Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 135

Hakuna Anayeweza Kubadilisha Hoja Kwamba Mungu Anashikilia Ukuu juu ya Hatima ya Binadamu

Katika mamlaka ya Mungu kila mtu anakubali waziwazi au kimyakimya ukuu Wake na mipangilio Yake, na haijalishi ni vipi ambavyo mtu anashughulika katika mkondo wa maisha yake, haijalishi ni njia ngapi mbovu ambazo mtu ametembelea, mwishowe atarudi tu kwenye mzingo wa hatima ambayo Muumba amempangia yeye. Hii ndiyo hali isiyoshindika ya mamlaka ya Muumba, namna ambavyo mamlaka Yake yanavyodhibiti na kutawala ulimwengu. Ni hii hali ya kutoshindika, mfumo huu wa kudhibiti na kutawala, ambao unawajibikia sheria zinazoamuru maisha ya mambo yote, zinazoruhusu binadamu kuweza kuhama hadi kwenye mwili tofauti baada ya kifo tena na tena bila uingiliaji kati, zinazofanya ulimwengu kugeuka mara kwa mara na kusonga mbele, siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka. Mmeshuhudia hoja hizi zote na unazielewa, haijalishi kama ni za juujuu ama ni za kina; kina cha ufahamu wako kinategemea kile unachopitia na maarifa ya ukweli, na maarifa yako kuhusu Mungu. Kujua kwako vyema uhalisia wa ukweli, ni kiwango kipi ambacho umepitia matamshi ya Mungu, ni vipi unajua vyema hali halisi ya Mungu na tabia yake—hii inawakilisha kina cha ufahamu wako wa ukuu na mipangilio ya Mungu. Je, uwepo wa ukuu wa Mungu na mipangilio unategemea kama binadamu wanainyenyekea? Je, hoja kwamba Mungu anamiliki mamlaka haya inaamuliwa na kama binadamu watayanyenyekea? Mamlaka ya Mungu yapo licha ya hali mbalimbali; katika hali zote, Mungu anaamuru na kupangilia hatima ya kila binadamu na mambo yote kulingana na fikira Zake, mapenzi Yake. Hali hii haitabadilika kwa sababu binadamu hubadilika, na iko huru wala haitegemei mapenzi ya binadamu, haiwezi kubadilishwa na mabadiliko yoyote ya muda, anga, na jiografia, kwani mamlaka ya Mungu ndiyo hali yake halisi kabisa. Kama binadamu anaweza kujua na kuukubali ukuu wa Mungu, na kama binadamu anaweza kuunyenyekea, haiwezi kwa vyovyote vile kubadilisha hoja kwamba ukuu wa Mungu upo juu ya hatima ya binadamu. Hivi ni kusema kwamba, haijalishi ni mtazamo gani ambao binadamu atachukua kwa ukuu wa Mungu, hauwezi tu kubadilisha hoja kwamba Mungu anashikilia ukuu juu ya hatima ya binadamu na juu ya mambo yote. Hata kama hutanyenyekea katika ukuu wa Mungu, angali Anaamuru hatima yako; hata kama huwezi kujua ukuu Wake, mamlaka Yake yangali yapo. Mamlaka ya Mungu na hoja ya ukuu wa Mungu dhidi ya hatima ya binadamu viko huru dhidi ya mapenzi ya binadamu, havibadiliki kulingana na mapendeleo na machaguo yako ya binadamu. Mamlaka ya Mungu yapo kila mahali, kila saa, kila muda. Kama mbingu na nchi zingepita, mamlaka Yake yasingewahi kupita, kwani Yeye ni Mungu Mwenyewe, Anamiliki mamlaka ya kipekee, na mamlaka Yake hayazuiliwi au kuwekewa mipaka na watu, matukio, au vitu, na anga au na jiografia. Siku zote Mungu hushikilia mamlaka Yake, huonyesha uwezo Wake, huendeleza usimamizi Wake wa kazi kama kawaida; kila wakati Anatawala viumbe wote, hutosheleza viumbe wote, huunda na kupangilia viumbe wote, kama Alivyofanya siku zote. Hakuna anayeweza kubadilisha hili. Hii ni hoja; huu umekuwa ukweli usiobadilika tangu zama za kale!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp