Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 104

Mwa 19:1-11 Na jioni malaika wawili walikuja Sodoma; naye Lutu aliketi katika lango la Sodoma: na baada ya Lutu kuwaona aliinuka kwenda kuwakaribisha; na akasujudu; Naye akasema, Tazama saa hii, bwana zangu, ingieni ndani, nawaomba, ndani ya nyumba ya mtumishi wenu, na mbaki usiku mzima, na msafishe miguu yenu, na mtaamka mapema, na mshike njia zenu. Nao wakasema, La; lakini tutaketi katika uwanja usiku mzima. Na akawaomba sana; na wakamjia na kuingia katika nyumba yake; na akawaandalia karamu, na kupika mikate bila chachu, na hawakula. Lakini kabla ya wao kujilaza, watu kutoka mjini, hata wenyeji wa Sodoma, waliizunguka nyumba hiyo, wazee na pia vijana, watu wote kutoka kila sehemu: Na wakamwita Lutu, na kumwambia, Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako leo usiku? Walete kwetu, ili tupate kuwajua. Naye Lutu akatoka mlangoni mahali walipokuwa, na akafunga mlango nyuma yake, Na kusema, nawaomba, ndugu, msitende maovu hivyo. Tazameni sasa, ninao mabinti wawili ambao ni mabikira; mniruhusu, nawaomba, niwalete nje kwenu, na mwafanyie mwonavyo kuwa vizuri katika macho yenu: ila kwa hawa wanaume msifanye chochote: kwani wamekuja chini ya kivuli cha paa langu. Na walisema. Toka. Na wakasema tena, Mtu huyu mmoja aliingia kwetu kukaa kwa muda, naye anatamani kuhukumu: sasa tutakushughulikia kwa njia mbaya zaidi, kuliko wao. Na wakamshinikiza sana mtu huyo, hadi Lutu, na wakawa karibu kuuvunja mlango. Lakini watu wale wakanyosha mbele mkono wao, na kumvuta Lutu katika nyumba walikokuwa, na kuufunga mlango. Na wakawagonga wale watu waliokuwa katika mlango wa nyumba na upofu, wakubwa na wadogo: kiasi kwamba walijichosha kuutafuta mlango.

Mwa 19:24-25 Kisha Yehova alinyesha kwa Sodoma na Gomora kibiriti na moto kutoka Yehova kutoka mbinguni; Na akaiangusha hiyo miji, na mabonde yote, na wenyeji wote wa miji hiyo, na kile kilichomea kutoka ardhini.

Kutoka kwenye mafungu haya, si vigumu kuona kwamba dhambi ya Sodoma na kupotoka kwake tayari vilikuwa vimefikia kiwango kilichochukiza binadamu na Mungu, na kwamba kwa macho ya Mungu mji ulifaa kuangamizwa. Lakini nini kilichofanyikia mji huu hapo awali kabla haujaangamizwa? Ni nini tunachoweza kujifunza kutoka kwenye matukio haya? Je, mtazamo wa Mungu katika matukio haya unatuonyesha nini kuhusu tabia yake? Ili kuelewa hadithi nzima, hebu na tuweze kusoma kwa makini kile kilichorekodiwa katika Maandiko …

Kupotoka kwa Sodoma: Kunakasirisha Binadamu, Kunaghadhibisha Mungu

Kwenye usiku huo, Lutu alipokea wajumbe wawili kutoka kwa Mungu na akawatayarishia karamu. Baada ya chajio, kabla hawajalala, watu kutoka kila pahali kwenye mji walizunguka makazi ya Lutu na kumwita nje Lutu. Maandiko yanawarekodi wakisema, “Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako leo usiku? Walete kwetu, ili tupate kuwajua.” Ni nani aliyesema maneno haya? Alikuwa akiwaambia kina nani? Haya yalikuwa maneno ya watu wa Sodoma, walipiga mayowe nje ya makazi ya Lutu wakinuia kumwita Lutu. Je, unahisi vipi ukiyasikia maneno haya? Unaghadhibishwa? Je, maneno haya yanakuhuzunisha? Je, unabubujikwa na hasira kali? Je, Huoni kwamba maneno haya yananuka Shetani? Kupitia kwa maneno haya, unaweza kuhisi uovu na giza vilivyomo kwenye mji huu? Je, unaweza kuhisi ukatili na ushamba wa tabia za watu hawa kupitia kwa maneno yao? Je, unaweza kuhisi kina cha kupotoka kwao kupitia kwa tabia yao? Kupitia kwa maudhui ya hotuba yao, si vigumu kuona kwamba asili yao ya dhambi na tabia yao iliyopotoka ilikuwa imefikia kiwango kilichokuwa zaidi ya wao kuidhibiti. Isipokuwa Lutu, kila mtu katika mji huu hakuwa tofauti na Shetani; ule mtazamo tu wa mtu mwingine uliwafanya watu hawa kutaka kudhuru na kuwapotosha wao…. Mambo haya hayampatii tu mtu hisia ya asili potovu na ya kutisha ya mji huu, lakini pia yanamwonyesha harufu ya kifo iliyouzunguka mji huu; yanampa pia mtu hisia za dhambi na umwagikaji wa damu.

Alipojipata uso kwa uso na genge la majambazi waliojaa ukatili, watu waliokuwa wamejaa na maono ya kupotosha nafsi, Lutu aliitikia vipi? Kulingana na Maandiko: “Nawaomba … msitende maovu hivyo. Tazameni sasa, ninao mabinti wawili ambao ni mabikira; mniruhusu, nawaomba, niwalete nje kwenu, na mwafanyie mwonavyo kuwa vizuri katika macho yenu: ila kwa hawa wanaume msifanye chochote: kwani wamekuja chini ya kivuli cha paa langu.” Lutu alimaanisha yafuatayo katika maneno yake: Alikuwa radhi kuwatoa binti zake wawili ili kuwalinda wale wajumbe. Kutokana na akili razini, watu hawa wangekubali masharti ya Lutu na kuwaacha wale wajumbe wawili pekee; kwani hata hivyo, wajumbe hao walikuwa watu wageni kabisa kwao, watu ambao hawakuwa na chochote katu kuhusiana na wao; wajumbe hawa wawili walikuwa hawajawahi kudhuru masilahi yao. Hata hivyo, wakiwa na motisha ya asili yao ya dhambi, hawakuliwachia suala hili hapo. Badala yake, walizidisha tu jitihada zao. Hapa mojawapo ya mabishano yao yanaweza bila shaka kumpatia mtu maono zaidi kuhusu asili ya kweli na potovu ya watu hawa; wakati uo huo yanatujuza na kutufanya tuelewe sababu ya Mungu kutaka kuuangamiza mji huu.

Kwa hivyo walisema nini baadaye? Kama vile Biblia inavyosoma: “Toka. Na wakasema tena, Mtu huyu mmoja aliingia kwetu kukaa kwa muda, naye anatamani kuhukumu: sasa tutakushughulikia kwa njia mbaya zaidi, kuliko wao. Na wakamshinikiza sana mtu huyo, hadi Lutu, na wakawa karibu kuuvunja mlango.” Kwa nini walitaka kuuvunja mlango? Sababu ni kwamba walikuwa na hamu kubwa zaidi ya kuwadhuru wale wajumbe wawili. Wale wajumbe walikuwa wakifanya nini Sodoma? Kusudio lao la kuja hapo lilikuwa ni kumwokoa Lutu na familia yake; hata hivyo, watu wa mji huo walifikiri kimakosa kwamba walikuwa wamekuja kuchukua nyadhifa zao rasmi. Bila ya kuulizia kusudio lao, ilikuwa tu hali ya kujiamulia kufanya mambo kabla ya kujua ukweli wake, iliyoufanya mji huo kutaka kuwadhuru vibaya wajumbe hawa wawili; walitaka kuwadhuru watu wawili ambao hawakuhusiana kwa vyovyote vile na wao. Ni wazi kwamba watu wa mji huu walikuwa wamepoteza kabisa ubinadamu na akili zao razini. Kiwango cha wendawazimu wao na kukosa ustaarabu kwao kilikuwa tayari si tofauti na asili potovu ya Shetani ya kudhuru na kudanganya binadamu.

Walipowaamuru watu hawa watoke kwa Lutu, Lutu alifanya nini? Kutoka kwenye maandishi yanayofuata tunajua kwamba Lutu hakuwakabidhi wajumbe hawa kwa watu hawa. Je, Lutu aliwajua wajumbe hawa wawili wa Mungu? Bila shaka la! Lakini kwa nini aliweza kuwaokoa watu hawa wawili? Je, alijua ni nini walichokuwa wamekuja kufanya? Ingawaje hakujua kuhusu sababu yao ya kuja, alijua kwamba walikuwa ni watumishi wa Mungu, na kwa hivyo aliwapokea. Kwamba aliweza kuwaita watumishi hawa wa Mungu mabwana yaonyesha kwamba Lutu kwa kawaida alikuwa ni mfuasi wa Mungu, tofauti na wale wengine waliokuwa ndani ya Sodoma. Kwa hivyo, wakati wajumbe wa Mungu walipomjia, alihatarisha maisha yake binafsi ili kuwapokea watumishi hao wawili; aidha, aliwakabidhi binti zake wawili badala ya watumishi hao wawili ili kuwalinda watumishi hao. Hiki ndicho kitendo cha haki ya Lutu; vilevile ni onyesho linaloonekana waziwazi kuhusu asili na hali halisi ya Lutu, na ndiyo pia sababu ya Mungu kuwatuma watumishi Wake ili kumwokoa Lutu. Wakati alipokabiliwa na changamoto, Lutu aliwalinda watumishi hawa wawili bila kujali chochote kingine; alijaribu hata kufanya biashara ya kuwabadilisha binti zake wawili mradi tu watumishi hawa wapate usalama. Mbali na Lutu, kulikuwa na mtu yeyote mwingine ndani ya mji ambaye angefanya jambo kama hili? Kama vile hoja zinavyothibitisha—la! Kwa hivyo, ni wazi kabisa kwamba kila mtu katika Sodoma, isipokuwa Lutu, alikuwa mlengwa wa kuangamizwa pamoja na mlengwa aliyestahili kuangamizwa.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp