Kupata Mwili kwa Mungu Hukumu ya Siku za Mwisho Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Kuhusiana na Majina ya Mungu Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme Wokovu na Wokovu Kamili Njia ya Uzima wa Milele Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu Kumjua Kristo Kumjua Mungu Biblia na Mungu Kuijua Sauti ya Mungu Maana ya Kweli ya Unyakuo Mungu Ameshuka Nchini China Kanisa la Mungu na Dini Kuwatambua Mafarisayo Njia ya Kweli Imekuwa Ikiteswa Daima Ufafanuzi wa Utatu Ukweli na Mafundisho ya Dini Kufanya Mapenzi ya Mungu
  • Aina 20 za Ukweli wa Injili
    • Kupata Mwili kwa Mungu
    • Hukumu ya Siku za Mwisho
    • Hatua Tatu za Kazi ya Mungu
    • Kuhusiana na Majina ya Mungu
    • Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme
    • Wokovu na Wokovu Kamili
    • Njia ya Uzima wa Milele
    • Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu
    • Kumjua Kristo
    • Kumjua Mungu
    • Biblia na Mungu
    • Kuijua Sauti ya Mungu
    • Maana ya Kweli ya Unyakuo
    • Mungu Ameshuka Nchini China
    • Kanisa la Mungu na Dini
    • Kuwatambua Mafarisayo
    • Njia ya Kweli Imekuwa Ikiteswa Daima
    • Ufafanuzi wa Utatu
    • Ukweli na Mafundisho ya Dini
    • Kufanya Mapenzi ya Mungu
Biblia na Mungu

Dunia ya kidini inaamini kwamba maandiko yote yametolewa na msukumo wa Mungu na yote ni maneno ya Mungu; mtu anafaaje kuwa na utambuzi mintarafu ya kauli hii?

Si kila kitu katika Biblia ni rekodi ya maneno aliyoyasema Mungu. Kimsingi Biblia inaandika hatua mbili za awali za kazi ya Mungu, ambapo sehemu moja ni rekodi ya utabiri wa kale wa manabii, na sehemu nyingine ni uzoefu na maarifa yaliyoandikwa na watu waliotumiwa na Mungu katika enzi zote. Uzoefu wa kibinadamu umetiwa doa na maoni na maarifa ya kibinadamu, kitu ambacho hakiepukiki. Katika vitabu vingi vya Biblia kuna dhana nyingi za kibinadamu, upendelevu wa binadamu, na ufasiri wa ajabu wa binadamu. Ni kweli, maneno mengi ni matokeo ya kupatiwa nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu, na ni tafsiri sahihi—lakini haiwezi kusemwa kuwa ni udhihirishaji sahihi kabisa wa ukweli. Maoni yao juu ya vitu fulani si chochote zaidi ya maarifa uzoefu binafsi, au kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu. Utabiri wa manabii ulikuwa umetolewa na Mungu mwenyewe: Unabii wa Isaya, Danieli, Ezra, Yeremia, na Ezekieli, ulitoka moja kwa moja kwa Roho Mtakatifu, watu hawa walikuwa ni waonaji maono, walipokea Roho ya Unabii, wote walikuwa ni manabii wa Agano la Kale. Wakati wa Enzi ya Sheria watu hawa, ambao walikuwa wamepokea ufunuo wa Yehova, walizungumza unabii mwingi, ambao ulisemwa na Yehova moja kwa moja.

Biblia ilikusanywa na mwanadamu, sio na Mungu; Biblia haiwezi kumwakilisha Mungu

Hata hivyo, kipi ni kikubwa: Mungu au Biblia? Kwa nini ni lazima kazi ya Mungu iwe kulingana na Biblia? Je, inaweza kuwa kwamba Mungu hana haki ya kuwa juu ya Biblia? Je, Mungu hawezi kujitenga na Biblia na kufanya kazi nyingine? Kwa nini Yesu na wanafunzi Wake hawakutunza Sabato? Ikiwa Angetunza Sabato na matendo mengine kulingana na amri za Agano la Kale, kwa nini Yesu Hakutunza Sabato baada ya kuja, lakini badala yake Aliitawadha miguu, Alivunja mkate, na kunywa divai? Je, sio kwamba haya yote hayapatikani katika amri za Agano la Kale? Ikiwa Yesu aliliheshimu Agano la Kale, kwa nini Aliyakataa mafundisho haya. Unapaswa kujua ni kipi kilitangulia, Mungu au Biblia! Kuwa Bwana wa Sabato, je, Asingeweza pia kuwa Bwana wa Biblia?

Hakuna njia ya uzima wa milele ndani ya Biblia; mwanadamu akiishika Biblia na kuiabudu, basi hatapata uzima wa milele

Njia ya maisha si kitu ambacho kinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, wala hakipatikani kwa urahisi na wote. Hiyo ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote.

Ni nini imani ya kweli katika Mungu? Ni kwa jinsi gani mtu anafaa kumwamini Mungu ili kupata sifa Zake?

“Imani katika Mungu” inamaanisha kuamini kuwa kuna Mungu; hii ndiyo dhana rahisi zaidi ya imani katika Mungu. Zaidi ya hayo, kuamini kuwa kuna Mungu si sawa na kuamini katika Mungu kwa ukweli; bali, ni aina ya imani sahili ikiwa na vipengee vya uzito vya kidini. Imani ya kweli katika Mungu ina maana kupitia maneno na kazi ya Mungu kwa msingi wa imani kuwa Mungu ndiye mkuu juu ya vitu vyote. Kwa hivyo mtawekwa huru kutokana na tabia yenu ya upotovu, mtatimiza hamu ya Mungu, na mtapata kumjua Mungu. Ni kwa kupitia safari ya aina hii tu ndio mnaweza kusemekana kuwa mnaamini katika Mungu.

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp