Imeandikwa wazi katika Biblia kwamba Bwana Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu, na wale wote wanaomwamini Bwana pia wanaamini kwamba Bwana Yesu ni Kristo na kwamba Yeye ni Mwana wa Mungu. Na bado unashuhudia kuwa Kristo mwenye mwili ni onyesho la Mungu, kwamba Yeye ni Mungu Mwenyewe. Utatuambia tafadhali kama Kristo mwenye mwili kweli ni Mwana wa Mungu, au ni Mungu Mwenyewe?

07/06/2019

Jibu:

Kristo aliyepata mwili ni Mungu Mwenyewe au Mwana wa Mungu? Hasa ni swali ambalo waumini wengi huwa na tatizo kulielewa. Wakati Bwana Yesu aliyepata mwili Alikuja kufanya kazi ya kuwakomboa wanadamu, Mungu aligeuka kuwa Mwana wa Adamu, Akionekana na kufanya kazi miongoni mwa wanadamu. Hakuifungua tu Enzi ya Neema, lakini alianzisha pia enzi mpya ambamo Mungu alikuja mwenyewe katika ulimwengu wa wanadamu kuishi na mwanadamu. Kwa ibada kuu, mwanadamu Alimwita Bwana Yesu kama Kristo, Mwana wa Mungu. Wakati huo, Roho Mtakatifu pia alishuhudia ukweli kwamba Bwana Yesu ni Mwana mpendwa wa Mungu, na Bwana Yesu alimwita Mungu wa mbinguni Baba. Kwa namna hii, fikira ya uhusiano huu wa Baba-Mwana uliundwa katika ulimwengu wa dini. Sasa hebu tufikirie kwa muda mfupi. Je, Mungu anasema mahali popote katika Mwanzo kwamba Ana Mwana? Sasa wakati wa Enzi ya Sheria, je, Yehova Mungu aliwahi kusema kwamba Alikuwa na Mwana? Hili linathibitisha kwamba kuna Mungu mmoja tu, hakuna uhusiano wa Baba-Mwana wa kuzungumziwa. Sasa watu wengine wanaweza kuuliza: Wakati wa Enzi ya Neema, kwa nini Bwana Yesu alisema kwamba Yeye ni Mwana wa Mungu? Je, Bwana Yesu Kristo alikuwa Mwana wa Mungu au Mungu Mwenyewe? Mngesema kwamba, hili ni swali ambalo sisi waumini tumelijadili kotekote katika enzi. Watu huhisi kinzano iliyo ndani ya suala hili, lakini hawajui jinsi ya kuieleza. Bwana Yesu ni Mungu, lakini pia ni Mwana wa Mungu, kwa hiyo pia kuna Mungu Baba? Watu hawawezi hata kulieleza suala hili. Kwa zaidi ya milenia mbili zilizopita, kumekuwa na wachache sana waliotambua kwamba Bwana Yesu Kristo ni Mungu Mwenyewe, ni kuonekana kwa Mungu. Kwa kweli, kuna rekodi wazi ya hili katika Biblia. Katika Yohana 14:8, Filipo alimuuliza Bwana Yesu: “Filipo akamwambia, Bwana, tuonyeshe Baba, na hiyo itatutosha.” Wakati huo, Bwana Yesu alimjibu Filipo vipi? Bwana Yesu alimwambia Filipo: “Yesu akasema kwake, nimekuwa nanyi kwa muda mrefu, na bado hujanijua, Filipo? Yeye ambaye ameniona amemwona Baba; na unasemaje basi, Tuonyeshe Baba? Huamini kwamba mimi niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi? Maneno ninenayo kwenu sineni juu yangu, ila Baba aishiye ndani yangu, anazifanya kazi hizo. Niamini kwamba niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi, la sivyo niamini kwa ajili ya kazi hizo(Jhn 14:9–11). Hapa, Bwana Yesu alisema waziwazi sana, “Yeye ambaye ameniona amemwona Baba.” Kama mnavyoona, Bwana Yesu ni kuonekana kwa Mungu Mwenyewe. Bwana Yesu hakusema hapa kwamba Yeye na Mungu wana uhusiano wa Baba-Mwana. Alisema tu, “Niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya Mimi” na pia alisema, “Mimi na yeye Baba yangu tu mmoja(Yohana 10:30). Sasa, kulingana na maneno ya Bwana Yesu, je, hatuwezi kuthibitisha kwamba Bwana Yesu ni Mungu Mwenyewe, kuna Mungu mmoja tuna hakuna “uhusiano wa Baba-Mwana” wa kuzungumzia?

Watu wengine wanaweza kuuliza, ikiwa Bwana Yesu ni Mungu Mwenyewe, basi mbona wakati Bwana Yesu anaomba, bado Anaomba kwa Mungu Baba? Kweli kuna siri kwa Bwana Yesukumwita Mungu wa mbinguni Baba katika maombi Yake. Wakati Mungu anapata mwili, Roho wa Mungu anajificha ndani ya mwili,mwili wenyewe haujui kuhusu uwepo wa Roho. Kama tu tusivyoweza kuhisi roho zetu ndani yetu. Zaidi ya hayo, Roho wa Munguhafanyi chochote cha ajabu ndani ya mwili Wake. Kwa hiyo, hata ingawa Bwana Yesualikuwa Mungu aliyepata mwili, kama Roho wa Mungu hangenenana kushuhudia kwa Mungu Mwenyewe, Bwana Yesu hangeweza kujua kwambaAlikuwa kupata mwili kwa Mungu. Kwa hivyo katika Biblia inasemekana, “Lakini kuhusu siku hiyo na saa hiyo hakuna mwanadamu aijuaye … wala Mwana, bali Baba.(Marko 13:32). Kabla ya Bwana Yesu kutekeleza huduma Yake, Aliishi ndani ya ubinadamu wa kawaida. Hakujua kweli kwamba Alikuwa kupata mwili kwa Mungu kwa sababu Roho wa Mungu ndani ya mwiliHakufanya kazi kwa namna ya ajabu, Alifanya kazi katika mipaka ya kawaida, kama tu mwanadamu yeyote mwingine. Hivyo, kwa kawaida, Bwana Yesu angeombakwa Baba wa mbinguni, ambalo ni kusema, kutoka kwa ubinadamu Wake wa kawaida, Bwana Yesu aliomba kwa Roho wa Mungu. Hili ni la maana kabisa. Wakati Bwana Yesu alitekeleza huduma Yake rasmi, Roho Mtakatifu alianza kunena na kutangaza, Akishuhudia kwamba Alikuwa Mungu aliyepata mwili. Ni wakati huo tu ndipo Bwana Yesualitambua utambulisho Wake wa kweli, kwamba Alikuwa amekuja kufanya kazi ya ukombozi. Lakini wakati Alitakiwa kupigiliwa misumari msalabani, bado Aliomba kwa Mungu Baba. Hili linaonyesha kwamba kiini cha Kristokinamtii Mungu kabisa.

Hebu tusome vifungu vingine viwili vya neno la Mwenyezi Mungu ili kubainisha ufahamu wetu wa suala hili. Mwenyezi Mungu asema, “Yesu alipomwita Mungu wa mbinguni kwa jina la Baba alipokuwa akiomba, hili lilifanywa katika mitazamo ya mwanadamu aliyeumbwa, kwa sababu Roho wa Mungu alikuwa amevaa mwili wa kawaida na Alikuwa na umbile la nje la mwanadamu aliyeumbwa. Hata ikiwa ndani yake mlikuwa na Roho wa Mungu, umbo Lake la nje bado lilikuwa lile la mtu wa kawaida; kwa maana nyingine, Alikuwa ‘Mwana wa Adamu’ jambo ambalo watu wote, akiwemo Yesu Mwenyewe, walilizungumzia. Na kwa sababu Anaitwa Mwana wa Adamu, Yeye ni mtu (Mwanamke au mwanamume, kwa vyovyote vile mwenye umbo la nje la mwanadamu) aliyezaliwa katika familia ya kawaida ya watu wa kawaida. Kwa hivyo, Yesu kumwita Mungu wa mbinguni kwa jina la Baba kulikuwa sawa na mlivyomwita mara ya kwanza Baba; Alifanya hivyo kutokana na mtazamo wa Mwanadamu aliyeumbwa. Je, mnakumbuka Sala ya Bwana ambayo Yesu aliwafundisha kukariri? ‘Baba Yetu Uliye mbinguni….’ Aliwaambia wanadamu wote wamwite Mungu wa Mbinguni kwa jina la Baba. Na kwa kuwa Naye pia alimwita Baba, alifanya hivyo kutoka kwa mtazamo wa mtu aliye katika daraja moja nanyi nyote. Kwa kuwa mlimuita Mungu wa mbinguni Baba, hili linaonyesha kuwa Yesu alijichukulia kuwa katika daraja sawa nanyi, kama mwanadamu duniani aliyeteuliwa na Mungu (yaani, Mwana wa Mungu). Kama mnamwita Mungu ‘Baba,’ je, hii si kwa sababu nyinyi ni wanadamu walioumbwa? Haijalishi Yesu alikuwa na mamlaka makubwa kiasi gani duniani, kabla ya kusulubiwa, Alikuwa tu Mwana wa Adamu, akiongozwa na Roho Mtakatifu (yaani, Mungu), Akiwa miongoni mwa viumbe wa duniani, kwani bado Alikuwa hajaikamilisha kazi Yake. Kwa hivyo, kumwita kwake Mungu wa mbinguni Baba kulikuwa tu unyenyekevu na utiifu Wake. Yeye kumwita Mungu (yaani, Roho aliye mbinguni) kwa namna ile, hata hivyo, hakudhibitishi kuwa Yeye ni Mwana wa Roho wa Mungu aliye mbinguni. Badala yake, ni kuwa mtazamo wake ni tofauti, si kwamba ni nafsi tofauti. Uwepo wa nafsi tofauti ni uongo. Kabla ya kusulubiwa kwake, Yesu alikuwa Mwana wa Adamu aliyefungwa katika udhaifu wa kimwili, na Hakuwa na mamlaka kamilifu ya Roho. Hiyo ndiyo maana Angeweza tu kutafuta mapenzi ya Mungu Baba kutoka katika mtazamo wa kiumbe. Ni kama tu Alivyoomba mara tatu huko Gethsemane: ‘Si kama Nitakavyo, bali kama Utakavyo.’ Kabla Atundikwe msalabani, Hakuwa zaidi ya Mfalme wa Wayahudi; alikuwa Kristo, Mwana wa Adamu, na wala si mwenye utukufu. Hiyo ndiyo maana, kutokana na mtazamo wa mwanadamu, Alimwita Mungu Baba(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?).

Aidha kuna wale wasemao, ‘je, si Mungu alitaja wazi kuwa Yesu ni Mwanawe mpendwa?’ Yesu ni Mwana mpendwa wa Mungu, ambaye anapendezwa naye—haya bila shaka yalitamkwa na Mungu Mwenyewe. Huyu alikuwa Mungu akijitolea ushuhuda Mwenyewe, ila kutoka katika mtazamo tofauti, ule wa Roho aliye mbinguni akitolea ushuhuda kupata Mwili Kwake. Yesu ni kupata mwili Kwake, si Mwanake mbinguni. Je, unaelewa? Je, maneno ya Yesu, ‘Mimi ni ndani ya Baba naye Baba yu ndani yangu,’ hayaonyeshi kuwa Wao ni Roho mmoja? Na si kwa sababu ya kupata mwili kulikosababisha kutenganishwa Kwao kati ya mbinguni na duniani? Uhalisi ni kwamba Wao ni kitu kimoja; hata iweje, ni Mungu anajitolea ushuhuda Mwenyewe. Kutokana na kubadilika kwa enzi, mahitaji ya kazi, na hatua mbalimbali za mpango Wake wa usimamizi, vilevile jina wamwitalo wanadamu hubadilika. Alipokuja kufanya hatua ya kwanza ya kazi, Angeweza kuitwa tu Yehova, mchungaji wa Waisraeli. Katika hatua ya pili, Mungu mwenye mwili Angeweza kuitwa tu Bwana, na Kristo. Lakini wakati huo, Roho aliye mbinguni alikariri tu kwamba Alikuwa Mwana mpendwa wa Mungu, bila kutaja kuwa Alikuwa Mwana wa pekee wa Mungu. Hili halikufanyika kabisa. Mungu angewezaje kuwa na Mwana wa pekee? Basi, Mungu asingekuwa mwanadamu? Kwa kuwa Alikuwa Mwili, Aliitwa Mwana mpendwa wa Mungu na kutokana na hili, kukazuka uhusiano wa Baba na Mwana. Ni kwa sababu tu ya utengano kati ya mbingu na dunia. Yesu aliomba kutokana na msimamo wa mwili. Kwa sababu Alikuwa Amepata mwili wa ubinadamu wa kawaida, ni kutokana na msimamo wa mwili ndipo Alisema: ‘Umbo Langu la nje ni la kiumbe. Kwa sababu Nilijivisha mwili kuja duniani, sasa Niko mbali, mbali sana na mbinguni.’ Kwa sababu hii, Angeomba tu kwa Baba kutokana na msimamo wa mwili. Huu ulikuwa wajibu Wake, ambao ni sharti Roho wa Mungu aliyepata mwili anapaswa kupewa. Haiwezekani kusema kwamba Hawezi kuwa Mungu kwa sababu tu Anamwomba Baba kutokana na msimamo wa mwili. Ijapokuwa Anaitwa Mwana mpendwa wa Mungu, Yeye bado ni Mungu Mwenyewe, ni vile tu Yeye ni mwili wa Roho, na kiini chake bado ni Roho(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?).

Mwenyezi Mungu ameonyesha mambo waziwazi sana. Wakati Bwana Yesu alikuwa Akifanya kazi miongoni mwa wanadamu, kwa kweli alikuwa Roho wa Mungu aliyevaa mwili kama mwanadamu Akifanya kazi na kuonekana kwa mwanadamu. Haijalishi jinsi Bwana Yesu alikuwa akionyesha neno Lake au kuomba kwa Mungu Baba, Kiini Chake kilikuwa uungu, sio ubinadamu. Mungu ni Roho, asiyeonekana kwa mwanadamu. Wakati Mungu anavishwa mwili, mwanadamu anaona mwili tu, hawezi kuona Roho wa Mungu. Kama Roho Mtakatifu angekuwa ameshuhudia moja kwa moja ukweli kwamba Bwana Yesu aliyepata mwili alikuwa Mungu, mwanadamu hangekubali hilo. Kwa sababu, wakati huo, hakuna aliyejua hata kilichomaanisha kwa Mungu kupata mwili. Walikutana tu na kupata mwili kwa Mungu na walikuwa na ufahamu kidogo sana. Hawakuwahi kufikiri kwamba huyo Mwana wa Adamu wa kawaida angekuwa mfano halisi wa Roho wa Mungu, yaani, kuonekana kwa Mungu katika mwili. Hata ingawa Bwana Yesu alionyesha kiasi kikubwa cha neno Lake wakati wa kufanya kazi Yake, Alimletea mwanadamu njia, “Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu,” na Alidhihirisha miujiza mingi, Akifichua kwa ukamilifu mamlaka na nguvu za Mungu, mwanadamu alikosa kumtambua kutoka kwa neno na kazi ya Bwana Yesu kwamba Bwana Yesu alikuwa Mungu Mwenyewe yaani, Alikuwa kuonekana kwa Mungu. Kwa hiyo mwanadamu alikuwa na ufahamu wa aina gani wa Bwana Yesu wakati huo? Wengine walisema kwamba alikuwa Yohana Mbatizaji, wengine walisema alikuwa Eliya. Wengine hata walimwita Bwana. Kwa hiyo, Mungu alifanya kazi tu kulingana na kimo cha watu wakati huo, Hakufanya mambo kuwa magumu kwao. Roho Mtakatifu angeweza tu kushuhudia ndani ya ufahamu wa watu wakati huo, kwa hiyo Alimwita Bwana Yesu Mwana Mpendwa wa Mungu, Akiruhusu kwa muda mwanadamu afirikire Bwana Yesu kuwa Mwana wa Mungu. Namna hii ilifaa vizuri zaidi na dhana za watu, na ilikuwa rahisi zaidi kukubali kwa kuwa, wakati huo, Bwana Yesu alikuwa Akifanya kazi ya ukombozi tu. Haijalishi vile watu walimwita Bwana Yesu, jambo muhimu lilikuwa kwamba walikubali kwamba Bwana Yesu alikuwa Mwokozi, Alisamehe dhambi zao, na hivyo walistahili kufurahia neema ya Mungu. Kwa hiyo, Roho wa Mungu alishuhudia kwa Bwana Yesu kwa namna hii kwa sababu ilifaa zaidi kwa kimo cha watu wakati huo. Hili linatimiza kabisa neno la Bwana Yesu: “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo(Yohana 16:12-13).

Licha ya ukweli kwamba hatuwezi kuona Roho wa Mungu, wakati Roho wa Mungu anavishwa mwili, tabia ya Mungu, chote ambacho Anacho na Alicho, uweza na hekima Yake vyote vinadhihirishwa kupitia kwa mwili Wake. Kutoka kwa neno na kazi ya Bwana Yesu Kristo na tabia Anayoonyesha, tunaweza kuwa na hakika kabisa kwamba Bwana Yesu ni Mungu Mwenyewe. Neno na kazi ya Bwana Yesu vimejaa mamlaka na nguvu. Kile Anachosema kinakuwa kweli, kile Anachodai kinatimika. Mara tu Anaponena, maneno Yake yanakuwa hakika. Kama tu vile neno moja kutoka kwa Bwana Yesu lilitosha kusamehe dhambi ya mwanadamu na kuwafufua wafu. Neno moja lilituliza pepo na bahari na kadhalika. Kutoka kwa neno na kazi ya Bwana Yesu, tunaweza kuona mamlaka na nguvu za Mungu, ambazo zinatawala vitu vyote, na tujauona uweza, hekima, na kazi za ajabu za Mungu. Bwana Yesu alionyesha njia katika maneno Yake, “Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu.” Alianzisha Enzi ya Neema, Akihitimisha Enzi ya Sheria, Alionyesha tabia ya Mungu ya huruma na upendo na Akakamilisha kazi ya ukombozi wa wanadamu. Bwana Yesu alifanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Neno na kazi ya Bwana Yesu ni onyesho la moja kwa moja la Roho wa Mungu. Je, hili si thibitisho kwamba Roho wa Mungu alikuja katika mwili kunena na kufanya kazi kwa ajili ya mwanadamu, kuonekana kwake? Yawezekana kwamba bila kujali namna Roho wa Mungu ananena na kufanya kazi katika mwili, hatuwezi kumtambua? Je, gamba hili la nje la mwili linaweza kweli kutuzuia kutambua kiini kitakatifu cha Kristo? Yawezekana kwamba, wakati Roho wa Mungu anavishwa mwili kunena na kufanya kazi, bila kujali ni jinsi gani tunapitia bado hatungeweza kutambua kuonekana na kazi ya Mungu? Ikiwa ni hivi, basi sisi ni wapumbavu sana katika imani yetu. Ni vipi vingine tunaweza kupata sifa ya Mungu?

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp