini kinachoendelea hapa? Je, watu hawafanyi kosa kubadilisha bila ya kuwa waangalifu kitu kimoja na kingine? Vitu hivi viwili havina uhusiano wowote na hakuna ulinganisho wowote kati yavyo, ilhali watu bado hawawezi kuelewa. Je, haya yatatuliwe vipi? Kama ungependa kwa kweli kupata suluhu, njia ya pekee ni kuelewa na kujua mamlaka ya kipekee ya Mungu. Baada ya kuelewa na kujua mamlaka ya Muumba, hutataja kwa mkupuo mmoja nguvu za binadamu na mamlaka ya Mungu.

Nguvu za binadamu zinarejelea nini? Kwa ufupi, ni uwezo au mbinu inayowezesha tabia potoshi, matamanio na malengo ya binadamu kuweza kupanuliwa au kutimizwa hadi kiwango cha juu zaidi. Je, haya yatumike kumaanisha mamlaka? Haijalishi ni vipi ambavyo malengo na matamanio ya binadamu yalivyo makubwa au yenye faida, mtu huyu hawezi kusemekana amemiliki mamlaka; kama amezidi sana, haya majivuno na ufanisi ni maonyesho tu ya upumbavu wa Shetani miongoni mwa binadamu, kama imezidi sana, ni upuzi ambao Shetani anaendeleza kama babu yake mwenyewe ili kutimiza maono yake ya kuwa Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

God’s Authority Is a Symbol of His Identity

I

God is life, the source of all living beings. God’s authority makes all things obey His words. God’s word makes them come into being. When God commands, they will live and reproduce. God rules all living beings, and there’ll be no deviation forever and ever. The power of God can create things of any form that have life and vitality. And this is determined by the life of God.

II

This power, no person nor object holds. The Creator is the only One who has it. It’s a symbol of His unique identity, substance, status, and it’s called authority. God rules all living beings, and there’ll be no deviation forever and ever. The power of God can create things of any form that have life and vitality. And this is determined by the life of God.

III

Remember, apart from Him, no man or thing has anything to do with the word “authority” or its essence. God rules all living beings, and there’ll be no deviation forever and ever. The power of God can create things of any form that have life and vitality. And this is determined by the life of God.

from Follow the Lamb and Sing New Songs

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp