Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 52
25/05/2020
Uhusiano Kati ya Mungu kumpa Shetani Ayubu na Malengo ya Kazi ya Mungu
Ingawaje watu wengi sasa wanatambua kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu na kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu, utambuzi huu hauwapi uelewa mkubwa zaidi wa nia ya Mungu. Wakati huohuo wakionea wivu ubinadamu na ushughulikaji wa Ayubu, wanamuuliza Mungu swali lifuatalo: Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu sana, watu walimpenda sana, kwa hivyo kwa nini Mungu akamkabidhi kwa Shetani na kumpitishia maumivu haya makali? Maswali kama hayo yanatarajiwa kuwepo katika mioyo ya watu wengi—au, kushuku huku ndiko hasa swali katika mioyo ya watu wengi. Kwa sababu kushuku huku kumeshangaza watu wengi sana, lazima tuliwasilishe swali hili waziwazi na kulielezea kikamilifu.
Kila kitu ambacho Mungu anafanya kinahitajika, na kina umuhimu usio wa kawaida, kwani kila kitu anachofanya ndani ya binadamu kinahusu usimamizi wake na wokovu wa wanadamu. Kiasili kazi ambayo Mungu alimfanyia Ayubu si tofauti, ingawaje Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu mbele ya macho ya Mungu. Kwa maneno mengine, licha ya kile ambacho Mungu anafanya au mbinu ambazo Anatumia kufanya, licha ya gharama, au lengo Lake, kusudio la hatua Zake halibadiliki. Kusudio Lake ni kuweza kumshughulikia binadamu ili maneno ya Mungu yaingie ndani yake, mahitaji ya Mungu, na mapenzi ya Mungu kwa binadamu; kwa maneno mengine, ni kufanyia kazi huyu binadamu ili vyote ambavyo Mungu Anasadiki kuwa vizuri kulingana na hatua Zake, kumwezesha binadamu kuuelewa moyo wa Mungu na kufahamu kiini cha Mungu, na kumruhusu yeye kutii ukuu na mipangilio ya Mungu, na hivyo basi kumruhusu binadamu kuweza kufikia kiwango cha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu—yote ambayo ni kipengele kimoja ya kusudio la Mungu katika kila kitu Anachofanya. Kipengele kingine ni kwamba, kwa sababu Shetani ndiye foili na chombo cha huduma katika kazi ya Mungu, mara nyingi binadamu hukabidhiwa Shetani; hizi ndizo mbinu ambazo Mungu hutumia ili kuwaruhusu watu kuweza kuona maovu, ubaya, kudharaulika kwa Shetani katikati ya majaribio na mashambulizi ya Shetani na hivyo basi kuwasababisha watu kumchukia Shetani na kuweza kutambua kile ambacho ni kibaya. Mchakato huu unawaruhusu kwa utaratibu kuanza kuwa huru dhidi ya udhibiti wa Shetani, na dhidi ya mashtaka, uingiliaji kati, na mashambulizi ya Shetani—mpaka, kwa sababu ya maneno ya Mungu, maarifa yao na utiifu wao kwa Mungu, na imani yao kwa Mungu na kuweza kwao kumcha Mungu, wanashinda dhidi ya mashambulizi ya Shetani na kushinda dhidi ya mashtaka ya Shetani; hapo tu ndipo watakapokuwa wamekombolewa kabisa dhidi ya utawala wa Shetani. Ukombozi wa watu unamaanisha kwamba Shetani ameshindwa, unamaanisha kwamba wao si tena chakula kwenye kinywa cha Shetani—kwamba badala ya kuwameza wao, Shetani amewaachilia. Hii ni kwa sababu watu kama hao ni wanyofu, kwa sababu wanayo imani, utiifu na wanamcha Mungu, na kwa sababu wako huru kabisa dhidi ya Shetani. Wamemletea Shetani aibu, wamemfanya kuonekana mjinga, na wamemshinda kabisa Shetani. Imani yao katika kumfuata Mungu, na utiifu na kumcha Mungu kunamshinda Shetani, na kumfanya Shetani kukata tamaa kabisa na wao. Watu kama hawa ndio ambao Mungu amewapata kwa kweli, na hili ndilo lengo kuu la Mungu katika kumwokoa binadamu. Kama wangependa kuokolewa, na wangependa Mungu awapate kabisa, basi wote wanaomfuata Mungu lazima wakabiliane na majaribio na mashambulizi yakiwa makubwa na hata madogo kutoka kwa Shetani. Wale wanaoibuka katika majaribio na mashambulizi haya na wanaweza kumshinda Shetani ni wale waliookolewa na Mungu. Hivi ni kusema kwamba wale waliookolewa na Mungu ni wale ambao wamepitia majaribio ya Mungu, na ambao wamejaribiwa na kushambuliwa na Shetani mara nyingi. Wale waliookolewa na Mungu wanayaelewa mapenzi na mahitaji ya Mungu, na wanaweza kuukubali ukuu na mipangilio ya Mungu na hawaachi njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu katikati ya majaribio ya Shetani. Wale waliookolewa na Mungu wanamiliki uaminifu, wao ni wakarimu, na wanaweza kutofautisha upendo na chuki, wanayo hisia ya haki na urazini, na wanaweza kumtunza Mungu na kuthamini sana kila kitu ambacho ni cha Mungu. Watu kama hao hawatekwi bakunja, kufanyiwa upelelezi, kushtakiwa au kudhulumiwa na Shetani, wako huru kabisa, wamekombolewa na kuachiliwa kabisa. Ayubu alikuwa mtu kama huyo mwenye uhuru na huu ndio umuhimu hasa wa kwa nini Mungu alikuwa amemkabidhi kwa Shetani.
Ayubu alidhulumiwa na Shetani, lakini pia aliweza kupata uhuru na ukombozi wa milele, na kupata haki ya kutowahi kukabidhiwa tena kwa upotovu, unyanyasaji, na mashtaka ya Shetani, na badala yake kuishi katika nuru ya udhibiti wa Mungu usio na pingamizi na kuishi katikati ya baraka kutoka kwa Mungu. Hakuna ambaye angechukua au kuangamiza, au kupata haki hii. Ilipewa kwa Ayubu kutokana na imani, bidii, na utiifu wake kwa na kumcha Mungu; Ayubu alilipia gharama ya maisha yake ili kuweza kupata shangwe na furaha duniani, ili kufanikiwa kupata haki na kuweza kustahili, kama ilivyoamriwa mbinguni na kutambuliwa na dunia, ili kumwabudu Muumba bila ya uingiliaji kati kama kiumbe wa kweli wa Mungu duniani. Hivyo pia ndivyo yalivyokuwa matokeo makubwa zaidi ya majaribio yaliyovumiliwa na Ayubu.
Wakati watu bado hawajaokolewa, maisha yao mara nyingi yanaingiliwa kati na hata kudhibitiwa na, Shetani. Kwa maneno mengine, watu ambao hawajaokolewa ni wafungwa wa Shetani, hawana uhuru, hawajaachiliwa na Shetani, hawajafuzu wala kustahili kumwabudu Mungu, na wanafuatiliwa kwa karibu na kushambuliwa kwa ukali na Shetani. Watu kama hawa hawana furaha ya kuzungumzia, hawana haki ya uwepo wa kawaida wa kuzungumzia, na zaidi hawana heshima ya kuzungumzia. Ni pale tu unaposimama imara na kupigana na Shetani, kwa kutumia imani yako katika Mungu na utiifu kwake, pamoja na kumcha Mungu kama silaha ambazo utatumia kupigana vita vya maisha na mauti dhidi ya Shetani, kiasi cha kwamba utamshinda kabisa Shetani na kumsababisha kukata tamaa na kuwa mwoga kila anapokuona wewe, ili aache kabisa mashambulizi na mashtaka yake dhidi yako—hapo tu ndipo utakapookolewa na kuwa huru. Kama umeamua kutengana kabisa na Shetani lakini huna silaha zitakazokusaidia kupigana na Shetani, basi bado utakuwa katika hatari; kwa kadri muda unaposonga, baada ya wewe kuteswa na Shetani kiasi cha kwamba huna hata usuli wa nguvu uliobakia ndani mwako, lakini bado hujaweza kuwa na ushuhuda, bado hujajifungua kabisa kuwa huru dhidi ya mashtaka na mashambulizi ya Shetani dhidi yako, basi utakuwa na tumaini dogo la wokovu. Mwishowe, wakati hitimisho la kazi ya Mungu itakapotangazwa, bado utakuwa katika mashiko ya Shetani, usiweze kujiachilia kuwa huru, na hivyo hutawahi kuwa na fursa au tumaini. Matokeo yake, hivyo basi, ni kwamba watu kama hao watakuwa mateka kabisa wa Shetani.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video