Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 109

Unaweza kuona hali halisi ya hasira ya Mungu katika kuangamiza Kwake kwa Sodoma? Je, kuna jambo lolote lililochanganyika kwenye hasira Yake kali? Je, hasira kali ya Mungu ni safi? Ili kutumia maneno ya binadamu, je, hasira kali ya Mungu imetiwa najisi? Je, kunayo hila yoyote katika hasira Yake? Je, kunayo njama yoyote? Je, zipo siri zozote zisizotamkika? Ninaweza kukwambia wazi na kwa makini: Hakuna sehemu ya hasira ya Mungu inayoweza kumwongoza mtu kwa shaka. Ghadhabu yake haina kasoro, ni hasira ambayo haijatiwa najisi na haijasheheni nia au shabaha zozote zingine. Sababu ya ghadhabu Yake ni safi, haina lawama na haipingiki. Ni ufunuo wa kawaida na onyesho la hali Yake halisi ya utakatifu; ni kitu ambacho hakuna kiumbe chochote kinamiliki. Hii ni sehemu ya tabia ya kipekee ya haki ya Mungu, na ni utofauti wa wazi kati ya hali halisi husika ya Muumba na uumbaji Wake.

Haijalishi kama mtu anakuwa na ghadhabu akiwa mbele ya wengine au wakiwa hawako naye, kila mtu anayo nia na kusudi tofauti. Pengine wanajenga heshima zao, au pengine wanatetea masilahi yao binafsi, na kuendeleza taswira yao au kulinda sura yao. Baadhi yao huendeleza hali ya kuzuia ghadhabu yao, huku nao wengine wanakimbilia na wanapandwa na hasira kali kila wanapopenda bila ya hata kiwango kidogo zaidi cha kujizuia. Kwa ufupi, ghadhabu ya binadamu inatokana na tabia yake iliyopotoka. Haijalishi kusudi lake, ni la mwili na ni la asili; halina uhusiano wowote na haki au ukiukaji wa haki kwa sababu hakuna kitu katika asili ya binadamu na hali halisi vinavyolingana na ukweli. Kwa hivyo, hasira ya binadamu wapotovu na hasira ya Mungu vyote havifai kutajwa kwa kiwango sawa. Bila ya kuacha, tabia ya binadamu iliyopotoshwa na Shetani inaanza kwa tamanio la kusalimisha kupotoka, na inatokana na kupotoka; hivyo basi, ghadhabu ya binadamu haiwezi kutajwa kwa kiwango sawa na hasira ya Mungu, haijalishi ni bora namna gani kinadharia. Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake kali, nguvu za giza zinakaguliwa, mambo ya giza yanaangamizwa, huku mambo ya haki na mazuri yakifurahia utunzaji wa Mungu, ulinzi, na yote yanaruhusiwa kuendelea. Mungu hushusha hasira Yake kwa sababu ya mambo dhalimu, mabaya na ya giza, yanayozuia, yanayotatiza au kuangamiza shughuli na maendeleo ya kawaida ya mambo ya haki na mazuri. Shabaha ya ghadhabu ya Mungu si kusalimisha hadhi na utambulisho Wake binafsi, lakini kusalimisha uwepo wa mambo ya haki, mazuri, ya kupendeza na kuvutia, kusalimisha sheria na mpangilio wa kuwepo kwa kawaida kwa binadamu. Hiki ndicho chanzo asilia cha hasira ya Mungu. Hasira kali ya Mungu ni bora sana, ya kiasili na ufunuo wa kweli wa tabia Yake. Hakuna makusudi yoyote katika hasira Yake kali, wala hakuna udanganyifu au njama yoyote; au hata zaidi, hasira Yake kali haina tamanio lolote, ujanja, mambo ya kijicho, udhalimu, maovu, au kitu kingine ambacho binadamu wote waliopotoka huwa navyo. Kabla ya Mungu kushusha hasira Yake kali, huwa tayari Ametambua hali halisi ya kila suala kwa uwazi na ukamilifu zaidi, na huwa tayari Amepangilia ufafanuzi na hitimisho sahihi na zilizo wazi. Hivyo basi, lengo la Mungu katika kila suala Analofanya ni wazi kabisa, vile ulivyo mtazamo Wake. Yeye si mtu aliyechanganyikiwa; Yeye si kipofu; Yeye si mtu wa kuamua ghafla; Yeye si mzembe; na zaidi, Yeye si mtu asiyefuata kanuni. Hii ndiyo dhana ya kimatendo ya hasira ya Mungu, na ni kwa sababu ya dhana hii ya kimatendo ya hasira ya Mungu kwamba binadamu wamefikia uwepo wao wa kawaida. Bila ya hasira ya Mungu, binadamu wangeishia kuishi katika mazingira yasiyo ya kawaida; viumbe vyote vyenye haki, virembo na vizuri vingeangamizwa na kusita kuwepo. Bila ya hasira ya Mungu, sheria na mpangilio unaotawala uumbaji vingekiukwa au hata kupinduliwa kabisa. Tangu uumbwaji wa binadamu, Mungu ametumia bila kusita, tabia Yake ya haki kusalimisha na kuendeleza uwepo wa kawaida wa binadamu. Kwa sababu tabia Yake ya haki inayo hasira na adhama, watu wote waovu, vitu, vifaa na vitu vyote vinavyotatiza na kuharibu uwepo wa kawaida wa binadamu vinaadhibiwa, vinadhibitiwa na kuangamizwa kwa sababu ya hasira Yake. Kwenye milenia mbalimbali zilizopita, Mungu ameendelea kutumia tabia Yake ya haki kuangusha na kuangamiza kila aina za roho chafu na za giza ambazo zinampinga Mungu na kuchukua nafasi ya wasaidizi wa Shetani na kusaidia katika kazi Yake ya kuwasimamia binadamu. Hivyo basi, kazi ya Mungu ya wokovu wa binadamu siku zote imeimarika kulingana na mpango Wake. Hivi ni kusema kwamba kwa sababu ya uwepo wa hasira ya Mungu, sababu ya haki zaidi miongoni mwa binadamu haijawahi kuangamizwa.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp