Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 176

Kazi ya Roho Mtakatifu ni kuhusu kuwasaidia watu kupata faida; ni kuwaadilisha watu; hakuna kazi ambayo haiwanufaishi watu. Haijalishi kama ukweli ni wa kina au usio wa kina, na haijalishi tabia ya wale wanaopokea ukweli huo ilivyo, chochote ambacho Roho Mtakatifu Anafanya, yote hayo huwanufaisha watu. Lakini kazi ya Roho Mtakatifu haiwezi kufanywa moja kwa moja; ni lazima ifanywe na wanadamu wanaoshirikiana Naye. Ni kwa njia hii pekee ndiyo matokeo ya kazi ya Roho Mtakatifu yanaweza kupatikana. Bila shaka, inapokuwa ni kazi ya moja kwa moja ya Roho Mtakatifu, haijachanganywa na kitu chochote kabisa; lakini inapotumia mwanadamu kama chombo, inakuwa imechanganywa sana na sio kazi halisi ya Roho Mtakatifu. Kwa njia hii, ukweli hubadilika katika viwango tofauti. Wafuasi hawapokei maana halisi ya Roho Mtakatifu bali wanapokea muungano wa kazi ya Roho Mtakatifu na uzoefu na maarifa ya mwanadamu. Sehemu ya kazi ya Roho Mtakatifu inayopokelewa na wafuasi ni sahihi. Uzoefu na maarifa ya mwanadamu yanayopokewa yanatofautiana kwa sababu watenda kazi ni tofauti. Watenda kazi wanapokuwa na nuru na uongozi wa Roho Mtakatifu, wanakuwa wanapata uzoefu kulingana na nuru na uongozi huu. Ndani ya uzoefu huu kuna akili ya mwanadamu na uzoefu, vile vile asili ya ubinadamu, ambapo wanapata maarifa na kuona vile walivyopaswa kuona. Hivi ndivyo inavyokuwa baada ya mwanadamu kuujua ukweli. Namna hii ya kutenda siku zote haifanani kwa sababu watu wana uzoefu tofauti na vitu ambavyo watu wanavipitia ni tofauti. Kwa njia hii, nuru ile ile ya Roho Mtakatifu inaleta maarifa tofauti na desturi kwa sababu wale wanaopokea nuru hiyo ni tofauti. Baadhi ya watu hufanya makosa madogo wakati wa utendaji ilhali wengine hufanya makosa makubwa, na baadhi hawafanyi chochote ila ni makosa tu. Hii ni kwa sababu uwezo wa kuelewa mambo unatofautiana na kwa sababu tabia zao halisi pia zinatofautiana. Baadhi ya watu wanaelewa hivi baada ya kuusikia ujumbe, na baadhi ya watu wanauelewa vile baada ya kuusikia ukweli. Baadhi ya watu wanapotoka kidogo; na baadhi hawaelewi kabisa maana ya ukweli. Kwa hiyo, kwa jinsi yoyote mtu aelewavyo ndivyo atakavyowaongoza wengine; hii ni kweli kabisa, kwa sababu kazi yake inadhihirisha asili yake tu. Watu wanaoongozwa na watu wenye uelewa sahihi wa ukweli pia watakuwa na uelewa sahihi wa ukweli. Hata kama kuna watu ambao uelewa wao una makosa, ni wachache sana, na sio watu wote watakuwa na makosa. Watu wanaoongozwa na watu ambao wana makosa katika kuuelewa ukweli bila shaka watakuwa wenye makosa. Watu hawa watakuwa na makosa katika kila njia. Kiwango cha kuuelewa ukweli miongoni mwa wafuasi kinategemea kwa kiasi kikubwa watenda kazi. Bila shaka, ukweli kutoka kwa Mungu ni sahihi na hauna makosa, na ni hakika. Lakini, watenda kazi hawako sahihi kikamilifu na hatuwezi kusema kwamba ni wa kutegemewa kabisa. Ikiwa watenda kazi wana njia ya kuuweka ukweli katika njia ya matendo, basi wafuasi pia watakuwa na njia ya kuutenda. Ikiwa watenda kazi hawawezi kuuweka ukweli katika matendo bali wanashikilia mafundisho tu, wafuasi hawatakuwa na uhalisia wowote. Tabia na asili ya wafuasi vinaukiliwa na kuzaliwa na havihusiani na watenda kazi. Lakini kiwango ambacho kwacho wafuasi wanauelewa ukweli na kumfahamu Mungu kinategemeana na watenda kazi (hii ni kwa baadhi ya watu tu). Vyovyote alivyo mtenda kazi, hivyo ndivyo wafuasi anaowaongoza watakavyokuwa. Kile ambacho mtenda kazi anakidhihirisha ni asili yake mwenyewe, bila kuacha chochote. Yale anayowaambia wafuasi wake watende ndiyo yeye mwenyewe yuko radhi kuyafikia au ni yale anayoweza kutimiza. Watenda kazi wengi huwaambia wafuasi wao kufuata mambo fulani kulingana na yale wao wenyewe wanayoyafanya, licha ya kuwepo mengi ambayo watu hawawezi kuyafikia kabisa. Kile ambacho watu hawawezi kufanikisha kinakuwa kizuizi katika kuingia kwao.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp