Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku

Tangu mwanzo wa kazi Yake katika ulimwengu mzima, Mungu ameamulia kabla watu wengi kumhudumia Yeye, wakiwemo watu kutoka kila nyanja ya maisha. Kusudio Lake ni kutimiza mapenzi Yake Mwenyewe na kuhakikisha kwamba kazi Yake hapa ulimwenguni imetimia. Hili ndilo kusudio la Mungu katika kuwachagua watu wa kumhudumia Yeye. Kila mtu anayehudumia Mungu lazima aelewe mapenzi haya ya Mungu. Kupitia kazi hii Yake, watu wanaweza kuona vizuri zaidi hekima ya Mungu na uweza wa Mungu, pamoja na kuona kanuni za kazi Yake hapa ulimwenguni. Mungu huja hapa ulimwenguni kimatendo ili kufanya kazi Yake na kuwasiliana na watu ili nao waweze kuona vizuri zaidi matendo Yake. Leo, ni bahati kubwa kwa kundi hili lenu kumhudumia Mungu wa vitendo. Hii ni baraka kubwa kwenu. Kwa kweli Mungu anawainua. Wakati Mungu anapomteua mtu ili amhudumie Yeye, siku zote Yeye huwa na kanuni zake binafsi. Kumhudumia Mungu hakika si suala tu la kuwa na shauku, kama vile watu wanavyofikiria. Leo mtu anaweza kumhudumia Mungu akiwa mbele Yake, kama mnavyoweza kuona, kwa sababu anaongozwa na Mungu na anafanya kazi kupitia kwa Roho Mtakatifu; na kwa sababu anatafuta ukweli wake. Haya ndiyo mahitaji ya kiwango cha chini zaidi ya mtumishi wa Mungu.

Kumhudumia Mungu si kazi rahisi. Wale ambao tabia yao potovu haibadiliki hawawezi kamwe kumhudumia Mungu. Kama tabia yako haijahukumiwa na kuadibiwa na neno la Mungu, basi tabia yako bado inawakilisha Shetani. Hii inatosha kuthibitisha kwamba huduma yako kwa Mungu ni kutokana na nia yako nzuri wewe binafsi. Ni huduma inayotokana na asili yako ya kishetani. Unamhudumia Mungu na hulka yako ya kiasili, na kulingana na mapendeleo yako ya kibinafsi; na zaidi, unaendelea kufikiria kwamba Mungu anapenda chochote kile unachopenda, na kwamba Mungu anachukia chochote kile ambacho hupendi, na kazi yako inaongozwa kabisa na mapendeleo yako binafsi. Je, huku kunaweza kuitwa kumhudumia Mungu? Hatimaye tabia yako ya maisha haitabadilishwa hata chembe. Kwa hakika, utakuwa msumbufu zaidi kwa sababu umekuwa ukimhudumia Mungu, na itafanya tabia yako potovu kukita mizizi zaidi. Kwa njia hii, utaendeleza kwa ndani sheria kuhusu huduma kwa Mungu zitokanazo kimsingi na hulka yako binafsi, na uzoefu unaotokana na kuhudumu kwako kulingana na tabia yako binafsi. Hii ni uzoefu na mafunzo ya kibinadamu. Ni filosofia ya maisha ya binadamu. Watu kama hawa wanapatikana miongoni mwa Mafarisayo na wale wajumbe wa kidini. Kama hawatawahi kuzinduka na kutubu, basi hatimaye watageuka na kuwa wale Mkristo wa uwongo watakaoonekana siku za mwisho. Watakuwa wadanganyifu. Mkristo wa uwongo na wadanganyifu waliozungumziwa watatokana na aina ya watu kama hawa. Kama wale wanaomhudumia Mungu watafuata hulka yao na kutenda kulingana na mapenzi yao binafsi, basi watakuwa katika hatari isiyoisha ya kutupwa nje. Wale wanaotumia miaka yao mingi ya uzoefu kwa kumhudumia Mungu ili kutega mioyo ya watu, kusomea na kuwadhibiti watu, kujiinua wao wenyewe—na wale katu hawatubu, katu hawakiri, katu hawakatai nguvu manufaa ya cheo—watu hawa watasambaratika mbele ya Mungu. Hawa ni watu walio kama Paulo, waliojaa majivuno na wanaoonyesha ukubwa wao. Mungu hatawakamilisha watu kama hawa. Aina hii ya huduma huzuia kazi ya Mungu. Watu wanapenda kushikilia vitu vya kale. Wanashikilia fikira za kale, wanashikilia vitu vya kale. Hiki ni kizuizi kikuu katika huduma yao. Kama huwezi kudondosha vitu hivi, vitu hivyo vitayakaba maisha yako yote. Mungu hatakupongeza, hata kwa uchache wowote, hata kama utapoteza miguu yako au kuuvunja mgongo wako ukitia bidii, au hata kuuliwa ukiwa katika “huduma” ya Mungu. Kinyume cha Mambo ni kwamba: Atasema wewe ni mtenda maovu.

Kuanzia leo, Mungu ataweza kuwafanya watu wasiokuwa na fikira za kidini kuwa watimilifu kwa njia rasmi, ambao wako tayari kuweka pembeni nafsi zao za kale, na ambao wanamtii tu Mungu, pamoja na kuwafanya kuwa watimilifu wale wanaotamani neno la Mungu. Watu hawa wanafaa kusimama na kumhudumia Mungu. Kwake Mungu kunayo na hekima nyingi na isiyoisha. Kazi yake ya kustaajabisha na matamshi yake yenye thamani ni vitu ambavyo vipo ili watu wengi zaidi kuweza kufurahia. Kama ilivyo sasa, vitu hivi vipya haviwezi kukubaliwa na wale walio na fikira za kidini, wanaochukua hali ya ukubwa, na wale ambao hawaweki pembeni nafsi zao za kale. Roho Mtakatifu hana fursa ya kuwafanya watu kama hao kuwa watimilifu. Kama mtu hana hamu ya kutii, na hana kiu cha neno la Mungu, basi mtu huyo hataweza kupokea mambo mapya. Wataendelea tu kuasi zaidi na zaidi, kuwa wajanja zaidi na zaidi, na hatimaye kujipata kwenye njia mbaya. Katika kazi ya Mungu ya sasa, Atawainua watu zaidi wanaompenda Yeye kwa kweli na wanaoweza kukubali mwangaza mpya. Na Atakatiza kabisa maafisa wa kidini wanaoonyesha ukubwa wao. Hataki mtu hata mmoja anayekataa mabadiliko. Je, unataka kuwa mmoja wa watu hao? Je, unatekeleza huduma yako kulingana na mapendeleo yako, au unafanya kile Mungu anachotaka? Hili ni jambo ambalo lazima ujijulie mwenyewe. Je, wewe ni mmojawapo wa maafisa wa kidini, au wewe ni mtoto mchanga aliyezaliwa na anayefanywa kuwa mtimilifu na Mungu? Je, ni kiwango kipi cha huduma yako ambacho kinapongezwa na Roho Mtakatifu? Kati ya kiwango hiki ni kipi ambacho Mungu hatakumbuka? Baada ya miaka mingi ya huduma, umeleta mabadiliko kiasi kipi katika maisha yako? Je, uko wazi kuhusu mambo haya yote? Kama unayo imani ya kweli, basi utaweka pembeni fikira zako za kale za kidini na utahudumia Mungu kwa njia bora zaidi na kwa njia mpya. Kama utajitahidi zaidi sasa, hujachelewa sana. Fikira za kale za kidini zitamnyima mtu maisha mazuri. Uzoefu ambao anapata utamwongoza mbali na Mungu, kufanya mambo kwa njia yake mwenyewe. Kama hutatupilia mbali vitu hivi, vitakuwa kikwazo katika kukua kwa maisha yako. Mungu siku zote amewafanya wote wanaomhudumia Yeye kuwa watimilifu. Hawatupilii mbali vivihivi tu. Kutakuwa na mustakabali kwako kama tu utakubali kwa kweli hukumu na vilevile kuadibiwa kwa neno la Mungu, kama unaweza kuweka pembeni matendo na mafundisho ya kidini yako ya kale ya kidini, na kuepuka kutumia fikira za kale za kidini kama kipimo cha neno la Mungu hii leo. Lakini kama utashikilia vitu vya kale, kama bado unavithamini, basi huwezi kupata wokovu. Mungu hatawatambua watu kama hao. Kama kweli unataka kufanywa kuwa mtimilifu, basi lazima uamue kutupilia mbali kabisa kila kitu cha kale. Hata kama kile kilichokuwa kimefanywa awali kilikuwa sahihi, hata kama ilikuwa ni kazi ya Mungu, utaiweka pembeni; hufai kuishikilia. Hata kama ilikuwa kazi ya Roho Mtakatifu iliyo wazi, iliyofanywa moja kwa moja na Roho Mtakatifu, leo lazima uiweke pembeni. Hufai kuishikilia. Hivi ndivyo Mungu anavyotuamuru. Kila kitu lazima kipate upya wake. Katika kazi ya Mungu na neno la Mungu, Mungu harejelei vitu vya kale ambavyo vilishapita, na vilevile hafukui historia ya kale. Mungu siku zote ni mpya na hajawahi kuwa mzee. Hashikilii hata maneno Yake mwenyewe aliyoyasema kale. Hii inaonyesha kwamba Mungu hafuati mafundisho ya dini yoyote. Katika hali hii, kama mwanadamu, kama siku zote unashikilia kabisa vitu vya kale na kuvitumia vivyohivyo fomula huku naye Mungu hafanyi kazi tena katika njia Alizokuwa akifanya awali, basi maneno yako na matendo yako hayakatizi? Je, hujawa adui wa Mungu? Je, uko radhi kuyaharibu maisha yako yote kwa sababu ya mambo haya ya kale? Mambo haya ya kale yanakufanya kuwa mtu anayezuia kazi ya Mungu. Je, mtu kama huyu ndiye wewe unataka kuwa? Kama kweli hutaki kuwa hivyo, basi acha mara moja kile unachofanya na ubadilike; anza tena upya. Mungu hakumbuki huduma yako ya kale.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp