Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa

Nimewatafuta wengi duniani wawe wafuasi Wangu. Kati yao ni wale wanaohudumu kama makuhani, wanaoongoza, wanaojumuisha wana, wanaojumuisha watu, na wale wanaotoa huduma. Ninawagawa katika makundi haya tofauti kwa msingi wa uaminifu wanaonionyesha. Wakati wanadamu wote wameainishwa kulingana na aina, yaani, asili ya kila aina ya mwanadamu inapowekwa wazi, basi Nitamhesabu kila mwanadamu miongoni mwa aina yake kamili na kuweka kila aina katika nafasi yake kamili ili Nikamilishe lengo Langu la ukombozi wa mwanadamu. Moja baada ya mwingine, Ninayaita makundi ya wale Ningependa kuwaokoa kurejea katika nyumba Yangu, kisha Ninawauliza wakubali kazi Yangu katika siku za mwisho. Wakati uo huo, Ninawaainisha wanadamu kulingana na aina, kisha Ninawatunukia au kuwaadhibu kila mmoja kulingana na matendo yake. Hizi ndizo hatua zinazojumuishwa katika kazi Yangu.

Sasa Ninaishi duniani na Ninaishi miongoni mwa wanadamu. Wanadamu wote wanashuhudia kazi Yangu na kulitazama neno Langu, na pamoja na hili Ninatawaza ukweli kwa kila mfuasi Wangu ili waweze kupokea uzima kutoka Kwangu na hivyo wapate njia ya kufuata. Kwa maana Mimi ni Mungu, Anayepeana uhai. Katika miaka mingi ya kazi Yangu, mwanadamu amepokea vitu vingi na kujinyima vitu vingi, lakini bado Ninasema kuwa mwanadamu haniamini kikamilifu. Kwa maana mwanadamu anakubali kijuujuu tu kuwa Mimi ni Mungu lakini hakubaliani na ukweli Ninaounena, na pia haweki ukweli katika matendo Ninavyomuamuru. Hiyo ni kusema, mwanadamu anakubali tu uwepo wa Mungu, lakini sio ule wa ukweli; mwanadamu hukubali uwepo wa Mungu, lakini sio wa uhai; mwanadamu anakubali tu jina la Mungu, lakini sio kiini Chake. Kutokana na ari yake, mwanadamu ni chukizo mbele Zangu. Kwa kuwa mwanadamu anatumia tu maneno yanayofurahisha masikio kunihadaa, na hakuna anayeniabudu kwa moyo wa kweli. Maneno yenu yanabeba majaribu ya ibilisi. Na maneno yenu ni yenye kiburi kupindukia, ni vile tu kama yamesemwa na malaika mkuu. Zaidi ya hayo, matendo yenu yamechakaa; tamaa zenu zisizo na kiasi na nia zenu zenye tamaa ni za kukera zikisikizwa. Nyote mmegeuka nondo katika nyumba Yangu na kuwa vyombo vya chukizo na kukataliwa na Mimi. Kwa maana hapana kati yenu anayependa ukweli, ni wanadamu wanaopenda baraka tu, walio na matumainiyo ya kupaa mbinguni, na wale hupendezewa kuona ukuu wa Kristo anapoonyesha nguvu Zake duniani. Mmewahi kuwaza jinsi mwanadamu mpotovu kama nyinyi, asiyejua Mungu ni nini, je, anafaa kumfuata Mungu? Mnawezaje kupaa mbinguni? Mnawezaje kufaa kuuona uzuri wa ukuu usio na kifani? Vinywa vyenu vimejaa maneno ya uongo na uchafu, usaliti na kiburi. Kamwe hamjanena maneno ya ukweli na utakatifu Kwangu, wala maneno ya kulijua neno Langu na kunitii. Hii ni imani ya aina gani? Nyoyo zenu zimejaa tamaa na mali; mawazo yenu yamejaa mali ya kiulimwengu. Kila siku, mnafanya hesabu jinsi mtakavyofaidika kutoka Kwangu, mkihesabu kiasi cha mali na vitu vya kidunia mlivyopata kutoka Kwangu. Kila siku, mnangoja baraka zaidi ziwashukie ili muweze kufurahia, hata zaidi na mema zaidi na vitu zaidi vya raha. Vilivyo katika mawazo yenu kila wakati si Mimi wala ukweli utokao Kwangu, bali ni mume (mke), wanao, au mkulacho na kuvaa, na vile mtakavyoburudika na starehe nzuri zaidi. Hata mlishindilie tumbo lenu kwa vyakula hadi pomoni, je, si nyinyi bado ni zaidi ya maiti tu? Hata muvike miili yenu kwa kifahari, si nyinyi bado ni maiti inayotembea isiyo na uhai? Mnafanya kazi kwa bidii kwa ajili ya tumbo lenu mpaka mnapotokwa na mvi, ilhali hakuna aliye tayari kuutoa unywele mmoja kwa ajili ya kazi Yangu. Mnasafiri, mnafanya kazi, na kupiga bongo kwa ajili ya miili yenu, na kwa sababu ya watoto wenu, ilhali hakuna anayepatwa na wasiwasi au kufikiri juu ya lililo moyoni Mwangu au ndani ya mawazo Yangu. Mna matamanio ya kufaidi nini kutoka Kwangu?

Siharakishwi katika kazi Yangu kamwe. Hata mwanadamu anifuate vipi, Mimi hufanya kazi Yangu kulingana na kila hatua, iliyo katika mpango Wangu. Kwa hivyo, hata ingawa mnaweza kuasi dhidi Yangu sana, Sisimamishi kazi Yangu na Ninaendelea kunena maneno Ninayotaka kunena. Ninawaita katika nyumba Yangu wale Niliowajaalia kulisikiliza neno Langu, kisha Ninawaweka wote wanaotii na kulitarajia neno Langu mbele ya kiti Changu cha enzi. Wale wanaolisaliti neno Langu, wale wasiotii na kujisalimisha Kwangu, na wale wanaonipinga kwa uwazi, watatupwa kando wakingoja adhabu ya mwisho. Wanadamu wote wanaishi katika upotovu na chini ya mkono wa yule mwovu, kwa hivyo sio wengi wanaonifuata wako na hamu ya ukweli. Hiyo ni kusema, wengi wao hawaniabudu kwa moyo wa kweli au kwa ukweli, lakini wanajaribu kupata uaminifu Wangu kupitia ufisadi, uasi na njia nyinginezo danganyifu. Ni kwa sababu hii ndio Nasema, “Wengi wameitwa, lakini ni wachache wamechaguliwa.” Wote walioitwa ni wafisadi kupindukia na wanaishi katika enzi sawa, lakini wale waliochaguliwa ni ile sehemu tu ya wanaoamini, kuukubali na kutia ukweli katika matendo. Wanadamu hawa ni sehemu ndogo tu ya wanadamu wote, na kutoka miongoni mwa wanadamu hawa Nitapata utukufu zaidi. Ukijipima kulingana na maneno haya, je, mnajua kama nyinyi mumo kati ya waliochaguliwa? Je, hatima yenu itakuwa ipi?

Tayari Nimeshasema kuwa wale wanaonifuata ni wengi lakini wanaonipenda kwa moyo wa kweli ni wachache. Huenda ikawa wengine wanasema, “Ningeweza kujinyima mengi kiasi hicho ikiwa sikupendi Wewe? Ningeendelea bado kukufuata ikiwa sikupendi?” Unazo sababu nyingi kwa hakika. Kwa hakika, upendo wako ni mkubwa, lakini nini umuhimu wa mapenzi yako Kwangu? “Upendo,” kama unavyoitwa, unaashiria hisia safi isiyo na dosari, ambapo unatumia moyo wako kupenda, kuhisi, na kuwa na mawazo. Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi na hakuna kutenga. Katika upendo hakuna shaka, hakuna uongo na hakuna ujanja. Katika upendo hakuna kukaa mbali na hakuna kitu kisicho safi. Ukipenda, basi hudanganyi, hulalamiki, huasi na hupeani au kuchukua rushwa. Ukipenda, basi unajinyima bila kusononeka, unavumilia hali ngumu, na unaambatana na Mimi. Ungeacha vitu vyako vyote kwa sababu Yangu: familia yako, siku zako za baadaye, ujana wako, na ndoa yako. La sivyo, basi upendo wako si upendo hata kidogo, bali ni uongo na usaliti! Upendo wako ni upendo wa aina gani? Je, ni upendo wa kweli? Je, ni wa uongo? Umejinyima kiasi gani? Umejitolea kiasi gani? Je, Nimepata upendo kiasi gani kutoka kwako? Je, unajua? Moyo wenu umejaa maovu, usaliti na uongo. Kwa hivyo kiwango kipi cha upendo wenu ni kichafu? Mnaamini kuwa mmewacha kila kitu kwa ajili Yangu; Mnaamini kuwa upendo wenu Kwangu tayari umetosha, ila ni kwa nini maneno yenu na matendo yenu huambatana na uasi na uongo? Mnanifuata, ilhali hamkubali neno Langu. Je, hili linachukuliwa kama upendo? Mnanifuata, kisha mnanitenga na kuniweka kando. Je, huu ni upendo? Mnanifuata, ilhali mko na shaka na Mimi. Je, huu unachukuliwa kama upendo? Mnanifuata, ilhali hamkubali kuwepo Kwangu. Je, huu ni upendo? Mnanifuata, ilhali hamnitendei vile Ninavyopaswa kutendewa na mnafanya mambo yawe magumu Kwangu katika kila hatua. Je, hii inachukuliwa kama mapenzi? Mnanifuata, ilhali mnanichukua kama mjinga na kunidanganya Mimi katika kila jambo. Je, haya ni mapenzi? Mnanihudumia, ilhali hamnichi. Je, huu ni upendo? Mnanipinga katika kila hali na kila jambo. Je, yote haya yanachukuliwa kama upendo? Mmejinyima mengi, huu ni ukweli, ilhali hamjawahi kuyafanya Ninayowaagiza mfanye. Je, huu unaweza kuwa upendo? Uchunguzi wa makini unaashiria kuwa hamna upendo Kwangu ndani yenu. Baada ya miaka hii mingi ya kazi na maneno mengi Niliyosambaza, ni kiasi kipi mlichopokea kwa hakika? Je, hii haistahili mtazamo mwangalifu wa nyuma? Ninawaonya: Wale Niwaitao sio wale ambao hawajapotoshwa, bali wale Ninaowachagua ni wale wanaonipenda kwa ukweli. Kwa hivyo, mnapaswa kuwa makini na maneno na matendo yenu, na muichunguze azma na mawazo yenu ili vitu hivi visije vikavuka mipaka. Wakati wa mwisho, fanyeni jitihada ili muonyeshe mapenzi yenu Kwangu, isije ghadhabu yangu ikabaki kwenu milele!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp