Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Kazi na Kuingia (8) | Dondoo 195

Nimezungumza mara nyingi sana kwamba kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kwa ajili ya kubadilisha roho ya kila mtu, kubadilisha nafsi ya kila mtu, ili kwamba moyo wake, ambao umeteseka sana na kiwewe, ubadilishwe, hivyo kuokoa roho yake, ambayo imeumizwa kwa kina zaidi na Shetani; ni ili kuamsha roho za watu, kuyeyusha mioyo yao baridi, na kuwaruhusu kurudisha nguvu za ujana. Haya ndiyo mapenzi makubwa ya Mungu. Weka pembeni mazungumzo kuhusu jinsi maisha na uzoefu wa mwanadamu yalivyo ya kiburi au ya kina; mioyo ya watu itakapokuwa imeamshwa, watakapokuwa wameamshwa kutoka katika ndoto zao na kujua kikamilifu madhara yaliyoletwa na joka kuu jekundu, kazi ya huduma ya Mungu itakuwa imekamilika. Siku ambayo kazi ya Mungu itakuwa imekamilika ni wakati ambapo mwanadamu ataanza rasmi kutembea kwenye njia ya imani sahihi katika Mungu. Wakati huu, huduma ya Mungu itakuwa imekamilika: Kazi ya Mungu kuwa mwili itakuwa imekamilika kabisa, na mwanadamu atakuwa ameanza rasmi kufanya kazi ambayo anapaswa kufanya—atatekeleza huduma yake. Hizi ni hatua za kazi ya Mungu. Hivyo, mnapaswa kutafuta kwa kupapasa njia yenu ya kuingia katika misingi ya kuyajua mambo haya. Haya yote ndiyo mnayopaswa kuyaelewa. Kuingia kwa mwanadamu kutakuwa bora tu wakati ambapo mabadiliko yametokea ndani kabisa mwa moyo wake, maana kazi ya Mungu ni wokovu kamili wa mwanadamu—mwanadamu aliyekombolewa, ambaye bado anaishi chini ya nguvu za giza, na ambaye hajawahi kuzinduka—kutoka katika eneo hili la kusanyiko la mapepo; ni ili kwamba mwanadamu aweze kuwekwa huru dhidi ya milenia ya dhambi, na kupendwa na Mungu, kulikanyaga kabisa joka kuu jekundu, kuanzisha ufalme wa Mungu, na kuupumzisha moyo wa Mungu haraka, ni kutoa mawazo bila woga, bila kubania, kwa chuki inayowaghadibisha, kuondoa kabisa vijidudu hivyo, kuwafanya muache maisha haya ambayo hayana tofauti na maisha ya ng’ombe au farasi, ili msiwe watumwa tena, ili msiweze kukanyagwa tena au kuamrishwa na joka kuu jekundu; hamtakuwa tena wa taifa hili lililoanguka, hamtakuwa tena wa joka kuu jekundu la kuchukiza, hamtafungwa nalo tena. Kiota cha mapepo hakika kitachanwachanwa na Mungu, na mtasimama kando ya Mungu—nyinyi ni wa Mungu, na sio wa dola hii ya watumwa. Mungu ameichukia sana jamii hii ya giza toka zamani. Anasaga meno Yake, Akitamani kumkanyaga joka huyu mwovu wa zamani wa kuchukiza, ili kwamba asiinuke tena, na hatamnyanyasa tena mwanadamu; Hatasamehe matendo yake ya zamani, Hatavumilia udanganyifu wake kwa mwanadamu, atalipiza kisasi kwa kila kosa alilofanya katika enzi zote; Mungu hatamhurumia hata kidogo huyu kiongozi wa uovu wote, Atamharibu kabisa.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana