Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 174

Kazi ya mwanadamu inawakilisha uzoefu wake na ubinadamu wake. Kile ambacho mwanadamu anatoa na kazi ambayo anafanya vinamwakilisha yeye. Mwanadamu kuona, mwanadamu kufikiri, mantiki ya mwanadamu na uwezo mkubwa wa kufikiri vyote vinajumuishwa katika kazi yake. Kimsingi, uzoefu wa mwanadamu, unaweza zaidi kuwakilisha kazi yake na kile ambacho mtu amekipitia kitakuwa ni sehemu ya kazi yake. Kazi ya mwanadamu inaweza kudhihirisha uzoefu wake. Pale ambapo baadhi ya watu wanakuwa katika hali ya kukaa tu bila kufanya kujishughulisha, sehemu kubwa ya ushirika wao inakuwa na mambo ya uasi. Kama uzoefu wao ni mzuri na wanapita katika njia ya upande mzuri, kile wanachoshiriki kinatia moyo sana, na watu wanaweza kupokea mambo mazuri kutoka kwao. Ikiwa mfanyakazi atakuwa katika hali ya kukaa tu wakati huu, ushirika wake siku zote utakuwa na mambo ya uasi. Aina hii ya ushirika ni ya kuvunja moyo, na wengine watavunjika mioyo bila kujua kwa kufuata ushirika wa yule mfanyakazi. Hali ya wafuasi inabadilika kutegemea na hali ya kiongozi. Vile ambavyo mfanyakazi alivyo ndani, ndivyo hivyo anavyojidhihirisha, na kazi ya Roho Mtakatifu mara nyingi inabadilika kulingana na hali ya mwanadamu. Anafanya kazi kulingana na uzoefu wa mwanadamu na wala hamshurutishi mwanadamu bali anamsihi mwanadamu kulingana na hali yake ya kawaida ya uzoefu wake. Hii ni kusema kwamba ushirika wa mwanadamu unatofautiana na neno la Mungu. Ushirika wa mwanadamu hueleza vile anavyotazama mambo na uzoefu wake, ukidhihirisha kile wanachokiona na kupitia uzoefu wao juu ya msingi wa kazi ya Mungu. Wajibu wao ni kutafuta, kazi au maneno ya Mungu, kile wanachopaswa kufanya au kuingia kwacho, halafu kukiwasilisha kwa wafuasi. Hivyo, kazi ya mwanadamu inawakilisha kuingia au matendo yake. Kazi hiyo imechanganyikana na masomo ya kibinadamu na uzoefu au mawazo ya kibinadamu. Haijalishi namna ambavyo Roho Mtakatifu Anafanya kazi, ama Anavyomfanyia kazi mwanadamu au Mungu mwenye mwili, siku zote watenda kazi ndio wanaodhihirisha vile walivyo. Ingawa ni Roho Mtakatifu ambaye hufanya kazi, kazi hiyo imejengwa katika msingi wa mwanadamu alivyo kwa asili, kwa sababu Roho Mtakatifu hafanyi kazi pasipo msingi. Kwa maneno mengine, kazi haifanyiki pasipokuwa na kitu, lakini siku zote hufanyika kulingana na mazingira halisi na hali halisi. Ni kwa njia hii pekee ndio tabia ya mwanadamu inaweza kubadilishwa, kwamba mitazamo yake ya zamani na mawazo yake ya zamani yanaweza kubadilishwa. Kile ambacho mwanadamu hukidhihirisha ni kile anachokiona, kupitia uzoefu na kukitafakari. Hata kama ni mafundisho au mitazamo, haya yote hufikiwa na fikra za mwanadamu. Bila kujali ukubwa wa kazi ya mwanadamu, haiwezi kuzidi mawanda ya uzoefu wa mwanadamu, kile ambacho mwanadamu huona, au kile ambacho mwanadamu anaweza kukitafakari au kuingia akilini mwake. Kile ambacho Mungu anadhihirisha ndivyo hivyo Mungu Mwenyewe alivyo, na hii ni nje ya uwezo wa mwanadamu, yaani, nje ya uwezo wa kufikiri kwa mwanadamu. Anadhihirisha kazi Yake ya kuwaongoza wanadamu wote, na hii haihusiani na undani wa uzoefu wa mwanadamu, badala yake inahusu usimamizi Wake. Mwanadamu anadhihirisha uzoefu wake wakati Mungu akidhihirisha hali Yake—hali hii ni tabia Yake ya asili na uko nje ya uwezo wa mwanadamu. Uzoefu wa mwanadamu ni kuona kwake na kupata maarifa kulingana na udhihirishaji wa Mungu wa hali Yake. Kuona huko na maarifa vinaitwa asili ya mwanadamu. Vinadhihirishwa kwa msingi wa tabia ya asili ya mwanadamu na tabia yake halisi; hivyo pia vinaitwa asili ya mwanadamu. Mwanadamu anaweza kushiriki kile anachokipitia na kukiona. Kile ambacho hajawahi kukipitia au kukiona au akili yake haiwezi kukifikia, yaani, vitu ambavyo havipo ndani yake, hawezi kuvishiriki. Ikiwa kile ambacho mwanadamu anakidhihirisha sio uzoefu wake, basi ni kile anachokitafakari au mafundisho ya kidini. Kwa ufupi, hakuna ukweli wowote katika maneno yake. Kama hujawahi kukutana na maswala ya jamii, huwezi kushiriki kwa uwazi kwenye mahusiano changamani katika jamii. Kama huna familia na watu wengine wanazungumza juu ya masuala ya familia, huwezi kuelewa kiasi kikubwa cha kile walichokuwa wakisema. Kwa hivyo, kile ambacho mwanadamu anakifanyia ushirika na kazi anayofanya vinawakilisha hali yake ya ndani. Ikiwa mtu anafanya ushirika kuhusu uelewa wake wa kuadibu na hukumu, lakini huna uzoefu wake, usithubutu kukana maarifa yake, badala yake kuwa na uhakika wa anachokisema kwa asilimia mia moja. Hii ni kwa sababu kile anachokifanyia ushirika ni kitu ambacho hujawahi kupata uzoefu wake, kitu ambacho hujawahi kukifahamu, na akili yako haiwezi kukitafakari. Unaweza tu kujifunza kutoka kwa ufahamu wake njia za maisha yajayo yanayohusiana na kuadibu na hukumu. Lakini njia hii inaweza kufanya kazi tu kama uelewa uliojikita katika fundisho na haiwezi kuchukua nafasi ya ufahamu wako, na zaidi sana uzoefu wako. Pengine unafikiri kwamba kile anachokisema ni sahihi, lakini unapokipitia, unagundua kwamba hakitekelezeki katika mambo mengi. Pengine unahisi kwamba maarifa fulani unayoyasikia hayatekelezeki kabisa; unakuwa na mtazamo kuhusu maarifa hayo kwa wakati fulani, na ingawa unayakubali, unafanya hivyo shingo upande. Lakini unapopata uzoefu, maarifa yanayokupatia mtazamo ndiyo yanayoongoza matendo yako. Na kadri unavyotenda, ndivyo unavyozidi kuelewa thamani halisi na maana ya maneno yake. Baada ya kuwa na uzoefu, sasa unaweza kuzungumza juu ya maarifa unayopaswa kuwa nayo kuhusu vitu ulivyovipitia. Aidha, unaweza pia kutofautisha kati ya wale ambao maarifa yao ni halisi na yanayotekelezeka na wale ambao maarifa yao yamejikita katika mafundisho ya kidini na hayana thamani. Kwa hivyo, kama maarifa ambayo unayazungumzia yanapatana na ukweli basi kwa kiasi kikubwa yanategemea na iwapo una uzoefu wa kivitendo. Pale palipo na ukweli katika uzoefu wako, maarifa yako yatakuwa yanatekelezeka na yenye thamani. Kupitia uzoefu wako, pia unaweza kupata utambuzi na umaizi, kukuza maarifa yako, na kuongeza hekima yako na akili ya kuzaliwa katika kujiongoza. Maarifa yanayozungumzwa na watu ambao hawana ukweli ni fundisho la kidini tu, bila kujali yana nguvu kiasi gani. Mtu wa aina hii anaweza kuwa mwenye akili sana yanapokuja masuala ya kimwili lakini hawezi kutofautisha yanapokuja masuala ya kiroho. Hii ni kwa sababu watu kama hao hawana uzoefu wowote katika masuala ya kiroho. Kuna watu ambao hawajapata nuru katika masuala ya kiroho na kwa hivyo hawaielewi roho. Bila kujali unazungumzia kipengele gani cha maarifa, ilimradi ni asili yako, basi ni uzoefu wako binafsi, maarifa yako halisi. Kile ambacho watu wenye mafundisho tu huzungumzia, yaani, wale ambao hawana ukweli au uhalisi, huzungumzia yaweza kusemwa kuwa ni asili yao, kwa sababu mafundisho yao yamefikiwa kwa njia ya kutafakari sana na ni matokeo ya akili yao kutafakari kwa kina, lakini ni mafundisho tu, si kitu chochote zaidi ya fikra dhahania.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp