Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 170

Tumejadili mada nyingi na maudhui yanayohusiana na kirai hiki “Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote,” lakini mnajua ndani ya mioyo yenu ni vitu vipi Mungu anatoa kwa wanadamu mbali na kuwapa ninyi neno Lake na kutenda kazi Yake ya kuadibu na hukumu kwenu? Watu wengine huenda wakasema, “Mungu hunipa neema na baraka, na kunipa nidhamu, faraja, na utunzaji na ulinzi kwa kila njia iwezekanayo.” Wengine watasema, “Mungu hunipa chakula cha kila siku na kinywaji,” ilhali wengine hata watasema, “Mungu hunipa kila kitu.” Kuhusu vitu hivi ambavyo watu wanaweza kukutana navyo katika maisha yao ya kila siku, nyote mnaweza kuwa na majibu yanayohusiana na matukio mnayopitia katika maisha yenu ya kimwili. Mungu humpa kila mtu vitu vingi, ingawa tunachojadili leo hakijajikita tu katika mipaka ya eneo la mahitaji ya watu ya kila siku, lakini kinamruhusu kila mmoja wenu kutazama mbali zaidi. Kutokana na mtazamo mkubwa, kwa vile Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote, Anadumisha vipi uhai wa vitu vyote? Ili vitu vyote viweze kuendelea kuwepo, ni nini ambacho Mungu huleta kwa vitu vyote ili kudumisha kuwepo kwa vitu hivyo na kudumisha sheria za kuwepo kwa vitu hivyo? Hilo ndilo wazo kuu la kile tunachojadili leo. … Natumai mtaweza kuunganisha mada hii pamoja na vitu Ninavyoenda kuzungumzia kwa matendo ya Mungu, na sio kuviunganisha kwa ufahamu wowote au kuvihusisha na desturi zozote za binadamu au uchunguzi. Ninazungumza tu kuhusu Mungu na kuhusu Mungu Mwenyewe. Hilo ni pendekezo Langu kwenu. Unaelewa, sivyo?

Mungu ametoa vitu vingi kwa wanadamu. Nitaanza kwa kuzungumza kuhusu kile ambacho watu wanaweza kuona, yaani, wanachoweza kuhisi. Hivi ni vitu ambavyo watu wanaweza kuvielewa na wanaweza kukubali. Hivyo basi kwanza tuanze na ulimwengu yakinifu kujadili kile ambacho Mungu amewapa wanadamu.

1. Hewa

Kwanza, Mungu aliumba hewa ili mwanadamu aweze kupumua. Je, “hewa” hii si hewa ya maisha ya kila siku ambayo wanadamu hukutana nayo kila mara? Je, hewa hii si kitu ambacho wanadamu hutegemea kila wakati, hata wanapolala? Hewa ambayo Mungu aliumba ina umuhimu mkubwa sana kwa wanadamu: ni kijenzi muhimu cha kila pumzi yao na cha uhai wenyewe. Kiini hiki, kinachoweza tu kuhisiwa lakini hakionekani, kilikuwa zawadi ya Mungu ya kwanza kwa vitu vyote. Baada ya kuumba hewa, je, Mungu aliacha kufanya kazi? Baada ya kuumba hewa, je, Mungu alizingatia uzito wa hewa? Je, Mungu alizingatia yaliyomo kwenye hewa? (Ndio.) Mungu alikuwa anafikiria nini alipoumba hewa? Kwa nini Mungu aliumba hewa, na fikira Yake ilikuwa gani? Wanadamu wanahitaji hewa, na wanahitaji kupumua. Kwanza kabisa, uzito wa hewa unapaswa kukubaliana na pafu la mwanadamu. Kuna yeyote anayejua uzito wa hewa? Hili si jambo ambalo watu wanahitaji kujua; hakuna haja ya kujua hili. Hatuhitaji idadi kamili kuhusiana na uzito wa hewa, na kuwa na wazo la jumla ni vizuri. Mungu aliumba hewa yenye uzito ambao ungefaa zaidi mapafu ya mwanadamu kupumua. Yaani, wanadamu wanafurahia na haiwezi kudhuru mwili wanapoivuta. Hili ndilo wazo kuhusu uzito wa hewa. Basi tutaongea kuhusu yaliyomo kwenye hewa. Kwanza, yaliyomo ndani ya hewa si sumu kwa wanadamu na hivyo hayatadhuru pafu na mwili. Mungu alihitaji kuzingatia haya yote. Mungu alihitaji kuzingatia kwamba hewa ambayo wanadamu wanapumua inapaswa kuingia na kutoka taratibu, na kwamba, baada ya kuvuta hewa, kadiri na kiasi cha hewa vinapaswa kuhakikisha damu pamoja na hewa chafu ndani ya mapafu na mwili vingejenga na kuvunjavunja kemikali mwilini vizuri, na pia kwamba hewa hiyo haipaswi kuwa na vijenzi vyovyote vya sumu. Kuhusu viwango hivi viwili, Sitaki kuwalisha mafungu ya maarifa, lakini badala yake nataka tu mjue kwamba Mungu alikuwa na mchakato maalum wa mawazo akilini mwake Alipoumba kila kitu—bora zaidi. Kuhusu kiasi cha vumbi katika hewa, kiasi cha vumbi, mchanga na uchafu duniani, na vilevile vumbi inayoelekea chini kutoka angani, Mungu alikuwa na mpango wa vitu hivi pia—njia ya kuondoa au kutatua vitu hivi. Huku kukiwa na vumbi kiasi, Mungu aliiumba ili vumbi isidhuru mwili na upumuaji wa mwanadamu, na kwamba vipande vya vumbi viwe na ukubwa usiokuwa na madhara kwa mwili. Je, uumbaji wa Mungu wa hewa haukuwa wa ajabu? Je, ulikuwa rahisi kama kupuliza pumzi ya hewa kutoka kinywani Mwake? (La.) Hata katika uumbaji wake wa vitu rahisi sana, maajabu ya Mungu, akili Zake, mawazo Yake, na hekima Yake vyote ni dhahiri. Je, Mungu ni mwenye uhalisi? (Ndiyo.) Hiyo ni kusema, hata katika kuumba kitu rahisi, Mungu alikuwa akifikiria kuhusu mwanadamu. Kwanza kabisa, hewa ambayo wanadamu hupumua ni safi, yaliyomo yanafaa kwa upumuaji wa mwanadamu, si sumu na hayasababishi madhara kwa wanadamu, na uzito huo umekadiriwa kwa upumuaji wa wanadamu. Hewa hii ambayo wanadamu huvuta pumzi na kutoa ni muhimu kwa mwili wao, umbo lao. Ili wanadamu waweze kupumua kwa uhuru, bila kizuizi au wasiwasi. Waweze kupumua kwa kawaida. Hewa ni kile ambacho Mungu aliumba mwanzo na ambacho ni cha lazima kwa upumuaji wa wanadamu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp