Kupitia Kuelewa Siri ya Majina ya Mungu, Naenda Sambamba na Nyayo za Mwanakondoo

15/01/2020

Na Mu Zhen, Taiwan

Nilipokuwa mdogo, nilikuwa mtoto mwerevu na mwenye busara na kwa hiyo daima nilipokea utunzaji wenye upendo wa wazazi, jamaa na marafiki zangu. Kwa sababu daima nilipata alama nzuri shuleni na nilikuwa karimu na mpole, nilipendwa sana na walimu na wanafunzi wenzangu. Wakati huo, nilikuwa nimejawa na matumaini kwa ajili ya siku za baadaye. Hata hivyo, nilishangaa kwambaulipofika wakati wa kufanya mtihani wa kuingia katika shule ya sekondari, nilikosa nafasi ya kujiunga na shule bora ya wasichana kwa nusu alama na badala yake nikachukuliwa na shule ya daraja la pili. Nilishindwa kabisa kukubali kilichotokea kiasi kwamba nilijifungia chumbani mwangu kwa siku mbili na kukataa kula ama kunywa. Hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kupitia kushindwa maishani mwangu—nilihisi kana kwamba nilikuwa nimeanguka katika lindi kuu na niliangaishwa na maumivu makali na uchungu.

Shule ilipoanza tena, nilihudhuria maelekezo ya mazingira nikihisi huzunika sana. Wakati wa maelekezo ya mazingira, mwanafunzi mwenza wa kike aliyekuwa katika kidato cha kutangulia alinihubiria injili ya Bwana Yesu. Nilipohudhuria mikutano zaidi ya kanisa na niliposikiza uzoefu zaidi wa ndugu, nilihisi kwamba neema ya Mungu ilikuwa halisi na ingeweza kutegemewa. Niliamini kwamba alimradi ningemwomba na kumsihi Bwana Yesu Kristo, basi ningepokea ulinzi na utunzaji Wake, na ningefurahia hisia ya amani na usalama moyoni mwangu. Kutoka mahali hapo pa huzuni mbaya, kwa utaratibu nilipata tena hali yangu ya msimamo wa kutegemea mazuri na kufikiria mema. Baadaye, katika mwaka wangu wa pili wa shule ya sekondari, nilibatizwa kama Mkristo.

Ili kujifunza zaidi kuhusu ukweli wa Biblia, nilienda kwa shule ya watawa katika chuo kikuu na kama mwanafunzi mpya wa chuo kikuu nilijifunza kozi iliyofunzwa na mchungaji iliyoitwa “Utangulizi kwa Dini.” Wakati wa darasa moja, mchungaji alituambia, “Sura ya 13, aya ya 8 ya Waebrania inasema, ‘Yesu Kristo ni yuyo huyo jana, na leo na daima.’ Bwana Yesu ndiye Mwokozi mmoja wa pekee. Yeye ni mwaminifu na mwenye kutegemewa na jina Lake halitabadilika kamwe, bila kujali enzi. Ni kwa kuliamini jina la Yesu pekee ndipo tunaweza kuokolewa….” Kutoka kwa usemi wake, nilijifunza kwamba ni kwa kupitia wokovu wa Bwana Yesu pekee ndipo tunaweza kukombolewa kutokana na uovu na kifo na ni kwa kuliamini jina la Bwana Yesu pekee ndipo tunaweza kuokolewa. Iliingia mawazoni mwangu kwamba huenda sababu ya mwanafunzi huyo mwenza wa kike aliyekuwa katika kidato cha kutangulia aliyenileta kanisani kuonekana kuwa mwenye furaha na mwenye kujiamini daima huenda ni kwa ajili ya nguvu maishani aliyopata kutoka kwa imani yake katika Bwana. Baada ya darasa hilo, niliamua kumfuata Bwana Yesu na kuweka jitihada zangu zote katika kumtumikia. Ili kufanya hivyo, nilitumia wakati wangu wote baada ya darasa kushiriki katika ushirika, mafunzo ya Biblia, kazi ya misheni ya injili, na sikuwahi kukosa kuhudhuria mahubiri ama mkutano hata mara moja.

Baada ya muda, nilitambua kwamba mahubiri ya wachungaji na wazee yalizungumzia mambo yale yale daima—hakukuwa na nuru mpya katika kile walichosema, na sisi, kama waumini, hatukupata ruzuku ya kiroho hata kidogo kutoka kwa maneno yao. Ndugu wengine waliishi katika udhaifu—hawakuwahi kuhudhuria mikutano na hakuna aliyeshughulika kuwasaidia ama kuwafadhili. Baadhi ya ndugu wangesinzia katika mikutano na kisha kujaribu kuwauzia watu bidhaa na bima baada ya mikutano. Watu wengine hata waliwasaidia wateuliwa wa kisiasa kugombea cheo. Nilijiwazia, “Bado wewe ni Mkristo ikiwa unamwamini Kristo huku ukitafuta tu faida ya kibinafsi na kutofuatilia maendeleo katika maisha yako ya kiroho? Wachungaji na wazee hata hawajaribu kukomesha mambo haya yasitukie—kweli hili linakubaliana na mapenzi na mahitaji ya Bwana?” Hali katika kanisa ilinifanya kuwa na hasira na kusikitishwa. Kwa sababu sikuwa nimepokea ruzuku yoyote ya kiroho kwa muda mrefu, nilihisi dhaifu na hafifu kiroho. Aidha, kwa sababu nilikuwa na kazi nyingi na mara nyingi nilifanya kazi ya ziada wakati wa wikendi, niliishia hata kutoshughulika kuhudhuria mikutano. Ni wakati tu nilipokumbana na masuala fulani ndipo ningesoma Biblia yangu na kuomba katika jina la Bwana. Nilihisi asiye na matumaini na lengo maalum, aliyepotea na asiyejiweza.

Mnamo Oktoba mwaka wa 2016, nilikutana na Ndugu Wang wa Kanisa la Mwenyezi Mungu mtandaoni. Ndugu Wangu alinijulisha kwa Ndugu Jin na ndugu wengine wachache. Ushirika wa Ndugu Jin ulinisaidia kuelewa ukweli mwingi ambao sikuwa nimeuelewa awali. Ushirika wake kuhusu ukweli wa kupata mwili kwa Mungu hasa ulikuwa wa busara na dhahiri nami nilipata mengi kutoka kwa ushirika huo. Nilikuwa nimemwamini Bwana kwa miaka mingi, nikasoma Biblia, na kusikiza mahubiri mengi mno ya watu mashuhuri wa kidini, wachungaji na wazee, lakini sikuwa nimewahi kumsikia yeyote akishiriki kuhusu kipengele hiki cha ukweli kwa werevu na wazi sana. Roho yangu ilinyunyizwa, na hamu ya kutafuta ikaibuka ndani yangu. Baada ya hapo, nilihudhuria mikutano yao ya mtandaoni mara nyingi.

Katika mkutano mmoja kama huo, Ndugu Jin alishiriki akisema, “Ili kuwaokoa wanadamu kabisa, Mungu alianzisha mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita, Akaugawanya katika enzi tatu tofauti naye Anatenda hatua mpya ya kazi katika kila enzi. Jina la Mungu hubadilika pamoja na kazi tofauti Atendazo. Kwa mfano, katika Enzi ya Sheria, Mungu alitenda kazi Yake chini ya jina ‘Yehova,’ akitangaza sheria na amri, na kuwaongoza Waisraeli wa kwanza katika maisha yao duniani. Hata hivyo, punde Mungu alipomaliza kazi Yake katika Enzi ya Sheria na kuanza kazi Yake ya ukombozi katika Enzi ya Neema, jina Lake lilibadilika kutoka ‘Yehova’ na kuwa ‘Yesu.’ Sasa tuko katika siku za mwisho, na Mungu anatenda kazi ya hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu juu ya msingi wa kazi ya ukombozi ya Yesu. Amehitimisha Enzi ya Neema, kuikaribisha Enzi ya Ufalme, na katika kufanya hivyo, jina Lake limebadilika na kuwa ‘Mwenyezi Mungu.’” Nilipomsikia Ndugu Jin akisema jina la Mungu lilikuwa limebadilika, nilijiwazia, “Biblia inasema wazi: ‘Yesu Kristo ni yuyo huyo jana, na leo na daima’ (Waebrania 13:8). Bwana Yesu ambaye namwamini ni Mungu mmoja wa kweli na jina la Bwana Yesu halitabadilika kamwe. Ni kupitia jina la Bwana Yesu tu ndipo tunaweza kuokolewa—unawezaje kusema kwamba jina la Mungu limebadilika? Ikiwa, katika maombi yetu, hatuliiti jina la Yesu, lakini tutumie jina jingine, hiyo inawezaje bado kuambatana na Biblia?” Ushirika wa Ndugu Jin ulipinga imani yangu kwa kina. Alitoa analojia ifuatayo, akisema “Dada Mu Zhen, kampuni fulani ingekufanya Ofisa wa Mipango mwaka mmoja na Meneja mwaka ufuatao, basi uwe Ofisa wa Mipango ama Meneja, mahitaji ya kazi yako yangeamua badiliko la jina lako. Watu wangekuita Ofisa wa Mipango Mu, lakini sasa wanakuita Meneja Mu—licha ya badiliko la jina na cheo, wewe mwenyewe ungebadilika? Si bado ungekuwa wewe?” Nilijibu, “Bado ningekuwa mimi,” na sikupinga, lakini moyoni mwangu bado sikuweza kukubali kile alichokuwa akisema. Nilijiwazia, “Jina la Mungu haliwezi kubadilika kamwe. Ni kwa kuliamini jina la Bwana Yesu pekee ndipo tunaweza kuokolewa. Hutanishawishi kwa urahisi. Nitakupuuza tu kuanzia sasa na kuendelea na hivyo ndivyo mambo yatakavyokuwa.” Baada ya mkutano kuisha, niliwazuia ndugu wote wa Kanisa la Mwenyezi Mungu katika programu ya kuongea.

Nilishangaa kwamba katika siku baada ya kuwazuia ndugu wote wa Kanisa la Mwenyezi Mungu, mnamo saa mbili usiku, nilipokuwa nikiosha vyombo jikoni, ghafla nilisikia kengele ya mlango ikilia. Nilifungua mlango na mbele yangu walisimama wasichana wawili ambao sikuwa nimewahi kuwaona awali. Msichana mmoja alinikabidhi habari fulani. Mara ya kwanza nilikuwa mpole sana kwa wasichana hao, lakini nilipoona kwamba kijitabu ambacho msichana huyo alikuwa amenipa kilisema, “Kurudi kwa Kristo—Bwana Yesu Amerudi Pamoja na Mawingu” kwa herufi kubwa, ghafla niligundua kwamba walikuwa wanakuja kuhubiri injili. Kwa sababu niliamini wakati huo kwamba jina la Bwana Yesu halingewahi kubadilika, nilikasirishwa kidogo na hao wasichana wawili na kurudisha kijitabu walichokuwa wamenipa. Walionekana kuhuzunika kiasi na walipogeuka kuondoka, dada mmoja aliniuliza, “Dada, huwezi kukubali habari hii kwa sababu humwamini Mungu au kwa sababu unatoka katika dhehebu lingine? Umewahi kuchunguza na kutafuta ukweli kwa uangalifu?” Bila kujali walichosema dada hao, kweli sikutaka kuwapa muda wangu mwingine tena, kwa hivyo nilirudi tu kuosha vyombo jikoni. Nilipokuwa nikiosha vyombo, niliendelea kukumbuka swali la dada huyo, “Umewahi kuchunguza na kutafuta ukweli kwa uangalifu?” Nilijiwazia, “Huenda kweli sijawahi kuutafuta ukweli kwa uangalifu.” Nilikumbuka jinsi Ndugu Wang na wengine walivyokuwa wameshiriki kuhusu jina la Mungu kubadilika na kisha nikafikiri kuhusu jinsi suala hili lilikuwa limetofautiana na ufahamu wangu mwenyewe. Lakini hata wakati sikuwa nimeelewa, sikuwa na tamaa ya kuatafuta ukweli, na nilikuwa nimechunguza alichokuwa amesema kwa kutumia maarifa yangu ya Biblia. Nilikuwa nimekubali vipengele hivyo vya ushirika wao ambavyo nilikubaliana navyo, lakini nilikuwa nimekosa kutafuta ama kutilia maanani vipengele hivyo ambavyo sikukubaliana navyo. Ni hapo tu ndipo nilipogundua kwamba maarifa yangu ya Biblia yalikuwa yamenisababisha kupoteza usafi na wepesi wangu wa moyo. Nilikuwa nimechukua mtazamo wa kujidai kwa ukweli—hakika ningewezaje kujichukulia kama mtu aliyetafuta ukweli?

Nilipotulia kidogo, nilikumbuka jambo ambalo ndugu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu walishiriki mara nyingi: “Kondoo wa Mungu huisikia sauti ya Mungu—ikiwa tunataka kukaribisha kurudi kwa Bwana, lazima tuisikilize sauti ya Mungu, tuitambue sauti Yake na kuelewa ukweli ni nini.” Ushirika uliotolewa na ndugu ulikuwa katika kupatana na Biblia. Wanawali wenye busara walilazimika kuisikiliza sauti ya Mungu, na je, si Petro wa Enzi ya Neema aliweza kumfuata Bwana Yesu kwa sababu alikuwa ameisikia sauti ya Mungu katika maneno ya Bwana? Baada ya kugundua jambo hili, nilichukua Biblia yangu kwa haraka na kufungua Kitabu cha Ufunuo sura ya 3, aya za 20-22, ambapo inasema, “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi. Kwa yeye ambaye hushinda nitamruhusu aketi nami katika kiti Changu cha enzi, jinsi mimi pia nilivyoshinda, na nimeketi na Baba Yangu katika kiti Chake cha enzi. Yeye ambaye ana sikio, hebu asikize lile ambalo Roho huambia makanisa.” Nilifikiria kifungu hiki cha Maandiko kwa uangalifu na kujiwazia, “Mungu anatuomba kwamba wakati wowote Roho Mtakatifu anaponena, lazima tusikilize. Nimekuwa na bahati ya kutosha sasa kusikia kuhusu kurudi kwa Bwana na kuwa na fursa ya kujua kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, kwa hiyo mbona bado nakubali mawazo yangu yanizuie? Kwa nini nakataa kusikiliza fikira zozote ambazo sielewi ama zinazotofautiana na fikira zangu? Hata kama siwezi kukubali mara moja kwamba jina la Mungu limebadilika, napaswa angalau kutafuta na kuchunguza suala hili na kufanya uamuzi punde ninapopata ufahamu kamili!” Kisha nikapata kifungu kifuatacho bila kutarajia katika Mathayo sura ya 7, aya ya 7: “Ombeni, na mtapatiwa; tafuteni, na mtapata; pigeni hodi, na mtafunguliwa.” “Ikiwa Mungu kweli Amekuja akibisha,” Niliwaza, “na kwa sababu ya kudanganywa na fikira zangu mwenyewe, nifunge masikio yangu na kumfungia nje katika kutojali kwangu kabisa na kuukosa wokovu wa Mungu katika siku za mwisho, si hiyo itakuwa aibu mbaya sana?”

Usiku huo, sikuweza kulala nami niliendelea kukumbuka yote ambayo yalitukia jioni hiyo. Nilijiwazia, “Nimeishi hapa kwa miaka 18 na hii ndiyo mara ya kwanza ambapo yeyote amewahi kuja kueneza injili, Dada huyo hata aliniuliza ikiwa nimewahi kuutafuta na kuuchunguza ukweli kwa uangalifu—inawezekana kwamba ulikuwa mpango wa Mungu kwa dada hawa wawili ambao sikuwa nimewahi kukutana nao waje kunienezea injili? Kisha nilipokuwa nikihisi mwenye wahaka baada ya kuwakataa na kuisoma Biblia ili kupata majibu, Mungu alinielekeza kwa kifungu kuhusu Bwana kupiga hodi mlangoni—je, nilikuwa na makosa kuwafukuza? Je, Mwenyezi Mungu kweli ni Bwana Yesu aliyerudi?” Nikiwa na fikira hizi akilini, nilitoka kitandani mara moja na kumwomba Bwana, nikimwomba mwongozo na nuru Yake. Baada ya kumaliza maombi yangu, niliwasha kompyuta yangu na kuenda kwa tovuti rasmi ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, ambayo inaitwa “Injili ya Kushuka kwa Ufalme” na kutafuta vifungu vilivyohusiana na jina la Mungu. Nilipata kifungu hiki cha maneno ya Mwenyezi Mungu: “Wengine wanasema kwamba jina la Mungu halibadiliki, hivyo, mbona basi jina la Yehova likawa Yesu? Ilitabiriwa kuja kwa Masihi, hivyo mbona basi mwanadamu kwa jina Yesu alikuja? Mbona jina la Mungu lilibadilika? Kazi kama hiyo haikufanyika muda mrefu uliopita? Hawezi Mungu leo kufanya kazi mpya? Kazi ya jana inaweza kubadilishwa, na kazi ya Yesu inaweza kufuata baada ya hiyo ya Yehova. Haiwezi kazi ya Yesu kurithiwa na kazi nyingine? Ikiwa jina la Yehova linaweza kubadilishwa kuwa Yesu, basi jina la Yesu haliwezi kubadilishwa pia? Hakuna jambo lolote hapa lisilo la kawaida; ni kwamba tu watu ni punguani sana. Mungu daima atakuwa Mungu. Bila kujali mabadiliko ya kazi Yake na jina Lake, tabia na maarifa Yake hayabadiliki milele. Ikiwa unaamini kwamba Mungu anaweza tu kuitwa na jina Yesu, basi unajua machache sana(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?). Baada ya kusoma kifungu hiki, nilielewa kwamba Mungu hufanya kazi mpya katika kila enzi na huchukua jina jipya kama kazi Yake mpya inavyohitaji. Nilifikiri kuhusu jinsi, katika Enzi ya Sheria, jina la Mungu lilikuwa Yehova, na chini ya jina hili Mungu aliwaongoza Waisraeli. Hata hivyo, wakati Bwana Yesu alipokuja kufanya kazi Yake, je, jina la Mungu halikubadilika kutoka Yehova na kuwa Yesu? Mwenyezi Mungu alikuwa sasaAmeeleza suala hili kwa uwazi mkubwa—ni nani angefichua siri kama hizi ikiwa Mungu hangekuja kuuonyesha ukweli? Nilikuwa nimekataa kutafuta na kuchunguza wazo la jina la Mungu kubadilika kwa sababu halikuwa limepatana na maoni yangu mwenyewe. Ikiwa Mwenyezi Mungu kweli alikuwa kuonekana tena kwa Bwana Yesu, na nikamfungia Bwana nje hata Alipopiga hodi mlangoni mwangu mara kwa mara, ingekuwa aibu mbaya sana ikiwa basi ningepoteza fursa ya kukaribisha kurudi kwa Bwana. Kwa hiyo, niliamua kuitafuta na kuichunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho kwa uangalifu.

Baadaye, nilikoma kuwazuia ndugu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu mtandaoni na kuwaambia kuhusu uzoefu niliokuwa nao usiku huo. Katika mkutano, ndugu walishiriki kifungu hiki cha Maandiko nami: “Mnafikiri vipi? Iwapo mtu ana kondoo mia moja, na mmoja wao apotee, je, hawaachi hao tisini na tisa, na kuenda milimani, na amtafute huyo ambaye amepotea?(Mathayo 18:12). Ndugu walisema kwamba nilikuwa tu kama yule kondoo aliyepotea na kwamba Mungu alikuwa Ametoka nje ili kunitafuta na kunirudisha mbele Zake. Kweli ilikuwa kwa sababu ya neema ya Mungu ndipo, nilipopotoka, Mungu aliniongoza kukoma kuwazuia ndugu na kuendelea kuhudhuria mikutano. Namshukuru Mungu kwa kutoniacha!

Papo hapo, Dada Xiling aliniuliza, “Dada Mu Zhen, je, uliwazuia watu wote ghafla kwa sababu hukuelewa kipengele fulani cha ukweli?” Niliashiria kwa kichwa, nikisema, “Biblia inasema wazi, ‘Yesu Kristo ni yuyo huyo jana, na leo na daima’ (Waebrania 13:8). Hii inathibitisha kwamba Yesu Kristo habadiliki kamwe. Hata Mungu atakaporudi katika siku za mwisho, bado Anapaswa kutumia jina Yesu—jina hili halitawahi kubadilika. Lakini Ndugu Jin alishiriki akisema kwamba jina la Mungu katika siku za mwisho ni Mwenyezi Mungu na siwezi kukubali jambo hili kabisa. Tangu nibatizwe, daima nimeomba kwa kuliita jina la Bwana Yesu, kwa hiyo nawezaje kumwita kwa jina jingine?” Nilipokuwa nimemaliza, Dada Xiling alinitunia kifungu kifuatacho cha maneno ya Mungu: “Kuna wale ambao wanasema kuwa Mungu habadiliki. Hiyo ni sahihi, lakini inaashiria kutobadilika kwa tabia ya Mungu na kiini Chake. Mabadiliko ya jina lake na kazi hayathibitishi ya kuwa kiini chake kimebadilika; kwa maneno mengine, Mungu siku zote Atakuwa Mungu, na hii kamwe haitabadilika. Iwapo utasema kuwa kazi ya Mungu daima inabaki vile vile, basi Angekuwa na uwezo wa kumaliza mpango wake wa usimamizi wa miaka elfu sita? Wewe hujua tu kwamba Mungu habadiliki milele, lakini je, unajua kuwa Mungu ni mpya milele na kamwe si wa zamani? Kama kazi ya Mungu kamwe haikubadilika, basi Angeweza kulea mwanadamu hadi leo? Kama Mungu habadiliki, basi mbona Yeye tayari Amefanya kazi ya nyakati mbili? … Maneno haya ‘Mungu daima ni mpya na kamwe si wa zamani’ yanarejelea kazi yake, na maneno haya ‘Mungu habadiliki’ kinarejelea kile ambacho Mungu anacho na alicho kiasili. Bila kujali, huwezi kubaini kazi ya miaka elfu sita kwa mtazamo mmoja, ama kwa kuielezea tu kwa maneno ambayo hayabadiliki. Huo ni ujinga wa mwanadamu. Mungu si wazi kama mwanadamu anavyofikiria, na kazi yake haitasimama katika enzi moja. Yehova, kwa mfano, haliwezi daima kusimamia jina la Mungu; Mungu pia hufanya kazi yake kwa kutumia Jina la Yesu, ambayo ni ishara ya vile ambavyo kazi ya Mungu daima husonga kwenda mbele(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)).

Kisha Dada Xiling akasema, “Maneno ya Mwenyezi Mungu yanaeleza hivi wazi sana: Tunaposema kwamba ‘Mungu habadiliki,’ tunamaanisha tabia na dutu Yake. Hii haimaanishi kwamba jina la Mungu halibadiliki kamwe. Mungu ni mpya daima na kamwe si mzee, kazi ya Mungu inasonga mbele daima, na jina Lake lazima libadilike ili kuonyesha mabadiliko katika kazi Yake. Hata hivyo, bila kujali jinsi jina la Mungu linavyoweza kubadilika, dutu ya Mungu haibadiliki kamwe—Mungu bado ni Mungu. Na bado hatuelewi ‘habadiliki‘ inamaanisha nini kweli na hatuoni jinsi kazi ya Mungu ni mpya daima na si nzee kamwe, na kwa hiyo ni rahisi sana kwetu kuiwekea kazi ya Mungu mipaka na hata kumpinga Mungu kwa msingi wa fikira na mawazo yetu. Kwa mfano, Mafarisayo walishikilia fikira kwamba ‘Yehova ni Mungu wa pekee, hakuna mwokozi ila Yehova.’ Kwa hiyo, Mungu alipokuja kufanya kazi Yake kwa jina ‘Yesu’, na Mafarisayo wakaona kwamba jina la Yehova lilikuwa limebadilika lakini kwamba Hakuwa akiitwa ‘Masiya’ kama ilivyotabiriwa na unabii, walikataa kwamba Bwana Yesu alikuwa Kristo, kwamba Yeye alikuwa Mungu Mwenyewe, na walishutumu na kumpinga Bwana Yesu kwa hasira, hadi mwishowe walishirikiana na mamlaka ya Kirumi kumtundika Bwana Yesu msalabani. Kwa sababu ya dhambi hii mbaya sana, walipata adhabu ya Mungu. Vivyo hivyo, tukiendelea katika kuishikilia Biblia bila kufikiria, na tushikilie fikira kwamba jina la Mungu halibadiliki, na tuikatae kazi ya Mungu ya siku za mwisho, basi tutakuwa tofauti na Mafarisayo, waliodai kumwamini Mungu lakini walioifuata njia ya kumpinga Mungu?”

Kisha, alinisihi nisome vifungu vingine viwili vya maneno ya Mungu: “Katika kila enzi, Mungu Anafanya kazi mpya na huitwa kwa jina jipya; Je, anawezaje kufanya kazi sawa katika enzi tofauti? Itakuwaje Yeye kugandamana na yale ya zamani? Jina la Yesu lilichukuliwa kuwa la kazi ya ukombozi, hivyo bado Yeye Anaweza kuitwa kwa jina moja wakati Atarudi katika siku za mwisho? Je, bado Yeye Atafanya kazi ya ukombozi? Ni kwa nini Yehova na Yesu ni kitu kimoja, ilhali wanaitwa kwa majina tofauti katika enzi hizi tofauti? Je, si kwa sababu enzi za kazi Yao ni tofauti? Jina moja linawezaje kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake? Kwa njia hii, lazima Mungu aitwe kwa jina tofauti katika enzi tofauti, lazima Atumie jina kubadilisha enzi na kuwakilisha hiyo enzi, kwa kuwa hakuna jina moja linaweza kumwakilisha Mungu mwenyewe kikamilifu. Na kila jina linaweza tu kuwakilisha kipengele cha wakati cha tabia ya Mungu katika enzi fulani; yote linahitaji kufanya ni kuwakilisha kazi Yake. Kwa hivyo, Mungu Anaweza kuchagua jina lolote ambalo linafaa tabia yake kuwakilisha enzi nzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)). “Je, Jina la Yesu—‘Mungu pamoja nasi,’—linaweza kuwakilisha tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake? Je, linaweza kueleza Mungu kwa ukamilifu? Kama mwanadamu atasema ya kwamba Mungu Ataitwa tu Yesu, na hawezi kuwa na jina lingine kwa sababu Mungu hawezi kubadilisha tabia yake, basi maneno hayo ni kufuru! Je, unaamini kwamba jina la Yesu, Mungu pamoja nasi, linaweza kumwakilisha Mungu kikamilifu? Mungu Anaweza kuitwa majina mengi, lakini baina ya majina haya mengi, hamna moja ambalo linaweza kujumlisha yote ambayo Mungu Anamiliki, na hamna jina moja ambalo linaweza kumwakilisha Mungu kikamilifu. Na hivyo Mungu Ana majina mengi, lakini majina haya mengi hayawezi kuelezea tabia ya Mungu kikamilifu, kwa kuwa tabia ya Mungu ni tajiri sana, na yanazidi uwezo wa mwanadamu kumjua Yeye. … Neno au jina moja maalum halina uwezo wa kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake. Kwa hivyo, je, Mungu Anaweza kuchukua jina moja lisilobadilika? Mungu ni mkuu sana na mtakatifu sana, kwa hivyo mbona wewe huwezi kumruhusu Yeye abadili jina Lake katika kila enzi mpya? Kwa hivyo, katika kila enzi ambayo Mungu binafsi hufanya kazi yake mwenyewe, Yeye hutumia jina ambalo linafaa enzi hiyo ili kujumlisha kazi ambayo anaifanya. Yeye hutumia hili jina haswa, ambalo linamiliki umuhimu wa wakati, kuwakilisha tabia yake katika enzi hiyo. Mungu hutumia lugha ya mwanadamu kuelezea tabia yake mwenyewe(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)).

Dada Xiling alishiriki akisema, “Mungu hutenda tu sehemu moja ya kazi ya mpango Wake katika enzi yoyote naye huonyesha tu kipengele kimoja cha tabia Yake. Jina Analochukua katika enzi fulani linawakilisha tu tabia Anayoonyesha na kazi Afanyayo katika enzi hiyo. Kwa mfano, katika Enzi ya Sheria, jina Yehova lilitumika kuwakilisha kazi ambayo Mungu alifanya na vilevile kuonyesha vipengele vya uadhama, hasira, huruma na lawama vya tabia Yake. Chini ya jina Yehova, Mungu alitangaza sheria na amri na kuwaongoza wanadamu katika maisha yao duniani. Nayo tabia ya watu iligeuka kuwa yenye kufuata utaratibu zaidi na zaidi, nao wakajifunza jinsi ya kumwabudu Mungu. Mwishoni wa Enzi ya Sheria, kwa sababu watu walikuwa wamepotoshwa na Shetani zaidi na zaidi, waliacha kufuata sheria na amri na kuwa katika hatari ya kushutumiwa na kuuawa. Ili kuwaokoa watu kutokana na ukali wa sheria, Mungu alitenda kazi ya ukombozi chini ya jina la Yesu, hivyo kuanzisha Enzi ya Neema na kuhitimisha Enzi ya Sheria. Alionyesha tabia Yake ya upendo na rehema, Akahubiri njia ya toba na hatimayeAkawakomboa wanadamu kupitia kusulubiwa Kwake. Wale wote waliomkubali Bwana Yesu kama Mwokozi na kuomba katika jina la Bwana ili kukiri na kutubu walisamehewa. Kutoka kwa jambo hili, tunaweza kuona kwamba jina ambalo Mungu huchagua katika kila enzi lina maana. Kila jina linawakilisha tu sehemu ya kazi ya Mungu na kipengele cha tabia Yake—jina moja haliwezi kumwakilisha Mungu mzima. Ikiwa, katika Enzi ya Neema, Mungu angekuja kwa jina Yehova na si Yesu, basi kazi ya Mungu ingekoma kuendelea nje ya Enzi ya Sheria, na sisi, kama wanadamu wapotovu, hatungewahi kupokea ukombozi wetu, lakini badala yake tungeshutumiwa na kuuawa kwa sababu ya kukiuka sheria na amri. Vivyo hivyo, ikiwa, wakati Mungu aliporudi katika siku za mwisho, Angekuwa bado anaitwa Yesu, basi kazi ya Mungu ingekoma kuendelea nje ya Enzi ya Neema. Dhambi zetu zingesamehewa, lakini bado tungeishi katika mzunguko huo wa kutenda na kukiri dhambi na hatungeweza kujinasua kutoka kwa minyororo ya dhambi na kupata utakaso. Kwa hiyo, ili kutukomboa kabisa kutoka kwa minyororo ya dhambi na kupata utakaso, Mungu amepata mwili tena ili kuonyesha maneno Yake na kutenda kazi ya hukumu na utakaso, ili kuanzisha Enzi ya Ufalme na kuhitimisha Enzi ya Neema. Huku enzi zikibadilika, jina la Mungu pia limebadilika na kuwa ‘Mwenyezi Mungu,’ jambo ambalo linatimiza unabii katika Kitabu cha Ufunuo sura ya 1, aya ya 8 inayosema, ‘Mimi ndiye Alfa na Omega, Mwanzo na tena mwisho, Akasema Bwana, ambaye yuko, na ambaye alikuweko, na ambaye atakuja, Mwenyezi.’”

Kupitia ushirika uliotolewa na ndugu, nilipata kuelewa jinsi kifungu cha Maandiko kinachosema, “Yesu Kristo ni yuyo huyo jana, na leo na daima” (Waebrania 13:8) hakimaanishi kwamba jina la Mungu halitabadilika kamwe, lakini badala yake kwamba dutu ya Mungu haibadiliki. Pia nilijifunza kwamba Mungu aligawa mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita katika enzi tatu—Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme—na kwa kila hatua mpya ya kazi, Mungu huchukua jina jipya ili kuwakilisha kazi na tabia Yake wakati wa enzi hiyo. Pia Yeye hutumia kuchukua kwa jina jipya ili kuikaribisha enzi mpya. Jina la Mungu lina maana sana katika kila enzi! Ikiwa, kama nilivyoamini awali, jina la Mungu halikubadilika kamwe na, Aliporudi, bado Aliitwa Yesu, si kazi Yake basi ingebaki ikiwa imesimama?

Baada ya mkutano, tena nilitafuta vifungu fulani kutoka kwa Ufunuo: “Mimi ndiye Alfa na Omega, Mwanzo na tena mwisho, Akasema Bwana, ambaye yuko, na ambaye alikuweko, na ambaye atakuja, Mwenyezi(Ufunuo 1:8). “Yule ambaye anashinda nitamfanya awe nguzo katika hekalu lake Mungu wangu, na hatatoka nje tena: na nitaandika kwake jina lake Mungu wangu, na jina la mji wake Mungu wangu, ambao ni Yerusalemu mpya, ambao hukuja chini kutoka kwa Mungu wangu mbinguni: na nitaandika kwake jina langu jipya(Ufunuo 3:12). Kila kitu kilikuwa wazi ghafla baada ya kusoma vifungu hivi, nami nikajiwazia, “Nimesoma vifungu hivi viwili awali, kwa hiyo mbona sikutambua vilimaanisha nini kweli? Vifungu hivi viwili vya Maandiko vinatabiri kwa uwazi jinsi, Mungu atakaporudi katika siku za mwisho, hataitwa Yesu tena na jina Lake jipya litakuwa ‘mwenye Uweza.’ Daima nilikuwa nimeshikilia dondoo hiyo kutoka kwenye Biblia inayosema, ‘Yesu Kristo ni yuyo huyo jana, na leo na daima’ (Waebrania 13:8), nikifikiri kwamba jina la Mungu halingebadilika kamwe, lakini sikuwahi kufikiri kuchunguza vifungu vingine vya Maandiko, nami nikaendelea tu kukataa na kupinga kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Nilikuwa mjinga kweli!” Kupitia ushirika uliotolewa na ndugu, pamoja na unabii katika Biblia kuhusu jina la Mungu, sikuwa tena na mashaka kuhusu jina ambalo Mungu amechagua katika siku za mwisho.

Muda fulani baadaye, katika mkutano, tulisoma kifungu kingine cha maneno ya Mungu: “Nilijulikana kama Yehova wakati mmoja. Pia niliitwa Masihi, na wakati mmoja watu waliniita Yesu Mwokozi kwa sababu walinipenda na kuniheshimu. Lakini leo Mimi si yule Yehova au Yesu ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita—Mimi ni Mungu ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu ambaye Ataikamilisha enzi. Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye Anainuka kutoka mwisho wa dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu. Watu hawajawahi kushirikiana na Mimi, hawajawahi kunifahamu, na daima hawaijui tabia Yangu. Tangu uumbaji wa dunia hadi leo, hakuna mtu yeyote ambaye ameniona. Huyu ni Mungu anayemtokea mwanadamu katika siku za mwisho lakini Amejificha kati ya wanadamu. Anaishi kati ya wanadamu, ni wa kweli na halisi, kama jua liwakalo na moto unaochoma, Aliyejaa nguvu na kujawa mamlaka. Hakuna mtu au kitu chochote ambacho hakitahukumiwa kwa maneno Yangu, na mtu au kitu chochote ambacho hakitatakaswa kupitia moto unaowaka. Hatimaye, mataifa yote yatabarikiwa kwa ajili ya maneno Yangu, na pia kupondwa na kuwa vipande vipande kwa sababu ya maneno Yangu. Kwa njia hii, watu wote katika siku za mwisho wataona kuwa Mimi ndiye Mwokozi aliyerejea, Mimi ndiye Mungu Mwenyezi ambaye Anawashinda binadamu wote, nami Nilikuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu wakati mmoja, lakini katika siku za mwisho Ninakuwa pia miale ya Jua linalochoma vitu vyote, na pia Jua la haki Linalofichua vitu vyote. Hivyo ndivyo ilivyo kazi Yangu ya siku za mwisho. Nilichukua jina hili nami Ninamiliki tabia hii ili watu wote wapate kuona kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki, na Mimi ni jua linachoma, na moto unaowaka. Ni hivyo ili watu wote waweze kuniabudu, Mungu pekee wa kweli, na ili waweze kuuona uso Wangu wa kweli: Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, na Mimi si Mkombozi tu—Mimi ni Mungu wa viumbe vyote katika mbingu na dunia na bahari(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”).

Dada Xiling alishiriki akisema, “Katika siku za mwisho, Mungu ameanza kazi ya hukumu kwa maneno katika Enzi ya Ufalme chini ya jina ‘Mwenyezi Mungu,’ na Amefichua kwa wanadamu tabia Yake ya haki na yenye uadhama, isiyovumilia kosa. Maneno ambayo Mwenyezi Mungu ameonyesha yanafunua uhalisi wa Shetani kuwapotosha wanadamu pamoja na chanzo cha upinzani wetu kwa Mungu. Maneno ya Mungu hutoa hukumu kwa uasi na udhalimu wetu na kutuonyesha njia na mwelekeo tunaohitaji kufuata ili kubadili tabia zetu. Alimradi tunalenga kuufuatilia ukweli katika vitu vyote, tuutumie ukweli kuzing’oa tabia zetu potovu, na tutende na kuwatendea wengine kulingana na madai ya Mungu, tunaweza kuepuka tabia zetu potovu polepole na kupata wokovu kamili wa Mungu. Kazi ya Mwenyezi Mungu duniani itakapokamilika, wale wote walioikubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho na kupata utakaso na wokovu wa Mungu wataongozwa na Mungu hadi katika ufalme Wake ili kufurahia baraka za Mungu na ahadi Yake. Kwa wale walioikataa kazi ya Mungu katika siku za mwisho na hata wakampinga, kumshutumu, kumkashifu na kumkufuru, wote wataangamizwa na maafa makubwa ya nyakati za mwisho na wataadhibiwa na kuangamizwa na Mungu, Kwa hiyo, Mungu huchukua jina ‘Mwenyezi Mungu’ ili kuonyesha tabia Yake ya haki na uadhama isiyovumilia kosa la wanadamu wote, Yeye huwatenga watu kulingana na aina yao, huihitimisha enzi hii ya uovu na kumaliza kazi yote ya mpango wa Mungu wa usimamizi wa miaka elfu sita. Mungu anataka tuone kwamba Yeye si Bwana na Muumba wa vitu vyote pekee, Anaweza pia kutumika kama sadaka yetu ya dhambi na hata Anaweza kuwakamilisha, kuwabadili na kuwatakasa wanadamu. Mungu ndiye Alfa na Omega na matendo Yake ya ajabu hayaeleweki kwa mwanadamu. Kwa hiyo, Mungu kuchukua jina ‘Mwenyezi Mungu’ ina maana hasa. Kwa sasa, Roho Mtakatifu hulinda tu kazi iliyofanywa chini ya jina la Mwenyezi Mungu. Wote wanaiokubali kazi ya Mungu ya siku ya mwisho na kuomba katika jina la Mwenyezi Mungu wanaweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu, na ruzuku ya maji yaliyo hai ya uzima. Makanisa ya Enzi ya Neema yamekuwa bila matumaini na yenye ukiwa—imani ya waumini wao inakuwa baridi, mahubiri yao hayana maana, hawaguswi katika maombi, na wengi wao zaidi na zaidi wanapotoshwa na mitindo ya kidunia. Chanzo cha shida zao kiko katika ukweli kwamba Mungu anatenda kazi mpya, na kazi ya Roho Mtakatifu imehama kutoka katika makanisa ya Enzi ya Neema hadi katika makanisa ya Enzi ya Ufalme. Wameshindwa kwenda sambamba na nyayo za Mwanakondoo, wameshindwa kuikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu, na kwa hiyo, hawawezi kupata ruzuku ya maji yaliyo hai ya uzima na lazima wagaagae gizani bila njia ya kutoka.”

Kupitia kusoma maneno ya Mungu na kuusikia ushirika wa dada, nilipata ufahamu wa kina zaidi wa maana ya Mungu kuchukua majina tofauti katika enzi tofauti. Pia nilipata maarifa kuhusu kazi ya Mungu ya hukumu na tabia Anayoonyesha katika siku za mwisho—hii ni muhimu kwa ukombozi wetu kutoka kwa pingu za dhambi na kwa kuokolewa kwetu na Mungu! Kama ilivyotukia, sababu ambayo sikuwa nimehisi kukimiwa niliposikiza mahubiri katika miaka ya karibuni, na kwa nini imani ya ndugu zangu iligeuka na kuwa dhaifu na mahubiri yakakosa maana ilikuwa kwa sababu kazi ya Roho Mtakatifu ilikuwa imehama tayari: Roho Mtakatifu sasa Analinda tu kazi iliyofanywa chini ya jina Mwenyezi Mungu. Kwa sababu hatukuwa tumekubali jina jipya la Mungu na hatukuwa tukienda sambamba na nyayo za Mwanakondoo, tulikuwa tumetumbukia gizani. Ni hapo tu ndipo nilipojua moyoni mwangu kwamba Mwenyezi Mungu kweli ni Bwana Yesu aliyerudi.

Baadaye, ndugu zangu walishiriki nami kuhusu jinsi ya kutambua makanisa ya kweli kutoka kwa makanisa bandia, jinsi ya kutofautisha kazi ya Roho Mtakatifu na kazi ya Shetani, na vipengele vingine vya ukweli. Nilinufaika sana kutokana na ushirika huu. Kila wakati nilipoungana na ndugu zangu ili kutazama filamu na video za injili, nilihisi kutimizwa kiroho na hisia ya amani na usalama iliujaza moyo wangu. Maneno ya Mwenyezi Mungu hayakutatua tu maswali mengi niliyokuwa nayo awali katika kumwamini kwangu Bwana, lakini pia yalitatua shida nyingi nilizokuwa nazo maishani mwangu. Pia nilipata tena hisia ya imani niliyokuwa nayo nilipoanzakumwamini Bwana kwa mara ya kwanza. Nilifurahia kwamba Mungu alinichagua kuikubali kazi Yake ya siku za mwisho nami nikaanza kuenda sambamba na nyayo za Mwanakondoo. Sasa, ninasoma maneno ya Mwenyezi Mungu kila siku. Kadri ninavyozidi kusoma, ndivyo ninavyozidi kuhisi mwangaza ukiujaza moyo wangu, na kwa dhati nina uhakika kabisa kwamba neno la Mwenyezi Mungu ndilo ukweli nalo ni sauti ya Mungu. Nilikuwa na uhakika kabisa kwamba Mungu ameonekana sasa naye Anafanya kazi kama Mwenyezi Mungu, nami nikakubali jina la Mwenyezi Mungu na kujiunga kirasmi na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniokoa!

Inayofuata: Sauti Hii Yatoka Wapi?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kukutana na Bwana Tena

Na Jianding, AmerikaNilizaliwa katika familia ya Kikatoliki, na tangu nikiwa na umri mdogo mamangu alinifunza kusoma Biblia. Wakati huo,...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp