Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 178

Mungu si Mungu wa watu Wake wateule pekee. Wewe sasa unamfuata Mungu, na Yeye ni Mungu wako, lakini kwa wale walio nje ya watu wanaomfuata Mungu, je, Mungu ni Mungu wao? Je, Mungu ni Mungu wa watu wote walio nje ya wale wanaomfuata Yeye? (Ndiyo.) Basi Mungu ni Mungu wa vitu vyote? (Ndiyo.) Basi Mungu hutenda kazi Yake na kutekeleza matendo Yake kwa wale tu wanaomfuata Yeye? (La.) Eneo lake ni ulimwengu mzima. Kutoka kwa mtazamo mdogo, eneo lake ni wanadamu wote na miongoni mwa vitu vyote. Kutokana na mtazamo mkubwa, ni ulimwengu mzima. Hivyo tunaweza kusema kwamba Mungu hufanya kazi Yake na kutekeleza matendo Yake miongoni mwa wanadamu wote. Hili ni la kutosha kuwafanya watu wajue yote kuhusu Mungu Mwenyewe. Ikiwa unataka kumjua Mungu na upate kweli kumjua na kumfahamu Yeye, basi usizuiwe tu katika hatua tatu za kazi ya Mungu, na usizuiwe tu katika hadithi za kazi ambayo Mungu alitekeleza wakati mmoja. Ukijaribu kumjua hivyo, basi unajaribu kumzuilia Mungu kwa mipaka fulani. Unamwona Mungu kama asiye na maana sana. Ni athari gani ungepata kutoka kwa matokeo kama hayo? Hungeweza kujua maajabu na mamlaka ya juu kabisa ya Mungu, na hungeweza kamwe kujua nguvu za Mungu na kudura na eneo la mamlaka Yake. Ufahamu kama huo ungeathiri uwezo wako wa kukubali ukweli kwamba Mungu ni Mtawala wa vitu vyote, na vilevile maarifa yako ya utambulisho wa kweli na hadhi ya Mungu. Kwa maneno mengine, iwapo ufahamu wako wa Mungu umewekewa mipaka katika eneo, unachoweza kupokea pia kimewekewa mipaka. Ndiyo maana ni lazima upanue eneo na kufungua upeo wa macho yako. Iwe ni eneo la kazi ya Mungu, usimamizi wa Mungu, na utawala wa Mungu, au vitu vyote vinavyotawaliwa na kusimamiwa na Mungu, unapaswa kujua yote na kupata kujua matendo ya Mungu yaliyo ndani. Kupitia njia hii ya ufahamu, utahisi bila kujua kwamba Mungu anatawala, anasimamia na kupeana vitu vyote miongoni mwao. Wakati huo huo, utahisi kweli kwamba wewe ni sehemu ya vitu vyote, na kiungo cha vitu vyote. Mungu anapovipa vitu vyote, wewe pia unakubali utawala na upeanaji wa Mungu. Huu ni ukweli usioweza kupingwa na yeyote. Vitu vyote viko chini ya mamlaka ya sheria zao, ambazo ziko chini ya utawala wa Mungu, na vitu vyote vina sheria zao za kuendelea kuishi, ambazo pia ziko chini ya utawala wa Mungu, huku majaliwa ya wanadamu na wanachohitaji pia vikihusiana kwa karibu na utawala wa Mungu na upeanaji Wake. Ndiyo maana, chini ya utawala wa Mungu na uongozi, wanadamu na vitu vyote vinahusiana, vinategemeana, na vinafumana. Hili ni kusudi na thamani ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp