Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 372

25/08/2020

Wanadamu waliutambua upendo Wangu, walinipa huduma itokayo moyoni, na walinitii kwa kweli na kunifanyia kila kitu katika uwepo Wangu. Lakini wanadamu leo hii hawajui kuifikia hali hii ya maisha, bali sasa wanaweza tu kulalamika katika nafsi zao kana kwamba ziliibiwa na mbwa mwitu wakali. Wanaweza tu kunitazama na macho yenye hamu, na kunililia wakitaka msaada. Lakini kutoka mwanzo hadi mwisho, hawawezi kujiondoa katika matatizo yanayowakumba. Ninakumbuka jinsi ambavyo watu wa kale waliweka ahadi mbele Zangu, wakiapa kwa mbingu na dunia mbele Zangu kulipiza ukarimu Wangu kwa upendo. Walilia kwa uchungu mbele Yangu, na kilio chao kilikuwa cha kuvunja moyo na kigumu kuvumilia. Mara kwa mara, Niliwapa wanadamu msaada kwa sababu ya nia zao. Wanadamu wamekuja mbele Zangu mara nyingi kunitii, na mienendo yao ya kupendeza imekuwa ya kukumbukwa. Mara nyingi wanadamu wamekuja kunionyesha upendo kwa imani isiyotingisika, na hisia zao za kweli zimekuwa za kutamanika. Kwa mara nyingi, wamehatarisha maisha yao ili wanionyeshe upendo, wakanipenda Mimi hata zaidi ya wanavyojipenda wenyewe, na kwa vile Nimeona upendo huu ni wa kweli, Nimeukubali. Mara tena na tena wamejitoa kama sadaka mbele Yangu, bila kujali mauti kwa sababu Yangu, na Nimepangusa wasiwasi huo nyusoni mwao, na kwa uangalifu nimekadiria maumbile yao. Kuna nyakati zisizohesabika ambapo Nimewapenda kama mali Yangu ya thamani, na kuna wakati mwingine mwingi ambao Nimewachukia kama adui Zangu. Hivyo ndivyo Nilivyo—mwanadamu hawawezi kutambua kilicho fikirani Mwangu. Wanadamu wakiwa na huzuni, Mimi huja kuwafariji, na wakiwa wanyonge Mimi huja kuwasaidia katika mwendo. Wanapopotea njia, Mimi huwapa mwelekeo. Wanapolia, Mimi hufuta machozi yao. Hata hivyo, Nionapo huzuni, nani anaweza kunifariji kwa moyo wake? Ninapopatwa na hofu, ni nani hujali hisia Zangu? Ninapoona huzuni, ni nani aniondoleaye uchungu Ninaohisi? Ninapohitaji mtu karibu Nami, ni nani anayeshirikiana na Mimi? Inawezekana kuwa malengo yao ya kale Kwangu yamebadilika yasiweze kurudi tena? Ni kwa nini hakuna hata jambo moja kati ya haya wanalokumbuka? Inawezekanaje kuwa wanadamu wameyasahau yote haya? Je, si mambo haya yanatendeka kwa sababu mwanadamu amepotoshwa na adui zake?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 27

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp