Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatua Tatu za Kazi | Dondoo 27

28/09/2020

Katika kazi ya siku za mwisho, neno ni kubwa zaidi ya udhihirisho wa ishara na maajabu, na mamlaka ya neno yanashinda yale ya ishara na maajabu. Neno linaweka wazi tabia zote potovu katika moyo wa mwanadamu. Huwezi kutambua binafsi wewe mwenyewe. Yatakapofunuliwa kwako kupitia kwa neno, utakuja kujua mwenyewe; hutaweza kuyakataa, na utashawishika kikamilifu. Je haya si mamlaka ya neno? Haya ndiyo matokeo yanayopatikana kwa kazi ya wakati huu ya neno. Kwa hivyo, mwanadamu hawezi kuokolewa kikamilifu kutoka kwa dhambi zake kwa kuponya magonjwa na kukemea mapepo na hawezi kufanywa mkamilifu kabisa kwa udhihirisho wa ishara na maajabu. Mamlaka ya kuponya na kukemea mapepo yanapatia mwanadamu neema tu, lakini mwili wa mwanadamu bado ni wa Shetani na tabia potovu za kishetani zitabaki ndani ya mwanadamu. Kwa maneno mengine, yale ambayo hayajatakaswa bado inahusu dhambi na uchafu. Ni baada tu ya mwanadamu kufanywa safi kupitia kwa maneno ndipo mwanadamu atakapopatwa na Mungu na kutakaswa. Wakati mapepo yalikemewa kutoka kwa mwanadamu na alikombolewa, hii ilimaanisha tu kwamba alipokonywa kutoka kwa mikono ya Shetani na kurudishwa kwa Mungu. Hata hivyo, hajafanywa msafi ama kubadilishwa na Mungu, anabaki kama mpotovu. Ndani ya mwanadamu bado kuna uchafu, pingamizi na uasi; mwanadamu amerudi tu kwa Mungu kupitia kwa ukombozi Wake, lakini mwanadamu hana maarifa hata kidogo kumhusu Mungu na bado anaweza kumpinga na kumsaliti. Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi ya Shetani ilikuwa imepandwa ndani yake tayari. Baada ya miaka mingi ya upotovu wa Shetani, mwanadamu tayari ana asili ndani yake inayompinga Mungu. Hivyo, mwanadamu atakapokombolewa, hakitakuwa kitu kingine ila ni ukombozi, ambapo mwanadamu ananunuliwa kwa gharama kuu, lakini asili ya sumu ndani yake haijaondolewa. Mwanadamu ambaye amechafuliwa lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa wa kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuutupa nje upotovu wake na kufanywa safi. Badala ya kuichukua hatua hii ya kazi kuwa ile ya wokovu, itafaa zaidi kusema kuwa ni kazi ya utakaso. Kwa kweli hatua hii ni ile ya ushindi na pia hatua ya pili ya wokovu. Mwanadamu anatwaliwa na Mungu kupitia hukumu na kuadibu na neno; kwa kutumia neno kusafisha, hukumu na kufichua, uchafu wote, fikira, nia, na matumaini ya mtu mwenyewe katika moyo wa mwanadamu zinafuliwa. Ingawa mwanadamu amekombolewa na kusamehewa dhambi zake, inachukuliwa kuwa Mungu hakumbuki makosa ya mwanadamu na kutomtendea mwanadamu kulingana na makosa yake. Hata hivyo, mwanadamu anapoishi katika mwili na hajaachiliwa huru kutoka kwa dhambi, ataendelea tu kutenda dhambi, akiendelea kufunua tabia yake potovu ya kishetani. Haya ndiyo maisha ambayo mwanadamu anaishi, mzunguko usiokoma wa dhambi na msamaha. Wengi wa wanadamu wanatenda dhambi mchana kisha wanakiri jioni. Hivi, hata ingawa sadaka ya dhambi ni ya manufaa kwa binadamu milele, haitaweza kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi. Ni nusu tu ya kazi ya wokovu ndiyo imemalizika, kwani mwanadamu bado yuko na tabia potovu. Kwa mfano, wakati ambapo watu walijua kwamba walitoka kwa Moabu, walitoa maneno ya malalamiko, hawakutafuta tena uzima, na wakawa hasi kabisa. Je, hili halionyeshi kwamba bado hawawezi kutii kwa ukamilifu kutawaliwa na Mungu? Je, hii siyo tabia ya kishetani ya upotovu kabisa? Ulipokuwa hupitii kuadibu, mikono yako iliinuliwa juu zaidi ya wengine wote, hata ile ya Yesu. Na ulilia kwa sauti kubwa: “Kuwa mwana mpendwa wa Mungu! Kuwa mwandani wa Mungu! Ni heri tufe kuliko kumtii Shetani! Muasi Shetani wa zamani! Liasi joka kuu jekundu! Acha joka kuu jekundu lianguke kabisa kutoka mamlakani! Acha Mungu atufanye kamili!” Vilio vyako vilikuwa vikubwa zaidi ya wengine. Lakini kisha ukaja wakati wa kuadibu na, mara tena, tabia ya upotovu ya watu ilifichuliwa. Kisha, vilio vyao vikakoma, na hawakuwa tena na azimio. Huu ni upotovu wa mwanadamu; unaingia ndani zaidi kuliko dhambi, ulipandwa na Shetani na umekita mizizi ndani zaidi ya mwanadamu. Sio rahisi kwa mwanadamu kuzifahamu dhambi zake; mwanadamu hawezi kufahamu asili yake iliyokita mizizi. Ni kupitia tu katika hukumu na neno ndipo mabadiliko haya yatatokea. Hapo tu ndipo mwanadamu ataendelea kubadilika kutoka hatua hiyo kuendelea. Mwanadamu alipiga kelele hivyo wakati uliopita kwa sababu mwanadamu hakuwa na ufahamu wa tabia yake potovu ya asili. Huo ndio uchafu ulio ndani ya mwanadamu. Kotekote katika kipindi kirefu hivyo cha hukumu na kuadibu, mwanadamu aliishi katika mazingira ya mvutano. Je, haya yote hayakutimizwa kupitia kwa neno? Wewe pia hukulia kwa sauti ya juu kabla ya majaribio ya watendaji huduma? Ingia katika ufalme! Wale wote ambao wanalikubali jina hili wataingia katika ufalme! Wote watashiriki Mungu! Wakati ambapo majaribio ya watendaji huduma yalikuja, hukulia tena. Mwanzoni, wote walilia, “Mungu! Popote Uniwekapo, nitatii kuongozwa na Wewe.” Baada ya kusoma maneno ya Mungu, “Nani atakuwa Paulo Wangu?” watu walisema, “Niko radhi!” Kisha wakayaona maneno, “Na kuhusu imani ya Ayubu?” Kwa hiyo akasema, “Niko radhi kuichukua imani ya Ayubu. Mungu, tafadhali nijaribu!” Majaribio ya watendaji huduma yalipokuja, walizirai mara moja na kusimama tena kwa nadra sana. Baada ya hilo, uchafu ndani ya moyo wa wao ulipungua polepole. Je, hili halikutimizwa kupitia kwa neno? Kwa hiyo, kile ambacho mmepitia wakati wa sasa ni matokeo ambayo hutimizwa kupitia kwa neno, hata makuu zaidi ya yale ambayo hutimizwa kupitia kwa Yesu kufanya ishara na maajabu. Utukufu wa Mungu na mamlaka ya Mungu Mwenyewe ambayo ninyi huona hayaonekani tu kupitia kwa usulubishaji, uponyaji wa magonjwa na ufukuzaji wa pepo, lakini zaidi kupitia kwa hukumu ya neno Lake. Hili hukuonyesha wewe kwamba sio tu ufanyaji wa ishara, uponyaji wa magonjwa na ufukuzaji wa pepo ndiyo mamlaka na nguvu za Mungu, bali kwamba hukumu ya neno la Mungu inaweza kuwakilisha vyema zaidi mamlaka ya Mungu na kufichua uweza Wake.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp