Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 157

Kuna usawa mwingi kati ya desturi ya kitamaduni na ushirikina, ni tu kuwa desturi ya kitamaduni ina hadithi fulani, vidokezo, na vyanzo fulani. Shetani ametunga na kuunda ngano ama hadithi nyingi katika vitabu vya historia, na kuacha watu na hisia za kina za desturi ya kitamaduni ama watu wa kishirikina. Chukua kwa mfano Watu Wanane Wasiokufa Wanaovuka Bahari, Safari ya kwenda Magharibi, Mfalme Mkuu Jade, Nezha Anamshinda Joka Mfalme, na Uchunguzi wa Miungu, zote za Uchina. Haya hayajakita mizizi katika akili za mwanadamu? Hata iwapo baadhi yenu hawajui maelezo yote, bado mnajua hadithi za jumla, na yaliyomo kwa jumla ndiyo yanayokwama katika moyo wako na yanakwama katika akili yako, na huwezi kuyasahau. Haya ni mambo ambayo Shetani alimwekea mwanadamu kitambo sana, baada ya kusambaza katika nyakati tofauti mawazo yake au hekaya. Haya mambo yanadhuru moja kwa moja na kumomonyoa nafsi za watu na kuweka watu chini ya fingo moja baada ya jingine. Hiyo ni kusema kwamba baada ya wewe kukubali mambo haya yanayotoka kwa desturi ya kitamaduni, hadithi ama ushirikina, baada ya mambo haya kuwekwa kwa akili yako, baada ya hayo kukwama katika moyo wako, ni kama tu apizo—unakamatwa na kushawishika na hizi tamaduni, haya mawazo na hadithi za kitamaduni. Yanashawishi maisha yako, mtazamo wako wa maisha na pia yanashawishi maoni yako ya mambo. Hata zaidi yanashawishi ufuataji wako wa njia sahihi ya maisha: Hii bila shaka ni apizo. Unajaribu lakini huwezi kuyatupilia mbali; unayakatakata lakini huwezi kuyakata chini; unayapiga lakini huwezi kuyapiga chini. Sivyo? (Ndiyo.) Zaidi ya hayo, baada ya mwanadamu bila kujua kuwekwa chini ya aina hii ya apizo, bila kujua, anaanza kumwabudu Shetani, kukuza taswira ya Shetani katika moyo wake. Kwa maneno mengine, anamweka Shetani kama sanamu, kifaa cha yeye kuabudu na kutazamia, hata kwenda mbali kiasi cha kumchukulia kama Mungu. Bila kujua, mambo haya yako katika mioyo ya watu yakidhibiti maneno na matendo yao. Aidha, kwanza unachukulia hadithi na hekaya hizi kuwa uongo, na kisha bila kujua unakubali kuwepo kwa hadithi hizi, kuzitengenezea sanamu halisi na kuzibadili kuwa mambo halisi yaliyopo. Katika kutojua, unapokea haya mawazo bila kufahamu na kuwepo kwa vitu hivi. Pia unapokea bila kufahamu mashetani, Shetani na sanamu ndani ya nyumba yako na ndani ya moyo wako—hii bila shaka ni apizo. Je, mnahisi sawa? (Ndiyo.) Kuna yeyote miongoni mwenu ambao wamechoma ubani na kuabudu Budha? (Ndiyo.) Kwa hivyo madhumuni ya kuchoma ubani na kumwabudu Budha yalikuwa yapi? (Kuombea amani.) Kwa kuifikiria sasa, ni ujinga kuombea amani kutoka kwa Shetani? Shetani analeta amani? (La.) Je, mlikuwa wajinga hapo nyuma? (Ndiyo.) Namna ya aina hiyo ni ya upuuzi, jinga na nyofu, siyo? Shetani anafikiria tu jinsi ya kukupotosha na hawezi kukupa amani; anaweza tu kukupa nafasi ya kupumua ya muda mfupi. Lakini lazima uchukue kiapo na ukivunja ahadi yako ama ukivunja kiapo ulichofanya, basi utaona jinsi anavyokuadhibu. Kwa kukufanya uchukue kiapo, kwa kweli anataka kukudhibiti. Wakati mlipoombea amani, mlipata amani? (La.) Hamkupata amani, lakini kinyume na hayo alileta bahati mbaya, majanga yasiyoisha—kweli bahari isiyo na mipaka ya uchungu. Amani haiko miongoni mwa miliki ya Shetani, na hili ni ukweli. Haya ndiyo matokeo kwa wanadamu ya ushirikina wa kikabila na desturi ya kitamaduni.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp