Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 176

Nafaka, matunda na mboga, na kila aina ya njugu vyote ni vyakula vya wala mboga. Hata kama ni vyakula vya wala mboga, vina lishe za kutosha kuridhisha mahitaji ya mwili wa mwanadamu. Kwa hali yoyote, Mungu hakusema: “Kuwapa wanadamu hiki kunatosha. Wanadamu wanaweza tu kula vitu hivi.” Mungu hakuachia hapo na badala yake aliwatayarishia wanadamu vitu vyenye ladha nzuri zaidi. Vitu hivi ni gani? Ni aina mbalimbali ya nyama na samaki wengi wenu mnaweza kuona na kula kila siku. Kuna aina nyingi sana za nyama na samaki ambazo Mungu amemtayarishia mwanadamu. Samaki wote huishi majini; umbile asili la nyama yao ni tofauti na la nyama inayokuzwa juu ya ardhi na wanaweza kuwapa wanadamu lishe mbalimbali. Sifa za samaki zinaweza kubadilisha baridi na joto ndani ya mwili wa mwanadamu, kwa hiyo ni za manufaa makubwa sana kwa wanadamu. Lakini kilicho na ladha nzuri hakitakiwi kuliwa zaidi. Bado msemo ni huo huo: Mungu huwapa wanadamu kiasi sahihi kwa wakati sahihi, ili watu waweze kufurahia kwa kawaida na vizuri vitu hivi kulingana na msimu na wakati. Ndege wa kufugwa wanahusisha nini? Kuku, kware, njiwa, n.k. Watu wengi hula pia bata na bata bukini. Ingawa Mungu alifanya matayarisho, kwa watu waliochaguliwa na Mungu, bado Mungu aliwawekea masharti na alikuwa ameweka eneo fulani katika Enzi ya Sheria. Sasa eneo hili linatokana na kupendelea kwa mtu binafsi na ufahamu wa mtu binafsi. Aina hizi mbalimbali za nyama hupatia mwili wa mwanadamu lishe mbalimbali, zinazoweza kusheheneza protini na madini ya chuma, kusitawisha damu, kuimarisha misuli na mifupa, na kupeana nguvu zaidi. Haijalishi ni mbinu gani watu hutumia kupika na kula vitu hivyo, kwa ufupi, vitu hivi vinaweza kwa upande mmoja kuwasaidia watu kuendeleza ladha na hamu ya chakula, na kwa upande mwingine kuridhisha matumbo yao. Kitu cha muhimu zaidi ni kwamba zinaweza kupatia mwili wa mwanadamu mahitaji yao ya lishe ya kila siku. Hizi ndizo fikira ambazo Mungu alikuwa nazo Alipowatayarishia wanadamu chakula. Kuna vyakula vya wala mboga na pia nyama—je, hiyo si ya fahari na nyingi? Lakini watu wanapaswa kuelewa kusudi la asili la Mungu lilikuwa gani Mungu alipowatayarishia wanadamu vyakula vyote. Je, ilikuwa ni kuwaacha wanadamu wafurahie kwa ulafi vyakula hivi vya kimwili? Na je, watu wakijihusisha katika ridhaa hii ya kimwili? Je, hawapati lishe kupita kiasi? Je, lishe kupita kiasi haileti kila aina ya magonjwa kwa mwili wa mwanadamu? (Ndiyo.) Hiyo ndiyo maana Mungu hutoa kiasi sahihi kwa wakati sahihi na kuwaacha watu wafurahie vyakula mbalimbali kulingana na vipindi vya wakati na misimu. Kwa mfano, baada ya kuishi katika majira ya joto sana, watu watakusanya kiasi fulani cha joto, la kusababisha ukavu wa viini na unyevunyevu katika miili yao. Majira ya kupukutika kwa majani yakija, matunda ya aina nyingi sana yataiva, na watu watakapokula baadhi ya matunda unyevunyevu wao utaondolewa. Wakati huo huo, ng’ombe na kondoo watakuwa wamekua na kupata nguvu, ili watu wale nyama kiasi kama lishe. Baada ya kula aina mbalimbali za nyama, miili ya watu itakuwa na nguvu na joto la kuisaidia kustahimili baridi ya majira ya baridi, na kutokana na hayo wataweza kupita katika majira ya baridi kwa amani. Wakati upi wa kutayarisha vitu vipi kwa ajili ya wanadamu, na wakati upi wa kuacha vitu vipi vikue, vizae matunda na kuiva—yote haya yanadhibitiwa na kupangwa na Mungu kwa kupimwa kabisa. Hii ni mada kuhusu “jinsi Mungu alitayarisha chakula kilicho muhimu kwa maisha ya mwanadamu ya kila siku.” Mbali na aina zote za chakula, Mungu pia huwapa wanadamu vyanzo vya maji. Watu huhitaji kunywa maji kiasi baada ya kula. Je, kula matunda tu kunatosha? Watu hawataweza kustahimili kula matunda pekee, licha ya hayo, huwa hakuna matunda katika misimu mingine. Hivyo tatizo la wanadamu la maji litawezaje kutatuliwa? Kwa Mungu kutayarisha vyanzo vingi vya maji juu ya ardhi na chini ya ardhi, ikiwemo maziwa, mito, na chemchemi. Vyanzo hivi vya maji vinaweza kunywewa maji katika hali ambazo hakuna kuchafuliwa kokote, au maendeleo ya wanadamu au uharibifu. Yaani, kuhusu vyanzo vya chakula kwa maisha ya miili ya wanadamu, Mungu amefanya matayarisho sahihi sana, yasiyo na hitilafu yoyote na ya kufaa sana, ili maisha ya watu yawe ya fahari na yenye wingi na yasiyokosa chochote. Hiki ni kitu ambacho watu wanaweza kuhisi na kuona.

Kuongezea, miongoni mwa vitu vyote, iwe ni wanyama, mimea, au kila aina ya nyasi, Mungu aliumba pia baadhi ya mimea ambayo ni muhimu kwa kutatua madhara au magonjwa kwa mwili wa mwanadamu. Utafanya nini, kwa mfano, ukichomeka? Je, unaweza kuosha kwa maji? Je, unaweza kutafuta kitambaa na kufunika mahali hapo? Huenda pakajaa usaha au kuambukizwa kwa njia hiyo. Utafanya nini, kwa mfano, ukiungua kwa bahati na moto au na maji moto? Unaweza kumimina maji juu yake? Kwa mfano, ukipata homa, upate mafua, upate majeraha kutokana na kazi ya viungo, maradhi ya tumbo kutokana na kula kitu kibaya, au kupata magonjwa fulani kwa sababu ya mienendo ya maisha au masuala ya hisia, kama vile magonjwa ya mishipa ya damu, hali za kisaikolojia au magonjwa ya ogani zilizo ndani ya mwili—kuna mimea inayolingana ya kutibu haya yote. Kuna mimea inayoendeleza mzunguko wa damu kuondoa ukwamaji, kutuliza maumivu, kukomesha kutokwa na damu, kutia ganzi, kuwasaidia watu kupata tena ngozi ya kawaida, kuondoa ukwamaji wa damu mwilini, na kuondoa sumu mwilini. Kwa ufupi, yote inaweza kutumiwa katika maisha ya kila siku. Ni ya kufaa watu na imetayarishwa na Mungu kwa ajili ya mwili wa mwanadamu iwapo inahitajika. Baadhi ya hiyo iliruhusiwa na Mungu kugunduliwa bila uangalifu na mwanadamu, ilhali mingine iligunduliwa kutoka kwa vitu fulani maalum au na watu fulani waliotayarishwa na Mungu. Baada ya ugunduzi wao, wanadamu wangeipitisha kwa wengine, na halafu watu wengi wangejua kuihusu. Kwa njia hii, uumbaji wa Mungu wa mimea hii unakuwa na thamani na maana. Kwa ufupi, vitu hivi vyote vinatoka kwa Mungu na vilitayarishwa na kupandwa Alipowaumbia wanadamu mazingira ya kuishi. Vitu hivi vyote ni muhimu sana. Je, fikira Zake Mungu zilifikiriwa vizuri sana kuliko za wanadamu? Unapoona yote ambayo Mungu amefanya, unaweza kuhisi upande wa Mungu wa vitendo? Mungu alifanya kazi katika siri. Kabla ya mwanadamu kuingia katika ulimwengu huu, kabla ya kukutana na wanadamu hawa, Mungu alikuwa tayari ameviumba vitu hivi vyote. Kila kitu alichofanya kilikuwa kwa ajili ya wanadamu, kwa ajili ya kuendelea kuishi kwao, na kwa ajili ya kufikiria juu ya kuwepo kwa wanadamu, ili wanadamu waweze kuishi kwa furaha katika ulimwengu huu yakinifu wa ufahari na wingi ambao Mungu aliwatayarishia, bila kuwa na wasiwasi kuhusu chakula au nguo, na bila kukosa chochote. Wanadamu wanaendelea kuzaa na kuendelea kuishi katika mazingira hayo.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp