Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 189

Kwa roho yoyote, kupata kwake mwili mpya na nafasi anayochukua—nafasi yake ni ipi katika haya maisha—atazaliwa katika familia gani, na maisha yake yatakuwaje vinahusiana kwa karibu na maisha yake ya zamani. Kila aina ya watu huja katika dunia ya wanadamu, na nafasi zao ni tofauti, kama zilivyo kazi wazifanyazo. Na hizi ni kazi gani? Watu wengine wanakuja kulipa deni: Ikiwa walikuwa na pesa nyingi za watu katika maisha yao ya awali, wanakuja kulipa deni. Katika maisha haya Wakati uleule, watu wengine, wamekuja kuchukua madeni yao: Walitapeliwa vitu vingi sana, na pesa nyingi sana katika maisha yao yaliyopita, na kwa hiyo, baada ya kuwasili katika ulimwengu wa kiroho, ulimwengu wa kiroho utawapa haki na kuwapa fursa ya kukusanya madeni yao katika maisha haya. Watu wengine wamekuja kulipa deni la shukrani: katika maisha yao yaliyopita—kabla hawajafa—mtu alikuwa mkarimu kwao, na katika maisha haya wamepatiwa fursa nzuri kupata mwili ili kwamba waweze kuzaliwa upya ili kulipa upya deni hili la shukrani. Wakati uleule, wengine wamezaliwa upya katika haya maisha ili kudai uhai. Na wanadai uhai wa nani? Uhai wa mtu aliyewaua katika maisha yao yaliyopita. Kwa ujumla, maisha ya sasa ya kila mtu yana uhusiano mkubwa na maisha yao yaliyopita, yameungana kwa njia isiyoachana. Yaani, maisha ya sasa ya kila mtu yanaathiriwa pakubwa na maisha yao yaliyopita. Kwa mfano, kabla ya kufariki, Zhang alimtapeli Li kiwango kikubwa cha pesa. Je, Zhang ana deni la Li? Kwa kuwa analo, ni kawaida kwamba Li anapaswa kuchukua deni lake kutoka kwa Zhang? Hivyo basi baada ya wao kufa, kuna deni kati yao ambalo linatakiwa kulipwa. Wakati wanapata mwili mpya na Zhang anakuwa mwanadamu, je, Li anapataje deni hili kutoka kwake? Mbinu moja ni kwamba Li anapata deni lake kwa kuzaliwa upya kama mwana wa Zhang, Zhang akiwa babake. Hili ndilo litafanyika katika maisha ya sasa. Babake Li, Zhang, anapata pesa nyingi, na zinaliwa na mwana wa, Li. Haijalishi Zhang anapata pesa nyingi kiasi gani, mwana wa Li “anamsaidia” kwa kuzitumia. Haijalishi Zhang anapata kiasi gani cha pesa, katu hazitoshi, na mwana wake, wakati uleule, kwa namna fulani daima anazitumia pesa za babake kupitia njia na mbinu mbalimbali. Zhang anachanganyikiwa: “Ni nini kinaendelea? Kwa nini mwanangu daima amekuwa kisirani? Mbona wana wa watu wengine ni wema sana? Ni kwa nini mwanangu hana lengo, ni kwa nini hana maana na hana uwezo wa kuchuma pesa zozote, kwa nini daima ninapaswa kumsaidia? Kwa kuwa ni lazima nimsaidie, nitamsaidia, ila kwa nini hata nimpe pesa kiasi gani, daima anataka zaidi? Ni kwa nini asifanye kazi halali? Kwa nini yeye ni lofa, anakula, anakunywa, anazini, anacheza kamari—akiyafanya yote? Nini kinaendelea?” Halafu Zhang anafikiria kidogo: “Inaweza kuwa ni kwa sababu nilikuwa na deni lake katika maisha ya zamani. Sawa basi, nitalilipa! Haya hayataisha hadi nilipe kikamilifu!” Inaweza kufika siku ambayo Li anafidia deni lake, na akiwa na umri wa miaka arobaini au hamsini, itafika siku ambayo atajitambua: “Sijafanya kitu kizuri hata kimoja katika hii nusu ya kwanza ya maisha yangu! Nimefuja pesa zote alizozipata baba—ninapaswa kuwa mtu mwema! Nitajikakamua: nitakuwa mtu ambaye ni mwaminifu, na anayeishi ipasavyo, na sitamletea babangu huzuni tena!” Kwa nini anafikiria hivi? Mbona anageuka kuwa mwema ghafla? Kuna sababu ya hili? Ni sababu gani? (Kwa sababu Li amepokea deni lake; Zhang amelipa deni lake.) Katika hili, kuna chanzo na matokeo. Kisa kilianza zamani sana, kabla hawa wawili hawajazaliwa, na hiki kisa cha maisha yao ya zamani kimeletwa katika maisha yao ya sasa, na hakuna anayeweza kumlaumu mwingine. Haijalishi Zhang alimfundisha nini mwanake, mwanake hakumsikiliza, na hakufanya kazi halali hata ya siku—lakini siku ambayo deni lilipwa, hapakuwa na haja ya kumfundisha; mwanake alielewa kiasili. Huu ni mfano rahisi, na bila shaka kuna mifano mingine kama huu. Na unawafunza watu kitu gani? (Wanapaswa kuwa wema na hawapaswi kutenda maovu.) Kwamba hawapaswi kutenda maovu, na kutakuwa na adhabu kwa maovu yao! Wengi wa wasioamini, hutenda maovu mengi na utendaji maovu wao umekutwa na adhabu, sawa? Je, hii adhabu ni ya kinasibu? Kila linalokutwa na adhabu lina asili na sababu. Unadhani hakuna litakalotendeka baada ya kumlaghai mtu pesa? Unadhani baada ya kuwatapeli pesa zao hakutakuwa na matokeo kwako baada ya kuchukua pesa zao? Hilo halitawezekana, na kutakuwa na athari! Bila kujali wao ni nani, au kama wanaamini ama hawaamini kuwa kuna Mungu, kila mtu ni lazima atawajibikia mienendo yake na kubeba matokeo ya matendo yake. Kwa kurejelea huu mfano rahisi—Zhang kuadhibiwa, na Li kulipwa—je hii si haki? Watu wakifanya vitu kama hivyo, kuna aina hiyo ya matokeo. Na je, imejitenga na utawala wa ulimwengu wa kiroho? Haitenganishwi na utawala wa ulimwengu wa kiroho. Licha ya kuwa wasioamini, wale wasiomwamini Mungu, uwepo wao uko chini ya amri za peponi na sheria ambazo haziwezi kuepukika na yeyote na hakuna mtu anayeweza kuuepuka ukweli huu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp