Utendaji (6)

Leo, watu wengi hawawezi kufikia akili alizokuwa nazo Petro—sembuse kuweza kufikia akili alizokuwa nazo Paulo. Hata hawajitambui kama alivyojitambua Paulo. Ingawa Paulo aliangushwa na Bwana kwa sababu alimtesa Bwana Yesu, baadaye alikuwa na azimio la kufanya kazi na kuteseka kwa ajili ya Bwana. Yesu alimpa ugonjwa, na baadaye, Paulo aliendelea kuugua ugonjwa huu mara tu alipoanza kufanya kazi. Kwa nini alisema kuwa alikuwa na mwiba kwenye mwili wake? Kwa kweli, mwiba huo ulikuwa ugonjwa—na kwa Paulo, ulikuwa udhaifu mbaya sana. Haijalishi alifanya kazi kiasi gani au jinsi azimio lake la kuteseka lilivyokuwa kubwa, hakuweza kuondoa mwiba huo. Lakini Paulo alikuwa mwenye ubora mzuri zaidi wa tabia kuliko ninyi watu wa leo, na pia alijitambua na alikuwa na akili nyingi kuwaliko ninyi. Baada ya Paulo kuangushwa na Yesu, aliacha kuwatesa wafuasi wa Yesu, na akaanza kuhubiri na kuteseka kwa ajili ya Yesu. Na ni kitu gani kilichomtia moyo avumilie mateso? Paulo aliamini kwamba, kwa kuwa alikuwa ameuona mwangaza mkuu, ilimlazimu awe na ushuhuda kwa Bwana Yesu, asiwatese tena wafuasi wa Yesu, na asiipinge kazi ya Mungu tena. Paulo alikuwa mmoja wa watu wenye vyeo vya juu katika dini. Alikuwa mwenye maarifa na mwenye vipawa sana, aliwadharau watu wa kawaida, na alikuwa na hulka nzito kuliko watu wengi. Lakini baada ya “mwangaza mkuu” kumwangazia, aliweza kumfanyia Bwana Yesu kazi, akaweka azimio lake kuteseka kwa ajili ya Mungu na kujitoa kwa Mungu, jambo ambalo lilithibitisha kwamba alikuwa na akili. Wakati ambapo alikuwa akiwatesa na kuwakamata wafuasi wa Yesu, Yesu alionekana kwake na kumwambia: “Paulo, mbona wanitesa?” Paulo alianguka chini mara moja na kusema: “Wewe ni nani, Bwana?” Sauti kutoka mbinguni ikasema: “Mimi ndiye Yesu ambaye unamtesa.” Mara moja, Paulo aliamka, na hapo tu ndipo alijua kwamba Yesu alikuwa Kristo, ya kwamba alikuwa Mungu. “Lazima nitii. Mungu amenipa neema hii—nilimtesa hivyo, lakini Hakuniangusha, wala Hakunilaani. Lazima niteseke kwa ajili Yake.” Paulo alitambua kuwa alikuwa amemtesa Bwana Yesu Kristo na sasa alikuwa anawaua wafuasi Wake, kwamba Mungu hakuwa amemlaani, lakini Alikuwa amemwangazia nuru. Hili lilimtia moyo, na akasema: “Ingawa sikuuona uso Wake, niliisikia sauti Yake na nikaona mwangaza Wake mkuu. Ni sasa tu ndipo naona kweli kuwa Mungu ananipenda sana, na kwamba kwa kweli Bwana Yesu Kristo ndiye Mungu anayemhurumia mwanadamu na kuzisamehe dhambi za wanadamu milele. Ninaona kweli kuwa mimi ni mtenda dhambi.” Ingawa, baadaye, Mungu alitumia vipawa vya Paulo kufanya kazi, lisahau hili kwa sasa. Azimio lake wakati huo, akili yake ya kawaida ya binadamu, na kujitambua kwake—ninyi hamwezi kufanikisha mambo haya. Je, leo hamjapata mwanga mwingi? Je, watu wengi hawajaona kuwa tabia ya Mungu ni ile ya uadhama, ghadhabu, hukumu na kuadibu? Laana, majaribu, na usafishaji vimewapata watu mara nyingi—na wamejifunza nini? Umepata nini kutokana na kufundishwa nidhamu na kushughulikiwa? Maneno makali, mapigo, na hukumu vimekupata mara nyingi, lakini huvitilii maanani. Huna hata akili kidogo aliyokuwa nayo Paulo—je, wewe hujasalia nyuma sana? Pia kulikuwa na mengi ambayo Paulo hakuona kwa dhahiri. Alijua tu kuwa mwangaza ulikuwa umemwangazia, lakini hakujua ya kwamba alikuwa ameangushwa; yeye binafsi aliamini kwamba baada ya mwangaza kumwangazia, lazima ajitumie kwa ajili ya Mungu, ateseke kwa ajili ya Mungu, afanye kila kitu ili amwandalie Bwana Yesu Kristo njia, na awapate watenda dhambi wengi zaidi ili wakombolewe na Bwana. Hili ndilo lilikuwa azimio lake, na kusudi la pekee la kazi yake—lakini alipofanya kazi, ugonjwa huo bado haukumwacha, hadi kifo chake. Paulo alifanya kazi kwa zaidi ya miaka ishirini. Aliteseka sana, na akapitia mateso na dhiki nyingi, ingawa, bila shaka, haya yalikuwa machache sana kuliko majaribu aliyopitia Petro. Je, ni jambo la kusikitishaje ikiwa ninyi hamna hata akili ya Paulo? Hali ikiwa hivi, Mungu anawezaje kuanza kazi kubwa hata zaidi ndani yenu?

Alipokuwa akieneza injili, Paulo alipitia mateso makubwa. Kazi aliyofanya, azimio lake, imani yake, uaminifu, upendo, uvumilivu, na unyenyekevu wake wakati huo, na mambo mengine mengi ya nje aliyoishi kwa kudhihirisha, yalikuwa ya kiwango cha juu kuliko yenu ninyi watu leo. Kusema kwa ukali zaidi, ndani yenu, hakuna akili ya kawaida; hamna hata dhamiri au ubinadamu wowote. Mmepungukiwa na mengi sana! Hivyo, wakati mwingi, hakuna akili ya kawaida na hakuna dalili za kujitambua katika kile mnachoishi kwa kudhihirisha. Ingawa wakati huo Paulo alikuwa akiugua ugonjwa wa mwili, aliendelea kusali na kutafuta: “Ugonjwa huu ni nini kweli? Nimemfanyia Bwana kazi hii yote, kwa nini shida hii hainiachi? Inawezekana kuwa Bwana Yesu ananijaribu? Je, Ameniangusha? Angekuwa ameniangusha, ningekufa wakati huo, na singeweza kumfanyia kazi hii yote, wala singeweza kupokea mwangaza mwingi hivyo. Pia alitambua azimio langu.” Paulo alihisi daima kwamba ugonjwa huu ulikuwa ni Mungu aliyekuwa akimjaribu, kwamba ulikuwa unaichovya imani na utashi wake—hivi ndivyo alivyoona Paulo. Kwa kweli, ugonjwa wake ulikuwa maafa ya ugonjwa yaliyoachwa kutoka wakati ambapo Bwana Yesu alimwangusha. Yalimweka katika shinikizo la hisia, na yakaudhibiti uasi wake. Mkijipata katika hali kama ya Paulo, je, mtafanyaje? Je, azimio na uwezo wenu wa kuteseka unaweza kulingana na ule wa Paulo? Leo, mkikumbwa na ugonjwa fulani, au mpitie jaribio kubwa, na msababishwe kuteseka, ni nani anayejua jinsi mtakavyokuwa. Kama mngefungiwa kwenye tundu la ndege na mruzukiwe kila mara, mngekuwa sawa. La sivyo mngekuwa tu kama mbwa mwitu, msio na ubinadamu wowote. Kwa hivyo mnapopitia shida au kikwazo kidogo, ni yenye manufaa kwenu; kama lingekuwa jambo rahisi kwenu basi mngeangamia, na kisha mngelindwaje? Leo, ni kwa sababu mnaadibiwa, kuhukumiwa, na kulaaniwa ndiyo mnapewa ulinzi. Ni kwa sababu mmeteseka sana ndiyo mnalindwa. Kama sivyo, mngekuwa tayari mmepotoka. Huku si kufanya mambo yawe magumu kwenu kwa makusudi—asili ya mwanadamu ni ngumu kubadili, na lazima iwe hivyo ili tabia zao zibadilishwe. Leo, hamna hata dhamiri au akili ambazo Paulo alikuwa nazo, wala hamwezi hata kujitambua kama yeye. Lazima mushurutishwe kila wakati, na kila wakati lazima muadibiwe na kuhukumiwa ili roho zenu zichangamshwe. Kuadibu na hukumu ndivyo bora kabisa kwa maisha yenu. Na inapolazimu, lazima pia ukweli unaowafikia uadibiwe; ni hapo tu ndipo mtakapotii kikamilifu. Asili zenu ni kana kwamba bila kuadibu na kulaani, hamngetaka kuinamisha vichwa vyenu, hamngetaka kutii. Bila ukweli ulio mbele yenu, hakungekuwa na matokeo. Ninyi ni duni sana na msio na thamani katika tabia! Bila kuadibu na hukumu, itakuwa vigumu kwenu kushindwa, na itakuwa vigumu kwa udhalimu na kutotii kwenu kushindwa. Asili yenu ya zamani imekita mizizi sana. Kama mngewekwa juu ya kiti cha enzi, hamngefahamu urefu wa mbingu na kina cha dunia, sembuse kujua mnakoelekea. Hamjui hata mlikotoka, hivyo mngewezaje kumjua Bwana wa uumbaji? Bila kuadibiwa na kulaaniwa kwa wakati unaofaa leo, siku yenu ya mwisho ingekuwa imeshawadia kitambo. Hiyo ni kando na majaaliwa yenu—je, hayo hayatakuwa katika hatari ya karibu zaidi? Bila kuadibu na hukumu hii ya wakati unaofaa, ni nani anayejua jinsi ambavyo mngekuwa wenye kiburi, au jinsi ambavyo mngekuwa wapotovu. Kuadibu huku na hukumu hii vimewafikisha leo, na vimehifadhi kuwepo kwenu. Kama bado “mngeelimishwa” kwa kutumia njia zile zile kama za “baba” yenu, ni nani ajuaye mngeingia katika ulimwengu upi! Hamna uwezo wa kujidhibiti na kutafakari kujihusu wenyewe hata kidogo. Kwa watu kama ninyi, mkifuata na kutii tu bila kusababisha ukatizaji au usumbufu wowote, malengo Yangu yatatimia. Je, hamfai kufanya vema zaidi katika kukubali kuadibu na hukumu ya leo? Je, mna chaguo gani jingine? Paulo alipomwona Bwana Yesu akizungumza na kufanya kazi, bado hakuamini. Baadaye, baada ya Bwana Yesu kusulubiwa msalabani na kisha kufufuka, alijua ukweli huu, lakini aliendelea kutesa na kupinga. Hii ndiyo maana ya kutenda dhambi kwa makusudi, na kwa hivyo aliangushwa. Mwanzoni, alijua kwamba kulikuwa na Mfalme kati ya Wayahudi aliyeitwa Yesu, alikuwa amesikia hili. Baadaye, alipokuwa akihubiri hekaluni na kuhubiri nchini kote, alikwenda kinyume na Yesu, akikataa kwa kiburi kumtii mtu yeyote. Vitu hivi vilikuwa kizuizi kikubwa kwa kazi ya wakati huo. Yesu alipokuwa Akifanya kazi, Paulo hakuwatesa na kuwakamata watu moja kwa moja, lakini alitumia mahubiri na maneno kuiharibu kazi ya Yesu. Baadaye, baada ya Bwana Yesu Kristo kusulubiwa msalabani, alianza kuwakamata wafuasi, akikimbia kutoka mahali pamoja hadi pengine na kufanya kila awezalo kuwatesa. Ni baada tu ya “mwangaza” kumwangazia ndipo alizinduka na kupitia majuto makubwa. Baada ya kuangushwa, ugonjwa wake haukuwahi kumwacha. Wakati mwingine, alihisi kuwa ugonjwa wake ulikuwa umezidi kuwa mbaya, na hakuweza kutoka kitandani. Aliwaza: “Ni nini kinachoendelea? Je, nimeangushwa kweli?” Ugonjwa huo haukuwahi kumwacha, na ni kwa sababu ya ugonjwa huu ndiyo alifanya kazi nyingi. Inaweza kusemwa kwamba Yesu alimwekea Paulo ugonjwa huu kwa sababu ya kiburi chake na ukaidi wake; ilikuwa ni adhabu kwa Paulo, lakini ilifanyika pia ili kutumia vipawa vya Paulo katika kazi ya Mungu, ili kazi Yake iweze kupanuliwa. Kwa kweli, halikuwa kusudi la Mungu kumwokoa Paulo, bali kumtumia. Lakini tabia ya Paulo ilikuwa ya kiburi na ukaidi sana, na kwa hivyo “mwiba” uliwekwa ndani yake. Mwishowe, kufikia wakati ambapo Paulo alimaliza kazi yake, ugonjwa huo haukuwa mateso makubwa sana kwake, na kazi yake ilipokuwa ikiisha, aliweza kusema maneno “Nimepigana vita vizuri, nimeutimiza mwendo wangu, nimeihifadhi imani: Kutoka sasa kuendelea taji la haki limewekwa kwangu”—ambayo alisema kwa sababu hakuijua kazi ya Mungu. Kuna wengi kati yenu kama Paulo, lakini kweli mkiwa na azimio la kufuata hadi mwisho wa njia, hamtadhulumiwa. Hatutajadili hapa njia ambazo Paulo alikuwa mwasi na mpinzani; acha tusalie katika sehemu yake ambayo ilikuwa nzuri na yenye kusifika: Alikuwa na dhamiri, na baada ya kupokea “mwangaza” mara moja, aliweza kujitolea kwa Mungu na kuteseka kwa ajili ya Mungu. Hii ilikuwa sifa yake nzuri. Hata hivyo, ikiwa kuna wale ambao wanaamini kwamba kwa sababu alikuwa na sifa nzuri basi alikuwa mtu aliyebarikiwa, ikiwa wanafikiri kwamba hakupasa kuadibiwa, basi haya ni maneno ya watu wasio na akili.

Watu wengi wanapoomba na kusoma maneno ya Mungu, wao husema kuwa wako tayari kumtii Mungu, lakini kisha wanakuwa waasherati faraghani, na wanaona kuwa hilo silo jambo. Maneno ya Mungu yanasemwa tena na tena, yakifichua safu baada ya safu, na ni mpaka tu safu ya chini kabisa ya watu inapofunuliwa ndipo wao “hupata amani” na kuwa wenye kiwango kidogo cha majivuno na ukaidi na wasio na kiburi sana. Hali zenu zikiwa kama zilivyo leo, lazima bado mpigwe kikatili na kufunuliwa, na kuhukumiwa kwa undani kabisa, ili msipate nafasi ya kupumzika. Kwenu, ni bora kuadibu na hukumu kali visiwaache, na shutuma na laana visiwe mbali na ninyi, hili likiwaruhusu muone kwamba mkono wa amri za utawala wa Mungu hauwaachi kamwe. Kama tu katika Enzi ya Sheria, Haruni alipoona ya kuwa Yehova hakuwahi kumwacha (alichokiona kilikuwa mwongozo na ulinzi wa kila wakati wa Yehova; mwongozo wa Mungu mnaouona ninyi leo ni kuadibu, laana, na hukumu), leo pia mkono wa amri za utawala wa Yehova hauwaachi, pia. Hata hivyo, kuna jambo moja ambalo mnaweza kukosa kuwa na wasiwasi kulihusu: Haijalishi jinsi mnavyopinga, kuasi, na kuhukumu, hakutakuwa na madhara yoyote kwa miili yenu. Lakini ikiwa kuna watu wanaovuka mipaka katika upinzani wao na kuizuia kazi, hili halikubaliki; kuna mpaka. Usiyakatize au kuvuruga maisha ya kanisa, na usiikatize kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa mengine, unaweza kufanya chochote unachotaka. Ukisema hutaki kufuatilia maisha na unatamani kurudi katika ulimwengu, basi harakisha na uende! Mnaweza kufanya chochote mnachotaka mradi hakizuii kazi ya Mungu. Lakini kuna jambo moja zaidi unalohitaji kujua: Mwishowe, watenda dhambi wakaidi kama hao wote wataondolewa. Leo, huenda usikaripiwe, lakini mwishowe, ni sehemu tu ya watu ndio watakaoweza kushuhudia—na wengine wote watakuwa hatarini. Ikiwa hutaki kuwa kwenye mkondo huu, hiyo ni sawa. Watu wa leo hutendewa kwa uvumilivu; Sikuwekei mipaka, mradi huogopi kuadibiwa kesho. Lakini ikiwa uko kwenye mkondo huu, lazima ushuhudie, na lazima uadibiwe. Ikiwa unataka kukataa hili na urudi katika ulimwengu, hiyo ni sawa—hakuna mtu anayekuzuia! Lakini ukifanya kazi inayoharibu na kuvuruga kazi ya Mungu, huwezi kusamehewa kwa ajili ya hilo hata kidogo! Na kuhusu yale ambayo macho yako yanaona na masikio yako kusikia kuhusu ni watu gani wanaoadibiwa, na ni gani ambao familia zao zinalaaniwa—kuna mipaka na vizuizi kwa haya yote. Roho Mtakatifu hafanyi mambo kiholela. Kulingana na dhambi ambazo mmetenda, kama mngetendewa na kuchukuliwa kwa uzito kwa kutegemea udhalimu wenu wenyewe, ni nani kati yenu angeweza kusalia? Ninyi nyote mngepatwa na msiba, na hakuna hata mmoja wenu angekuwa na matokeo mazuri. Lakini leo, watu wengi wanatendewa kwa uvumilivu. Hata ingawa mnahukumu, mnaasi, na kupinga, mradi hamkatizi, basi Nitakutana na ninyi kwa tabasamu. Ikiwa kweli mnafuatilia maisha, basi lazima mwadibiwe kiasi, na lazima mvumilie uchungu wa kutengana na kile mnachopenda ili muende kwenye meza ya upasuaji kufanyiwa upasuaji; lazima ustahimili maumivu, kama tu vile Petro alivyokubali majaribu na mateso. Leo, uko mbele ya kiti cha hukumu. Katika siku zijazo, lazima mwende kwenye “gilotini,” ambao utakuwa wakati ambapo “mnajitoa” wenyewe.

Wakati wa hatua hii ya mwisho ya kazi katika siku za mwisho, labda unaamini kuwa Mungu hatauangamiza mwili wako, na inaweza kusemwa kwamba huenda usipate maradhi yoyote hata ingawa unampinga na kumhukumu Yeye—lakini maneno makali ya Mungu yatakapokujia, wakati uasi na upinzani wako na sura zako mbaya zitakapofunuliwa, hutaweza kujificha. Utajikuta umeshikwa na hofu, usijue la kufanya. Leo, lazima ninyi muwe na dhamiri kiasi. Msichukue nafasi za waovu ambao wanampinga na kumwasi Mungu. Unapaswa kumpa kisogo babu yako wa zamani; hiki ndicho kimo unachopasa kuwa nacho, na huu ndio ubinadamu ambao unapaswa kuwa nao. Wewe daima huwezi kuweka kando matarajio yako ya baadaye au starehe za leo. Mungu anasema: “Mradi mnafanya yote mnayoweza ili kunifuata na kufuatilia ukweli, hakika Nitawafanya muwe wakamilifu. Mara mnapokamilishwa, mtakuwa na hatima nzuri—mtaletwa katika ufalme Wangu ili mfurahie baraka pamoja na Mimi.” Mmeahidiwa hatima nzuri, lakini mahitaji kutoka kwenu hayawezi kupunguzwa kamwe. Pia kuna sharti: Bila kujali kama mtashindwa au kukamilishwa, leo lazima mpitie kuadibu kiasi na mateso kiasi; lazima mpigwe na kufundishwa nidhamu; lazima msikilize maneno Yangu, mfuate njia Yangu, na mfanye mapenzi ya Mungu—hiki ndicho kile ninyi wanadamu mnapaswa kufanya. Bila kujali jinsi unavyofuatilia, lazima usikie waziwazi hivi. Ikiwa kweli una utambuzi halisi, basi unaweza kuendelea kufuata. Ikiwa unaamini kuwa hakuna matarajio au matumaini hapa, basi unaweza kwenda. Maneno haya yamezungumzwa wazi kwako, lakini ikiwa kweli unatamani kwenda, hili linaonyesha tu kuwa huna dhamiri hata kidogo; hiki kitendo chako kinatosha kuthibitisha kuwa wewe ni pepo. Ingawa unasema unayakabidhi yote katika mipango ya Mungu, kutegemea mwili wako na kile unachoishi kwa kudhihirisha, wewe bado unamilikiwa na Shetani. Ingawa Shetani pia yuko mikononi mwa Mungu, wewe mwenyewe bado ni wa Shetani na bado hujaokolewa kweli na Mungu, kwani wewe bado unaishi chini ya ushawishi wa Shetani. Je, unapaswa kufuatiliaje ili uokolewe? Chaguo ni lako—unapaswa kuchagua njia ambayo unapaswa kuchukua. Mwishowe, kama unaweza kusema: “Sina kitu bora zaidi, ninalipiza upendo wa Mungu kwa dhamiri yangu, na lazima niwe na ubinadamu kidogo. Siwezi kufanikisha chochote kikubwa zaidi, wala ubora wangu wa tabia si mkubwa sana; sielewi maono na maana ya kazi ya Mungu. Mimi hulipiza tu upendo wa Mungu, mimi hufanya chochote ambacho Mungu anataka, na kufanya yote niwezayo. Natekeleza wajibu wangu vizuri kama kiumbe wa Mungu,” kisha nitahisi kuridhika. Huu ni ushuhuda wa juu zaidi ambao unaweza kutoa. Hiki ndicho kiwango cha juu kabisa kinachohitajika kutoka kwa sehemu ya watu: kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu. Fanya tu kadiri ya uwezo wako; yanayohitajika kutoka kwako si ya juu sana. Mradi ufanye yote unayoweza kufanya, basi huu ndio ushuhuda wako.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp