Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 183

06/08/2020

Yesu Alikuwa duniani kwa miaka thelathini na tatu na nusu, Alikuja kufanya kazi ya usulubisho na kupitia usulubisho, Mungu Alipata sehemu moja ya utukufu. Mungu Alipokuja katika mwili, Aliweza kunyenyekea na kujificha, na Aliweza kustahimili mateso makubwa. Japokuwa Alikuwa Mungu Mwenyewe, bado Alipitia kila aina ya fedheha, na kila aina ya matusi, na Alipitia uchungu mkubwa kwa kuangikwa msalabani ili kukamilisha kazi ya ukombozi. Baada ya hatua hii ya kazi kutamatishwa, japokuwa watu waliona kuwa Mungu Alikuwa Amepata utukufu mkubwa, huu haukuwa ukamilifu wa utukufu Wake; ilikuwa tu sehemu moja ya utukufu Wake ambao Alikuwa Amepata kutoka kwa Yesu. Japokuwa Yesu Aliweza kupitia magumu ya kila aina, kuwa Mnyenyekevu na kujificha, kusulubishwa kwa ajili ya Mungu, Mungu Alipata tu sehemu moja ya utukufu Wake, na utukufu Wake ulipatikana Israeli. Mungu bado Ana sehemu nyingine ya utukufu: kuja duniani kufanya kazi na kufanya kundi la watu kuwa wakamilifu. Wakati wa hatua ya kazi ya Yesu, Alifanya baadhi ya mambo ambayo si ya kawaida, ila ile hatua ya kazi kwa yoyote ile haikuwa tu ili kufanya ishara na maajabu. Kimsingi ilikuwa kuonyesha kuwa Yesu Angeweza kuteseka na kusulubishwa kwa ajili ya Mungu, kwamba Yesu Angeweza kupitia uchungu mkubwa kwa kuwa Alimpenda Mungu, na kwamba japokuwa Mungu Alimtelekeza, bado Alikuwa radhi kuyatoa maisha Yake kwa ajili ya mapenzi ya Mungu. Baada ya Mungu kukamilisha kazi Yake Israeli na Yesu Kuangikwa msalabani, Mungu Alitukuzwa, na Mungu Alikuwa na ushuhuda mbele ya Shetani. Hamjui na wala hamjaona jinsi Mungu Amekuwa mwili nchini Uchina, basi mnaonaje kuwa Mungu Ametukuzwa? Mungu Anapofanya kazi nyingi ya ushindi kwenu, na mnasimama imara, basi hii kazi ya Mungu inakuwa ya mafanikio, na hii ni sehemu ya utukufu wa Mungu. Mnaliona hili tu na bado hamjafanywa na Mungu kuwa wakamilifu, bado hamjaitoa roho yenu kwa Mungu kikamilifu. Bado hamjauona huu utukufu kwa ukamilifu; mnaona tu kwamba Mungu Ameushinda moyo wenu tayari, kwamba hammuachi kamwe na kwamba mtamfuata Mungu mpaka mwisho na moyo wenu hautabadilika. Huu ndio utukufu wa Mungu. Ni katika kitu gani mnauona utukufu wa Mungu? Kwenye athari za kazi Yake kwa wanadamu. Watu huona kuwa Mungu anapendeza sana, wana Mungu mioyoni mwao, na hawako radhi kumuacha, na huu ni utukufu wa Mungu. Wakati ambapo uthabiti wa ndugu na dada wa makanisa unapotokea, na wanaweza kumpenda Mungu kutoka mioyoni mwao, na kuuona ukuu wa kazi inayofanywa na Mungu, ukuu usiomithilika wa maneno Yake, waonapo kwamba maneno yake yanabeba mamlaka na kwamba anaweza kuanzisha kazi Yake katika miji iliyohamwa katika bara ya Uchina, wakati ambapo, japo watu ni wanyonge, mioyo yao inasujudu mbele ya Mungu na wako radhi kuyakubali maneno ya Mungu, na wakati ambapo, japo ni wanyonge na wasiofaa, wanaweza kuona kuwa maneno ya Mungu ni ya kupendeza sana na yastahili utunzaji wao basi huu ndio utukufu wa Mungu. Siku ikija ambayo watu watafanywa wakamilifu na Mungu, na wanaweza kujisalimisha mbele Yake, na kuweza kumtii Mungu kabisa, na kuyawacha matarajio na majaliwa yao mikononi mwa Mungu, basi sehemu ya pili ya utukufu wa Mungu itakuwa imepatikana kikamilifu. Hii ni kusema kuwa wakati ambapo kazi ya Mungu wa vitendo itakapokuwa imekamilishwa kabisa, kazi Yake katika bara ya Uchina itafika kikomo; kwa maneno mengine, wakati wale walioamuliwa kabla na kuchaguliwa na Mungu watakapokuwa wamefanywa wakamilifu, Mungu Atatukuzwa. Mungu Alisema kwamba Ameleta sehemu ya pili ya utukufu Wake Mashariki, na bado hili halionekani kwa macho. Mungu Ameleta kazi Yake Mashariki: tayari Amekuja Mashariki, na huu ni utukufu wa Mungu. Leo ingawa kazi yake haijakamilika bado, kwa sababu Mungu Ameamua kufanya kazi, bila shaka itakamilika. Mungu Ameamua kuwa Ataikamilishia kazi yake Uchina, na Ameamua kuwafanya wakamilifu. Hivyo Hawapatii njia nyingine—tayari Ameishinda mioyo yenu, na lazima utaendelea upende usipende, na mnapokubaliwa na Mungu, Mungu Anatukuzwa. Leo hii bado Mungu Hajatukuzwa kikamilifu, kwa sababu bado hujafanywa kuwa wakamilifu, na ingawa moyo wako umerudi kwa Mungu, bado kuna udhaifu mwingi katika mwili wako, hauna uwezo wa kumridhisha Mungu, huwezi kushughulishwa na mapenzi ya Mungu, na kuna vitu vingi hasi ambavyo ni sharti vitokomezwe kutoka kwenu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp