Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 140

Mazungumzo kati ya Shetani na Yehova Mungu

Ayubu 1:6-11 Sasa kulikuweko na siku ambapo wana wa Mungu walikuja kujidhihirisha mbele za Yehova, naye Shetani akaja pia kati yao. Naye Yehova akasema kwa Shetani, Ni wapi umetoka? Basi Shetani akamjibu Yehova, na kunena, Natoka katika kuenda hapa na pale duniani, na katika kutembea juu chini humo. Naye Yehova akasema kwa Shetani, je, umemfikiria mtumishi wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu? Kisha Shetani akamjibu Yehova, na kusema, je, Ayubu anamcha Mungu bure? Wewe hujamzunguka kila upande na ukingo, na kila upande wa nyumba yake, na kila upande wa yote aliyo nayo? Umebariki kazi ya mikono yake, na mali yake inaongezeka nchini. Lakini nyosha mbele mkono wako sasa, na uguse yote aliyo nayo, na yeye atakulaani mbele ya uso wako.

Ayubu 2:1-5 Tena kulikuweko na siku ambapo wana wa Mungu walikuja kujidhihirisha mbele za Yehova, naye Shetani akaja pia kati yao ili kujidhihirisha mbele za Yehova. Naye Yehova akasema kwa Shetani, Ni wapi umetoka? Na Shetani akamjibu Yehova, na kunena, Natoka katika kuenda hapa na pale duniani, na katika kutembea juu chini humo. Naye Yehova akasema kwa Shetani, je, umemfikiria mtumishi wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu? Na bado anashikilia ukamilifu wake, ingawa ulinichochea dhidi yake, ili mimi nimwangamize bila sababu. Naye Shetani akamjibu Yehova, na akasema, Ngozi kwa ngozi, ndiyo, yote ambayo mtu anayo atayatoa kwa sababu ya uhai wake. Lakini nyosha mbele mkono wako sasa, na uguse mfupa wake na nyama yake, na yeye atakulaani mbele ya uso wako.

Katika mpango wa Mungu wa usimamizi wa miaka elfu sita, vifungu hivi viwili ambavyo Shetani anasema na mambo ambayo Shetani anafanya katika kitabu cha Ayubu yanawakilisha upinzani wake kwa Mungu, na hivi ndivyo Shetani akidhihirisha alivyo kwa kweli. Umeyaona maneno na matendo ya Shetani katika maisha halisi? Utakapoyaona, unaweza kutoyafikiria kuwa vitu vilivyoongelewa na Shetani, lakini badala yake kuyafikiria kuwa vitu vilivyoongelewa na mwanadamu, siyo? Kipi kilichowakilishwa, wakati mambo kama hayo yanazungumzwa na mwanadamu? Shetani anawakilishwa? Hata kama utamtambua, bado huwezi kuona kwamba ukweli unazungumzwa na Shetani. Lakini hapa na sasa umeona bila shaka kile ambacho Shetani mwenyewe amesema. Sasa una uelewa usio na shaka na ulio wazi kabisa wa uso wenye sura mbaya na uovu wa Shetani. Hivyo hivi vifungu viwili vilivyozungumzwa na Shetani ni vya thamani kwa watu wa leo kuweza kujua asili ya Shetani? Hivi vifungu viwili vinastahili kukusanywa ili binadamu leo aweze kutambua uso wenye sura mbaya wa Shetani, kutambua uso wa asili na wa kweli wa Shetani? Ingawa kusema jambo hili hakuonekani kufaa sana, kulieleza kwa njia hii bado kunaweza kuchukuliwa kuwa sahihi. Naweza tu kuliweka kwa njia hii na iwapo mnalielewa, basi imetosha. Tena na tena, Shetani anayashambulia mambo ambayo Yehova Mungu anafanya, akitoa mashtaka kuhusu kumcha Yehova Mungu kwa Ayubu. Anajaribu kumchochea Yehova Mungu kwa kutumia mbinu mbalimbali, kumfanya Yehova Mungu kumkubali kumjaribu Ayubu. Maneno yake basi yanachochea sana. Basi Niambieni, baada ya Shetani kuzungumza maneno haya, Mungu anaweza kuona wazi kile ambacho Shetani anataka kufanya? (Ndiyo.) Je, Mungu anaelewa kile anataka kufanya? (Ndiyo.) Katika moyo wa Mungu, huyu mtu Ayubu ambaye Mungu anamwangalia—huyu mtumishi wa Mungu, ambaye Mungu anamchukulia kuwa mwenye haki, mtu mtimilifu—anaweza kuyahimili majaribio ya aina hii? (Ndiyo.) Kwa nini Mungu anasema “ndiyo” kwa uhakika kama huo? Mungu huchunguza moyo wa binadamu daima? (Ndiyo.) Kwa hivyo Shetani anaweza kuchunguza moyo wa binadamu? (La.) Shetani hawezi. Hata kama Shetani anaweza kuona moyo wa mwanadamu, asili yake mbovu haiwezi kuamini kwamba utakatifu ni utakatifu, ama kwamba uchafu ni uchafu. Shetani mwovu hawezi kuthamini chochote kilicho takatifu, chenye haki ama chenye kung’aa. Shetani hawezi kuepuka kuumiza kwa kutenda kupitia asili yake, uovu wake, na kupitia mbinu hizi anazotumia. Hata kwa hatari ya yeye kuadhibiwa na kuangamizwa na Mungu, hasiti kumpinga Mungu kwa ukaidi—huu ni uovu, hii ni asili ya Shetani. Kwa hivyo katika kifungu hiki, Shetani anasema: “Ngozi kwa ngozi, ndiyo, yote ambayo mtu anayo atayatoa kwa sababu ya uhai wake. Lakini nyosha mbele mkono wako sasa, na uguse mfupa wake na nyama yake, na yeye atakulaani mbele ya uso wako.” Shetani anafikiri kwamba kumcha Mungu kwa mwanadamu ni kwa sababu mwanadamu amepata manufaa mengi kutoka kwa Mungu. Mwanadamu hupata manufaa mengi kutoka kwa Mungu, kwa hivyo anasema Mungu ni mwema. Lakini si kwa sababu Mungu ni mwema, ni kwa sababu tu mwanadamu amepata manufaa mengi na hivyo anaweza kumcha Mungu kwa njia hii: Punde Mungu anapomnyima manufaa haya, basi anaachana na Mungu. Katika asili yake mbovu, Shetani haamini kwamba moyo wa mwanadamu kwa kweli unaweza kumcha Mungu. Kwa sababu ya asili yake mbovu hajui utakatifu ni nini, na hata chini zaidi hajui heshima ya kuogopa ni nini. Hajui ni nini kumtii Mungu ama ni nini kumcha Mungu. Kwa sababu yeye mwenyewe hamchi Mungu, anafikiri mwanadamu hawezi kumcha Mungu pia haiwezekani. Niambieni, si Shetani ni mwovu? (Ndiyo!) Shetani ni mwovu. Isipokuwa kanisa letu, yawe ni makundi ya kidini na madhehebu mbalimbali, ama makundi ya kidini na ya kijamii, hakuna kati yao yanayoamini uwepo wa Mungu ama kuamini kwamba Mungu anaweza kufanya kazi hivyo wanafikiri, kwamba kile unachoamini si Mungu pia. Mfano wa mwanamume mzinzi, anaangalia na kuona kila mtu mwingine akiwa mzinzi, kama alivyo yeye. Mwanadamu anayedanganya kila wakati anaangalia na kuona hakuna mtu mwaminifu, anawaona wote wakidanganya. Mtu mwovu anawaona watu wote wakiwa waovu na anataka kupigana na kila mtu anayemwona. Wakati wale watu ambao walio na uaminifu kwa kulinganisha wanawaona wote kuwa waaminifu, na hivyo daima wanalaghaiwa, wanadanganywa, na hakuna wanachoweza kufanya kuhusu hilo. Nasema mifano hii michache ili kuwafanya kuwa na uhakika zaidi: asili mbovu ya Shetani si msukumo wa muda mfupi ama kitu kinachosababishwa na mazingira yake, wala si udhihirisho wa muda ulioletwa na sababu yoyote ama usuli wowote. Sivyo kabisa! Hana namna ila kuwa hivyo! Hawezi kufanya chochote chema! Hata anaposema kitu kinachofurahisha kusikia, anakushawishi tu. Kadiri maneno yake yanavyofurahisha, yenye busara zaidi, uungwana zaidi, ndivyo nia zake za husuda zinakuwa za kijicho zaidi nyuma ya maneno haya. Shetani anaonyesha uso na asili ya aina gani katika vifungu hivi viwili? (Ya kudhuru kwa siri, yenye kijicho, na mbovu.) Tabia yake ya msingi ni mbovu, hasa mbovu na yenye kijicho.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp