Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 160

20/07/2020

Mungu anafanya mengi kando na kuhakikisha usalama wa watu, kuhakikisha kwamba hawatamezwa na Shetani; pia hufanya kazi nyingi sana kwa kutayarisha kumchagua mtu na kumwokoa. Kwanza, una tabia gani, utazaliwa kwa familia ya aina gani, wazazi wako ni nani, una kaka na dada wangapi, hali na hadhi ya kiuchumi ya familia yako ni gani, hali ya familia yako ni gani—haya yote yanapangiwa wewe kwa uangalifu na Mungu. Je, unajua ni familia ya aina gani watu waliochaguliwa na Mungu wanazaliwa ndani mara nyingi, kama inavyohusu watu wengi? Ni familia mashuhuri? Kunaweza kuwa na nyingine. Hatuwezi sema kwa uhakika hakuna yoyote, lakini kuna chache sana. Ni familia za utajiri wa kupindukia, kama yenye mabilioni ama yenye mamilioni nyingi? Mara nyingi huwa si aina hii ya familia. Kwa hivyo Mungu anapangia watu hawa familia za aina gani zaidi? (Familia za kawaida.) Kwa hivyo familia za kawaida ni zipi? Ni familia zinazofanya kazi. Wafanyakazi wanategemea mishahara yao kuishi na wanaweza kumudu mahitaji ya kimsingi. Hawatakuruhusu kwenda njaa wakati wowote, lakini huwezi kutarajia mahitaji yako yote ya mwili kutoshelezwa. Kisha kuna familia za ukulima. Wakulima wanategemea kupanda mazao kwa chakula chao, na wana nafaka za kula, na kwa vyovyote vile, hutakuwa na njaa, lakini huwezi kuwa na nguo nzuri sana. Tena kuna familia zingine ambazo zinashughulika katika biashara ama zinazoendesha biashara ndogondogo, na zingine ambazo wazazi ni wenye akili, na hizi zinaweza kuhesabika kama familia za kawaida. Kuna baadhi ya wazazi ambao ni wafanyakazi wa ofisi ama maafisa wadogo wa serikali kwa kiwango zaidi, ambazo haziwezi kuhesabika kama familia mashuhuri pia. Watu wengi zaidi wanazaliwa katika familia za kawaida, na haya yote yanapangiliwa na Mungu. Kusema kwamba, kwanza kabisa mazingira haya unayoishi si familia ya uwezo mkubwa ambayo unaweza kufikiria, lakini badala yake ni familia uliyoamuliwa na Mungu, na watu wengi wataishi katika mipaka ya aina hii ya familia; hatutazungumza mambo ya pekee hapa. Kwa hivyo je, hadhi ya kijamii? Hali ya uchumi ya wengi wa wazazi ni wastani na hawana hadhi ya juu ya kijamii—kwao ni vizuri tu kuwa na kazi. Kuna wowote walio magavana? Kuna wowote walio maraisi? (La.) Kwa zaidi ni watu kama mameneja wa biashara ndogo ama wakubwa wa muda mfupi. Hadhi zao za kijamii ni kuwa katikati, na hali zao za uchumi ni wastani. Sababu nyingine ni mazingira ya kuishi ya familia. Kwanza kabisa, hakuna wazazi ambao wanaweza kushawishi kwa wazi watoto wao kutembea njia ya uaguzi na kupiga ramli; hawa pia ni wachache. Wazazi wengi ni wa kawaida kiasi na ni wa hali moja na nyinyi. Mungu anaweka mazingira ya aina hii kwa ajili ya watu wakati sawa na kuwachagua, na ni kwa manufaa sana ya kazi Yake ya kuokoa watu. Kwa nje, inaonekana kwamba Mungu hajafanya chochote kikuu kwa mwanadamu; Anafanya kila kitu kwa siri tu, kwa unyenyekevu na kwa kimya. Lakini kwa hakika, vyote ambavyo Mungu anafanya vinafanywa kuweka msingi wa wokovu wako, kuandaa njia mbeleni na kuandaa hali zote muhimu za wokovu wako. Mara moja wakati maalum wa kila mtu, Mungu anawarudisha mbele Yake—wakati unapofika kwako kusikia sauti ya Mungu, huo ndio wakati unapokuja mbele Yake. Wakati hili linafanyika, watu wengine wamekuwa wazazi tayari wenyewe, ilhali wengine ni watoto wa mtu tu. Kwa maneno mengine, watu wengine wameoa na kupata watoto ilhali wengine bado hawajaoa, na hawajaanza bado familia zao. Lakini licha ya hali za watu, Mungu tayari ameweka nyakati utakapochaguliwa na injili na maneno Yake yatakapokufikia. Mungu ameweka hali, ameamulia mtu fulani ama muktadha fulani ambamo injili itapitishwa kwako, ili uweze kusikia maneno ya Mungu. Mungu tayari amekuandalia hali zote muhimu ili, bila kujua, unakuja mbele Yake na unarudishwa kwa familia ya Mungu. Pia, bila kujua, unafuata Mungu na kuingia katika kazi Yake ya hatua kwa hatua, kuingia katika njia ya Mungu ya kazi ambayo, hatua kwa hatua amekuandalia. Ni njia za aina gani ambazo Mungu hutumia wakati Anapofanya mambo kwa ajili ya mwanadamu wakati huu? Kwanza, angalau kabisa ni utunzaji na ulinzi ambao mwanadamu hufurahia. Kando na hayo, Mungu huweka watu, matukio, na vitu mbalimbali ili mwanadamu aweze kuona kuwepo Kwake na matendo Yake miongoni mwao. Kwa mfano, kuna watu wengine wanaomwamini Mungu kwa sababu mtu katika familia yao ni mgonjwa, na wanasema “Mmoja wa familia yangu ni mgonjwa, nitafanya nini?” Watu wengine kisha wanasema “Mwamini Bwana Yesu!” Kwa hivyo wanaanza kumwamini Mungu, na imani hii kwa Mungu imekuja kwa sababu ya hali hii. Kwa hivyo ni nani aliyepangilia hali hii? (Mungu.) Kwa njia ya maradhi haya, kuna familia zingine ambamo wote ni waumini, vijana na wazee, ilhali kuna familia zingine ambamo imani ni ya kibinafsi. Inavyoonekana, unamwamini Mungu kwa sababu ya maradhi, lakini kwa hakika ni hali uliyopewa ili uje mbele ya Mungu—huu ni wema wa Mungu. Kwa sababu maisha ya familia ya watu wengine ni magumu na hawawezi kupata amani yoyote, fursa ya bahati inakuja ambapo mtu anapitisha injili na kusema, “Familia yako ina magumu. Mwamini Bwana Yesu. Mwamini Bwana Yesu na utakuwa na amani.” Bila fahamu, mtu huyu basi anakuja kumwamini Mungu katika hali asili, kwa hivyo hii si aina ya hali? (Ndiyo.) Na je, familia yake kuwa na amani si neema aliyopewa na Mungu? (Ndiyo.) Kisha kuna wengine wanaokuja kumwamini Mungu kwa sababu zingine. Kuna sababu tofauti na njia tofauti za imani, lakini licha ya sababu inakuleta kumwamini Yeye, yote hakika yamepangwa na kuongozwa na Mungu. Kwanza, Mungu hutumia njia kadhaa ili kukuchagua na kukuleta katika familia Yake. Hii ndiyo neema Mungu anayompa kila mwanadamu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp