Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Siri Kuhusu Biblia | Dondoo 276

10/08/2020

Leo, nani kati yenu anathubutu kusema kwamba maneno yote yaliyotamkwa na wale waliotumiwa na Roho Mtakatifu yalitoka kwa Roho Mtakatifu? Kuna anayethubutu kusema mambo kama haya? Ukisema mambo kama haya, basi mbona kitabu cha Ezra cha unabii kiliondolewa, na mbona jambo hilo pia likafanyiwa vitabu vya watakatifu na manabii wa kale? Kama yote yalitoka kwa Roho Mtakatifu, basi mbona mnathubutu kufanya maamuzi ambayo yanabadilika kama haya? Umehitimu kuchagua kazi ya Roho Mtakatifu? Hadithi nyingi kutoka Israeli pia zilitolewa. Na ukiamini kwamba maandishi haya yote ya kale yalitoka Roho Mtakatifu, basi mbona baadhi ya vitabu vilitolewa? Kama yote yalitoka kwa Roho Mtakatifu, yote yanapaswa kuwekwa, na kutumwa kwa ndugu na dada wa makanisa kuyasoma. Hayapaswi kuchaguliwa na kutolewa kwa matakwa ya mwanadamu; ni makosa kufanya hivyo. Kusema kwamba mazoefu ya Paulo na Yohana yalichanganywa na waliyoyaona binafsi hakumaanishi kwamba uzoefu na umaarifa wao ulitoka kwa Shetani, ila tu walikuwa na mambo yaliyotoka kwa mazoefu na waliyoyaona wao binafsi. Maarifa yao yalilingana na asili ya mazoefu halisi ya wakati huo, na ni nani anayeweza kusema kwa ujasiri kwamba yote yalitoka kwa Roho Mtakatifu? Kama Injili Nne zote zilitoka kwa Roho Mtakatifu, basi ilikuwaje kwamba Mathayo, Marko, Luka na Yohana kila mmoja alisema jambo tofauti kuhusu kazi ya Yesu? Msipoamini haya, basi angalia akaunti tofauti kwa Biblia ya jinsi Petro alivyomkana Yesu mara tatu: Yote ni tofauti, na kila moja ina sifa yake yenyewe. Wengi walio wajinga husema, Mungu wa mwili pia Alikuwa mwanadamu, kwa hivyo maneno Aliyoyazungumza yangeweza kutoka kikamilifu kwa Roho Mtakatifu? Kama maneno ya Paulo na Yohana yalichanganywa na matakwa ya mwanadamu, basi maneno Aliyoyasema yalikuwa kweli hayajachanganywa na matakwa ya mwanadamu? Watu wanaosema mambo kama haya ni vipofu na wajinga! Soma Injili Nne kwa kina; soma iliyorekodi kuhusu alichofanya Yesu, na maneno Aliyoyasema. Kila akaunti ilikuwa, kwa urahisi, tofauti, na kila ilikuwa na mtazamo wake. Kama vilivyoandikwa na waandishi wa vitabu hivi vyote vilitoka kwa Roho Mtakatifu, basi yote yanapaswa kuwa sawa na thabiti. Basi mbona kuna tofauti?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Majina na Utambulisho

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp